Ripoti Kamili ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

Ripoti Kamili ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

Informer

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,606
Reaction score
6,672
Screenshot 2019-04-10 at 11.41.40.png

Screenshot 2019-04-10 at 11.10.08.png


Wakuu,

Mnaweza kuipakua ripoti kamili hapa:


Lakini, endapo tovuti itakuwa na shida basi naambatanisha hapa mafaili yote

NB: Ripoti imesainiwa na Prof. Assad

Kwa ufupi...

BUNGENI Ofisi ya CAG imetisha mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma. Inatarajiwa kuwa CAG, Prof. Mussa Assad, atawaeleza waandishi wa habari kuhusu mukhtasari wa kile kilichomo kwenye ripoti yake ya ukaguzi wa mwaka 2017/18.

Miaka iliyopita, CAG alikuwa anatoa mukhtasari huo kwa waandishi wa habari bungeni mara tu baada ya ripoti yake kuwasilishwa kwenye chombo hicho.
Bunge limeshaazimia kutofanya kazi na Prof. Assad, hivyo ni wazi kwamba hawezi kuzungumza na waandishi wa habari bungeni.

=> CAG assad: Tumezoa kufanya mkutano huu mara tu baada ya ripoti hii kuwasilishwa.

=> CAG assad: Mimi nimetazama kwa TV ripoti imewasilishwa bungeni na 'order paper' (karatasi yenye orodha ya shughuli za kikao cha Bunge) ninayo hapa inaonyesha ripoti imekabidhiwa bungeni leo asubuhi na nimetazama ikiwasilishwa.

=> Prof Assad: Mwaka huu tumetoa ripoti yetu kwa CD ili kuepuka gharama nyingi za uchapishaji.

=> Prof Assad: Mapendekezo yetu tuliyotoa katika ripoti iliyopita yalikuwa 350 lakini ni 80 tu yaliyotekelezwa kikamilifu.

=> Prof Assad: Serikali kuu kulikuwa na mapendekezo 91, mawili tu ndiyo yametekelezwa kikamilifu.

=> Prof Assad: Halmashauri za Kigoma Ujiji na Nyng'wale zimepata hati zisizoridhisha na hati mbaya katika mwaka wa fedha 2017/18.

=> CAG Assad: Tumebaini kuwapo kwa malipo hewa ya mabilioni ya shilingi katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

=> Prof Assad: Pia tumebaini Wilaya ya Hanang' haikuwasilisha vitabu vya fedha na kuna upotevu wa mapato ya Sh. bilioni 1.4 na walilipa fedha kwa wakandarasi kwa kazi ya dharura pasipo kuwapo kwa kazi ya dharura.

=> Prof Assad: NEC ilinunua BVR 8,000 lakini mashine 5,000 kati ya hizo zilikuwa haziendani na mfumo uliotakiwa hivyo kuisababisha serikali hasara ya mamilioni ya shilingi.

=> Prof Assad: Kuna mafunzo kwa maofisa wa NEC hayakufanyika licha ya mzabuni kulipwa.

=> Prof Assad: Jeshi la Polisi lililipa Sh. bilioni 16 kwa ajili ya ununuzi wa sare za polisi bila kuwapo kwa ushahidi wa ununuzi.


=> Prof Assad: Jeshi la Polisi lilipa Sh. milioni 600 kwa ajili ya mafunzo ambayo hayakufanyika.

=> CAG Assad: Tumebaini Chadema ilinunua gari jipya aina ya Nisan Patrol kwa Sh milioni 147.5 lakini lililisajiliwa kwa jina la mwanachama badala ya Bodi ya Wadhamini.

=> CAG Assad: Tumebaini CCM haijawasilisha NSSF makato ya Sh. bilioni 3.74 ya wanachama wake.

=> CAG Assad: Majengo ya ofisi za CUF yamesajiliwa kwa majina ya watu badala ya Bodi ya Wadhamini.

=> CAG Assad: Kuna miradi 27 serikali za mitaa imekamilika lakini haitumiki licha ya kugharimu mabilioni ya shilingi.

=> Prof Assad: Tumebaini mashirika 14 yana matatizo makubwa ya kifedha na yanaendelea kutengeneza madeni makubwa.

=> CAG Assad: Tumebaini mradi wa umeme wa REA umetekelezwa kwa asilimia 36 tu ndani ya miaka mitano.

=> CAG Assad: Tunaishukuru Ofisi ya Rais na Ofisi ya Bunge kwa kutusaidia kukamilisha ripoti hii.

=> Prof Assad: Deni la Taifa limeongezeka lakini bado ni himilivu.

=> Prof Assad: Tumewaalika wenyeviti wa kamati za Bunge (PAC na LAAC) lakini hawajaja hapa. Tutawapatia nakala hizi.

=> Prof Assad: Hatujakurupuka kufanya mkutano huu hapa ofisini kwetu. Tulihisi mapema hatutakaribishwa bungeni. Tumeongea nanyi hapa kwetu, hata kama ninyi waandishi wa habari hamtatoa hiki tulichozungumza, sisi tutatoa kwa umma.

=> CAG: Neno 'dhaifu' naendelea kusisitiza ni lugha ya kawaida katika ukaguzi wetu. Na tutaendelea kulitumia.

=> Prof Assad: Kampuni ya Uhuru Publications haina mfumo mzuri wa udhibiti wa fedha.
 

Attachments

"Pia, nilibainisha kwamba kiwango cha malipo ya hitimisho la kazi kwa viongozi wa kisiasa hakijawekwa wazi kwenye sheria. Hii ni kutokana na marekebisho yaliyofanyika kwenye kifungu cha 21 (3) cha Sheria ya Mafao kwa Viongozi wa Kisiasa ya mwaka 1999 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2005) kwa kufuta kiwango kilichokuwa kimebainishwa; na badala yake kuipa nguvu mamlaka husika kutathmini kiwango cha malipo hayo. Hiyo itafanya malipo hayo yaathiriwe na maamuzi ya mamlaka hiyo"; CAG 2017/18 Audit Report; Pg. xxxii

Hii haina tafsiri nyingine zaidi ya "wanajipigia tu". Sisi walalahoi tunatungiwa sheria kedekede na vikokotoo vya terminal benefits ila wao hata hiyo sheria hawana! Hii nchi hii!
 
NB: Ripoti imesaimiwa na Prof. Assad

Kwani huyo si ndo mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali??

Ulitaka asaini Lusinde au Mgogo wa Joho [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
"Viongozi wa Kisiasa"; hawa ndio akina nani ambao CAG anabainisha kwamba hawana sheria inayo-guide terminal benefits (mafao) zao ilhali walalahoi tunatungiwa kila aina ya sheria, kanuni, vikokotoo, n.k. tena kwa jasho letu halali?
 
NB: Ripoti imesaimiwa na Prof. Assad

Kwani huyo si ndo mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali??

Ulitaka asaini Lusinde au Mgogo wa Joho [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu,

Sababu ya kuweka TANBIHI ni kufuatia biti la Ndugai kuwa endapo ripoti hii ingesainiwa na Prof. Assad wasingeipokea/ifanyia kazi.

Am I making myself clear?
 
Kutokana na utaalam wangu, ngoja niichambue then nione jiwe anavyojitapa kuwa yuko sahihi
 
"Serikali kupitia kwa Maafisa Masuuli iimarishe udhibiti na utaratibu wa kufanya mapitio ya uandaaji wa mafao. Hii itahakikisha kuwa waandaaji wa mafao ya kiinua mgongo na pensheni wanafuata kanuni na vigezo vya ukokotoaji na sheria kabla ya kuwasilisha kwa ukaguzi wa awali wa malipo. Aidha, kuepuka kucheleweshwa kwa mafao ya hitimisho la kazi na hasara kwa serikali"

"Serikali kupitia Mamlaka husika wafanyie marekebisho kifungu cha 21(3) cha Sheria ya Mafao ya Hitimisho la Kazi kwa Viongozi wa Kisiasa ya mwaka 1999 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2005) kwa kuainisha kiwango cha malipo ya posho la hitimisho la kazi."

... anashauri CAG; Uk. xxxiii
 
Back
Top Bottom