Profesa mchokozi sana! Kwenye hiyo barua ya uwasilishaji wa ripoti naona "akimkumbusha" Mkuu wa Nchi kwamba "Ripoti hii ya jumla itawasilishwa katika kikao cha Bunge cha mwezi Aprili 2019". Akijua mwenye kuiwasilisha Bungeni ni Rais mwenyewe sijui kwanini katumia neno "itawasilishwa" badala ya "unaombwa kuwasilisha"?
Itawasilishwa imekaa kama order zaidi japo ya kistaarabu flani hivi. Yaani alimaanisha "jogoo awike asiwike" ripoti lazima iende Bungeni ama kwa Rais mwenyewe kuipeleka au "kwa namna nyingine" maana ndivyo isemavyo KATIBA ya Jamhuri ya Watu wa Tanzania! Raha sana! Halafu Ndugai na Bunge lake wanataka kuleta utani!