Ripoti Maalum: Kutajwa kwa Vyombo vya Usalama na Wengine kwenye Madawa ya Kulevya ni Mtego kwa JK

Ripoti Maalum: Kutajwa kwa Vyombo vya Usalama na Wengine kwenye Madawa ya Kulevya ni Mtego kwa JK

Status
Not open for further replies.
Beka Ranger ni jirani yake na JK Huko Msoga pia ni mdogo wake wakili wa kujitegemea aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga,Jamani DAMU nzito kuliko Maji!
Kuna mwenzako humu kasema huyo Beka ndiyo alimchangia JK pesa za kampeni za urais, teh teh teh.
 
Miss Foxy please don't insult our intelligence!

Nchi hii haiongozwi na vatican wala kanisa.Inaongozwa na serikali ya chama cha mapinduzi!

Hii mifano yako inakuwaga ya hovyo sana.Nina wasiwasi kama kweli uko kwenye mfungo,maana una ile kasi ambayo I can almost be certain una kikombe cha ghahawa hapo pembeni na kinakuwa filled up every moment the coffe goes down.

Maana kwa wengine ghahawa ni kilevi kikali kiroba cha mtoto,trust me on this.

Vipi, hujasikia Maaskofu walioshikwa na madawa ya kulevya Tanzania? Nikukumbushe?

Haya jikumbushe hapa;

IMG_0532.jpg

Madawa ya kulevya.​

Aina ya magari yaliyokamatwa.​

IGP Mwema.​
​
Nabii Flora.​
Na Makongoro Oging'
MORIS Charles anayejitambulisha kuwa ni askofu wa kanisa moja la kiroho jijini Dar es Salaam amedakwa na unga hivi karibu katika Kijiji cha Mchingambili, mkoani Lindi.
Vyanzo vya habari vimeeleza kwamba Charles ambaye wakati fulani hujitambulisha kwa jina la Yusuph Mohamed Lutengwe alidakwa nyakati za usiku Januari 11, mwaka huu akiwa katika gari lake aina ya Toyota Land Cruiser (namba zinaifadhiwa ).
Taarifa hizo zimedai kwamba kudakwa kwa mtu huyo kulifuatia habari zilizowafikia polisi mapema ambapo waliarifiwa na aina ya gari analotumia Charles kupokea ‘unga' au dawa za kulevya aina ya Heroine kilo 210 zenye thamani ya shilingi bilioni 9.4.
MTEGO WA POLISI
Imeelezwa kwamba siku ya tukio polisi waliweka mtego baada ya kupata taarifa ya kiongozi huyo kuwa atakuja katika kijiji hicho na gari lake la kifahari, wakapewa namba na raia wema.
Habari zinasema ilipofika saa tano usiku waliliona gari kwa mbali na lilipowakaribia, walilisimamisha lakini inadaiwa kuna mtu alichomoka ndani ya gari hilo na kutokomea gizani.
Vyanzo hivyo vinadai kuwa jeshi la polisi halikumjua mtu huyo lakini baadaye wakaambiwa kuwa aliyekimbia ndiye huyo anayejiita Askofu Charles ambapo mtu mmoja aliyekuwa akiliendesha gari hilo alitiwa mbaroni.
Habari hizo zilieleza kwamba muda huo huo watu aliokuwa akiwapokea wakiwa na madawa walikamatwa na polisi wa kikosi kazi.
Waliokamatwa wametajwa kuwa ni pamoja na Ismail Adamu (28), Hamad Said (27), Morine Amatus (22) na Pendo Mohammed Chausi (67) ambaye ni mwenye nyumba yalipokamatwa madawa hayo. Tayari watu hao wamepandishwa kizimbani.
Habari zinasema polisi walimfuatilia askofu huyo na kugundua kuwa anaishi Mikocheni, jijini Dar es Salaam na wakafanikiwa kukamata mali nyingine ambazo ni magari mawili ya kifahari aina ya Porsche Cayenne na Jeep Wrangler.
Hata hivyo, imeelezwa kuwa askofu huyo amefanikiwa kuwakimbia polisi na ametorokea nje ya nchi Januari 15, mwaka huu.
Vyanzo hivyo vya habari vimedai kwamba kiongozi huyo wa dini huwa ana hati mbili za kusafiria, moja anatumia jina la Kiislam na huitumia anapotembelea nchi za Kiislam na nyingine yenye jina la Kikristo.
Uchunguzi wetu umebaini kuwa hata magari anayotumia, usajili wake una utata kwani tulipofuatilia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) anayedaiwa kumiliki gari hilo Toyota Land Cruiser lililokamatwa na polisi ni Rashida Abushir Jumanne na aliuziwa na huyo kiongozi Januari 16, mwaka huu.
Afisa mmoja wa TRA alisema mmiliki wa kwanza wa gari hilo ni Makame .O. Juma na kumbukumbu zao zinaonyesha kwamba Juni 9, 20011 aliliuza kwa kiongozi huyo anayejulikana pia kwa jina la Lutengwe.

UTATA WA GARI
Kinachoshangaza ni kwamba Lutengwe alikimbia nchini Januari 15, mwaka huu, iweje auze gari kwa Abushiri Januari 16, mwaka huu wakati gari hilo tangu likamatwe Januari 11, mwaka huu bado lipo polisi hadi sasa?
Hata hivyo, mwandishi wa habari hii akiwa TRA alipata namba ya simu ya Abushiri, alipopigiwa alipokea mtu ambaye alijitambulisha kuwa yupo Morogoro na alisema kwamba anamfahamu Abushiri ambaye anaishi Sinza jijini Dar es Salaam .
Kijana aliyepokea simu aliwasiliana na Abushiri alimpa namba ya mwandishi na akapiga simu. Katika mahojiano alikana kwamba yeye hana gari aina ya Toyota Land Cruiser na hajawahi kulimiliki, akadai inawezekana jina lake na namba yake ya simu inatumika vibaya na wahalifu.
Abushiri alipohojiwa zaidi na mwandishi sababu ya simu yake kumkabidhi mtu ambaye yuko Morogoro wakati yeye yupo Dar es Salaam alijitetea kuwa huyo ni mdogo wake, hivyo ameamua kumpa hiyo simu ili aitumie.
Uchunguzi umebaini kwamba hata baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa na madawa ya kulevya, simu zao zimegundulika kuwa waliosajiliwa ni marehemu waliokufa kati ya miaka miwili na mitatu na wengine walikuwa wakiishi Morogoro.
Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini, Godfrey Nzowa alipoulizwa kuhusu kiongozi huyo alisema kwamba hayupo tayari kulizungumzia suala hilo kwa vile bado linachunguzwa.
Hata hivyo, alikiri kwamba kuna mfanyabiashara mkubwa wa madawa ya kulevya aliyekimbilia nje ya chini na kwamba magari yake yanashikiliwa na jeshi la polisi.

VIONGOZI WA MAKANISA
Baadhi ya wachungaji wa makanisa waliozungumza na gazeti hili kufuatia kadhia hii ya dawa za kulevya nchini, wameitaka serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wafanyabiashara hiyo haramu.
John Said wa Kanisa la Victorious la Ubungo External amesema kwamba sasa imefikia muda wa serikali na jamii kwa ujumla kupiga vita biashara hiyo na wanaokamatwa na dawa wachukuliwe hatua kali haraka.
Nabii Flora Peter wa Kanisa la Huduma ya Maombezi lililopo Mbezi Beach, Dar es Salaam amesema kwamba wanaokamatwa na biashara hiyo wachukuliwe hatua mahakamani kwani wanaumiza nguvu kazi ya taifa kutokana na ukweli kwamba vijana wengi wanaangamia na dawa hizo.
Mchungaji Timoth Mwankenja alisema:
"Kunahitajika jitihada za pamoja kati ya raia na polisi ili kupambana na biashara hii haramu. Kanisa letu tumewahi kutoa elimu mitaani, kunahitajika ushirikiano katika vita hii. Kama kuna viongozi wa dini wanajihusisha wachukiliwe hatua kali."
Mchungaji Alponce Mtemela wa Kanisa la Pentekoste lililopo Kawe, amesema kwamba dawa za kulevya ni janga la taifa kwani wanaohusika na biashara hiyo haramu ni matajiri na wanaweza kufanya chochote, hivyo ameiomba serikali kuchukua hatua kali.
Mwanzoni mwa mwaka jana jeshi la polisi kitengo cha dawa za kulevya lilimkamata Askofu wa Kanisa la Lord Choose Chaersimatic Revived, aliyejulikana kwa jina la Chidi Okechuku.
Okechuku alikamatwa maeneo ya Mbezi Beach katika nyumba aliyopanga na alikutwa na kilo 81 za Heroine na kwa sasa kesi yake ipo mahakama kuu.
source: http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/askofu-mwingine-adakwa-na-unga

Mkiambiwa haya mambo ni makubwa na yanataka scientifica approach mnadhani tunatania au tunatetea. Kanisa liko nyumba ya haya mambo kwa hali ya juu sana. Na Kanisa lina nguvu kubwa sana Duniani. Inabidi uende nalo ki utaratibu na si kwa kukurupuka.

Tunajuwa chuki zenu nyingi kwa Kikwete zinazidi mambo kama haya yanapoibuliwa na Serikali yake.

Na Shigongo mtaacha kumchukia naye anawaanika?
 
Ghahawa mchagga ndiyo analima, mimi kijiwe changu kipo Kimara Temboni, ukishuka tu kituoni.

Mchagga analima na kuuza,na wengine pia wanachemsha na kuuza kama wewe.
 
Bado hawa wasanii wetu wanaowika leo halafu kesho wanaanza kuaga wanaenda kupiga shoo nje, kesho kutwa wana pesa ya kufa mtu.
Tutafika tu, taratibu.
Uchafu utaoshwa na pesa zake zitatoweka

Ishu ya Ali Kiba imeishia wapi?
 
FaizaFoxy,hao wachungaji wameitaka serikali iwachukulie hatua.Na aliyekamtwa,anajiita askofu,na pia ana majina yote ya kiislam na kikristo.

Hilo la kutaja maaskofu alikofanya JK na wewe kusema ni makanisa,ni hatua ya kufunika kombe mwanaharamu apite,ili issue isipigiwe kelele,sasa kusema ni makanisa,halafu hao wachungaji wanataka hatua zuchukuliwe,mkuu wa nchi kakalia listi,nani wa kulaumiwa?

Isome hiyo habari uliyoibandika uielewe vyema.
 
Last edited by a moderator:

Hakuna cha kufunika kombe, mambo yanaratibiwa kutoka Vatican na nimekubandikia hapo juu ukajisomee mwenyewe zaidi. Haya mambo si madogo na mnayajuwa hayo. Kama ni wenye kufikiri.
 
Mzee Mwanakijiji,kichwa chako cha habari kinanipa tafakuri ya kina kwa kuunganisha na scenario ya EPA.Kama mna memory nzuri,ni kwamba EPA scandal ilifumuka baada ya wenyewe wenye siri hiyo kutibuana na kambi pinzani ndani ya CCM na serikali yake kuitumia scandal hiyo kulipuana!the same applies to Richmond!naona mazingira yale yale kwenye hili.biashara hii inafanyika siku nyingi duniani kote,lakini ktk miaka ya hivi karibuni watz wamekuwa wakikamatwa sana na taarifa za mwenendo wa biashara hii ndani na nje ya nchi zikifumuka ghafla kwa kiwango kikubwa sana.kwenye EPA na Richmond tunafahamu vigogo waliong'oka au kuchafuka!kwenye hili inaonekana serikali nzima ya awamu ya nne iko hatarini kuchafuka!na hapa tunaelekea 2015,ambapo vita ya makundi ya kisiasa imepamba moto.najaribu kuunganisha dots hapa...mh!naungana nawe mzee,JK awe makini sana na hili na umakini wenyewe ni kuondoa uchafu ndani ya nyumba ili watu wakose wa kumnyooshea kidole ndani ya serikali yake!hata hivyo,kama mwananchi,nalaani tabia hii ya watu muhimu serikalini kujihusisha na biashara chafu.ni hatari kwa majeshi yetu kutumika katika dili hizo.nakumbuka nikiwa Morogoro kusikia kesi ya lori ya jeshi kubeba hard woods toka sehemu zenye misitu ya asili ambazo zilipigwa marufuku kuvunwa na askari hao kuwa na mtandao wa raia wanaowatumia kutafuta masoko na kufikisha mzigo kunakotakiwa.na hii huenda inafanyika huku jeshi lenyewe likiwa halina taarifa ya uwepo wa vitendo kama hivi kwa askari wake!these are serious allegations na zinatakiwa kufanyiwa kazi.mnasema tusipoangalia nchi itaongozwa na MAFIA,mie nasema tujichunguze,huenda tayari kenge washaingilia msafara bila mamba kujua!
 
Mi nafikiri viongoz wetu watusaidie pia kwa hili japo baadhi wanawatia doa ,ila wasikate tamaa Makanisani na Misikitini viongozi wetu walikemee kupitia mafundisho ya vitabu vinavyotuongoza ,kutapunguza angalau.
 
Hakuna cha kufunika kombe, mambo yanaratibiwa kutoka Vatican na nimekubandikia hapo juu ukajisomee mwenyewe zaidi. Haya mambo si madogo na mnayajuwa hayo. Kama ni wenye kufikiri.

Heroin ya Afghanistan na Pakistan huwa inapitishiwa na kuratibiwa na vatican?acha ufyatu.
 
Kuna mwenzako humu kasema huyo Beka ndiyo alimchangia JK pesa za kampeni za urais, teh teh teh.

Kwani hujui madawa ya kulevya ndiyo yanaendesha serikali ya CCM?Teeh teh teeeehhh Hata Mwenyekiti wa vikao vya bunge yumo ktk orodha ndefu na hakika hata wewe Ritz nawe umo.
 
Mzee Mwanakijiji,kichwa chako cha habari kinanipa tafakuri ya kina kwa kuunganisha na scenario ya EPA.Kama mna memory nzuri,ni kwamba EPA scandal ilifumuka baada ya wenyewe wenye siri hiyo kutibuana na kambi pinzani ndani ya CCM na serikali yake kuitumia scandal hiyo kulipuana!the same applies to Richmond!naona mazingira yale yale kwenye hili.biashara hii inafanyika siku nyingi duniani kote,lakini ktk miaka ya hivi karibuni watz wamekuwa wakikamatwa sana na taarifa za mwenendo wa biashara hii ndani na nje ya nchi zikifumuka ghafla kwa kiwango kikubwa sana.kwenye EPA na Richmond tunafahamu vigogo waliong'oka au kuchafuka!kwenye hili inaonekana serikali nzima ya awamu ya nne iko hatarini kuchafuka!na hapa tunaelekea 2015,ambapo vita ya makundi ya kisiasa imepamba moto.najaribu kuunganisha dots hapa...mh!naungana nawe mzee,JK awe makini sana na hili na umakini wenyewe ni kuondoa uchafu ndani ya nyumba ili watu wakose wa kumnyooshea kidole ndani ya serikali yake!hata hivyo,kama mwananchi,nalaani tabia hii ya watu muhimu serikalini kujihusisha na biashara chafu.ni hatari kwa majeshi yetu kutumika katika dili hizo.nakumbuka nikiwa Morogoro kusikia kesi ya lori ya jeshi kubeba hard woods toka sehemu zenye misitu ya asili ambazo zilipigwa marufuku kuvunwa na askari hao kuwa na mtandao wa raia wanaowatumia kutafuta masoko na kufikisha mzigo kunakotakiwa.na hii huenda inafanyika huku jeshi lenyewe likiwa halina taarifa ya uwepo wa vitendo kama hivi kwa askari wake!these are serious allegations na zinatakiwa kufanyiwa kazi.mnasema tusipoangalia nchi itaongozwa na MAFIA,mie nasema tujichunguze,huenda tayari kenge washaingilia msafara bila mamba kujua!

Kwanza JK awakamate wale wote aliosema ana orodha yao,vinginevyo usemi wa nani wa kumfunga Paka Kengele utakuwa unatimia.:embarrassed1:
 
FaizaFoxy,hao wachungaji wameitaka serikali iwachukulie hatua.Na aliyekamtwa,anajiita askofu,na pia ana majina yote ya kiislam na kikristo.

Hilo la kutaja maaskofu alikofanya JK na wewe kusema ni makanisa,ni hatua ya kufunika kombe mwanaharamu apite,ili issue isipigiwe kelele,sasa kusema ni makanisa,halafu hao wachungaji wanataka hatua zuchukuliwe,mkuu wa nchi kakalia listi,nani wa kulaumiwa?

Isome hiyo habari uliyoibandika uielewe vyema.

Jina pekee halimaanishi huyo ni mtu ni dini ipi. Hiyo point yako ni craaaap.
 
Nzee kama mimi nimepotea wewe ndio uko kichakani kabisa hebu niambie unaanzia wapi kama si kwa mlaji huyo ndiye anajua katoa kwa nani na huyo nani ataonyesha nani wake hadi tumpate yule papa. Unaposema victim sijui unamaanisha wanabugizwa kinguvu na bure au wananunua kwa hiari; kujinyonga ni kosa na kubugia dawa ni kosa na wanafungwa au tubadilishe na sheria kubugia isiwe kosa ili nawewe ukibugizwa uponee
Kuanzia kwao kama njia ya kukufikisha kwa hao mapapa ni sawa na wala sikatai, ninachopinga ni kuwa kwa sababu ni mtuamiaji naye auawe!Je hii si sawa na kusema mlevi yeyote anyongwe? Ninasema ni victim kwa sababu ukifuatilia utagundua kuwa wengi wao wanaingizwa bila utashi wao na bila kujua wnajikuta wamekuwa addicted. I hope katika ujana wako wewe hujawahi kuvuta sigara au kunywa pombe - utakuwa mmoja wa watu wachache sana...
 
Jina pekee halimaanishi huyo ni mtu ni dini ipi. Hiyo point yako ni craaaap.

We kweli fyatu,Wewe si ndiyo ulidai hao ni maaskofu nikakupa ukweli kuhusu majina mawili aliyonayo ya kiislam na kikristo?huyo anayejiita askofu na pia jina la kiislam anakupa wewe mamlaka gani ya kumuita kuwa ni askofu wa kanisa?

Baba yako na mama yako walikuwa na undugu wowote kabla ya kukuzaa?
 
Na kanisa ni la KiIslaam, mbona husemi hilo?
 
Heroin ya Afghanistan na Pakistan huwa inapitishiwa na kuratibiwa na vatican?acha ufyatu.

kaka hayo ya vatican..usiyapuuze !humu ndani watu wanajitahidi ku-edit mambo ili kupunguza ukali kwa sababu za kisheria,lakini tukisema tufunguke kila mtu aseme kwa uwazi anayoyajua duniani,kuna watu wakifunguka hapa hapatakalika na Jf itafungwa ndani ya masaa 24!hata hizi ID zinaficha meengi kweli mkuu!tuendelee hivi hivi mdogo mdogo kuokoa dental formula zetu zisibadilishwe!usitake kuletea watu matatizo kwa kutaka kujua mengi,we utabaki unabonya vitufe hapo chumbani kwako,huku mwenzio anafanyiwa acupancture ya ulimi na fizi getini kwake!aka!hebu nijiondokee humu!naona mdomo unaniwasha kulipuka..aargh,we mdomo kaa kimya!
 
Na kanisa ni la KiIslaam, mbona husemi hilo?
Anayejiita askofu ana kanisa?hivi unajuwa kwanini aliamuwa kutumia jina la kiislam katika mizunguko yake ya madawa?

Ngoma Pakistani...
 
kaka hayo ya vatican..usiyapuuze !humu ndani watu wanajitahidi ku-edit mambo ili kupunguza ukali kwa sababu za kisheria,lakini tukisema tufunguke kila mtu aseme kwa uwazi anayoyajua duniani,kuna watu wakifunguka hapa hapatakalika na Jf itafungwa ndani ya masaa 24!hata hizi ID zinaficha meengi kweli mkuu!tuendelee hivi hivi mdogo mdogo kuokoa dental formula zetu zisibadilishwe!usitake kuletea watu matatizo kwa kutaka kujua mengi,we utabaki unabonya vitufe hapo chumbani kwako,huku mwenzio anafanyiwa acupancture ya ulimi na fizi getini kwake!aka!hebu nijiondokee humu!naona mdomo unaniwasha kulipuka..aargh,we mdomo kaa kimya!
Ni kweli vatican ilianzia mafioso,hilo linajulikana.Issue hapa ni Tanzania na madawa ya kulevya yanayosambazwa na druglords ambao wengine ni viongozi wa chama tawala na serikali yake.
 
Namsubiri sana Mh.Idd Azzan(mb) jimbo la kinondoni kupitia CCM aitishe press conference tumsikilize na tupime hoja zake,nina iman ni mtu makini atajibu hizi allegations
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom