Ni kama yana DINI vile ukiangalia wanaotajwa sana na NCHI wanakokamatiwa kwa wingi.Madawa ya kulevya hayana chama wala itikadi za kisiasa, wavuta na wauza unga wapo kotekote.
Any way, kama ni kutajwa kwa uhalifu wowote ule nchi hii, huwa tunaishia hapo tu, kutajana, basi. Ntatoa mifano michache:
-Dr Slaa na ile "list of shame" pale MwembeYanga. Waliotajwa ni wazito kabisa nchi hii. Hawashtakiki;
-Lowasa na wengine waliotajwa Richmond. Ndio kwanza wanajiandaa kukamata DOLA come 2015, God willing or not;
-Wameuwawa watu hapa Tanzania hadharani, tena kwenye mikutano. Wametajwa watu hapa na pale. Wengine wamepandishwa vyeo, wengine wamevishwa nishani za UTUMISHI ULIOTUKUKA!
Hii ndio TANZANIA baada ya Mwalimu.