Ripoti madai ya sumu Mto Mara zina utata, zimetofautiana, wataalam wamezichambua

Tukiachana na hayo uliyo mention je kwanini ripoti zitofautiane?

Kuna mmoja katiyao ametudanganya? Kwanini atudanganye? Nani yuko nyuma ya huo uongo?
Umesomea nini ndugu yangu? Kama umesomea arts, siyo kosa lako.

Ile taarifa ya kwanza ilikuwa ni observation. Hii ya pili ni taarifa inayotokana na uchunguzi.

Na unapoanza uchunguzi, ni lazima uwe na hypothesis. Yawezekana kabisa hypothesis ilikuwa ni kuwa utando wa mafuta uliokuwa ukionekana juu, ukasema ni kemikali. Lakini baadaye uchunguzi ukaikataa hypothesis yako.

Jibu la uchunguzi ni uchunguzi wenyewe, siyo hypothesis au observation.
 
Ukweli ni kwamba hizo sumu zinatiririshwa kutoka mgodini, kwa maana nyingine hatua za kisheria zinapaswa kuchukuliwa...

NEMC wanatuabisha sana...
Wewe unajua mto uliko na mgodi uliko? Kuna siku ng'ombe watakufa Dodoma, watu watasema ni kwa sababu ya sumu za mgodi wa Barrick Buzwagi!!

Ujinga ni mzigo mzito kuliko mizigo yote, japo ujinga hauvunji mgongo.

Wanaotaka uchunguzi ufanyike tena wajiorodheshe, ikionekana ni wengi, iletwe timu ya wataalam hata kutoka nje, ufanye uchunguzi, lakini najua wanaotaka isemwe kuwa ni sumu za mgodini, jibu lisipokuwa hivyo, watasema Barrick wamehonga.

Tunaofanya na multinational companies, tunajua jinsi ilivyo ngumu kwa makampuni hayo kukupa hela ya hongo.

Ni rahisi sana kampuni inayomilikiwa na mtu mmoja au watu wachache kuliko hizo public companies.
 
Mkuu samahani, naomba nikuulize kidogo, vipi unafahamu zaidi kuhusu "Chemical speciation"
 
Aisee....hii ripoti ya huu utafiti imezua maswali mengi zaidi, wakati ilitakiwa itoe majibu.

Inabidii hii ripoti ipingwe kwa utafiti sio maneno tu.
 
Kama kawaida yenu kukimbilia elimu ambayo haikidhi hata mahitaji.

Taarifa ya mwanzo ilisema matokeo ya kimaabara yamebaini kuna kiwango kikubwa cha mafuta. ( we uliyesoma sayansi mtu akisema matokeo ya kimaabara nadhani unamuelewa vizuri)

Taarifa ya pili haijazungumzia hata kidogo uwepo wa mafuta kwenye maji.

"Chanzo cha samaki kufa mto Mara chatajwa | Mwananchi" Chanzo cha samaki kufa mto Mara chatajwa | Mwananchi
 
Kwa maoni ya wengi yalivyo na angepatikana kiongozi wa kupenda kukurupuka, sijui saa hii tungekuwa tunazungumza lugha moja?
 
Mungu njoo itawale Africa
 
Maprofessor tunazidi kukosa heshima mbele ya jamii sababu ya michongo.
 
Professor wa mchongo
Sisi seer au mystic huwez kutundaanya hata kama hatuna taaluma hiyo. Kwa hisia za ndani huyo prof.. niliona uwongo hasa kwa namna alivyokuwa anaeleza .
 
Mto Mara ni mto mkubwa kuliko mingi iliyopo hapa nchini.

Mara River - Wikipedia

Mto upi hapa nchini wasiokunywa na kujisaidia humo mifugo?

Kwamba yaliyotokea mto Mara madhara ya mifugo kujisaidia mle?

Inatupa taabu sisi kama wananchi kulielewa hili na hasa kumbukumbu zikituelekeza kuliko na kadhia tata kama hizi huko siku za nyuma:


Ni vyema serikali ikatoa ufafanuzi wa kina kuhusiana na ripoti hii ikiwamo kufanyika kwa uchunguzi huru.
 
Ikumbukwe,
Ni professor uyu uyu akiwa mkemia mkuu wa serikali aliempima LISSU mkojo kwenye ile kesi yake ya uchochezi.[emoji4]
 
Kiujumla ametumia formula zilezile zilizeta matokeo ya papai kuwa na COVID. Waambie wavivu waandike ripoti utaonyeshwa Hadi chanzo Cha sumu.
 
Kwani Profesa Msukuma anasemaje? Mtazamo wake kwenye hili kwenye enzi hizi za utandawazi, utaalamu na teknologia ni upi?😳😲
 
Kiujumla ametumia formula zilezile zilizeta matokeo ya papai kuwa na COVID. Waambie wavivu waandike ripoti utaonyeshwa Hadi chanzo Cha sumu.

Hii nchi ngumu sana. Wenyewe wakijivunia - the end to justify the means.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…