Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Jana kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalenda ndugu Zitto Zubeir Kabwe ameitisha mkutano wa waandishi wa habari na kuelezea mambo mazito ya ukiukwaji wa haki za binadamu wa kutisha uliofanywa na vyombo vya usalama huko Zanzibar.
Akieleza waandishi wa habari yaliyojiri, Ndugu Zitto alitoa takwimu za watu waliouawa kwa kupigwa risasi, kubakwa, kuteswa, na kufanyiwa kila aina ya ukatili.
Wakati huohuo, Ndugu Zitto ameeleza kuwa ameandika barua kwa jumuia za Kimataifa ikiwemo jumuia ya Madola, EAC, AU na ICC na kuambatanisha ushahidi juu ya matukio ya kinyama kanbisa yaiyojiri katika uchaguzi huo
Pia ndugu Zitto amesema Katibu wao mkuu wa Zanzibar ndugu Mazrui hajulikani alipowekwa na vyombo vya usalama, hajulikani kama yuko hai au la, akasema kuwa ndugu Mazrui kabla hata ya kukamatwa na polisi alikuwa anatumia dawa kutokana na kuwa aifanyiwa operesheni siku chache nyuma na kwa hiyo tangu akamatwe zaidi ya wiki sasa hana hizo dawa
Wakati huo, Chama cha ACT-Wazalendo kimetoa ripoti ya awali ya taarifa ya ukandamizaji wa kutisha, utesaji na ukatili waliofanyiwa watu wa Zanzibar
Ripoti hiyo imesambazwa mitandaoni na iko wazi kwa kila mtu kujionea.
MY TAKE
Vitendo hivi vya kutesa na kuumiza watu bila hatia havitapita hivihivi, wote waliohusika watakuja kulipia ushenzi na ukatili waioufanya kwa wananchi.
Ni aibu kubwa sana kwa vyombo vya usalama kutesa na kuumiza wananchi wanaotumia haki yao ya msingi ya kikatiba kufanya siasa au kutaka kumchagua wanayemtaka.
Vyombo vya usalama viwaambie wananchi wa Tanzania, hawa wananchi waliouawa kwa risasi huko Zanzibar wana kosa gani waliloifanya la kustahiki kupigwa risasi na kupotezewa maisha yao?
Tunaunga mkono jumuia ya Kimataifa kuchunguza mauaji haya ya Watanzania wasio na hatia ili sheria ichukue mkondo wake kwa waliohusika!