ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Mzabuni wa bei nafuu alitenda Dola 263 Wakamchukua wa Dola 478.
Kwa Hali hii Masanja anapendwa kuwa Ofisini Kwa Ajili ya nini?
Hawa wezi wasiishie kufutwa kazi tuu Bali wafikishwe Mahakama, TAKUKURU mnafanya nini?
---
SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) linakabiliwa na changamoto katika utekelezaji wa ujenzi wa reli ya kisasa - SGR ambazo zinajumuisha gharama kubwa, upotevu wa fedha na majadiliano ya mikataba yasiyolinda maslahi ya taifa na hivyo kuathiri ufanisi na utelekezaji wa mradi huo.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amesema TRC ilikataa zabuni mara mbili kwa ajili ya manunuzi ya vichwa vya treni na umeme, makochi ya abiria ambapo mzabuni aliyekuwa na bei ya chini alikuwa na dola za marekani milioni 263.4 na kufanya manunuzi yasiyo na ushindani kwa dola za marekani milioni 478.5.
Maamuzi haya yalisababisha ongezeko la dola za marekani milioni 215.4 sawa na ongezeko la asilimia 82. Hili ongezeko halikuwa la lazima.