Ripoti ya CAG 2021-2022: TRC ilimkataa mzabuni wa Tsh bilion 616.4 na kumpa mzabuni wa tsh trilion 1.119 bila sababu za msingi

Ripoti ya CAG 2021-2022: TRC ilimkataa mzabuni wa Tsh bilion 616.4 na kumpa mzabuni wa tsh trilion 1.119 bila sababu za msingi

Tungetegemea sasa kuona wanasiasa wanaitisha maandamano kesho kushinikiza wezi wa mali za umma wachukuliwe hatua kali ikiwemo wale waliotajwa kwenye report ya CAG.

Tulitegemea kesho watu waingie barabarani kushinikiza mawaziri wenye hizo wizara wote wajiuzuru nafasi zao na kuchunguzwa dhidi ya tuhumu za ubadhirifu.
Nasemaje Pumbavu haiwezekani..
 
Hata ukienda huko Kwa Machadema nako yamepeana hivyo hivyo Sasa hapa sio kutegemea Wanasiasa ni watu wenyewe kuliamsha ndio mabadiliko yatakuja.
Hao pia wezi wakitaka waunde serikali ya mseto wizara moja unachanganya watu Wana itikadi tofauti hata wageni ili wasiwe wanazoeana .
 
Kama mgeni akaingia leo hii bongoland halafu akasikia sifa kedekede kwenye vyombo vya habari kuhusu uongozi atajua tuko kwenye nchi ya ahadi, lakini akiingia field ndo atajua kumbe tuko kwenye dunia yetu ya mwisho tena ya wajingaaa na wapumbavuu.
 
Yote hii ni mikakati yao tu wasituzuge
Hela wanaiba wao halafu wanantuma CAG aongee tu
Wamewafanya mazuzu tu na majitu ya kuburuzwa kwa lolote wanalosema

Haiwezekani miaka yote ripoti chafu ila hakuna wa kufungwa
Sisi wote wapumbavu bali kuna mengi wanaficha hata kama wanakusanya kuendelea kushika dola

Hatuna shida ya report waendelee kuiba tu
 
Mshaambiwa urefu wa kamba ndiyo kigezo.
 
Mzabuni wa bei nafuu alitenda Dola 263 Wakamchukua wa Dola 478.



Kwa Hali hii Masanja anapendwa kuwa Ofisini Kwa Ajili ya nini?

Hawa wezi wasiishie kufutwa kazi tuu Bali wafikishwe Mahakama, TAKUKURU mnafanya nini?

---
SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) linakabiliwa na changamoto katika utekelezaji wa ujenzi wa reli ya kisasa - SGR ambazo zinajumuisha gharama kubwa, upotevu wa fedha na majadiliano ya mikataba yasiyolinda maslahi ya taifa na hivyo kuathiri ufanisi na utelekezaji wa mradi huo.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amesema TRC ilikataa zabuni mara mbili kwa ajili ya manunuzi ya vichwa vya treni na umeme, makochi ya abiria ambapo mzabuni aliyekuwa na bei ya chini alikuwa na dola za marekani milioni 263.4 na kufanya manunuzi yasiyo na ushindani kwa dola za marekani milioni 478.5.

Maamuzi haya yalisababisha ongezeko la dola za marekani milioni 215.4 sawa na ongezeko la asilimia 82. Hili ongezeko halikuwa la lazima.

Hela zinapigwa!
 
Trying to imagine.......Ni UPEPO, utapita tuu !!!!
 
Ripoti hio hapo
 

Attachments

  • FB_IMG_1743087413092.jpg
    FB_IMG_1743087413092.jpg
    77.9 KB · Views: 16
Hawa watu bado wako ofisini na kazi inaendelea. Kazi tunayo.
I am so shocked that hakuna hatua itachukuliwa, uzembe wote huu unalelewa.

Huku nilipo the moment report imetoka, jion unakutana na mail ya kujieleza and if wakikuya huna appropiate reason unakuwa fired

Is how wameweza kuwa efficiency miaka yote
 
Katiba ijayo lazma tuweke kipengele cha Raisi kutowalinda wezi. Kama akishindwa kumchukulia hatua mtuhumiwa yeyote yule ama kumuwajibisha aliyefanya ufisadi basi nae atoke hatufai. Hatuitaji tume wala ushuzi ni fasta mtu akasomewe mashitaka kesi iishe. Hatuwezi kuendelea kulipa kodi halafu zinapokusanywa zinaenda kuchezewa na wahuni wachache walio kwenye mamlaka za serikali.

Mahakama zipo, wasimamia haki wapo na wakamataji wapo. Tatizo ni lipi Raisi ashindwe kusema flani out. Hii ndio adha ya kuweka madarakani kwa ushkaji.
Na kinga ya viongoz iondolewe. Inawapa kiburi cha ku commit madudu maana wanajua hawata guswa
 
Back
Top Bottom