Ripoti ya CAG 2021-2022: TRC ilimkataa mzabuni wa Tsh bilion 616.4 na kumpa mzabuni wa tsh trilion 1.119 bila sababu za msingi

Ripoti ya CAG 2021-2022: TRC ilimkataa mzabuni wa Tsh bilion 616.4 na kumpa mzabuni wa tsh trilion 1.119 bila sababu za msingi

CAG: TRC ilimkataa mzabuni wa tsh bilion 616.4 na kumpa mzabuni wa tsh trilion 1.119 bila sababu za msingi​


Haya madudu haya alafu watu wamechukua chubuu maana wanajua hakuna watakachofanywa yataishia mdomoni tu alafu imetoka hio pesa wanazila, sitaki kutukana ila pumbavu stupid haiwezekani
 
Hii taarifa kubwa kabisa na ya kusikitisha iliyotolewa na CAG leo tarehe 29.03.2023 mbele ya Raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania DR.Samia suluhu hassani...
Moja ya mambo yaliyokera ni hili la TRC.

Hawa Jamaa ukiacha hasara pia walipovunja mkataba na wanunuzi wa Mabehewa Hawajadai Bil.12 ambazo Serikali ilipaswa kupata ila wamemalizana kinyemela.

Masanja kadogosa akamatwe haraka sana.
 
Hata hilo likivuko lililopelekwa Mombasa kwa madai Songoro Marines alihitaji dau kubwa litatokea kwenye reports zijazo za CAG.

Gharama zitakuwa mara mbili ya alizotaka Songoro na halitatengemaa kwa muda uliopo kwenye mkataba.

Stay tuned.
 
Mimi ningekuwa Rais, ningewapa TAKUKURU na Ofisi ya Mpelelezi wa Makosa ya Jinai hizi Ripoti za CAG halafu niwaambie huu ndio muda wenu wa kulisaidia taifa. Fanyeni kazi.

Baada ya hapo ningewaagiza wasaidizi wangu wasiruhusu mtu yoyote kuonana na mimi.

Hii nchi bila kufunga macho kidogo na kupunguza kujuana, itaendelea kunuka. Tunatoza makodi kila kona halafu watu wachache wanaiba kama hawana akili nzuri.
 
Je mamlaka ya uteuzi haiwezi kuzuia baadhi ya uchafu tunaouona? Jadili kulingana na siasa za TZ.
Itazuiaje wakati michakato yote hufanywa na taasisi husika na wao ndio Wataalamu?

Ni mpaka hizi taasisi za checks and balance zije zifanye Uchunguzi.

Pia TAKUKURU na ppra ndio zinafeli sana plus watu wa intelligence na kama ujuavho hapa Tanzania watu hufanya upigaji Kwa kisingizio Cha maagizo kutoka Juu.
 
Tunategemea baada ya ziara ya Kamala ,haya majizi kina Kadogosa yafukuzwe kazi mara Moja.
 
Katiba ijayo lazma tuweke kipengele cha Raisi kutowalinda wezi. Kama akishindwa kumchukulia hatua mtuhumiwa yeyote yule ama kumuwajibisha aliyefanya ufisadi basi nae atoke hatufai. Hatuitaji tume wala ushuzi ni fasta mtu akasomewe mashitaka kesi iishe. Hatuwezi kuendelea kulipa kodi halafu zinapokusanywa zinaenda kuchezewa na wahuni wachache walio kwenye mamlaka za serikali.

Mahakama zipo, wasimamia haki wapo na wakamataji wapo. Tatizo ni lipi Raisi ashindwe kusema flani out. Hii ndio adha ya kuweka madarakani kwa ushkaji.
 
Katiba ijayo lazma tuweke kipengele cha Raisi kutowalinda wezi. Kama akishindwa kumchukulia hatua mtuhumiwa yeyote yule ama kumuwajibisha basi nae atoke hatufai.

Mahakama zipo, wasimamia haki wapo na wakamataji wapo.
Hata ya Sasa Haina hicho kipengele shida ni kwamba utekelezaji wa Katiba hasa kuchukua maamuzi inategemea utashi wa Rais
 
Back
Top Bottom