Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Kila siku CAG anakuja na report kuhusu upotevu wa mabilioni kwenye secta ya umma lakini hakuna hatua zinazochukuliwa. Wakati CAG akija na hoja hizo mara nyingi PCCB hakuna sehemu anakuja na hoja zakuthibitisha huo wizi badala yake kesi nyingi uisha Kwa matumizi mabaya ya Ofisi.
Mtizamo wangu NI kwamba; CAG ripoti zake zinajikita zaidi kwenye sheria na endapo sheria ilikiukwa basi kiasi kilichohusika ndicho utumika kama wizi Jambo ambalo ni kosa.
Mfano; CAG anasema kuna changamoto ya taasisi inayosimamia manunuzi, Mhe. Rais anasema iangaliwe kama ina umuhimu kuwepo. Lakini tatizo kumbe siyo taasisi tatizo ni sheria ya manunuzi ambayo imejaa urasimu. Katika mazingira haya hasara inayotokana na urasimu WA kisheria tunaweza kusema NI wizi?Nani aliyeibiwa? Watendaji wakiuke sheria? Wakikiuka nayo haitaleta hoja ya ukaguzi?
Shirika la ndege linatangazwa kupata hasara, najiuliza ni lini lilimaliza kulipa madeni Hadi lianze kuhesabiwa linapata hasara? Return on investment imefanyika? Business plan ya shirika IPO? Kwanini CAG asituambie NI lini shrika kama ATCL lilianza kupata faida?
Shirika la TTCL linapolaumiwa kufanya vibaya tunaona tunatenda Haki? Kama TTCL pesa zake zote biashara wanazokusanya zinakwenda hazina nakupangiwa KAZI nyingine unategemea lipate faida? Lini shirika litaacha kuendesha Kwa hisani ya wizara ya fedha? Kila activity lazima wakaombe fedha hazina, hata ukimweka malkia lazima litafeli tu! Nilitegemea CAG hatupe mapungufu ya wizara ya fedha katika kutoa fedha lakini sijamsikia. Tusubirie kwenye bajeti tuone kitakachotokea.
Lakini pia TTCL itapataje faida wakati Airtel wapo ndani? Lini tumesikia Airtel wakipata hasara? Means watendaji awana makosa Bali wamiliki wa makampuni ya simu ambao NI viongozi WA chama ndiyo wanahujumu TTCL nakulifanya life wao waendelee kuneemeka. Lazima tukubali kuwa na shrika la mawasiliano lililo imari kama ilivyokuwa vision ya Magu. Tusipokubali kuwa na taasisi na mashirika ya serikali imara hakuna uchumi imara.
Nenda nchi za ulimwengu wa kwanza zote, serikali ndiyo yenye giant companies siyo watu.....Sisi tunatengeneza watu giant mwisho watakuja kutuamulia tulale muda gani na tuamke muda gani.
Tuachane na riport za mis- compliance tuje na riport zakuonyesha wizi na kuthibitisha huo wizi with evidences
Vinginevyo kila mwaka tutakuwa tunazalisha hoja zisizojibika Kwa kuacha professionalism kwenye auditing na kuweka siasa kuwafurahisha wanannchi