Ripoti ya CAG, kuna uwezekano Watanzania ni wajinga kushadadia kutibu matokeo badala ya kushughulika na chanzo?


Haina tija kabisa. Wizi ni wizi tu. Uwe wa mwaka jana, juzi au miaka 20 iliyopita. na wezi wanaoiba wengine wako kwa miaka yote.

Mikakati ya chui kuficha mabaka yake ni kama hii ya kusema ni ya 2020, sijui 2016 sijui nini...hopeless kabisa.

Nani ameshawajibika? Na aliye uplift invoice ya mwaka huu je? Naye ni wa mwaka gani? Tuache kucheza kiduku tukifikiria tuna akili sana...ni ngoma kama mahepe aliyocheza Marijani Rajab
 
Unatetea wezi na wewe ni mwizi.
 
Huyo bogus ana interest zake.
 
Paskali, ujumbe kwenye "video clip" ifuatayo yahusu hoja zako
Hayo ndiyo madhara ya watu kuingia madarakani kwa kunajisi box la kura. Katika mazingira hayo huwezi kukuta taasisi yoyote ikiwajibika ipasavyo, kwani kuanzia rais hadi viongozi wa chini yake ni tunda la wizi wa uchaguzi.
Paskali, "video clip" ifuatayo yahusu hoja zako
Your browser is not able to display this video.
 
Mwandishi wa hii habari bwana! Dah, that’s what audit is all about allover the World, watu wanafanya kazi yao as auditors then wana present their findings to the respective areas for action to be taken, and the have been doing that over and over again. The problem here is the system itself. No seriousness at all, same system and same people and you expect different results… that’s idiocy as you call it previously.
 

Hapana, ukaguzi unapofanyika na matatizo yakawa mengi, basi mkaguzi lazima aoneshe yote. Hii principle ya kusema mkaguzi aoneshe madhaifu machache ya msingi sio wa kweli kabisa. Inatakiwa auditor adhibitishe kasoro zote za kikaguzi ili yasijirudie tena.
 

Sikubaliani na wewe. Wizi hauna ukomo. Hata kama uliiba miaka mia iliyopita bado liability ipo. Tulianza kusema kama mtu aliiba mwaka juzi asisemwe basi tutatoa mwanya kwa mafisadi.
 
Wewe nawe ndo wale aliowataja Pascal kwamba ni stupid Kama ripoti ni ya 2021 na 2022 iweje CAG aweke vitu vya 2020? Huoni kwamba vimewekwa kutupoteza.Na vile walivyofanya vya sasa? Waachiwe waendelee? CAG anaichunguza serikali, nayo ijibu hoja. Siyo kusema eti serikali ya awamu hii haihusiki! Mbona madeni tunalipa tangu awamu ya 3?
 
Naunga mkono hoja!
 
Kile kibayari wanachokimbiza nchi nzima Sina imani nacho.
Kwa suala la kafara namuumga mkono Mwenyekiti wa Waganga Kanda ya Pwani Comrade MshanaJR
 
Kutokana na maelezo yako yote mimi binafsi nakuunga mkono lkn tatizo ni pale chanzo kinapotaka kutibiwa ninyi wasomi hukimbia na kukaa pembeni mnawaachi wajinga wapambane wakishindwa mnasema waroho wa madaraka sasa kama wewe ni mkweli na una uchungu kuwa mstari wa mbele kudai KATIBA ndio chanzo kikuu cha ufisadi hapo ndipo tulipojikwaa vinginevyo unatuonea bure kwa kututukana
 
Ulikua wapi kuyasema haya mwanzo? La pili wew ni mtafta fursa yani mchumia tumbo huna lolote na makala zako
 
Unaposema Ripoti ya CAG ya mwaka Jana Si mbaya kuliko Ripoti za CAG zilizopita unamaana Gani?
 
Chanzo cha upigaji na wizi ni CCM.
Huo ndio ukweli wenyewe. Tatizo kubwa la nchi hii ni CCM na viongozi wake wakihanikizwa na idadi kubwa ya wajinga, wanafiki, washenzi na machawa wao.

Never underestimate the power of stupid people in large numbers.

Itakuwa vyema basi kwanza mleta mada ajipambanue aliposimama miongoni mwa makundi hayo ndipo mjadala uweze kuendelea OBJECTIVELY. Awe honest.

Bila kufanya hivyo, mjadala utaishia kuwa zoezi la kuzunguka mbuyu au mbwa kufukuza mkia wake! Atakuwa na lengo la kutucheza shere kwa manufaa ya chama chake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…