Ulimuonya kama nani!acha ujuaji we popoma
Mtanzania yeyote, kwa mujibu wa katiba yetu hii mbovu ya 1977 na marekebisho yake, ana uhuru wa kutoa maoni, maonyo, mapendekezo au tahadhari kwa kiongozi au taasisi yoyote ya umma, kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali. Slaa alikuwa kiongozi wa CHADEMA, Hivyo mpaka wakati anajiuzulu, wanachama na watanzania wengine walikuwa na haki ya kutoa maoni yao: kumsifu, kumpongeza, kumkosoa, kumuonya, nk. CHADEMA ni taasisi ya umma inayopokea ruzuku ya serikali, ambayo. Ni fedha ya walipa kodi.
Slaa naye kwa upande wake ana uhuru wa kutoa maoni, maonyo na hata kukosoa lolote, hata huko alikohama, CHADEMA. Na amefanya hivyo mara nyingi sana. Mara baada ya kujitoa CHADEMA, akisaidiwa na CCM, Slaa alitoa hotuba kali ya kuushambulia CHADEMA, hotuba iliyotangazwa Mubashara na Chaneli 5 za televisheni, bila shaka kwa gharama na udhamini wa CCM, lengo likiwa kuisambaratisha CHADEMA, Na katika hilo alishindwa vibaya. Slaa ameendelea kutoa maoni yake kuhusu upinzani kwa ujumla, na CHADEMA pia, maoni ambayo daima ni kukejeli na kukosoa, ikiwa ni kulipa fadhila kwa mabosi wake wapya.
Kwa hiyo acha woga usio na sababu, acha ujinga. Elimika.