Ripoti ya IMF (2025): Tanzania Miongoni Mwa Nchi 10 za Afrika Zenye Deni Kubwa la IMF

Ripoti ya IMF (2025): Tanzania Miongoni Mwa Nchi 10 za Afrika Zenye Deni Kubwa la IMF

Ryan Holiday

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
3,499
Reaction score
5,956
Asilimia 77.4 ya deni la nje la Tanzania linashikiliwa na Central government, ikimaanisha kuwa serikali ndiyo mkopaji mkuu. Hii inaashiria utegemezi mkubwa wa mikopo ya kimataifa kwa ajili ya maendeleo, miundombinu, na mahitaji ya kifedha.

Tanzania ambayo deni lake la Taifa limepaa kwa kasi na kufikia kiasi cha shilingi za Kitanzania Tril 107.7 katika muda mfupi wa uongozi wa Raisi Samia Suluhu Hassan huku kukiwa hakuna mnyambulisho na mchanganuo bora juu ya matumizi ya mkopo huo kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla. Mkopo ukiwa umefunikwa na Giza zito la wanasiasa wasioitakia mema Tanzania.

Mtaalamu wa uchumi mzaliwa wa Zambia na Master's Graduate katika chuo cha Havard University, Dambisa Felicia Moyo, anapinga vikali dhana hii, akiwa na uzoefu mkubwa katika taasisi za kifedha kama World Bank na Goldman Sachs. Kupitia kitabu chake cha "Dead Aid: Why Aid Is Not Working and How There Is a Better Way for Africa", Anaweka bayana kwamba licha ya Afrika kupokea matrilioni ya dola za misaada katika kipindi cha zaidi ya miaka hamsini, bado bara hili limeendelea kuwa masikini, tegemezi, na lenye migogoro ya kijamii na kisiasa.

Tusipo kuwa makini Nchi hii itapigwa mnada ---> "In Ndugai Voice"

LIST & LINK BELOW

Opera Snapshot_2025-09-02_165554_africa.businessinsider.com.png


#DeadAid
 
Weka link hapa hakam ni IMF ya keko

USSR
 
Asilimia 77.4 ya deni la nje la Tanzania linashikiliwa na Central government, ikimaanisha kuwa serikali ndiyo mkopaji mkuu. Hii inaashiria utegemezi mkubwa wa mikopo ya kimataifa kwa ajili ya maendeleo, miundombinu, na mahitaji ya kifedha.

Tanzania ambayo deni lake la Taifa limepaa kwa kasi na kufikia kiasi cha shilingi za Kitanzania Tril 107.7 katika muda mfupi wa uongozi wa Raisi Samia Suluhu Hassan huku kukiwa hakuna mnyambulisho na mchanganuo bora juu ya matumizi ya mkopo huo kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla. Mkopo ukiwa umefunikwa na Giza zito la wanasiasa wasioitakia mema Tanzania.

Mtaalamu wa uchumi mzaliwa wa Zambia na Master's Graduate katika chuo cha Havard University, Dambisa Felicia Moyo, anapinga vikali dhana hii, akiwa na uzoefu mkubwa katika taasisi za kifedha kama World Bank na Goldman Sachs. Kupitia kitabu chake cha "Dead Aid: Why Aid Is Not Working and How There Is a Better Way for Africa", Anaweka bayana kwamba licha ya Afrika kupokea zaidi ya dola trilioni moja za misaada katika kipindi cha zaidi ya miaka hamsini, bado bara hili limeendelea kuwa masikini, tegemezi, na lenye migogoro ya kijamii na kisiasa.

Hii inafanya kuwa Deni la Tanzania kuwa kubwa zaidi kuliko la Malawi, Burundi, na Namibia, hali inayodhihirisha kuwa Tanzania inakopa kwa kasi zaidi ikilinganishwa na nchi hizo.

LIST & LINK BELOW

View attachment 3462764

#DeadAid
hili pekee lilikuwa linatosha kumfurusha huyu mama ofisini

watu hawana hata haya, hawawezi wanang'ang'ana tu
 
Hii ni rasmi Sasa, baada ya Ndugai kushauri tujitegemee, Rais Samia alimshukia vikali Hadi kumtambia kuwa kama kukopa atakopa sana.
Mungu si Abdul Wala Mchengerwa

Hii imepelekea deni la Taifa kukua Kwa zaidi ya TSH.60T Ndani ya miaka 4.

IMF wametoa orodha ya nchi kumi zenye madeni makubwa, Tanzania imekuwa nchi ya 8.

Ni matumaini yangu baada ya miaka 5 ya Rais Samia deni litakuwa kubwa zaidi nakuifanya Tanzania iingie kwenye Tano Bora Kwa nchi zenye deni kubwa Afrika.

Mama endelea kukopa sisi tunakuunga mikono.
 

Attachments

  • IMG_20250902_184730.jpg
    IMG_20250902_184730.jpg
    44.3 KB · Views: 33
  • IMG_20250902_184707.jpg
    IMG_20250902_184707.jpg
    34.8 KB · Views: 33
Kumbe majirani zetu wanadaiwa 3x ya deni letu, bado tupo vizuri hilo ni deni himilivu.
 
Back
Top Bottom