Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Kwanza natoa hongera kwa JK at least kwa hili lazima nikubali kwamba pamoja nakamati ya Bunge wangaliweza kufunika kila kitu kama Mkapa alivyofanya lakini JK ameona hapana wacha waseme . Then Kamati nzima ambayo imeleta ripoti hii .Lazima watu wakifanya vyema tukubali .Huu ndiyo Utaifa na Utanzania na hizi ndiyo Siasa komavu .Hongereeni sana .Spika hastahili Hongera zangu nangoja kuona anazima michango ya watu leo baadaye .

Kweli kabisa, JK anastahili sifa, bila ya yeye haya yasingetokeya.
 
Mwakyembe Mungu akubariki!

Nakubalina na wote waliosema ya kuwa kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania serikali imeanikwa wazi wazi . Nimesoma ripoti nadhani Mwakyembe amepiga msumari wa mwisho kwa Lowassa pale aliposema ...

Ibara ya 52 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inatamka wazi kuwa Waziri Mkuu ndiye mwenye madaraka ya juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hadi siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ndiye Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni. Kamati Teule haikufurahishwa hata kidogo na taarifa hizo zinazomgusa moja kwa moja Mhe. Waziri Mkuu katika kuipendelea Richmond Development Company LLC. Hata hivyo Kamati Teule imetimiza wajibu wake kwa uwazi na ukweli kama ilivyoagizwa na Bunge letu Tukufu. Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Mhe. Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shughuli za Serikali na uongozi wa nchi kwa ujumla, ni wajibu wake yeye mwenyewe kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya Bunge. Vile vile ni wajibu wa Bunge ambalo linathibitisha uteuzi wake kwa mujibu wa Ibara ya 51 inayothibitisha uteuzi wake. Kuangalia ikiwa matokeo ya uchunguzi huu hayajaathiri hadhi na uzito wake ndani ya Bunge.

Kwa maana nyingine Mwakyembe anasema ya kuwa Lowassa anatakiwa AFUKUZWE !
 
JKN aliona mbaali sana sasa naona mnakubali wenyewe wakati ni TOO late!
 
Huu ndio msumari kwa Lowassa

Ibara ya 52 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inatamka wazi kuwa Waziri Mkuu ndiye mwenye madaraka ya juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hadi siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ndiye Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni. Kamati Teule haikufurahishwa hata kidogo na taarifa hizo zinazomgusa moja kwa moja Mhe. Waziri Mkuu katika kuipendelea Richmond Development Company LLC. Hata hivyo Kamati Teule imetimiza wajibu wake kwa uwazi na ukweli kama ilivyoagizwa na Bunge letu Tukufu. Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Mhe. Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shughuli za Serikali na uongozi wa nchi kwa ujumla, ni wajibu wake yeye mwenyewe kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya Bunge. Vile vile ni wajibu wa Bunge ambalo linathibitisha uteuzi wake kwa mujibu wa Ibara ya 51 inayothibitisha uteuzi wake. Kuangalia ikiwa matokeo ya uchunguzi huu hayajaathiri hadhi na uzito wake ndani ya Bunge.
 
ripoti kali mno.

imoto inaunguza pande zote

mie liloniumiza ni jinsi gani watanzania tunavyokuwa wapenda majungu na wapenda domo nje ila tukiitwa tuthibitshe ukweli tunaanza kuuma uuma vidole.

ni aibu kutojiamini na kutokuwa jasiri wa kusema ukweli.

hii imeanza kunipa wasi wasi mkuu kuwa watanzania ni watu dhaifu na ni watu ambao tutachelewa sana kuendelea.

kumbe yanayosemwa amani yetu ni ya woga ni maneno ya kweli.

nnaamini kuna ukweli mwingi haujawekwa wazi kwa hofu.

nnaamini kuna mengi yatakuja juu mwaka huu.

hongera wenye kuitakia mema nchi yetu bila ya kujali itikadi zao iwe kisiasa au kidini cha msingi upuuzi wa kuinyonya tanzania na kuwakandamiza watanzania ukomeshwe
 
jamani nimeelemewa Dr. kweli amefanya kazi. Ndio maana sita alitaka kuondoka(kukimbia)
 
Lowasa kazoea maongezi ya rushwa somo hili kubwa toka kwa Mwekyembe anaweza kulielewa kweli ? Huyu ni JK kumtosa tu basi tuanze maisha na hapo JK credibility itakuwa juu na watajua kwamba si mla rushwa lakini kama atamezea basi twafa .
 
Ni kweli wamejitahidi sana, ila sifa ziende kwa kamati nzima maana Mwenyekiti peke yake asingeweza kufanya hayo yote.
Ni kweli tunatakiwa kuipongeza kamati nzima kwa mambo mzzuri waliyofanya kwa kufichua uozo wote na huyu PM anafanya nini mpaka sasa asijiuzuli na richmonduli yake?
 
DMussa,

[ame]https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=9560[/ame]
 
Safari ni ndefu lakini nafurahi mapinduzi yanakuja...CCM inaelekea kugawanyika na kuwa CCM Asili na CCM ya Mafisadi. Dr Mwakyembe amempa JK mwelekeo nzuri wa kurudisha hadhi ya Chama...kazi kwake JK kama ni kusuka ama kunyoa....wananchi wanajionea wenyewe yote haya Live.

Ikifika 2010 wananchi wenyewe wataamua..haya sio ya kusimuliwa...yapo wazi yanasemwa kwenye bunge lao kwa lugha ya kiswahili.

Wapinzani wajiandae kujenga hoja nyingine CCM na JK wanaelekea kujipanga kusafisha Chama...wakingangania hoja hii soon wanaishiwa mashiko maana CCM watasema tulikosea na sasa tumerekebisha.
 
hata na mm nnaaunguka kutoa pongezi zangu kwa kamati na wale wote waliosaidia kujulikana ukweli.

nnakumbuka msemo mmoja

babu jinga inama ufikiri mali yako inaliwaaaaaaaaaaa mali yako inaliwaaaaa
 
Jamani kama taarifa ya Tume ya Dr. Mwakyembe itafaniwa kazi kwa makini yumkini inahitaji kuondoa Mafisai wengi kuliko tulivyotegemea. makofi ya wabunge na melezo leo wakati wa kuwakilisha taarifa, na maelezo ya juzi walipoikataa semina kama yatakuwa yanatoka moyoni basi mimi nategemea.
1. Masilahi ya kivyama yakiwekwa pembeni, 2. ibara inayofuata baada ya ile ya 52 amabayo kamati imeiquaote itatumika.

tuliwahi kuipata hapa, naipaste tena.

PART TWELVE

MOTION FOR A VOTE-OF-NO-CONFIDENCE ON THE PRIME
MINISTER
111. - (1) Any Member may give a written notice to the Speaker on
Notice of
his intention to present a Motion for a Vote-of-no-confidence on the Prime
Motion for a
vote of no
Minister, pursuant to Article 53A of the Constitution. Such Motion shall
confidence on
be presented to the Assembly immediately after the lapse of fourteen days
the Prime
since that Motion was first submitted to the Speaker.
Minister

(2). A Motion moved under this Standing Order shall be debated
How to
Debate a
and decided upon in compliance with the requirements for debating
Motion for a
Motions prescribed by these Standing Orders, but the decision thereof
Vote-of-No-
shall be reached through secret ballot.
Confidence
on the Prime
Minister
 
The rotten ministry of energy and minerals!! its time to make all who participated, in one way or the other pay. Lowassa,Msabaha,Tanesco guyz, makamishna wa wizara yaani everybody, some body should put them in a big black bag and toss their asses off the cliff
 
Duh.

JK majaribuni?Kusuka au Kunyoa.Zile Tetesi amabzo muunganwa alikiri zipo,Leo anakata Mzizi wa Fitina.Ila Jameni Mamvii bwana...?

MWanangu Jk Naomba kwa kutufurahisha wanao tuliokuwa na wewe zamani zile club villa pale Dodoma,naomba umng;oe Huu Mjamaaa.

Imeosha!

Namalizia kusoma Ripoti then nitarudi hapa
jamani nijulisheni hiyo ripoti iko kwenye nini mana niliona pale dr mwakyembe aliruka kurasa kwa ajili ya muda.MUNGU IBARIKI KAMATI MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Nahisi kama niko ndotoni, hivi ni kweli hii inatokea Tanzania chini ya CCM????????? kazi ipo, hongera Mwakembe lakini bila kusahau wapinzani, JF na wananwaliokomalia jambo hili. Huu sasa ni mwanzo tu!!!!!!
 
Tafadhari naomba maelekezo nitaipataje hiyo taarifa kamili hapa, najaribu kuitafuta lakin siiioni
 
Mimi naona kwa sasa hongeza ziende kwa Mwakyembe na kamati yake, they have done their job without fear or favour. JK nitampongeza kama recommendations zilizotelewa atazifanyia kazi bila kumuangalia mtu usoni. Nitaboreka sana kama huu mpira nao ataamua kuwatupia PCCB, Polisi na Mwanasheria Mkuu, he needs to make a decision now.
Kwa upande mwingine, nadhani sasa wabunge wetu wameamka na hawataki tena kutumika kama rubber stamp which is a good thing kwetu walalahoi.
 
Safari ni ndefu lakini nafurahi mapinduzi yanakuja...CCM inaelekea kugawanyika na kuwa CCM Asili na CCM ya Mafisadi. Dr Mwakyembe amempa JK mwelekeo nzuri wa kurudisha hadhi ya Chama...kazi kwake JK kama ni kusuka ama kunyoa....wananchi wanajionea wenyewe yote haya Live.

Ikifika 2010 wananchi wenyewe wataamua..haya sio ya kusimuliwa...yapo wazi yanasemwa kwenye bunge lao kwa lugha ya kiswahili.

Wapinzani wajiandae kujenga hoja nyingine CCM na JK wanaelekea kujipanga kusafisha Chama...wakingangania hoja hii soon wanaishiwa mashiko maana CCM watasema tulikosea na sasa tumerekebisha.

kweli kabisa
 
Back
Top Bottom