Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
endeleeni kutupa utamu
Jamani vyombo vyetu vya habari viko chini sana. Yaani baada ya hii taarifa, jumptv wana taarifa wala hata hawaongelei kilichotokea bungeni. Nilitegemea iwe Breaking News.
Yaani nilichosikia leo, kingelikuwa hapa UK, madhara yake yangeitikisa mno serikali. Lowassa asingelipona, hivyo hivyo Karamangi, Msabaha, mwanasheria mkuu, Hosea wa PCCB pamoja na wafanyakazi kibao wa chini.
Ningetegemea magazeti bila kusubiri na kutoa toleo maalumu za mchana na picha ya Lowassa chini ya kichwa cha habari "GUILTY"
Lakini kwa Tanzania sijui kutakuwa na madhara kiasi gani kwa serikali ya JK.
Kwa standard ya West, hii report ni mawe hasa, ila sina uhakika na uwajibikaji wetu huko nyumbani.
Wacha tusubiri na kuona mwisho wake. Ila kamati wamejitahidi mno, maana kumgusa Wazir mkuu wa nchi sio kitu rahisi, pamoja na kukwepa kwepa lakini
wamechomelea misumari hasa.
Yaani nchi yetu inatia aibu, wataalamu wetu wanatia aibu kweli kweli. Yaani
ni taabu tupu, maana inaelekea hakuna wanachofanya zaidi ya kuchukua kamisheni zao.
Vijana someni mkachukue nchi maana hao watu tulio nao ni bomu mno!
Sijawahi Kulizwa na Riport za kamati za Bunge Lakini leo Nimelia...
.............kweli dalili za mwisho zimewadia.........
kazi kwa KIKWETE sasa kuwa fukuza maana ushahidi upo! au awakumbatie tujue kuwa anawalea
.............mungu saidia tanzania..........
Mtanzania, aisee mimi nipo huku porini sina communication yoyte.... Mkuu unaweza kutuwekea hata dondoo/summary manake sio mchezo inaonekana mambo yameenda vile wengi tulivyofikiria na kumuomba Molla atusaidie kuweka hawa mafisaid nje juani tuwakome....
Gigo, tunangojea nyeti kaka manake hii kitu ni ya kusomwa kweli kweli.....
Wale mnaoona hii mambo ina kikao kinaidiscuss au ndio kusomwa leo hoja next tyme???
Tuanzishe mada mpya. Mnyika naicopy ripoti yako ili kuanzisha mada (thread) mpya. Samahani
..JK ANAINGIA DODOMA MCHANA HUU ATAWEKA KAMBI CHAMWINO KAMA KAWAIDA YAKE BUNGE LINAPOKUWA LINAJADILI HOJA NZITO HUWA DODOMA.....LOLOTE LITAKALOTOKEA MJUE LINA BARAKA ZA KIKWETE!!!!!!!!!!!!!!!!!!