Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Field Marshall ES,
Sijakuelewa mkuu hapo juu kwani Agustoons kasema kuwa Hamad Rashid ni wa CUF na kichwa hasa..
lakini naposoma maelezo yako yanatisha na hayafanani na sifa kwa Rashid ama nimekosea?
 
Hapana mkuu Rashid, ninamfahamu toka akiwa deputy waziri wa ndani, ni mutu kichwa sana, ndio maana sikushangaa akiongea siasa ya kweli.
 
Kweli mzee wetu Malecela anashuka taratiiibu kutoka juu. Duh! namsikitikia sana. Kama ndio kusema ndio mzee kila wakati ili mkono uende kinywani hii yake imezidi!

Kweli umri ukizidi kusogea unaishiwa na point!
 
Tatizo si kukataa kubinafsisha, issue hapa ni kujifunza kwanza what went wrong tulipoanza kufanya biashara na kampuni binafsi kama mambo ya IPTL na Richmond, halafu tukosoe hitilafu zilizotokea katika vitu hivyo ndio tuweze kuwaachia kampuni nzima kabisa. T

Nani vile walikuwa maziri wa Nishati na Madini na wizara ya fedha wakati wa kutiwa sign mkataba wa IPTL...naona giza mimi hapo!! maana hao ndo wa kuanza nao...
 
Nani vile walikuwa maziri wa Nishati na Madini na wizara ya fedha wakati wa kutiwa sign mkataba wa IPTL...naona giza mimi hapo!! maana hao ndo wa kuanza nao...

Hakuwa Mkuu wa Kaya kweli?
 
Kweli mzee wetu Malecela anashuka taratiiibu kutoka juu. Duh! namsikitikia sana. Kama ndio kusema ndio mzee kila wakati ili mkono uende kinywani hii yake imezidi!

Kweli umri ukizidi kusogea unaishiwa na point!
Anaogopa wata-mkolimba. Si unajua tena wazee wanavyoogopa.....
 
mbona watu wote mnashabikia riport hatakabla ya kujua kilichok ndani yake? au ndo tabia za kitanzania? kuwa moved na kitu kwa hisia tu kuwa kunawatu wameumbuliwa? mtasema nini mkikuta mambo ni kinyume? na ripoti ikisema kuwa serikali ni safi na ili fanya hivyo kwa bahati mbaya? au ikisema hamna anaestahili kuwajibishwa kwa sababu walipewa zabuni kwa nia njema na kufuata taratibu? tuweni makini na wenye subira kitu kiwekwe wazi ndo tuseme!

......... hamna cha ajabu katika siasa za watanzania lolote lina wezekana... mbona TAKUKURU WALIWEZA KUWA SAFISHA RICHMOND??

Tusubiri tuone ya kamati ya bunge? maana pengine hao wanaotapatapa ni uoga wao tu kwa kuwa walitajwa tajwa tu na ina wezekana hawajaumbuliwa!

..............nasisitiza utulivu na tusikurupuke..........subira jamani
 
mbona wandugu mnaizungumzia ripoti kama vile mmeshaiona? au ndo tabia za kitanzania kushabikia tu kitu bila kuwa na undani? itakuwa vipi kama riport ikitolewa na ikawa haitofautiani na ya TAKUKURU?bunge ni lilelie lililo mtetea karamagi! nililelile lililotetea BOT! nililelie la CCM! kitu gani kinawapa matumaini hivyo? itakuwaje riport ikisema sawa na LOWASSA kuwa serikali inania njema?

kwa kifupi msiwe na aspiration kubwa! mnaweza kuwa disappointed mno! hii bado ni tanzania! chochote kinawezekana! mbona TAKUKURU ambayo ina wataalamu wa uchunguzi na mkuu wake ana PHD ya circumstancial evidence katika corruption lakini hakuweza kuestablish case against any?

........kuweni makini wasikivu na wadadisi.....msiwe kama SITTA...msikurupuke..... subira jamani.....
 
kaka usemalo ni kweli lakini,cant you see what have been written on the wall?
 
Wajameni Richmonduli Inasomwa Kule Bungeni Muda Huuu,alie Karibu Na Tv Aangalie
 
Nimeiona Jamani Namuona Mwakyembe Anataja Kabisa Kuwa El Amehusika,el Kainamma Hana Hamu...
 
Nimeiona Jamani Namuona Mwakyembe Anataja Kabisa Kuwa El Amehusika,el Kainamma Hana Hamu...

Naona issue iko tense sana ...sasa Mheshimiwa Edward Hosea mkuu wa Takukuru atatuambia nini sisi watanzania milion 40, aliposema RICHMOND imetulia?
 
Duh! Jamani hii report ni soo! PM na Rostam sioni watapitia wapi....
 
Patamu hapa! Ngoja nikachukue kikombe cha chai nakuja!

Kwa kweli mimi napiga mluzi tu hapa kwenye Kigoda nikisubiri usanii utakaofuata Tanzania kila kitu cha wezekana...
 
Karamangi na PCCB matatizoni. Kama wataifanyia kazi hii report huenda ikasaidia.
 
Back
Top Bottom