Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Udaku unasema ana jina la PM kapuni anasuburia tu!

Anasubiria nini? Yaani anataka atumie Bunge ili yeye (JK) asionekane ni mbaya kwa EL na RA? Kama watu wamemwangusha si aseme tu kwamba wamekuwa mzigo na hawabebeki tena so kila mtu aende kivyake!
 
Ni kweli wamejitahidi sana, ila sifa ziende kwa kamati nzima maana Mwenyekiti peke yake asingeweza kufanya hayo yote.
 
News za jana plus magazeti yalisema anakwenda kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri, sasa hicho kikao kitakalika kweli?
 
Hongera Mheshimiwa Mwakyembe kazi yako umeifanya, tusubiri utekelezaji wa mzee wa kaya
 
Duh.

JK majaribuni?Kusuka au Kunyoa.Zile Tetesi amabzo muunganwa alikiri zipo,Leo anakata Mzizi wa Fitina.Ila Jameni Mamvii bwana...?

MWanangu Jk Naomba kwa kutufurahisha wanao tuliokuwa na wewe zamani zile club villa pale Dodoma,naomba umng;oe Huu Mjamaaa.

Imeosha!

Namalizia kusoma Ripoti then nitarudi hapa
 
Jambo la maana ni kama wahusika watachukuliwa hatua kali bila kujali nyadhifa zao.Itakuwa fedheha kubwa kama kesho ripoti hii itajadiliwa kishabiki na Bunge letu kisha maamuzi ya ovyo yakatolewa kama tulivyozoea siku zilizopita.
 
Kwanza natoa hongera kwa JK at least kwa hili lazima nikubali kwamba pamoja nakamati ya Bunge wangaliweza kufunika kila kitu kama Mkapa alivyofanya lakini JK ameona hapana wacha waseme . Then Kamati nzima ambayo imeleta ripoti hii .Lazima watu wakifanya vyema tukubali .Huu ndiyo Utaifa na Utanzania na hizi ndiyo Siasa komavu .Hongereeni sana .Spika hastahili Hongera zangu nangoja kuona anazima michango ya watu leo baadaye .
 
Huwezi amini jinsi tulivyo na viongozi incompetent na wapenda rushwa na sijui kwanini bado hawajajiuzuru mpaka sasa,hii ni aibu sana na hawa watu lazima wachukuliwe hatua na Richmond washtakiwe kwa utapeli
 
Anasubiria nini? Yaani anataka atumie Bunge ili yeye (JK) asionekane ni mbaya kwa EL na RA? Kama watu wamemwangusha si aseme tu kwamba wamekuwa mzigo na hawabebeki tena so kila mtu aende kivyake!

Muungwana hataki lawama. Nadhani anachotaka kufanya ni ku-twist the knife once the stabbing has been done.
 
Koba,

Nimeambatanisha na mkataba wenyewe ili mtirirko uende vyema.

Au siyo?

Poa poa mkuu.
 
Leo ni litmus test kwa JK. Keshatafuniwa kila kitu imebaki yeye kumeza tu. Akishindwa hapa basi credibility yake itashuka sana.
 
Hii ndio executive summary yangu,Kama Muungwana akiwaacha Edward Lowassa,Nazir KaramagiKaramagi na Dk Mrisho Msabaha pamoja na makatibu wote wa wizara ya Nishati na Madini.Mkurugenzi wa Takukuru,Mkurugenzi wa upelelezi wa takukuru,Mwenyekiti wbosi ya wakurugenzi wa TANESCO basi mie naanda maandamano na niko Radhi kupigwa Risasi na kufa.

na ninaomba Kamatai kuu ya Chama Cha Mapunduzi Iwafute kina Rostam Azizi,Edward Lowassa,Karamagi ,Msbaha kuwa wanachama wa chama cha Mapinduzi sababu wamekitia doa chama chetu.Niliota hili na naamini Muungwana hatawaacha

Je Jakaya Mrisho uko tayari kumaliza ubia wa ko na EL?Je nini hatma ya Mavi na Uraisi wa TAnzania?Membe bwan...

Kubainisha Richmond Development Company LLC ni kina nani, na ni kampuni ya shughuli zipi na hivyo kupima uwezo wake kupatiwa zabuni ya kuleta nchini na kujenga mtambo wa umeme wa gesi wa MW 100;
Mheshimiwa Spika, vilevile Mhe. Rostam Aziz alitakiwa atoe maelezo kuhusu uhusiano wake na Kampuni za Richmond Development Company LLC na Dowans Holdings S.A


Mheshimiwa Spika, Mkataba wa uzalishaji umeme wa dharura unaielezea kwenye utangulizi Richmond Development Company LLC kuwa ni kampuni iliyosajiliwa chini ya sheria za Jimbo la Texas, Marekani na yenye anuani ifuatayo: 5825 Schumacher, Houston Texas 77057, Marekani


Kutathmini mchakato mzima wa jinsi zabuni waliyoshinda Richmond ilivyoshughulikiwa kuanzia Kamati ya Zabuni hadi mwisho ili kujiridhisha kuwa sheria, taratibu, miiko na maadili ya zabuni yanayotawala zabuni za aina hiyo vilifuatwa au vipi;

Mheshimiwa Spika, tarehe 22 Februari 2006 TANESCO iliomba idhini ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kutangaza zabuni hiyo kwa muda wa siku 10 badala ya siku 45 zinazoainishwa katika Kanuni za Ununuzi. Tarehe hiyo hiyo ya 22 Februari 2006, PPRA ikaijibu TANESCO kwa kuitahadharisha kuwa utaratibu huo utakuwa kinyume cha taratibu na Kanuni za ununuzi. Muda wa siku 10 hautoshi kuitisha zabuni ya kimataifa na kuweza kupata wazabuni wenye sifa zinazohitajika.


Kutathmini mkataba baina ya Richmond Development Company LLC na TANESCO ili kujiridhisha kuhusu uhalali wa masharti ya mkataba huo ukizingatia gharama na masharti mengine ukilinganisha na masharti yaliyomo katika mikataba ya aina hiyo iliyoafikiwa na TANESCO/Serikali;
Mheshimiwa Spika, tarehe hiyo hiyo 22 Februari, 2006 TANESCO ikaiarifu Wizara kuhusu ushauri wa PPRA. Wizara ikaukataa na kuiagiza TANESCO kutekeleza agizo la Waziri bila kukosa kwa kuitangaza zabuni hiyo. Zabuni hiyo ikatangazwa kwa utaratibu wa ndani tarehe 23 Februari 2006. Hatua hiyo iliishitua PPRA ambayo iliiandikia barua TANESCO kuelezea kushangazwa kwake na hatua ya shirika hilo kukaidi ushauri wa kitaalamu na wa kisheria. PPRA ikasisitiza kuwa, njia pekee kwa TANESCO kupata wazabuni wazuri na wenye sifa stahili katika kipindi kifupi ni kutumia utaratibu ilioupendekeza wa international shopping.

Kubainisha huduma na misaada mbalimbali waliyopewa Richmond kama vile kufunguliwa Letter of Credit na kupima uhalali wake;
Mheshimiwa Spika, TANESCO ikionyesha dhahiri kusukumwa tu na Wizara, ikaiandikia tena PPRA Jumapili tarehe 26 Februari 2006 kuelezea kuwa sasa imeagizwa na Serikali kuitangaza zabuni hiyo magazetini, hivyo mamlaka hiyo ya udhibiti wa ununuzi wa umma itoe idhini ya kutangaza zabuni ya kimataifa kwa siku chache kuliko zilizowekwa na sheria. TANESCO huku ikijua kabisa kuwa PPRA isingeweza kuipata na kuijibu barua hiyo Jumapili, ikatangaza zabuni hiyo magazetini tarehe 27 Februari 2006 na kuwataka wazabuni wawasilishe zabuni zao tarehe 6 Machi 2006 yaani siku 10 baada ya kuchukua nyaraka za zabuni tarehe 24 Februari 2006.

Mheshimiwa Spika, hoja ya kwamba kampuni hiyo ilikuwa na ubia na kampuni kubwa ya Pratt & Whitney, haikuwa ya kweli. Katika mchakato wote wa zabuni ndani ya TANESCO, moja ya masuala kadhaa yaliyoifanya Richmond Development Company LLC isitiwe maanani, ni ukosefu wa ushahidi wa kisheria wa ubia (consortium agreement) kati yake na Pratt & Whitney. Baada ya kubanwa na Kamati Teule kuhusu ushahidi wa mahusiano wa kampuni hizo mbili, Wajumbe wa Kamati ya Wataalamu waliwasilisha mbele ya Kamati Teule ushahidi wa aina mbili: kwanza business card ya mzungu mmoja aliyejulikana kwa jina la John Perun aliyejiita mwakilishi wa Pratt & Whitney, na pili, kivuli cha mkataba wa kurasa nne kati ya Richmond Development Company LLC na Pratt & Whitney wa kubadilishana taarifa na siyo kuzalisha umeme. Aidha mkataba huo ulikuwa haujathibitishwa na wakili au shahidi yeyote wa kuaminika kuwa mkataba halali. Kamati Teule imesikitishwa na kushangazwa kwa kiwango cha chini cha umakini kilichoonyeshwa na wataalam wetu hususan kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kushughulikia suala hili.


Mheshimiwa Spika, pamoja na maelekezo na ushauri huu wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Nishati na Madini siku hiyo hiyo ikaiandikia barua TANESCO kuitaka itekeleze maombi ya Richmond Development Company LLC mara moja kubadilisha masharti ya malipo:-

" . . . I wish to inform you that the proposed amendments to the existing Letter of Credit are acceptable and you are advised to liaise with CRDB Bank to effect the changes as soon as is practical. . . ." Barua ya Katibu Mkuu wa Nishati na Madini (Kumb. Na. CBD.214/324/01 ya tarehe 6/10/2006) inasomeka.
Mheshimiwa Spika, Kamati Teule imejiuliza bila kupata majibu: Ni nini kilifanyika hadi Wizara ya Nishati na Madini ikatoa kauli hii ambayo ni tofauti kabisa na ushauri ilioupata kutoka Wizara ya Fedha? Nini msingi wa ukereketwa au ufukukutwa bayana wa Wizara ya Nishati na Madini kuhusu Richmond?


Kuziangalia na kuzitolea maoni taarifa za TAKUKURU, PPRA na taarifa zozote nyingine zilizoangalia utaratibu wa zabuni ya Richmond

Hoja ya TAKURU kuwa kulikuwa na mapungufu, lakini mapungufu hayo yalikuwa ya kawaida ambayo hayajengi makosa ya jinai haina msingi. Kwa Wizara kuilazimisha taasisi nyingine ya ununuzi, yaani TANESCO, kusaini Mkataba ambao haukupitishwa na vyombo vyake vya maamuzi; kwa kampuni hiyo ya Kimarekani kujitambulisha kwa majina mbalimbali katika mchakato huo: mara Richmond Development Company LLC, mara RDC, RDVECO, na mara nyingine RDEVCO; yote haya kwa TAKURU ni makosa ya "kawaida ya kiutendaji"?
TAKURU haikuona hasara ambayo nchi ilipata kutokana na zabuni hiyo wakati kila mwananchi aliona hasara bayana kwa nchi kukosa umeme kwa kipindi kirefu na kuathiri uzalishaji mali na huduma za lazima nchini.
TAKURU iliamini kuwa hakukuwa na uzembe. Je, kwa Wizara na watendaji mbalimbali wa Serikali kuamini kuwa Richmond Development Company LLC na Pratt & Whitney zilikuwa na ubia bila kudai nyaraka za ubia; kwa viongozi wa Serikali kumwona tu mzungu na business card yake, na kuamini moja kwa moja kuwa ni mwakilishi wa Pratt & Whitney wakati siyo; kwa Serikali kuamua kusaini Mkataba na kampuni ambayo haijafanyiwa uchunguzi wa kina kujiridhisha kuwa si kampuni hewa au ya mkobani; hivyo vyote kweli si uzembe?


Kuangalia mambo mengine yoyote yenye uhusiano na mchakato mzima wa Richmond ili kutoa mapendekezo ya kuboresha taratibu za zabuni kwa siku zijazo, kwa maslahi ya Taifa letu
Siku hiyo hiyo tarehe 21 Juni 2006, Waziri wa Nishati na Madini akamwandikia dokezo Katibu Mkuu wake aiagize TANESCO iingie mkataba mara moja na Richmond Development Company LLC baada ya Waziri Mkuu kuidhinisha mapendekezo ya Wizara. Muda mfupi baadaye, kwa kutekeleza agizo la Waziri, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini akamwandikia barua Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO Balozi Fulgence Kazaura kumwagiza ahakikishe kuwa TANESCO inasaini mkataba na Richmond Development Company LLC.


Kamati Teule ikawaita kwa mara ya pili Dk. Msabaha (Mb) na Ndugu Mwakapugi kwa mahojiano zaidi. Wote wawili, wakiwa ndani ya kiapo, walikataa katakata kupokea maagizo kutoka kwa Waziri Mkuu ya kuipa Richmond upendeleo. Lakini Mhe. Dk. Msabaha (Mb), baada ya mahojiano chini ya kiapo, akaiuma sikio Kamati Teule kuwa katika suala hilo yeye atakuwa kondoo wa kafara tu au, kwa maneno yake mwenyewe, "Bangusilo" kwa lugha ya Kizaramo. Maelezo hayo ya ziada nje ya kiapo ya Mheshimiwa Waziri yaliyotoa ujumbe kuwa "si yeye ila mkuu wake wa kazi", yalioana na maelezo aliyoyatoa Balozi Kazaura nje ya kiapo tarehe 30 Novemba, 2007. Mara baada ya kumaliza mahojiano kwa kiapo na Kamati Teule, Balozi akatoa maelezo ya ziada kuwa Richmond ilikuwa mradi wa "Bwana Mkubwa" na "mshiriki wake mkubwa kibiashara", akimaanisha Mhe. Waziri Mkuu na Mhe. Rostam Aziz (Mb).
 
Leo ni litmus test kwa JK. Keshatafuniwa kila kitu imebaki yeye kumeza tu. Akishindwa hapa basi credibility yake itashuka sana.

Mistake ambayo JK alifanya ni kuweka mwizi/jambazi/mhuni kuwa waziri mkuu
 
Heko kwa kamati!
Jamani hii ripoti iko wapi wakuu?
 
dmussa ripoti iko humuhumu,imetumwa na mnyika na fd kaituma pia
 
Back
Top Bottom