Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

PM inabidi ajiuzulu tu,maana kama itakwenda kwenye kuijadili kesho,basi maadui zake wote watakuwa wamepandikiza watu kuchangia,hapa tunaongelea Mwandosya,Membe,Prof Maghembe,Diallo....sijui atatokea wapi
 
Naona kinyaa kwa nini nilizaliwa wakati huu wa kizazi cha viongozi hawa majambazi.Hawa magabachori siku zote Mtikila alituambia wazi kuwa ndo source ya ujambazi ndani ya nchi yetu kazi yao ni kutafuta Watanzania walafi kama akina Lowasa ili kufasilitake mambo yao.Hawana mapenzi na nchi hii.Ukiwafuatilia wote walioingia kwenye siasa ni majambazi tu.
Watanzania nchi hii ni yetu, kama JK hatochukua hatua yeyote kwa wote waliotajwa,ni jukumu letu sisi wenye nchi kuwafukuza na kuwachukulia hatua wote kuanzia JK,Lowassa,huyu Shihiri RA na wengine wote. SAA YA UKOMBOZI NI SASA
 
Nampendekeza Mizengo Kayanza Peter Pinda.
Jamaa anafaa sana.
 
Hawa jamaa wanaoguswa kwenye taarifa ya Mwakyembe wanapaswa kuachia ngazi usiku huu kabla ya kuanza kuchambuliwa kesho kwenye kikao cha BUnge kama watoto wadogo.

Najua wabunge karibu wote hawakubaliana na kizungumkuti chochote cha kuwabeba watu wenye sifa ya Ufisadi, na ingetegemewa kuwa wakati Rais JK anatua Dom, basi angalau mpatieni barua za kujiuzulu na kumsaidia, anawaonea aibu, maana madudu mliyoyafanya anayajua.

Lakini kwa upande mwingine, hivi mnataka watanzania wawafanye nini, maana sasa hivi ankara za umeme zimepanda kutokana na kashfa hii ya Richmond, na sasa wanalipia hata kile ambacho nyinyi na jamaa zenu mmejaza matumbo, Muogopeni Mungu jamani, na kwa hili mwapaswa kutubu.

Binadamu wote wameumbwa na Mungu lakini kuna wakati mwingine kutokana na jinsi ambavyo watu wengine walivyo tayari, kuchekelea maisha duni ya wenzao, uhakika wa dhana hii, unatia shaka.

Kama hamtaweza Kujiuzulu, basi, JK kwa kunusuru Taifa na UMoja wa kitaifa itabidi, avunje baraza la Mawaziri walau kabla ya Kikao cha nane cha Mkutano wa Kumi wa BUnge hapo kesho.

JK Charge, charge and shoot.

wabeja
 
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote
Nchi yangu Tanzania
Jina lako ni tamu sana!

Mafisadi wanajitanua
Wanapodhani wao miungu

Walalapo wanafikiria
Jinsi gani watatuibia

Wakibambwa wanajitetea,
Wapinzani wanawaonea.

Siri zao sasa zafichuka,
Wamebaki wanaweweseka!
 
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote
Nchi yangu Tanzania
Jina lako ni tamu sana!

Mafisadi wanajitanua
Wanapodhani wao miungu

Walalapo wanafikiria
Jinsi gani watatuibia

Wakibambwa wanajitetea,
Wapinzani wanawaonea.

Siri zao sasa zafichuka,
Wamebaki wanaweweseka!


mbona leo jina lako halipo kwa maandishi ya KIJANI?
 
Wapinzani huu ndio wakati muafaka wa kufanya maandamano ya kuunga mkono ripoti ya Dr Mwakyembe (regardless yeye ni CCM) na pia kushinikisha Serikali na hasa JK amwajibishe Lowassa, Msabaha, Karamagi na wote waliotajwa kwenye Riport.

Mkuu hapa umenena ningetegemea Kuanzia Kesho wapinzani na wana CCM(WAsiopenda UFISADI) wakimuomba Afande Tiba Kibali cha kuandamana, ikibidi waimize wenzao nchi nzima, Mbowe, Lipumba, Mbatia, Mrema, Makamba sasa mwenzenu kamaliza kazi yake.

Halafu kama kuna watu wamekuja Tanzania kuwa MAFISADI itabidi watafutiwe dawa mapema.

Itabidi tuwaorodheshe wote.
 
wamejitoa kwenye CCM, wameona CCM chama cha kijani kwa hiyo na wao watakuwa CCM

kumbe hawajui kijani ndio rangi ya uhai na progress ndio maana kwenye maendeleo huwa presented kwa rangi ya kijani
 
Currently Active Users Viewing This Thread: 288 (77 members and 211 guests)
kakindomaster, swabiri, macinkus, dwnmtz, Mlalahoi, Masikini Jeuri, Kalamu, mtu66, Majita, Omutwale, dash, Mtu wa Pwani, mwenekapufi, CMB, mshamba wa kijijini, sabasaba, IDIMI, Biggiebiggie, UFUNUO WA YOHANA, Misterdennis, Mzee Mwanakijiji, Yebo Yebo, care4all, djwalwa, Mtoto wa mkulima, mfwatiliaji, senator, BabaH, cola, Loi, NAJIKOPA MWENYE, Susuviri, nesindiso sir, mamaparoko, theodros, songambele, kudi shauri, Heri, Domo Kaya, kizimkazimkuu, bokoboko, Mtot wa Mkulima, Koba, Kasheshe, Mboni, amanigk, kapuli Amtoni, achwaya, tanzactive, Rashid Peter, Bobby, Bakari Muhogo, Siao, peace2007, mambo, Shiduki, makanyaga, muadilifu, humble servant, katibu tarafa, mburahati, amttu, Augustoons, musa_99, Mzalendohalisi, shukurani, mtimkavu, amagere, madsick, NG'WANENE, hausi, Akida, mkamap, Al, lawyer, shalom, gamba la nyoka
HIstoria imewekwa, naomba kuwakaribisha MAFISADI wote, Nazir, Aziz, Edward........, waje wachungulie hapa
 
Mie sasa nasubiri kauli za Tambwe Hizza na mwenzake Shaibu Akwilombe kuhusu kadhia hii, nisikie wanasemaje!
 



Rostam ni mafia...haongeia sana na wala hajipeleki kimbelembele kwenye haya madudu; yeye anatuma wakina Lowassa, Karamagi pamoja na JK mwenyewe wamfanyie kazi zake chafu. Ameitwa na hii kamati teule amekataaa...inathibisha wazi kuwa RA hagusiki; JK anajua hilo, Lowassa anajua, na wabunge wote wanajua.

Haya yote ni hadithi ya jana:

"In fact, in Tanzania we have two governments, one under Jakaya Kikwete and the other under Rostam Aziz. Rostam Aziz's government seems to be more powerful than Kikwete's because his government (comprising of corrupt businessmen) has the money which is badly needed by CCM". (from e-mail by Canadian Tanzanian Asians)

Kikwete is part and parcel of the team; it is ludicrous to think he has been unaware of all this and more.
 
NEXT PM?????? awe:JOHN POMBE MAGUFULI, mwasemaje wana JF?
 
Currently Active Users Viewing This Thread: 288 (77 members and 211 guests) kakindomaster said:
HIstoria imewekwa, naomba kuwakaribisha MAFISADI wote, Nazir, Aziz, Edward........, waje wachungulie hapa
 
Wale wapiga makofi wa CCM kila siku na walala Bungeni mchana wameamua kufanya kweli kwa kuzinduka nakusema no tunataka ukweli .Kwa mtaji huo Ndugu Lowasa amekatiliwa katika kikao ambacho sasa kinaendelea sirini .Badala yake kikao ambaye yeye huwa ni Mwenyekiti wale wamemchagua Malecela kuwa mwenyekiti wake .Wakati huo huo ndugu JK ametinga ndani ya mjini jioni hii . Habari ni ngumu kupatikana lakini tunajaribu toka hapa Dodoma kuleta tunalo weza kupata .Mwenye nyeti zaidi tafadhali aendeleze hapa , maana JF ina hazina kubwa .
 
Back
Top Bottom