Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Mag3
Hakuna cha umbumbumbu. Anachosema Mwakyembe ni kwamba bunge litengue kanuni zake ili huu mjadala ambao yeye anadhani ulishamalizika, urudiwe upya. Kuna kundi la mafisadi bungeni wanataka kujisafisha kwa kumlaumu Mwakyembe.Sasa yeye anachosema ni kuwa kwa mujibu wa kanuni za bunge ule mjadala wa Richmond umeshamalizika. Lakini kama kuna wabunge wanadhani bado kuna mambo ya kujadiliwa, basi waombe kanuni zitenguliwe na mjadala uanze upya na yeye atakuja na vibwagizo vipya. Simple as that. I hope umeelewa.
 
Mag3
Hakuna cha umbumbumbu. Anachosema Mwakyembe ni kwamba bunge litengue kanuni zake ili huu mjadala ambao yeye anadhani ulishamalizika, urudiwe upya. Kuna kundi la mafisadi bungeni wanataka kujisafisha kwa kumlaumu Mwakyembe.Sasa yeye anachosema ni kuwa kwa mujibu wa kanuni za bunge ule mjadala wa Richmond umeshamalizika. Lakini kama kuna wabunge wanadhani bado kuna mambo ya kujadiliwa, basi waombe kanuni zitenguliwe na mjadala uanze upya na yeye atakuja na vibwagizo vipya. Simple as that. I hope umeelewa.

Jasusi,

Nashukuru na nimeelewa ila post zingine humu ndani zinachanganya ati lol
 
Jasusi,

Nashukuru na nimeelewa ila post zingine humu ndani zinachanganya ati lol

Itabidi uivumilie JF. Tuko wa kila aina. Kuna wale wanaotaka kutoa hukumu papo kwa papo, kuna wale wanaotizama pande zote za issues, na pia kuna zealots kazi yao ni kulaani tu:-
 
Kuhani

Mkuu, usijaribu kabisa kupindisha hoja yangu na ndio maana nimesema nyie kazi yenu ni kuchukua vipande toka ktk maandishi mkaacha kile kilichotangulia...
Nimetanguliza neno - IT SOUND like!..Na hakuna mahala nimesema Mama ni CCM..acha ujinga mkuu..

Sawa Mkuu.

Lakini kabla sijauacha, ngoja tutafute huo ujinga, na nani kausema, ndio tutambue nani auache:

...Mama samahani lakini pamoja na kwamba unaonesha uchungu kwa nchi yetu lakini kidogo inanipa shida sana.. Uchungu wako ni ktk kuwapamba Mafisadi na kumfanya Mwakyembe mnafiki, mwongo hivyo report yake yote haina Ukweli...

To me it sound like His testimony has come under attack -He lied under oath, he should not be trusted..So the the convictions he helped must be overturned!..

Only Fisadis would love this!....

Unasema Mama anawapamba mafisadi, na anamfanya Mwakyembe mnafiki, mwongo. Anamshambulia Mwakyembe. Halafu unasema ni fisadi tu anaweza kupenda haya mashambulizi dhidi ya Mwakyembe. Lakini ni Mama hapa ambae unamkosoa kwa haya mashambulizi. Kwa maneno mengine unasema Mama nae fisadi kwa sababu ni "mafisadi tu ndio wanapenda haya" mashambulizi.

Yani hata mimi nililainisha ulichokisema nilipokuuliza "Mama anapenda mafisadi eeh?" Wewe umesema kibaya kuliko nilichosema umesema. Umesema anaependa mashambulizi dhidi ya Mwakembe ni fisadi: "Only Fisadis would love this!

Lakini kumbe hukukusudia kusema Mama fisadi, au anapenda mafisadi. Umetumia strongly worded language bila kuwa makini. Umeita mtu fisadi bila kujijua umemwita.

Nani mjinga?
 
Hivi Sasa Tukishakubali Mwakyembe Ni Fisadi..whats Next?

This BS ya overusing this word "fisadi" must stop. Watu kumkosoa Mwakyembe haina maana he is a fisadi necessarily. This myopic "you have to be 100% holier than thou else you are fisadi" one track mentality is pathetic.

It is obvious that Dr. Mwakyembe has done a great job of more signicance than most of us can hope to achieve, he is a hero of the anti-ufisadi movement.

That said, even heroes make mistakes.
 
don't put yourself down like that... Mwakyembe anajibu simu zake hata kama hajui nani anampigia, nenda kwenye tovuti ya Bunge na umpigie. Hoja mliyonayo ni ya msingi sana, lakini inatosha kumtosa mtu na kusema "hatufai"? I'm a realist, ukinipa uchaguzi wa Chitalilo na Mwakyembe kwenye kuongoza Kamati.. nitamchagua Mwakyembe! No sir, hatuwaachi mashujaa kwa kosa la kauli moja tena baada ya maneno na matendo ya kishujaa.

Nyinyi ambao viongozi kwenu hawakosei na wakikosea hata kwa kujing'ata ulimi tu basi wanatoshwa! Kuna vitu ambavyo tunaweza kutafuta kumhukumu Mwakyembe kwavyo, lakini la kauli hii tufike mahali tumtose tu ili tujithibitishie haki zetu wenyewe, ya kuwa ni jinsi gani sisi ni bora, watu ambao hatujawahi kuwa kwenye position kama hiyo ya kwake, kusimama na kusema yote aliyoyasema, halafu just like that tuyafute hayo yote kwa senteni moja! No sir!

Ni haki yenu kumtosa, na wengine haki yetu kumpa nafasi ya kutengeneza, kufafanua, au hata kufuta usemi wake! Kuna wakati rafiki anakosea tena vibaya, lakini kama kila rafiki akikosea anatoswa tena kosa la ulimi, basi wengi tusingekuwa na marafiki.

No sir, bado sijaona sababu ya kumtosa Mwakyembe sasa!!

Mwanakijiji,

Unafanya makosa ku generalize kama collectivist kwa kusema "nyie mnamtosa" nyie ni kina nani? watu tofauti wana object kauli za Mwakyembe tofauti kwa degrees tofauti.Personally naona hapa ni sehemu ya kuboresha effort kwa kutumia constructive criticism ambayo inaweza hata kumfaa Mwakyembe mwenyewe.Nimeeleza kuridhishwa kwangu na courage ya Mwakyembe, lakini kuna vitu anakosea na nimesema ni wapi.Kwa hiyo katika kuwakosoa wanaomkosoa Mwakyembe let us be very specific ili tu avoid kuwa lump wote kama "nyie".

Kuna watu wanasema Mwakyembe hana integrity kabisa, kuna wengine wanasema Mwakyembe amekosea kwa oversight tu, kuna wengine wanasema Mwakyembe alishajionyesha kuwa hana integrity siku nyingi tu, kuna wengine tulishaanza kutokubaliana na Mwakyembe kwenye issue ya "natural justice". Kwa hiyo huwezi kuwa lump wote hawa pamoja.

Be specific in your analysis please.
 
Pundit.. well noted.. niliposema wenye kumtosa nilimaanisha hivyo, I was not trying to be intentionally ambiguous. I really meant that. Sidhani kama wewe ni mmoja wa waliojaribu kumtosa. Ni jambo moja kusema mtu kakosea au kusema kitu ambacho si sahihi au kujaribu kuonesha kuwa amepotoka. Hilo mtu anaweza kufanyiwa na rafiki zake na mtu ambaye hakubali kukosolewa na rafiki, basi anastahili sifa za adui.

Kichwa cha habari cha muanzisha mada ni hoja ya mtu aliyemtosa Mwakyembe solely on this gaffe. Wapo ambao wanafikiri wamepata ile ammunition waliyokuwa wanaitafuta kuonesha kuwa Mwakyembe naye si kitu na alichofanya ni bure tu na uonevu. HIvyo kwao hii ni nafasi ya kupata cha kushangilia. Kufurahia kuanguka kwa rafiki, ni ishara ya uadui.

So, sikumaanisha wale wenye kumkosoa rafiki yao, bali wale wenye kumtosha kama adui!
 
Ivi mnajua kama si Mwakyembe Lowasa,Karamagi na Msabaha bado wangekuwa mawazili?
Kevo jifunze kuandika heading hatuuzi magazeti apa kwa kuandika a misleading statement front page!
Kila mtu ana mapungufu na to conceal mambo fulani kwa maslai ya umma ni sula la busara binafsi huwezi ropoka kila kitu kama gazeti la udaku.
Unaweza kuta kati ya izo siri mkuu wa kaya yumo,sasa si unaweza cause a state of commotion?
 
Ni KATIBA yetu ndio inayoendelea kututesa. Ingeweza kututenganishia kikamilifu BUNGE na SERIKALI, kulindiana heshima huku kungepungua sana.
 
Ingawa hapa sio mahali pa Dini, lakini ni lazima tuelimishane pia:-



Mkuu kwa sisi wa-Kristo kumkosoa Yesu ni kumkosoa Mungu, ni absolutely NO kwetu!



Yesu hakuwahi kuharibu hata siku moja, aliyeharibu ni Moses, pale aliamuru kwa hasira maji yapatikane na ndicho kilichompelekea kwenye kutangulia kwenye haki baada tu ya maji kupatikana, lakini Yesu hakuwahi kuharibu kwa sababu utabiri wa manabii uko clear kuwa hakuletwa dunaini kuharibu hata mara moja, Mungu ana sheria moja isiyopingika wala kuekebishika, ukiharibu ni lazima kuwe na malipo, nayo ni kifo, kifo cha Yesu hakikutokana na kuharibu kwake kama unavyodai, ila ilikuwa imeandikwa kuwa atakufa na kufufuka siku ya tatu na ndicho kilichotokea na baadaye atarudi mbinguni, bin-adam wanaoharibu huwa wakifa hawafufuki kama Moses bin-adam aliyeharibu.



Yesu alisema kuwa kama inawezekana Mungu naomba kiepushe kikombe hiki, lakini hakusema niepuishe na kikombe hiki, mkuu kwenye dini yetu tunafundishwa kila siku kuwa shetani ni mjanja sana kwa kugeuza maneno, ndivyo alivyoweza kumdanganya Hawa, Mungu alisema mkila matunda kwa hakika mtakufa, yeye akamwambia Hawa kuwa Mungu alisema tu kuwa mtakufa na kuliahca neno la kwa hakika, here you are na yale yale ya ujanja wa shetani kujaribu kubadili maneno ili utimize dhambi yako, no mkuu we know better!



Pilato alimuambia Yesu kuwa nina nguvu za kuweza kukuokoa na kukuua, Yesu alimuambia kuwa umepewa na Baba yangu, hakusema tumekupa sisi huu ni uongo wa mchana mkuu acha hizi za dini isiyokuwa yako maana ni aibu tupu!



Mwanafunzi wa Yesu, Petro alimkata askari mmoja sikio alipokuja kumkamata Yesu, lakini ni Yesu ndiye aliyemrudishia sikio yule askari na kumpa mikono yake baadaye ili amshike na kumchukua kama neno la Mungu lilivyoandika na kutabiri mapema sana hata kabla Yesu hajazaliwa, sasa kwa nini asikimbie pale alipoona askari anayetaka kumshika amekatwa sikio?

Ni wapi hapo panaposema kuwa Yesu alitaka kuchomoa? Halafu Yesu unamuingizaje kwenye mijadala ya siasa za Mwakyembe na mafisadi, mbona huna heshima kwa dini za wengine mkuu? Hivi kweli unataka tukuwekee hapoa jinsi Mtume Mohamed alivyokuwa akila Nguruwe na kuwakataza waumini wake wasile nyama hiyo tamu ambayo yeye alikuwa akiila kwa siri?

Sasa huyu utamlinganishaje na Mwakyembe, maana wewe ndiye bingwa wa kuchanganya dini na siasa, tuwekee hapa tumkome nyani? Wewe kijana usicheze na dini za watu umeshaonywa sana mambo ya kuleta dini hapa lakini husikii, acha ujinga!
nimemiss jukwaa la dini, we acha tu.
 
Quote:- Kuhani

Hakika.

Tena kwenye kupambana na ufisadi huyu Mwakyembe mimi siwezi kufunga kamba za viatu vyake. Hiyo haina maana, lakini, kwamba hawezi kuchemka.

Ni sawa kabisa kuwa huwezi kufunga kamba za viatu vyake, lakini ifike mahali uweze kufunga kamba angalau za kiongozi wetu mmoja wa taifa, kwa sababu haiwezekani kuwa wote hawafai,

Tizama michango yako kumi ya kwanza ndani ya hii forum, ni kwamba kwa maneno yako Mwalimu ahafai, since than kila kiongozi wa taifa letu aliyetajwa hapa amekuwa hafai, sasa umefika mahali hata Yesu naye hafai, sasa kama that is the case basi ni vyema JF tukafunga the shop, kwa sababu mimi nimezaliwa Tanzania, nimekua na kusoma shule ingawa kidogo Tanzania, mpka leo ni mtu mzima nina mke na watoto ni kutokana na kulelewa in some kind of system ya sheria, jamii na elimu ndio maana leo ninaweza kusimama as a human being nikasema na kueleweka, sasa haiwezekani kuwa leo ile system iliyonilea na kunikuza haifai kabisaaa na viongozi wake wote wa zamani mpaka wa leo hawafai kabisaa, hata mtoto wa Mungu naye hafai kabisaaa ana kasoro, ndugu yangu it is about time sasa ukaichunguza tena elimu uliyonayo ambayo haiwezi hata kukusaidia kuheshimu angalau kidogo viongozi wetu hata wenye uadilifu, kwa sababu haiwezekani tukawaongelea Mkapa na Mwakyembe katika level moja as far as personal ethic conduct is concerned,

Mwakyembe stands ver tall, uklilinganisha na viongozi wetu wengi tulionao katika serikali yetu ya sasa, hasa katika ishu ya ufisadi kwa sababu alichokifanya huenda kisije rudiwa na kiongozi yoyote wa taifa letu kwa miaka mingi sana ijayo, hasa unapoona kina pinda wanasema kuwa Meremeta ni mali ya jeshi. Mwakyembe angekuwa na dhambi kubwa sana hapa iwapo ansingesema wazi to the public kuwa kuna ambayo hakuyasema kwenye riopti yake kwa sababu ya kubanwa na sheria, baadaye wananchi tukaja kugundua wenyewe kuwa kumbe alituchezea, lakini the man amekuwa honest enough wa kusema wazi kuwa bado kuna yaliyofichwa ndani ya ile ripoti kwa sababu ya sheria za kulinda siri za serikali, then sasa ni wajibu wetu as wananchi wenye uchungu na taifa kuilazimisha serikali iruhusu ripoti yote isomwe wazi au kumbana Spika ili avunje kanuni na ripoti yote iwekwe wazi, hili la ripoti yote kutowekwa wazi na Mwakyembe kwa sababu ya sheria za kulinda siri za serikali sio la Mwakyembe, kama mbunge na mwenyekiti wa kamati teule ya bunge, ndipo uwezo wake ulipoishia na tunashukuru amesema wazi,

lakini hatuwezi kumshambulia Mwakyembe, Chenge, Msabaha, Karamagi, Lowassa kama vile wote wamelikosea taifa, hapana Mwakyembe amelisaidia sana taifa letu na hwezi kwuekwa kundi hili la mafisadi, labda Mwakyembe ana mapungufu mengine kiuongozi, basi yawekwe wazi lakini kwenye hili la ripoti na mafisadi, ninasema hapana ninamheshimu kama shujaa wa taifa kwani toka ile siku alipoisoma ile ripoti Tanzania hatutakuwa tena na zile siasa za kizamani za kulindana bila kufichuliwa wazi kwa public.

Ahsante Mkuu, na Mungu AWabariki Viongozi Wetu Waadilifu kama Mwakyembe.
 
Kuhani,


Mkuu, usijaribu kabisa kupindisha hoja yangu na ndio maana nimesema nyie kazi yenu ni kuchukua vipande toka ktk maandishi mkaacha kile kilichotangulia...
Nimetanguliza neno - IT SOUND like!..Na hakuna mahala nimesema Mama ni CCM..acha ujinga mkuu..
Sikatai kabisa mtu ku question Mwakyembe, Slaa au mtu yeyote yule isipokuwa nafuata maelezo yenu na hasa pale mnaposema maneno kama haya - Mwakyembe hutufai Watanzania. It's Cowardice...haya ni matusi ya nguoni na Mafisadi tu ndio wanaweza kufaidika.., hivyo angalieni mnachoandika kwa faida ya wananchi sio mafisadi. Hizi ni shtma ambayo ukweli wake hamna mikonnoni isipokuwa usemi wake mnautumia tena kwa kukisia..
Tofauti na Field Marshall Es, binafsi nachoelewa ni kwamba kuna info ambazo hakupata uhakika toka kwa wahusika ambao walikataa kuhojiwa.. Na kisheria hakuwa na nguvu ya kuwalazimisha pamoja na kwamba fununu hizi zimetoka ktk sehemu nyingi tofauti bila kiapo..
Hivyo sio hakuweza kuuweka kk report ile isipokuwa kama angeweza tu kuwabana Rostam Karamagi, na Mwanasheria mkuu ktk vikao vya bunge hawa jamaa wasingeweza kutoka..Na alikuwa na hakika kabisa kuwa kikao hicho kingempaka Lowassa zaidi. Kama alivyosema katika report yake hawezi kumhusisha Lowassa (waziri mkuu) moja kwa moja kwani hiyo sio kazi yake kutoa judgement...
Sasa baada ya hawa jamaa kusafishwa na baadhi Wabunge imeonekana kwamba Mwakyembe hana ukweli wa kuhusika kwao na kwa bahati mbaya Mwakyembe hawezi kutoa ushahidi aliokuwa nao kama hakuna Bunge halitakubali kusikiliza kesi hii wapate kuwapa kibano hao jamaa.. Hawa jamaa wameisha jiuzuru hawapo tena serikalini lakini bado ni wabunge hivyo kisheria kama kweli wabunge wanataka ukweli uonekane wakubali kuondoa kikwazo hicho.... mwongo atajulikana.
Mwakyembe hawezi kuwa mjinga kuingiza vitu ovyo ktk report ambavyo havina uhakika na ni fununu tupu..Na kama mnakumbuka hata Dr. Slaa alipoingiza ile list ya Mafia kina Patel alionekana muongo ku base argument yake ktk report za Mtandaoni hali zilikuwa kweli tupu..Kisheria kuina vikwazo bungeni na huwezi kuviruka..Dr. Slaa alikuwa na ukweli wa mengi kuhusiana na kundi hilo lakini hakusema yote siku ile.. Na nimesema hata Zitto anajua mengi kuhusiana na Buswagi hata kabla ya kuwepo ktk kamati lakini kisheria kama hakupata kuwahoji kina Sinclair hawezi kabisa kumhusisha mathlan Kikwete anahusika.. hata kama kuna report za juu juu ambazo zinamhusisha rais wake.. kisheria hawezi kumtosa rais direct isipokuwa kwa kikao maalum..
Ndivyo nilivyoelewa mimi.....

Note kuwa hapa kulikuwa na thread mbili zenye mantiki moja na zimeunganishwa. Kama naongopa mamods walizwe. tatizo lenu ni kwamba watu ambao mna interests nao hamtaki waguswe kabisaaa. This is stereotype business na MWAKYEMBE kachemsha big time hapa hakuna uCCM wala uCHADEMA. Kuna tofauti kubwa kati ya kumtosa mtu na kumkosoa, UKIONA RAFIKI YAKO ANAKUFAGILIA TUUUU; MUOGOPE. HUYO SI RAFIKI WA KWELI NI MNAFIKI MKUBWA kwa sababu anakuacha uendelee kufanya madudu huku anakushangilia mwisho wa siku unatoka nje ya mstari kabisa.


Kiongozi shujaa hawezi kutamka hadharani na kusema najua mengi lakini siyasemi!kama hutaki kusema kaa kimya kuliko kutishia nyau.
 
It is obvious that Dr. Mwakyembe has done a great job of more signicance than most of us can hope to achieve, he is a hero of the anti-ufisadi movement.

Ahsante sana kwa hili mkuu,

That said, even heroes make mistakes.

Ndio hasa tunachosema kuwa kama kweli Mwakyembe ana makosa, labda kwenye ishu zingine za uongozi wake, lakini sio kwenye hiili la ripoti yake kwa bunge hapana,

kubanwa na sheria za serikali na kuomba zivunjwe na Spika ili aweze kusema yote ya ufisadi, sio a mistake of a hero in fact huo ndio hasa ushujaa wa Mwakyembe, kama kuna mengine maovu ya uongozi wa Mwakyembe yapo yawekwe, lakini kwenye hili la ripoti tatizo ni sheria zetu na mpungufu yake sio Mwakyembe as a person au as kiongozi.
 
Kiongozi shujaa hawezi kutamka hadharani na kusema najua mengi lakini siyasemi!kama hutaki kusema kaa kimya kuliko kutishia nyau.

Mkuu hii statement yako haiko sawa ni misleading of facts, Mwakyembe amemuomba Spika avunje kanuni ili aweze kuiweka ripoti yote hadharani ya ufisadi wa Lowassa na wenziwe,

kwa hiyo kauli yako sio kweli kabisaa ni mis-leading either ni kwa makusudi on your part au kwa kutokuelewa!
 
uadilifu wake umepungua pale aliposema kuna mengine kayamezea. Kwa nini kayamezea, mwadilifu na shujaa wa wananchi hawezi kuficha siri ya adui wa wananchi (mafisadi serikalini). Kwa hili uadilifu wake utakuwa kwenye alama ya kuuliza hadi pale atakapoyasema hayo ambayo hajayasema.

Mkjj kuna sehemu amesema kwenye moja ya post zake kuhusu kupima matokeo ya kile unachotaka kusema / kufanya: kitakuwa na manufaa yoyote ukikisema / ukikifanya??

Kwa hili tumpe benefit of doubt Mwakyembe kwa sababu kamati nzima waliweigh nakuona labda kwa kusema yote waliyoyakuta ripoti yao ingeweza kuwekwa kapuni na isione mwanga wa jua tena.
 
Mkuu hii statement yako haiko sawa ni misleading of facts, Mwakyembe amemuomba Spika avunje kanuni ili aweze kuiweka ripoti yote hadharani ya ufisadi wa Lowassa na wenziwe,

kwa hiyo kauli yako sio kweli kabisaa ni mis-leading either ni kwa makusudi on your part au kwa kutokuelewa!

kwa mara ya pili naomba usinirifae mkuu, sitaki makuu kwa sifa za kijinga! onyesha kuniheshimu au kutokuniheshimu hakuondoi dignity yangu. Let refer mi plainly, ukishindwa kabisa basi sena mwanamama.

Hiyo bold hapo inajibu paragraph yako ya pili. Siwezi kuburuzwa kwa kitu ambacho kiko loud open. Twist kivingine.
 
Mkjj kuna sehemu amesema kwenye moja ya post zake kuhusu kupima matokeo ya kile unachotaka kusema / kufanya: kitakuwa na manufaa yoyote ukikisema / ukikifanya??

Kwa hili tumpe benefit of doubt Mwakyembe kwa sababu kamati nzima waliweigh nakuona labda kwa kusema yote waliyoyakuta ripoti yao ingeweza kuwekwa kapuni na isione mwanga wa jua tena.

Binafsi, naona haiingii akili kumtetea mtu shujaa, wakati hakua open to the most. Nakubali kumpa benefit of doubt, ila watetezi wake wasing'ang'anize eti ni shujaa per se na kuwa si halali kumkosoa implying ukimkosoa unamtosa!
 
kwa mara ya pili naomba usinirifae mkuu, sitaki makuu kwa sifa za kijinga! onyesha kuniheshimu au kutokuniheshimu hakuondoi dignity yangu. Let refer mi plainly, ukishindwa kabisa basi sena mwanamama.

Hiyo bold hapo inajibu paragraph yako ya pili. Siwezi kuburuzwa kwa kitu ambacho kiko loud open. Twist kivingine.[/
QUOTE]

Whatever this means, mkuu my point ni kwamba Mwakyembe kwa kudai sheria ya bunge ivunjwe na Spika, ili aweze kuanika uozo wote wa mafisadi hadharani haiwezi kuwa a mistake of a hero, ila ni ushujaa zaidi on his part as a leader,

hatuburuzani ila tunaelimishana na hatutachoka hata siku moja kwenye hili kwa sbabu ndio hasa sababu ya kuwepo hapa, sio kumtukana tu kila kiongozi wa taifa hapana!
 
Whatever this means, mkuu my point ni kwamba Mwakyembe kwa kudai sheria ya bunge ivunjwe na Spika, ili aweze kuanika uozo wote wa mafisadi hadharani haiwezi kuwa a mistake of a hero, ila ni ushujaa zaidi on his part as a leader,

hatuburuzani ila tunaelimishana na hatutachoka hata siku moja kwenye hili kwa sbabu ndio hasa sababu ya kuwepo hapa, sio kumtukana tu kila kiongozi wa taifa hapana!

For the third time nakuomba usiniite mkuu, mkuu ni wewe mzee wa dataz ili kuona unaheshimiwa kwazo.

Nashukuru sana kwa kukubali kuwa hakusema yote. On top of that your hero does not say all - your hero ni muoga. So the type of your hero is not mine, unless i miss the meaning of the word hero.

Kimasai ukamdunga simba na mkiku halafu akakimbia na usimwone tena wewe sio shujaa, shujaa ni yule anayeleta ukucha wa simba kumaanisha amemuua na akahakikisha kuwa kafa. Kwangu huyu pia ndiye shujaa, sio shujaa nusu nusu.

Kwangu huyu ni mtu (mwakyembe) anatimiza wajibu wake kazini, analipwa kwa kuwa bungeni na amelipwa kwa kukaa kama kamati. So he has to be responsible kwa chochote kile hata kuficha ukweli, amemess step kwani hakutimiza wajibu wake efficiently, he did it in pieces.

In the sense of kutukana labda Rais Kikwete ndio hajatukanwa kwenye hii forum, lakini mbunge wa kyela katukanwa sana.
 
Back
Top Bottom