Mag3
Hakuna cha umbumbumbu. Anachosema Mwakyembe ni kwamba bunge litengue kanuni zake ili huu mjadala ambao yeye anadhani ulishamalizika, urudiwe upya. Kuna kundi la mafisadi bungeni wanataka kujisafisha kwa kumlaumu Mwakyembe.Sasa yeye anachosema ni kuwa kwa mujibu wa kanuni za bunge ule mjadala wa Richmond umeshamalizika. Lakini kama kuna wabunge wanadhani bado kuna mambo ya kujadiliwa, basi waombe kanuni zitenguliwe na mjadala uanze upya na yeye atakuja na vibwagizo vipya. Simple as that. I hope umeelewa.
Jasusi,
Nashukuru na nimeelewa ila post zingine humu ndani zinachanganya ati lol
Kuhani
Mkuu, usijaribu kabisa kupindisha hoja yangu na ndio maana nimesema nyie kazi yenu ni kuchukua vipande toka ktk maandishi mkaacha kile kilichotangulia...
Nimetanguliza neno - IT SOUND like!..Na hakuna mahala nimesema Mama ni CCM..acha ujinga mkuu..
...Mama samahani lakini pamoja na kwamba unaonesha uchungu kwa nchi yetu lakini kidogo inanipa shida sana.. Uchungu wako ni ktk kuwapamba Mafisadi na kumfanya Mwakyembe mnafiki, mwongo hivyo report yake yote haina Ukweli...
To me it sound like His testimony has come under attack -He lied under oath, he should not be trusted..So the the convictions he helped must be overturned!..
Only Fisadis would love this!....
Hivi Sasa Tukishakubali Mwakyembe Ni Fisadi..whats Next?
don't put yourself down like that... Mwakyembe anajibu simu zake hata kama hajui nani anampigia, nenda kwenye tovuti ya Bunge na umpigie. Hoja mliyonayo ni ya msingi sana, lakini inatosha kumtosa mtu na kusema "hatufai"? I'm a realist, ukinipa uchaguzi wa Chitalilo na Mwakyembe kwenye kuongoza Kamati.. nitamchagua Mwakyembe! No sir, hatuwaachi mashujaa kwa kosa la kauli moja tena baada ya maneno na matendo ya kishujaa.
Nyinyi ambao viongozi kwenu hawakosei na wakikosea hata kwa kujing'ata ulimi tu basi wanatoshwa! Kuna vitu ambavyo tunaweza kutafuta kumhukumu Mwakyembe kwavyo, lakini la kauli hii tufike mahali tumtose tu ili tujithibitishie haki zetu wenyewe, ya kuwa ni jinsi gani sisi ni bora, watu ambao hatujawahi kuwa kwenye position kama hiyo ya kwake, kusimama na kusema yote aliyoyasema, halafu just like that tuyafute hayo yote kwa senteni moja! No sir!
Ni haki yenu kumtosa, na wengine haki yetu kumpa nafasi ya kutengeneza, kufafanua, au hata kufuta usemi wake! Kuna wakati rafiki anakosea tena vibaya, lakini kama kila rafiki akikosea anatoswa tena kosa la ulimi, basi wengi tusingekuwa na marafiki.
No sir, bado sijaona sababu ya kumtosa Mwakyembe sasa!!
nimemiss jukwaa la dini, we acha tu.Ingawa hapa sio mahali pa Dini, lakini ni lazima tuelimishane pia:-
Mkuu kwa sisi wa-Kristo kumkosoa Yesu ni kumkosoa Mungu, ni absolutely NO kwetu!
Yesu hakuwahi kuharibu hata siku moja, aliyeharibu ni Moses, pale aliamuru kwa hasira maji yapatikane na ndicho kilichompelekea kwenye kutangulia kwenye haki baada tu ya maji kupatikana, lakini Yesu hakuwahi kuharibu kwa sababu utabiri wa manabii uko clear kuwa hakuletwa dunaini kuharibu hata mara moja, Mungu ana sheria moja isiyopingika wala kuekebishika, ukiharibu ni lazima kuwe na malipo, nayo ni kifo, kifo cha Yesu hakikutokana na kuharibu kwake kama unavyodai, ila ilikuwa imeandikwa kuwa atakufa na kufufuka siku ya tatu na ndicho kilichotokea na baadaye atarudi mbinguni, bin-adam wanaoharibu huwa wakifa hawafufuki kama Moses bin-adam aliyeharibu.
Yesu alisema kuwa kama inawezekana Mungu naomba kiepushe kikombe hiki, lakini hakusema niepuishe na kikombe hiki, mkuu kwenye dini yetu tunafundishwa kila siku kuwa shetani ni mjanja sana kwa kugeuza maneno, ndivyo alivyoweza kumdanganya Hawa, Mungu alisema mkila matunda kwa hakika mtakufa, yeye akamwambia Hawa kuwa Mungu alisema tu kuwa mtakufa na kuliahca neno la kwa hakika, here you are na yale yale ya ujanja wa shetani kujaribu kubadili maneno ili utimize dhambi yako, no mkuu we know better!
Pilato alimuambia Yesu kuwa nina nguvu za kuweza kukuokoa na kukuua, Yesu alimuambia kuwa umepewa na Baba yangu, hakusema tumekupa sisi huu ni uongo wa mchana mkuu acha hizi za dini isiyokuwa yako maana ni aibu tupu!
Mwanafunzi wa Yesu, Petro alimkata askari mmoja sikio alipokuja kumkamata Yesu, lakini ni Yesu ndiye aliyemrudishia sikio yule askari na kumpa mikono yake baadaye ili amshike na kumchukua kama neno la Mungu lilivyoandika na kutabiri mapema sana hata kabla Yesu hajazaliwa, sasa kwa nini asikimbie pale alipoona askari anayetaka kumshika amekatwa sikio?
Ni wapi hapo panaposema kuwa Yesu alitaka kuchomoa? Halafu Yesu unamuingizaje kwenye mijadala ya siasa za Mwakyembe na mafisadi, mbona huna heshima kwa dini za wengine mkuu? Hivi kweli unataka tukuwekee hapoa jinsi Mtume Mohamed alivyokuwa akila Nguruwe na kuwakataza waumini wake wasile nyama hiyo tamu ambayo yeye alikuwa akiila kwa siri?
Sasa huyu utamlinganishaje na Mwakyembe, maana wewe ndiye bingwa wa kuchanganya dini na siasa, tuwekee hapa tumkome nyani? Wewe kijana usicheze na dini za watu umeshaonywa sana mambo ya kuleta dini hapa lakini husikii, acha ujinga!
i Was Just Airing Out My Opinion On What I Thought He Was Very Much Mistaken.
Quote:- Kuhani
Hakika.
Tena kwenye kupambana na ufisadi huyu Mwakyembe mimi siwezi kufunga kamba za viatu vyake. Hiyo haina maana, lakini, kwamba hawezi kuchemka.
Kuhani,
Mkuu, usijaribu kabisa kupindisha hoja yangu na ndio maana nimesema nyie kazi yenu ni kuchukua vipande toka ktk maandishi mkaacha kile kilichotangulia...
Nimetanguliza neno - IT SOUND like!..Na hakuna mahala nimesema Mama ni CCM..acha ujinga mkuu..
Sikatai kabisa mtu ku question Mwakyembe, Slaa au mtu yeyote yule isipokuwa nafuata maelezo yenu na hasa pale mnaposema maneno kama haya - Mwakyembe hutufai Watanzania. It's Cowardice...haya ni matusi ya nguoni na Mafisadi tu ndio wanaweza kufaidika.., hivyo angalieni mnachoandika kwa faida ya wananchi sio mafisadi. Hizi ni shtma ambayo ukweli wake hamna mikonnoni isipokuwa usemi wake mnautumia tena kwa kukisia..
Tofauti na Field Marshall Es, binafsi nachoelewa ni kwamba kuna info ambazo hakupata uhakika toka kwa wahusika ambao walikataa kuhojiwa.. Na kisheria hakuwa na nguvu ya kuwalazimisha pamoja na kwamba fununu hizi zimetoka ktk sehemu nyingi tofauti bila kiapo..
Hivyo sio hakuweza kuuweka kk report ile isipokuwa kama angeweza tu kuwabana Rostam Karamagi, na Mwanasheria mkuu ktk vikao vya bunge hawa jamaa wasingeweza kutoka..Na alikuwa na hakika kabisa kuwa kikao hicho kingempaka Lowassa zaidi. Kama alivyosema katika report yake hawezi kumhusisha Lowassa (waziri mkuu) moja kwa moja kwani hiyo sio kazi yake kutoa judgement...
Sasa baada ya hawa jamaa kusafishwa na baadhi Wabunge imeonekana kwamba Mwakyembe hana ukweli wa kuhusika kwao na kwa bahati mbaya Mwakyembe hawezi kutoa ushahidi aliokuwa nao kama hakuna Bunge halitakubali kusikiliza kesi hii wapate kuwapa kibano hao jamaa.. Hawa jamaa wameisha jiuzuru hawapo tena serikalini lakini bado ni wabunge hivyo kisheria kama kweli wabunge wanataka ukweli uonekane wakubali kuondoa kikwazo hicho.... mwongo atajulikana.
Mwakyembe hawezi kuwa mjinga kuingiza vitu ovyo ktk report ambavyo havina uhakika na ni fununu tupu..Na kama mnakumbuka hata Dr. Slaa alipoingiza ile list ya Mafia kina Patel alionekana muongo ku base argument yake ktk report za Mtandaoni hali zilikuwa kweli tupu..Kisheria kuina vikwazo bungeni na huwezi kuviruka..Dr. Slaa alikuwa na ukweli wa mengi kuhusiana na kundi hilo lakini hakusema yote siku ile.. Na nimesema hata Zitto anajua mengi kuhusiana na Buswagi hata kabla ya kuwepo ktk kamati lakini kisheria kama hakupata kuwahoji kina Sinclair hawezi kabisa kumhusisha mathlan Kikwete anahusika.. hata kama kuna report za juu juu ambazo zinamhusisha rais wake.. kisheria hawezi kumtosa rais direct isipokuwa kwa kikao maalum..
Ndivyo nilivyoelewa mimi.....
It is obvious that Dr. Mwakyembe has done a great job of more signicance than most of us can hope to achieve, he is a hero of the anti-ufisadi movement.
That said, even heroes make mistakes.
Kiongozi shujaa hawezi kutamka hadharani na kusema najua mengi lakini siyasemi!kama hutaki kusema kaa kimya kuliko kutishia nyau.
uadilifu wake umepungua pale aliposema kuna mengine kayamezea. Kwa nini kayamezea, mwadilifu na shujaa wa wananchi hawezi kuficha siri ya adui wa wananchi (mafisadi serikalini). Kwa hili uadilifu wake utakuwa kwenye alama ya kuuliza hadi pale atakapoyasema hayo ambayo hajayasema.
Mkuu hii statement yako haiko sawa ni misleading of facts, Mwakyembe amemuomba Spika avunje kanuni ili aweze kuiweka ripoti yote hadharani ya ufisadi wa Lowassa na wenziwe,
kwa hiyo kauli yako sio kweli kabisaa ni mis-leading either ni kwa makusudi on your part au kwa kutokuelewa!
Mkjj kuna sehemu amesema kwenye moja ya post zake kuhusu kupima matokeo ya kile unachotaka kusema / kufanya: kitakuwa na manufaa yoyote ukikisema / ukikifanya??
Kwa hili tumpe benefit of doubt Mwakyembe kwa sababu kamati nzima waliweigh nakuona labda kwa kusema yote waliyoyakuta ripoti yao ingeweza kuwekwa kapuni na isione mwanga wa jua tena.
kwa mara ya pili naomba usinirifae mkuu, sitaki makuu kwa sifa za kijinga! onyesha kuniheshimu au kutokuniheshimu hakuondoi dignity yangu. Let refer mi plainly, ukishindwa kabisa basi sena mwanamama.
Hiyo bold hapo inajibu paragraph yako ya pili. Siwezi kuburuzwa kwa kitu ambacho kiko loud open. Twist kivingine.[/QUOTE]
Whatever this means, mkuu my point ni kwamba Mwakyembe kwa kudai sheria ya bunge ivunjwe na Spika, ili aweze kuanika uozo wote wa mafisadi hadharani haiwezi kuwa a mistake of a hero, ila ni ushujaa zaidi on his part as a leader,
hatuburuzani ila tunaelimishana na hatutachoka hata siku moja kwenye hili kwa sbabu ndio hasa sababu ya kuwepo hapa, sio kumtukana tu kila kiongozi wa taifa hapana!
Whatever this means, mkuu my point ni kwamba Mwakyembe kwa kudai sheria ya bunge ivunjwe na Spika, ili aweze kuanika uozo wote wa mafisadi hadharani haiwezi kuwa a mistake of a hero, ila ni ushujaa zaidi on his part as a leader,
hatuburuzani ila tunaelimishana na hatutachoka hata siku moja kwenye hili kwa sbabu ndio hasa sababu ya kuwepo hapa, sio kumtukana tu kila kiongozi wa taifa hapana!
For the third time nakuomba usiniite mkuu, mkuu ni wewe mzee wa dataz ili kuona unaheshimiwa kwazo.
Nashukuru sana kwa kukubali kuwa hakusema yote. On top of that your hero does not say all - your hero ni muoga. So the type of your hero is not mine, unless i miss the meaning of the word hero.
Kimasai ukamdunga simba na mkiku halafu akakimbia na usimwone tena wewe sio shujaa, shujaa ni yule anayeleta ukucha wa simba kumaanisha amemuua na akahakikisha kuwa kafa. Kwangu huyu pia ndiye shujaa, sio shujaa nusu nusu.
Kwangu huyu ni mtu (mwakyembe) anatimiza wajibu wake kazini, analipwa kwa kuwa bungeni na amelipwa kwa kukaa kama kamati. So he has to be responsible kwa chochote kile hata kuficha ukweli, amemess step kwani hakutimiza wajibu wake efficiently, he did it in pieces.
In the sense of kutukana labda Rais Kikwete ndio hajatukanwa kwenye hii forum, lakini mbunge wa kyela katukanwa sana.