Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Huyu anayesema MWAKYEMBE HATUFAI TANZANIA ANADHANI ANAZUNGUMZIA KITOWEO?
Ili sasa tusome kimeoza na hakifai?
Hizi ni pumba!
Huyo nayefaa niwekeeni hapa na mimi niseme something.
Nyie mna nia mbaya....!Kwasababu nia yenu ni ya kisiasa tu!
Sisi tunataka ripoti zisomwe..Nyie mnalia na majina tuu!
Ripoti ya MWAKYEMBE NI ILE ILE!
Na huyo anayetaka kujisafisha...AISOME YEYE UPYA...NA KILA MBUNGE AISOME...NA SISI WANANCHI TUISOME..THEN TUTAJUA NANI NI NANI NA KWANINI.
Haya mambo ya kupiga kelele si mazuri hayana nia nzuri ya kuwapa wananchi ukweli...Ukweli kwamba...Hakukuwa na muda wa kutosha kusoma ripoti yote yenye kurasa elfu.
Ni waambia jana kuwa...Ripoti ni just summerization ya majumuisho ya yale yaliyotokea...Hiyo ni ya kisiasa...RIPOTI HALISI YA WAZALENDO NI...RIPOTI ZA KAGUZI...ama zile content zitakazotumika kisheria
Hao waliotajwa kwenye ripoti ndio wa kuanza nao...Watajitetea mahakamani!
Summerization zaweza kuwa different...
Kwani wazee hamjawahi kuandika essays tofauti kutoka kwenye kitabu kimoja CHENYE ONE THESIS?
 
KUDOS!!
Lakini nenda ado ado kwa Mh. Mwakyembe basi, funika kombe mwanaharamu apite! Tusijewapa mafisadi nafasi ya kupumulia, we need to suffocate them now by any means!

say what again?
 
Nauliza...can One Book With One Thesis Have Different Essays?
 
Mama na wenzio,
Nyie WAKUU vipi? Nimesoma hadi mwisho naona nyie mko katika moja ya haya au hata kuchanganya baadhi " Wabishi, Hamuambiliki, Wakorofi, Mnalenu jambo, Mwataka watu waseme Ni kikwete alifichwa, au ....." Sijui katika helu kweli nyie mko wapi. Mmeambiwa kuwa riport ilikuwa na karatasi zaidi ya elfu 1 na akapewa saa 1.5. Sasa kwa mtu mwenye akili zake toauti na zangu na zako, alitumia huo muda kusoma yale muhimu tu na kuacha kwenda detail. Unaweza kukuta hizo more detail na kuonyesha tu jinsi Lowassa livyoshiriki. Mtu mwenye akili zake alitumia huo muda na matokeo waziri mkuu na wengine huko wakaachia ngazi. Mengine ingawa yalikuwemo kwenye riport HAKUYASOMA/HAKUYASEMA. Si kwamba hayamo. Sasa huoni hili swala unatakiwa umpelekee spika? Mtu kawaambia Mdomo huo, nyie bado mwalia "mbona hukutuambia pua iko wapi? Wee mtu umeficha habari muhimu sana ....... " Jaribu kutumia hisia tano mlizopewa na Mungu. Hapa huhitaji kutumia ile ya sita.
Ila tatizo ni kuwa NYIE WATU hata mueleweshwe vipi ni au HAMTAKI kuelewa au MILELE HAMTAELEWA. Wakuu kila la kheri. Ehhh, mama kabla hujajibu, PUMUA KWANZA na ukiweza pata maji utulize donge la koo. Nothing personal. Naingia mitini kukikmbia scud maana hizo zaja.... hihiii massage sent.
 
Toka jana nilkuwa nawaambia wako off track wakawa wanabisha hadi wanakwenda personal.
 
One Book=ripoti
Thesis=contents Zitakazotumika Kisheria.
Essays=summerization Za Ripoti..haziwezi Kuzungumzia The Whole Book(ripoti)
Get It?
 


he he heeeee, kwi kwi kwi kwi: You made my day, L.O.L
 
Ndugu wa JF,

Duniani popote hata huko kwa wenzetu waliotangulia katika uwazi na demokrasia daima mambo yanayoitwa confidential kwa ajili ya usalama wa taifa/kuinusuru serikali hayakosekani. kama kuna mtu anabisha basi ataamua kubisha. Vivyo hivyo hata ndani ya familia kuna mambo watu hawataruhusu yaanikwe hadharani.

Na ndiyo maana wazee wenye busara watajaribu kupatanisha wanandoa lakini mwisho wa yote huweka nafasi wao wenyewe kuelewana kwani wanajua kuna mambo yanayo wahusu ambayo hawatapenda kuyaweka hadharani.

La muhimu ni uamuzi walioutoa uliyopelekea kujiuzuru kwa mawaziri na serikali kukiri uhuni uliyotumika kuweka mkataba wa Richmund. na bila shaka viongozi wahusika na waliojiuzuru wanajua ukweli, ila wanajaribu kutikisa kiberiti wakidhani wenzao watakuwa waoga kusema hata yale ambayo hayakuandikwa na kusomwa bungeni. Na jaribu kufuatilia baada ya mkwala wa mwakyembe na wajumbe wengine kama akina Lowasa na wenzake wataendelea kuleta fyokofyoko zao kwani wamejua kuwa watu wengine hawatishiwi nyau.
 

OMG! At last someone has just made my day! Thank you Sikonge, and I'm off.
 


Kitila... ni kazi gani ya mwanadamu inayoweza kufanywa kwa ukamilifu wa asilimia mia moja? Ni document gani ya mipango ambayo imeandaliwa na mwanadamu ambayo haikuwa na makosa, ya lugha, mfumo, mchakato, n.k? Show me one, and I'll show 100 that do!

Sijui ni kwa misingi gani watu walitarajia kuwa ripoti ya Mwakyembe iseme yote na hapa yote ina maana "yote"! kuhusiana na suala la Richmond. Kwanza kimantiki tu isingewezekana, lakini pia ni kwa sababu walioandaa ni wanadamu na wanafungwa na muda na vizuizi vingine. Kamati ilikatazwa na Spika kuangalia suala la Dowans na wakatakiwa wawe focused kwenye Richmond, sasa kama waligundua kitu kuhusu Dowans wangekiweka kwenye ripoti au la?

Katika ulimwengu ambapo magari hayazimiki, maji hayatoi mvuke, na mabaya hayatokei ripoti ya Mwakyembe ilitakiwa iwe kamilifu to the dot for in such a world imperfections hakuna. Bahati mbaya tunaishi katika ulimwengu wetu, ulimwengu ambapo mazuri na mabaya hutokea, na kidogo na mengi huwepo. Katika ulimwengu huu watu hufanya kile wanachoweza kufanya kwa nguvu na uwezo wao wote na wakati mwingine hukosea tena hukosea sana.

Katika ulimwengu huu wa kwetu, wana ujasiri wale wawahukumuo watu kwa ukali kiasi kwamba wako tayari kuwaruka na kuwatosa kwa sababu ya kutokuwa wakamilifu.

Mojawapo wa ripoti zilizofanyiwa uchunguzi wa kina sana ni ripoti ya Warren juu ya Kifo cha aliyekuwa Rais wa Marekani J.F Kennedy. Ni ripoti iliyoenda deep and wider than most reports that were later commissioned on various issues. Pamoja na yote hayo, kuna watu ambao bado hawaikubali ripoti ile jinsi ilivyo na hawakuridhika na utendaji wa hiyo commission. Wanaamini kuna mambo ambayo tume hiyo haikuyachunguza kwa kina au haikutoa maelezo ya kutosha. Well that is the nature of things.

Bado sijaona sababu ya kumtosa Mwakyembe simply kwa sababu sasa hivi naweza kuona mapungufu ya aina fulani katika utendaji kazi wa ripoti. Being a realist that I am, I recognize the limitations of man born of a woman. Kwangu mimi nampa nafasi mtu anayejitahidi kufanya the best anachoweza, akiwa mkweli, na muwazi katika hicho anachofanya. Wakati mwingine timu inaweza ikacheza kwa kujituma na kushambulia kuliko ile timu nyingine na mwisho wa gamu unaweza kusema "ndiyo kufunga wametufunga lakini chenga tumewala!".


Je ripoti ingeweza kuboreshwa zaidi? absolutely! Je kuna mambo ambayo walipaswa kuyaweka lakini hawakuyaweka? you betcha! Je kutokana na mapungufu hayo ripoti hiyo ilikuwa ni mbovu kabisa na Mwakyembe na character yake questionable, emphatic no!
 
MKJJ: Hakuna hata mahala ninapodai perfectionism kwenye report ya Mwakyembe. Nilichofanya mimi ni ku-point out clear flaws kwenye report ya Mwakyembe ambazo zinadhaifisha yote aliyokwisha kutueleza na yaliyomfanya aonekane ni hero. Flaws zenyewe ni hizi (narudia tena):

a) kushindwa kumhoji Lowasa huku akiwa ndiye mtuhumiwa mkuu wa ule mchezo mchafu juu ya Richmond-hii sitaki kueileza tena maana nimeshaieleza sana huko nyuma.

b) Kauli yake ya kuomba kibali cha spika ili amwage yale ambayo hakuyasema kwenye report yake ya awali. Hili la pili ni tatizo kubwa zaidi unless umesahau malalamiko ya Lowasa. Nikukumbushe kwamba moja ya tuhuma za Lowasa kwa Mwakyembe ni kwamba kamati iliandaa report mbili. Lowasa alidai kwamba katika report ambayo haikuwasilishwa hakutajwa kabisa kuhusika katika saga la Richomond lakini kwa shinikizo la spika, na kwa sababu za kisiasa na kigomvi zilizopo kati ya spika na Lowasa, akashinikizwa afanye mbinu ili Lowasa atiwe hatiani-hii ndiyo ikazaa report ya pili iliyowasilishwa bungeni. Unakumbuka haya au nawe unajifanya unayafumbia macho? Sasa kwa kauli yake Mwakyembe ameiimarisha madai ya Lowasa-hasa kwamba kulikuwa na report mbili na kwamba kamati ya Mwakyembe ilifanya kazi kwa lengo la kubomoa baadhi ya watu na kuwajenga wengine kisiasa na haikuwa na nia ya dhati ya kutafuta matatizo na majawabu kuhusu Richmond. Sasa you can't call these serious matters kwamba ni makosa ya kawaida katika report.

My friend, anachotakiwa kushukuru Mwakyembe ni kwamba sasa hivi watu wapo obsessed na matatizo ya ufisadi. Otherwise hii hoja yake ingeifanya ile report yake nzima iwe null and void na ingebidi awaombe msamaha wote aliwatuhumu na mchezo ungeanza upya!


Baada ya kusema yote haya mimi sitilii shaka "ushujaa" na uimara wa Mwakyembe. Hata hivyo, najua kwamba Mwakyembe hufanya makosa, tena makosa mengine ni ya kutisha, likwemo hili la juzi na lile la kukubali kutumika kutetea mauaji ya wananchi yaliyofanywa na polisi huko Zanzibar Januari 2001!!! Sasa tusipoyaona haya makosa hatumsaidii huyu shujaa wetu ili atuongoze vizuri katika mapambano tuliyo nayo!!
 

Ahsante sana Kitilya. Maelezo yako ni ya kituo na yako murua kabisa.
 
..off course ripoti ya Mwakyembe siyo perfect kwasababu ni kazi ya wanadamu.

..tatizo ni kwamba Mwakyembe ametamka mwenyewe kwamba kuna mambo hakuyasema/ameyaficha ili kulinda heshima ya nchi.

..kitendo hicho kinazua maswali mengi, lakini kwa hakika ni kitu ambacho kimefanywa kwa MAKUSUDI, kwa KUDHAMIRIA.

..wale mashahidi walioitwa mbele ya tume walikula kiapo kusema ukweli, kweli tupu[nothing but the truth]. sasa kama kuna mambo yamefichwa na Mwakyembe maana yake ni kwamba ripoti hiyo ni nusu-ukweli, labda theluthi-ukweli, labda robo-ukweli, etc etc.

..i would have cut Dr.Mwakyembe some slack if he had humanely erred in the conclusions of his findings or in the interpretation of the facts and evidence he had collected.

..Dr.Mwakyembe ameficha nini? je kuna mashujaa ambao hakuwataja? je ameficha mafisadi? je ameficha hujuma dhidi yetu? ni kitu gani hicho amekificha na kwa manufaa ya nani?
 

Huyu Mwakyembe naye karibia ataitwa fisadi hapa. Lowasa aliapa kupambana na Mwakyembe, Chenge alifikia uamuzi wa kuweka uchawi kwenye kiti cha Mwakyembe na sasa naona yanatimia. Kumchafua Mwakyembe ili kila mtu aonekane mchafu.
 

Mwanzo mzuri:


a) kushindwa kumhoji Lowasa huku akiwa ndiye mtuhumiwa mkuu wa ule mchezo mchafu juu ya Richmond-hii sitaki kueileza tena maana nimeshaieleza sana huko nyuma.

Hili ni kosa la kuangalia suala hili. Kamati ya Mwakyembe haikupewa jukumu la kumchunguza Lowassa, na katika hadidu rejea Lowassa hakutajwa kama target ya investigation. Kuwa "mtuhumiwa mkuu" yawezekana mbele ya vyombo vya habari na raia lakini si katika maagizo ya Bunge. Kukumbusha tu Kamati Teule ya Mwakyembe iliunda na kupewa majukumu yafuatayo:


Katika hadidu rejea, Waziri Mkuu Lowassa au Ofisi yake were not the target of the investigation. The target was Richmond. Hapa utaona kwa mbali kwanini Waziri Mkuu hakuhojiwa kama "mtuhumiwa mkubwa". He was not the target.

As a matter of fact, report nzima ya Kamati Teule inataja jina la Lowassa mara moja tu. Pale inaponukuu hii barua.


Utaona kuwa hapa kilichozungumzwa ni fact, kuna barua iliyoelekezwa kwa Waziri Mkuu iliyosema hivi na vile. Hii haimfanyi Lowassa kuwa mtuhumiwa "Mkubwa".

Lakini utaona kuwa cheo cha Waziri Mkuu kinatajwa mara thelathini ndani ya ripoti hiyo. Why? Ni kwa sababu katika mchakato mzima wa richmond Ofisi ya Waziri Mkuu ilikuwa inahusika. Ni kwa sababu hiyo mwishoni mwa ripoti hiyo Kamati ikapendekeza hivi:


Ni yeye Waziri Mkuu ambaye alipewa nafasi ya kujitetea kwenye Bunge akashindwa. Ni yeye ambaye kwa hiari yake mwenyewe aliamua kujiuzulu bila hata kumtaarifu Rais kwanza na kubwaga "manyanga" Bungeni siku ile ya kukumbukwa. Lowassa angetaka kujitetea na kuelezea upande wake alikuwa na nafasi hakuitumia. Yeye hakuwa target ya investigation lakini alionekana kuhusika na ndio maana nafasi ya yeye kujitetea ilikuwepo na alikuwa na nafasi ya kuelezea upande wake. Kujiuzulu kwa Lowassa si kosa la Mwakyembe! kujiuzulu kwa Msabaha na Karamagi si makosa ya Kamati Teule, kama waliona hawakutendewa haki walipewa jukwaa la kujitetea wakagwaya! Mzigo huo wanaubebea wao na wao peke yao.


sehemu ya jibu langu kuhusu Lowassa bado inasimama. Lowassa hakuwa part ya ripoti alijuaje zimeandaliwa ripoti mbili, moja ikimtaja na nyingine isiyomtaja? Ni yeye alikuwa na jukumu la kuionesha hiyo ripoti nyingine alipopewa nafasi. Hadi leo hii hiyo ripoti nyingine mbona haijatolewa mahali popote pale.

Ni kwa sababu hiyo, Mwakyembe katoa hoja itenguliwe kanuni ya Bunge ili kina Lowassa na hiyo "ripoti nyingine" watoe walichonacho, na wao kina Mwakyembe waelezee hiyo "ripoti" nyingine asili yake ni nini? Kwanini Bunge halijakubali kutengua ili mjadala wa Richmond uanze tena. Tatizo ni kuwa watu wanafikiri kuwa kwa yeye kutosema mambo mengine inamaana ameficha mabaya au kitu cha namna hiyo... yawezekana kisichoandikwa ni kile cha kumtaja Lowassa moja kwa moja na siyo Rais kama wengi wanavyofikiria.

My friend, anachotakiwa kushukuru Mwakyembe ni kwamba sasa hivi watu wapo obsessed na matatizo ya ufisadi. Otherwise hii hoja yake ingeifanya ile report yake nzima iwe null and void na ingebidi awaombe msamaha wote aliwatuhumu na mchezo ungeanza upya!




Kitila hii point ya kufanya makosa na kutoa maoni ili kumsaidia mtu niko nawe asilimia 100. Tatizo ni hii hoja kuwa "Mwakyembe hatufai Watanzania". Hii hoja haina cha kumsaidia kutoa maoni au kumuonesha njia, hoja iliyotolewa ni kuwa kwa vile hivi basi vile. Tunaweza kuangalia mambo mengine n.k na kuyajengea hoja, lakini kwa hili la "kulinda heshima ya serikali" ndio tumtose kuwa "hatufai Watanzania" sidhani kama wewe unakubali. It is one thing kumkosoa rafiki, na kitu kingine kumuangamiza.
 
Mgaya,

..hakuna uwezekano wa Mwakyembe kuchafuliwa, sana sana atajichafua mwenyewe.

..ni mambo gani hayo ambayo mwanzoni Dr.Mwakyembe aliona asiyasema kwa manufaa ya nchi, lakini sasa baada ya watu kuanza kuhoji ripoti yake anaona hayana manufaa tena na anatishia kuyasema?

Mwanakijiji,

..serikali ni ya wananchi, kwa ajili ya wananchi.

..hilo la kulinda heshima ya serikali haliko mikononi mwa Dr.Mwakyembe.

..alichopaswa kufanya Dr.Mwakyembe ni kusema ukweli wote. wananchi ndiyo tunaopaswa kutamka ndani ya demokrasia yetu kwamba serikali[wananchi] imevunjiwa heshima etc etc.

..i am very tempted kuamini kwamba kuna ufisadi/mafisadi wamefichwa na Mwakyembe. kwa mtizamo wake amefanya hivyo ili kulinda heshima ya serikali. nadhani mtizamo huo ni POTOFU, na haujengi nchi.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…