MKJJ: Hakuna hata mahala ninapodai perfectionism kwenye report ya Mwakyembe. Nilichofanya mimi ni ku-point out clear flaws kwenye report ya Mwakyembe ambazo zinadhaifisha yote aliyokwisha kutueleza na yaliyomfanya aonekane ni hero. Flaws zenyewe ni hizi (narudia tena):
Mwanzo mzuri:
a) kushindwa kumhoji Lowasa huku akiwa ndiye mtuhumiwa mkuu wa ule mchezo mchafu juu ya Richmond-hii sitaki kueileza tena maana nimeshaieleza sana huko nyuma.
Hili ni kosa la kuangalia suala hili. Kamati ya Mwakyembe haikupewa jukumu la kumchunguza Lowassa, na katika hadidu rejea Lowassa hakutajwa kama target ya investigation. Kuwa "mtuhumiwa mkuu" yawezekana mbele ya vyombo vya habari na raia lakini si katika maagizo ya Bunge. Kukumbusha tu Kamati Teule ya Mwakyembe iliunda na kupewa majukumu yafuatayo:
Tarehe 15 Novemba, 2007 Mhe. Spika aliipa Kamati Teule siku thelathini kukamilisha kazi yake na Hadidu za Rejea zifuatazo kwa ajili ya kutekeleza kazi hiyo ya uchunguzi;
1. Kubainisha Richmond Development Company LLC ni kina nani, na ni kampuni ya shughuli zipi na hivyo kupima uwezo wake kupatiwa zabuni ya kuleta nchini na kujenga mtambo wa umeme wa gesi wa MW 100,
2. Kutathmini mchakato mzima wa jinsi zabuni waliyoshinda Richmond ilivyoshughulikiwa kuanzia Kamati ya Zabuni hadi mwisho ili kujiridhisha kuwa sheria, taratibu, miiko na maadili ya zabuni yanayotawala zabuni za aina hiyo vilifuatwa au vipi,
3. Kutathmini mkataba baina ya Richmond Development Company LLC na TANESCO ili kujiridhisha kuhusu uhalali wa masharti ya mkataba huo ukizingatia gharama na masharti mengine ukilinganisha na masharti yaliyomo katika mikataba ya aina hiyo iliyoafikiwa na TANESCO/Serikali,
4. Kubainisha huduma na misaada mbalimbali waliyopewa Richmond kama vile kufunguliwa Letter of Credit na kupima uhalali wake,
5. Kuziangalia na kuzitolea maoni taarifa za TAKUKURU, PPRA na taarifa zozote nyingine zilizoangalia utaratibu wa zabuni ya Richmond, na
6. Kuangalia mambo mengine yoyote yenye uhusiano na mchakato mzima wa Richmond ili kutoa mapendekezo ya kuboresha taratibu za zabuni kwa siku zijazo, kwa maslahi ya Taifa letu.
Katika hadidu rejea, Waziri Mkuu Lowassa au Ofisi yake were not the target of the investigation. The target was Richmond. Hapa utaona kwa mbali kwanini Waziri Mkuu hakuhojiwa kama "mtuhumiwa mkubwa". He was not the target.
As a matter of fact, report nzima ya Kamati Teule inataja jina la Lowassa mara moja tu. Pale inaponukuu hii barua.
Siku hiyo hiyo ya tarehe 19 Juni 2006, Waziri wa Nishati na Madini alimwandikia dokezo Waziri Mkuu Mhe. Edward Ngoyai Lowassa, (Mb) kuwa majadiliano ya awali na Richmond Development Company LLC yamekamilika hivyo Serikali iiteue Kampuni hiyo kwa lengo la kuingia mkataba na TANESCO wa kuzalisha umeme wa dharura kwa miaka miwili. Sehemu ya barua hiyo inasomeka:
Kamati ya Serikali ya Majadiliano (GNT) inayojumuisha wataalam kutoka Wizara Fedha, Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Benki Kuu na TANESCO ilifanya majadiliano na Richmond Development Company LLC ya Houston, Marekani kutoka tarehe 8 hadi 16 Juni 2006, kwa kuzingatia maelekezo yako. (msisitizo tumeongezea)
Utaona kuwa hapa kilichozungumzwa ni fact, kuna barua iliyoelekezwa kwa Waziri Mkuu iliyosema hivi na vile. Hii haimfanyi Lowassa kuwa mtuhumiwa "Mkubwa".
Lakini utaona kuwa cheo cha Waziri Mkuu kinatajwa mara thelathini ndani ya ripoti hiyo. Why? Ni kwa sababu katika mchakato mzima wa richmond Ofisi ya Waziri Mkuu ilikuwa inahusika. Ni kwa sababu hiyo mwishoni mwa ripoti hiyo Kamati ikapendekeza hivi:
. Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Mhe. Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shughuli za Serikali na uongozi wa nchi kwa ujumla, ni wajibu wake yeye mwenyewe kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya Bunge. Vile vile ni wajibu wa Bunge ambalo linathibitisha uteuzi wake kwa mujibu wa Ibara ya 51 inayothibitisha uteuzi wake kuangalia ikiwa matokeo ya uchunguzi huu hayajaathiri hadhi na uzito wake ndani ya Bunge.
Ni yeye Waziri Mkuu ambaye alipewa nafasi ya kujitetea kwenye Bunge akashindwa. Ni yeye ambaye kwa hiari yake mwenyewe aliamua kujiuzulu bila hata kumtaarifu Rais kwanza na kubwaga "manyanga" Bungeni siku ile ya kukumbukwa. Lowassa angetaka kujitetea na kuelezea upande wake alikuwa na nafasi hakuitumia. Yeye hakuwa target ya investigation lakini alionekana kuhusika na ndio maana nafasi ya yeye kujitetea ilikuwepo na alikuwa na nafasi ya kuelezea upande wake. Kujiuzulu kwa Lowassa si kosa la Mwakyembe! kujiuzulu kwa Msabaha na Karamagi si makosa ya Kamati Teule, kama waliona hawakutendewa haki walipewa jukwaa la kujitetea wakagwaya! Mzigo huo wanaubebea wao na wao peke yao.
b) Kauli yake ya kuomba kibali cha spika ili amwage yale ambayo hakuyasema kwenye report yake ya awali. Hili la pili ni tatizo kubwa zaidi unless umesahau malalamiko ya Lowasa. Nikukumbushe kwamba moja ya tuhuma za Lowasa kwa Mwakyembe ni kwamba kamati iliandaa report mbili. Lowasa alidai kwamba katika report ambayo haikuwasilishwa hakutajwa kabisa kuhusika katika saga la Richomond lakini kwa shinikizo la spika, na kwa sababu za kisiasa na kigomvi zilizopo kati ya spika na Lowasa, akashinikizwa afanye mbinu ili Lowasa atiwe hatiani-hii ndiyo ikazaa report ya pili iliyowasilishwa bungeni. Unakumbuka haya au nawe unajifanya unayafumbia macho? Sasa kwa kauli yake Mwakyembe ameiimarisha madai ya Lowasa-hasa kwamba kulikuwa na report mbili na kwamba kamati ya Mwakyembe ilifanya kazi kwa lengo la kubomoa baadhi ya watu na kuwajenga wengine kisiasa na haikuwa na nia ya dhati ya kutafuta matatizo na majawabu kuhusu Richmond. Sasa you can't call these serious matters kwamba ni makosa ya kawaida katika report.
sehemu ya jibu langu kuhusu Lowassa bado inasimama. Lowassa hakuwa part ya ripoti alijuaje zimeandaliwa ripoti mbili, moja ikimtaja na nyingine isiyomtaja? Ni yeye alikuwa na jukumu la kuionesha hiyo ripoti nyingine alipopewa nafasi. Hadi leo hii hiyo ripoti nyingine mbona haijatolewa mahali popote pale.
Ni kwa sababu hiyo, Mwakyembe katoa hoja itenguliwe kanuni ya Bunge ili kina Lowassa na hiyo "ripoti nyingine" watoe walichonacho, na wao kina Mwakyembe waelezee hiyo "ripoti" nyingine asili yake ni nini? Kwanini Bunge halijakubali kutengua ili mjadala wa Richmond uanze tena. Tatizo ni kuwa watu wanafikiri kuwa kwa yeye kutosema mambo mengine inamaana ameficha mabaya au kitu cha namna hiyo... yawezekana kisichoandikwa ni kile cha kumtaja Lowassa moja kwa moja na siyo Rais kama wengi wanavyofikiria.
My friend, anachotakiwa kushukuru Mwakyembe ni kwamba sasa hivi watu wapo obsessed na matatizo ya ufisadi. Otherwise hii hoja yake ingeifanya ile report yake nzima iwe null and void na ingebidi awaombe msamaha wote aliwatuhumu na mchezo ungeanza upya!
Baada ya kusema yote haya mimi sitilii shaka "ushujaa" na uimara wa Mwakyembe. Hata hivyo, najua kwamba Mwakyembe hufanya makosa, tena makosa mengine ni ya kutisha, likwemo hili la juzi na lile la kukubali kutumika kutetea mauaji ya wananchi yaliyofanywa na polisi huko Zanzibar Januari 2001!!! Sasa tusipoyaona haya makosa hatumsaidii huyu shujaa wetu ili atuongoze vizuri katika mapambano tuliyo nayo!!
Kitila hii point ya kufanya makosa na kutoa maoni ili kumsaidia mtu niko nawe asilimia 100. Tatizo ni hii hoja kuwa "Mwakyembe hatufai Watanzania". Hii hoja haina cha kumsaidia kutoa maoni au kumuonesha njia, hoja iliyotolewa ni kuwa kwa vile hivi basi vile. Tunaweza kuangalia mambo mengine n.k na kuyajengea hoja, lakini kwa hili la "kulinda heshima ya serikali" ndio tumtose kuwa "hatufai Watanzania" sidhani kama wewe unakubali. It is one thing kumkosoa rafiki, na kitu kingine kumuangamiza.