Sasa Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni, Waziri Mkuu, Mhe. Misengo Kayanza Peter Pinda, ndio amekamata nyundo mkononi kwake, na anapigilia misumari ya mwisho kwenye jeneza la Richmond.
Mhe, Pimba amekiri kuwa kauli ya Dr. Slaa, kuhusu uamuzi wa kuimaliza Richmond kwa mtindo huu ni uamuzi wa kisiasa, imemtatiza sana, alitegemea Dr. Slaa angetoa ufafanuzi, kwa vile hakutoa, basi anaamini Dr. Slaa aliteleza tuu!.
Pinda anasema yaliyopita si ndele, tumejifunza nini kwa sakata la Richmond, amesema life will never be the same again kwani mambo mengi yatabadilika. Moja wapo ni ujio wa muswada wa kutenganisha uongozi na biashara.
Uwajibikaji wa Eddo na wale washirika wake 2, ni ishara tosha ya serikali inayowajibika, amemsafisha EL na kumnasihi amkabidhi Mungu, Inshaalah, itajafika siku wakarejea kwenye utumishi wa umma.Makofi mengi.
Amesema pamoja na lugha kali, jazba, hasira kelele, ila mwisho wa yote, wote ni wamoja wanawatumikia Watanzania.
Anesisitizia uadilifu kwa watumishi wa umma na kuishi na kutenda kwa mifano.
Serikali inawajibu wa kujipanga upya katika eneo la mikataba.