Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Ngeleja, ameunga mkono hoja kwa asilimia 100% na amesema sana tuu, ili jambo moja amenifurahisha sana waziri huyu kijana, ni moja tuu, aliposema hoja za Dr. Slaa nazikubali na kulichukua kama changamoto. Kwa kauli hii pekee, Ngeleja nae, akisimama imara, atahesabiwa!.

Sasa anazungumza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Philip Marmo, (sijua kama jaa huyu anachekaga). Kwa kifupi Marmo anaonyesha serikali kupitisha kifungu kwa kifungu, just procedures.

Atakayezungumza kwa impact ni Mhe. Pinda, ambaye naamini atanza kwa kushukuru, 'kufa kufaana'!.
 
Sasa Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni, Waziri Mkuu, Mhe. Misengo Kayanza Peter Pinda, ndio amekamata nyundo mkononi kwake, na anapigilia misumari ya mwisho kwenye jeneza la Richmond.

Mhe, Pimba amekiri kuwa kauli ya Dr. Slaa, kuhusu uamuzi wa kuimaliza Richmond kwa mtindo huu ni uamuzi wa kisiasa, imemtatiza sana, alitegemea Dr. Slaa angetoa ufafanuzi, kwa vile hakutoa, basi anaamini Dr. Slaa aliteleza tuu!.

Pinda anasema yaliyopita si ndele, tumejifunza nini kwa sakata la Richmond, amesema life will never be the same again kwani mambo mengi yatabadilika. Moja wapo ni ujio wa muswada wa kutenganisha uongozi na biashara.

Uwajibikaji wa Eddo na wale washirika wake 2, ni ishara tosha ya serikali inayowajibika, amemsafisha EL na kumnasihi amkabidhi Mungu, Inshaalah, itajafika siku wakarejea kwenye utumishi wa umma.Makofi mengi.

Amesema pamoja na lugha kali, jazba, hasira kelele, ila mwisho wa yote, wote ni wamoja wanawatumikia Watanzania.

Anesisitizia uadilifu kwa watumishi wa umma na kuishi na kutenda kwa mifano.

Serikali inawajibu wa kujipanga upya katika eneo la mikataba.
progress.gif
 
Pinda amemalizia kwa kusema, Watanzania wote, lazima tukubali, tusipoendesha nchi hii, kwa kufuata katiba, sheria, taratibu na kanuni, tutakuwa hatuwatendei haki Watanzania!
Makofi mengi.
Jeneza limeshafungwa...! Richmond Tumpeleke tumpeleke.....!
 
Mtoa hoja, William Shelukindo ameitwa tena sasa ni kuweka tuu mchanga, as procedures, hoja za Kiwira hazikupata pingamizi, hivyo ameomba kutoa hoja.
Na sasa anahitimisha Richmond kwa kuomba bunge liyakubali, hoja za Dr. Slaa kapuni.
Lile jiwe kubwa la kufunika kaburi la Richmond, sasa ndio linaanza kuvurumishwa, MC ni Spika Six amahoji wanaoafiki waseme ndiyo...ndiyo kubwa...! Wasioafiki wasema Siyo....! siyo nyembamba!
Spika Sitta ameufunga rasmi mjadala.

Richmond is now a history!. Kombe limefunikwa, mwanaharamu kapita!. Alamsiki!.
 
Things haz orede fallen Apart.
wat to do?
wananchi wanaona kinachoendelea.
 
Jamani, kama ishu ya richmond iliyokuwa wazi vile imeenda kidizaini namna hiyo, itakuwaje kwa ishu ambazo wananchi wengi hatuzielewi zimekaaje???????? Mungu isaidie Tanzania!!! uuuuwiiiiiiiiii...
 
CCM na collective responsibility hii ilishawahi kumjeruhi mzee wa kiraracha naamini siasa kama cinema actors/actress wote wana tahadhari na hili. Kama sio ndoto za mchana, labda hiyo CCJ iwe ya ukweli vinginevyo safari bado ndefu na kamanda wa kweli hajapatikana bado we are still day dreaming!!
 
- Masuala yote yanayohusu wizi wa mali za wananchi ni ya uvunjaji wa sheria, hayawezi kumalizwa popote nje ya sheria, hizi ni siasa tu kila kitu kina wakati na msimu wake Yona na Mramba wanaelewa vizuri sana hili, acha hawa wajidanganye kwamba huu ndio mwisho wa Richimonduli, Lowassa na wenzake wanajua vizuri sana kwamba huu ni mwanzo.

- Halafu ungetegemea maandamano mazito kutoka kwa wananchi, lakini badala yake wanauliza Mama kilango yuko wapi? Zitto ameenda mpaka Jangwani kuwashinikiza wamke, wao wanashangaa Hummer! na kwenda kulala usingizi siku imeisha, sasa eti Mama Kilango yuko wapi? maana ndiye mwenye hili taifa!

Mungu Aibariki Tanzania na siku moja kuwaamsha hawa wananchi masikini ya Mungu!

Respect.


FMEs!
 
Wakati tunasema hiki ni Chama Cha Majambazi mlikuwa hamuelewi sasa mnalalamika nini? Chini ya serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete Chama Cha Majambazi hakiwezi kubadilika ni azimio lile lile kula pesa ya walipa kodi hadi kiama. Ati wanamwachia fedhuli mkuu aamue! Aamue vipi wakati pesa ya walipa kodi iliteketea tangu rafiki na swaiba wake mkuu alipoachia madaraka na fadhila yeye anaziona za kwenda kubembea Caribbean etc.

Nchi ambazo wanabadilisha viongozi kwa demokrasia ya Kitanzania hakuna hapa ulimwenguni. Kama kweli vyama vya upinzani na watanzania wangekuwa na matatizo na haya yanayotokea basi mngeona leo maandamano pale bungeni na katika kila kona ya mji lakini wapi ka-nchi haka watu wameridhika.

Pesa za walipa kodi zimepotea wezi wa kuku na bilinganya wako keko lakini hawa bado wanapeta tu.
 
Tanzaniaa Tanzania
Nakupenda kwa Moyo wote
Nchi yangu Tanzania, Mafisadi wanakumaliza

Nilalapo nakuwaza weee
Tuendako ni kheri ya jana
Tanzaniaa Tanzania, Mafisadi wanakumaliza
 
Kama hili la Richmond limepita bila kusikia hata kelele moja ya waliokuwa wanajiita wapiganaji wa ufisadi narudi kule kule kwa Slaa kwamba humo CCM hakuna mpiganaji hata mmoja ni wanafiki tu wanataka wasikike nafikiri wananchi tuendelee na hivi hivi vyama vyetu vya upinzani tusitegemee eti mtetezi ndani ya CCM
 
- CCM sio chama cha majambazi, na kama ni kweli basi wananchi wa taifa hili ni majambazi zaidi kuliko hata CCM yenyewe!

- Sio wananchi wote wa Tanzania tumekata tamaa, wengine tunaamini through history kwamba kila mwnzo una mwisho, ila one thing dua la kuku halimpati mwewe Rome haikujengwa kwa siku moja, kwanza tunahitaji wananchi walioelimika kisiasa pole pole litawezekana!


- Otherwise, mimi na wananchi wengi wa Tanzania hatujawahi kuwapigia kura majambazi, maana mimi sio jambazi so are wananchi wapiga kura!

Es!
 
- Masuala yote yanayohusu wizi wa mali za wananchi ni ya uvunjaji wa sheria, hayawezi kumalizwa popote nje ya sheria, hizi ni siasa tu kila kitu kina wakati na msimu wake Yona na Mramba wanaelewa vizuri sana hili, acha hawa wajidanganye kwamba huu ndio mwisho wa Richimonduli, Lowassa na wenzake wanajua vizuri sana kwamba huu ni mwanzo.

- Halafu ungetegemea maandamano mazito kutoka kwa wananchi, lakini badala yake wanauliza Mama kilango yuko wapi? Zitto ameenda mpaka Jangwani kuwashinikiza wamke, wao wanashangaa Hummer! na kwenda kulala usingizi siku imeisha, sasa eti Mama Kilango yuko wapi? maana ndiye mwenye hili taifa!

Mungu Aibariki Tanzania na siku moja kuwaamsha hawa wananchi masikini ya Mungu!

Respect.

FMEs!

Is true acha wajidanganye hii kesi haijesha hata miaka 10 ijayo kuna mtu mmoja kichaa atatokea atazifufua kesi za aina hii
 


SAFI nakuunga mkono hoja yako,

Hapa kuna swala lasisi watanzania kubadilika jamani, ivi idadi ya wabunge bungeni ni wangapi na sie wapiga kura ni wangapi? mbali na hilo sie watanzania ndi chanzo cha hayo yote mtu anakuja kukuhonga vijisenti na kesho waenda mchagua wategemea hao viongozi watatukumbuka tena????

Tuendelee kupigwa danadana mpaka siku wajukuu zetu watakapo amua sasa inatosha ndipo nchi itasonga mbele





Kaka pole,
Hoja ya kuunganisha nguvu hasa sisi vijana kwa nia ya kuwatupa nje hao mafisadi imeshaingia doa tena kubwa sana, tutaendelea kuhongwa pilau, khanga, kofia, na mikopo ya sh.50,000 so long as watoto wetu wanaendelea ku-score zero mashuleni. Kama wanafunzi 65,000 wamepata zero, baada ya miaka 10 wakiendelea kupata zero kwa idadi kama hiyo itakuwa ni asset kubwa kwa CCM kuwatumia katika kuchagua viongozi wa chama hicho. Ukitaka kumtawala mtu mnyime elimu, utamfanya chochote kile unachotaka.
 
From LEVINA KATO in Dodoma,
10th February 2010


NATIONAL Assembly Speaker Samuel Sitta declared formal closure of the debate on the controversial emergency power generation contract to Richmond Development Company and Kiwira Coal Mine privatisation in the House this evening.

"With your approval, I am glad to announce that we have now officially closed debate on the Richmond and Kiwira in the National Assembly," Mr Sitta said after the House endorsed reports tabled by the Parliamentary Energy and Minerals Committee.

The Speaker warned MPs who would continue raising the issues in the House after the official closure of the debate, saying such a move was against Parliamentary Standing Orders and defiant legislators are to face the music.

He further pointed out at Mr Rostam Aziz (Igunga - CCM) who had earlier said he would go to court before a three-member panel of judges to seek an injunction against Parliamentary Committee's recommendations, saying the move is untenable because it was unconstitutional.

Mr Sitta reminded the legislator that the Parliament, just as the Executive and the Judiciary, were independent organs of the state. "Each of the three organs functions independently," he said, basing his argument on Parliamentary Standing Order 54(4).

Prime Minister Mizengo Pinda expressed the government's appreciation on the MPs' frank and extensive debate on the controversial Richmond Development Company contract and Kiwira Coal Mine privatisation.

He said the government was from the beginning committed to implementation of all the recommendations by the committee.

He further told the House that the government has learned on the importance of diligence and honesty as important attributes in public service.

"One may be well educated and a very good lawyer, but if he is not honest then he is useless in the public service," Mr Pinda stressed.

He also admitted limitations in the Attorney General's Chambers, particularly shortage of experts on complicated commercial contracts. "The government has already drawn up capacity building strategies in the chambers," he added.

The National Assembly has also ordered for fresh audit of 17bn/-misappropriated during the rehabilitation of Kiwira Coal Mine and stocktaking to verify the firm's assets. The order follows a report presented by Dr Harisson Mwakyembe (Kyela - CCM).

Meanwhile, the House yesterday resolved to postpone to the next session debate on the Tanzania International Container Terminal Services and Tanzania Railway Limited.
 
hii nchi imeanzishwa na HEROES na sasa wameachiwa ZEROS.

viongozi wengi wa sasa hivi tuliokuwa nao hawana uchungu na nchi yetu hata kidogo.hawajui thamani ya nchi yetu,hawana akili na elimu ya kuwa viongozi .wengi wao wababaishaji kwa vile wanajua kwamba hawachaguliwi kwa utendaji wao wa kazi bali kwa nguvu ya pesa.

wao wanafikiri kila jambo linatatuliwa kwa nguvu na ubabe wa kuwakataza watu wasizungumzie.kama ni hivyo haina haja ya kuwa na bunge. hela zote zinazotumika kuwalipa wabunge na kuendesha bunge zipelekwe kwenye uduma za jamii kulikoni kuwanufaisha "puppets".
 
Kama hayana akili tu! Kelele zote hizo za nini sasa! subiri tutakavyo wasurubisha huko majimboni! unafikiri wananchi vijijini hawajui! Wapinzani hii ni habari njema tumieni mwanya huu! Tuwazomee CCM kwenye mikutani yote, yaani zomea zomea! wakitoa tarkrima kula! halafu kimaliza endelea kuzomea!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom