Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Khaaaa! mbona sikupati!! Blaah blaah tu ndo hivyo! Hivi bunge limerudi enzi za Mkapa?
 
Ameanza kuchangia Mhe. Mpendazoe, amejiuma uma, hatimaye kakubali kuunga mkono hoja, ila anaonekana, bado anahuzuni moyoni haswa kuhusu Kiwira.

Sasa anazungumza Mhe. Mnyaa. Jamaa angalau anasema kitu, ila mwishowe naye ataunga hoja!
 
Asante Pasco, lakini hiyo mijamaa inatuletea fadhaa kweli!
 
Natazama na kusikiliza kinachoendelea bungeni sasa hivi mintaarafu kuwasilishwa kwa Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu Kiwira na Richmond kama zilivyowasilishwa na Dr Mwakyembe na Shellukindo.

Ninaweza kuielezea hali hii kwa kukubaliana na msemo wa wahenga kwamba CCM, serikali yake na Bunge linahodhiwa na chama hicho limeamua kufanya kinachoitwa ‘funika kombe, mwanaharamu apite’. Watoto wa mjini wanaweza kuelezea hali hiyo kuwa ni ‘tumepigwa mchanga wa macho’. Bunge limerejea kule kule kwa kuwa kama mchezo wa kuigiza kwa kuruhusu usanii wa kisiasa wa serikali; kipeo cha juu cha unafiki wa wanadamu.

Kamati umeshatangaza kwamba imeshaliza kazi yake, Bunge nalo litangaze kufunga huo mjadala kwa bunge zima badala yake sasa ufuatiliaji uachwe kwa kamati za kisekta. Kwa hiyo sasa ripoti za utekelezaji zitapelekwa kwenye kamati za kisekta kwa kuwa kamati husika imesharidhika mpaka sasa kwa utekelezaji ambao serikali imefanya mpaka sasa.

Wakati Kamati ikiyasema hayo inasema kuhusu Kiwira kuwa inaendelea kumshauri CAG afanye ukaguzi kuhusu bilioni 17 zilizoingizwa na serikali kwenye kiwira .(Tujiulize, muda gani agizo hili lilitoka? Kwanini mpaka sasa ukaguzi haujafanyika). Kwa maneno mengine, baada ya serikali kuamua kuuchukua upya mgodi, tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka za kina Mkapa, Yona na wenzao sasa sinaelekea kufunikwa kwa nguvu zote.

Usanii mkubwa zaidi unajidhihirisha kwenye sakata zima la Richmond, ambayo mitambo yake dada ya Dowans ipo mpaka sasa hapa jimboni ubungo. Zikitafutwa kila namna za kuingiza mitambo husika kwenye mkondo wa kuhudumia na kulipwa na serikali ya Tanzania.

Kamati inakiri kwamba ni kweli kuna double payment kwenye ulipwaji wa dola milioni tatu kwa kampuni ya Dowans, kamati inasema tu kwamba inaishauri serikali hizo fedha zirudishwe. (Toka kwa kampuni ya Dowans- ambayo kama ilivyo kwa Richmond inaonyesha kwamba ni kampuni hewa, uhalali wa usajili wake una mushkeli mkubwa). Kamati inatamka kwamba watendaji husika mamlaka zao za kinidhamu zimeona hawana hatia. Kamati inasema viongozi wa kisiasa wakina Msabaha, Karamagi nk uchunguzi wa ndani kuhusu ushiriki wao kwa ajili ya kuwajibishwa umeshakamilika, lakini sasa serikali imeanza uchunguzi wa nje wa kimataifa unaendelea. Kamati inatamka kwamba sasa suala hili likikamilika lipelekwa kwa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Usalama( Sasa sio Bungeni tena). Ajabu sana! Suala hili lilianza mwaka 2007; maazimio ya Bunge ni kujiuzulu kwa Lowassa ilikuwa 2008; mpaka leo uchunguzi unaendelea. Kituko kikubwa zaidi ni hitimisho la Kamati, kwamba kuhusu kumwajibisha Mkurugenzi wa TAKUKURU Hosea kwa TAKUKURU(Wakati huo TAKURU) kuisafisha Richmond; kwamba kamati haiwezi kulizungumzia tena suala hilo na wala haitarajii bunge ilizungumzie kwa kuwa Hosea naye anawachunguza wa bunge(rejea tuhuma kuhusu posho mbili). Hivyo kamati inasema suala hili sasa inaachiwa mamlaka ya juu zaidi(Soma Rais Kikwete). Ningeweza kuchambua azimio moja baada ya lingine katika ya maazimio 13 ambayo yalibaki kabla ya 23 (Hata yale 10 mengine yalikuwa mchanga wa macho).

Lakini yatosha kusema kwamba suala hili ni ishara kwamba sasa makundi ndani ya CCM (lile linalojiita la wapambanaji dhidi ya ufisadi na lile linaloitwa la mafisadi) yanakaribiana kufunika tofauti zao kwa maslahi ya chama chao na utawala wao tunapoelekea uchaguzi wa mwaka 2010. Inaonyesha kamati ya chama (party caucus) imefanya kazi yake!. Hii inaweza kutoa ishara kuhusu nini kitatokea kwenye ripoti ya Kamati ya Mwinyi na mwelekeo wa chama hicho tawala kwa ujumla. Haya ni madhara ya kuwa na hodhi(dominance/monopoly) ya chama kimoja bungeni.

Hii ni changamoto kwa umma tunapoelekea katika uchaguzi mkuu. Tukumbuke maneno ambayo CHADEMA tuliyasema mwaka 2005; Kwamba mabadiliko ya kweli katika taifa letu, hayawezi kuletwa na mafisadi wale wale, wa chama kile kile, chenye uoza ule ule, wakiendeleza yale yale kwa Ari, nguvu na Kasi mpya. Kwa falsafa ya chukua chako mapema(ccm), Tanzania yenye neema haiwezekani. Tuunganishe nguvu ya umma kuchagua viongozi mbadala wenye dira na uadilifu tuweze kujenga taifa lenye uwajibikaji kwa kubadili mfumo wa utawala; mabadiliko ya kweli yanawezekana. Tuwe wakala wa mabadiliko tunayotaka kuyaona; Mwenyezi Mungu atuwezeshe kufika salama.

JJ
 
Kengele ya pili imelia kabla Mhe. Mnyaa hajahitimisha kuunga mkono hoja. Sasa anayechangia ni Eng. Stela Manyanya, ameanza kwa kuunga mkono hoja kwa asilimia 100.

Sasa anapiga nyundo media eti ndio waliolikuza Richmond!
Bunge ni wajibu kuisimamia serikali, eti media inawachonganisha bunge na serikali.
CCM kiboko!.
Amempongeza EL kwa kuwajibika na anaipongeza serikali kwa kulisikiliza bunge, anaisifu kwa kuwajibika kwa bunge.

Anasema huku anasitasita, ameingiza wasifu wa serikali ya Chama cha Mapinduzi, ameisifu serikali kwa kutekeleza mazimio mengi ya bunge.

Eng. Manyanya noma, eti anasema leo wananchi msishangae wote tunaunga mkono, tunaomba mtuelewe, tunaelekea kwenye uchaguzi, hivyo tunawaomba wananchi, mturudishe sisi tuliotimiza wajibu wetu.
Spika atetea shule ya Dr. Matayo na kuliahirisha mpaka jioni.
 
Kengele ya pili imelia kabla Mhe. Mnyaa hajahitimisha kuunga mkono hoja. Sasa anayechangia ni Eng. Stela Manyanya, ameanza kwa kuunga mkono hoja kwa asilimia 100.

Sasa anapiga nyundo media eti ndio waliolikuza Richmond!
Bunge ni wajibu kuisimamia serikali, eti media inawachonganisha bunge na serikali.
CCM kiboko!.
Amempongeza EL kwa kuwajibika na anaipongeza serikali kwa kulisikiliza bunge, anaisifu kwa kuwajibika kwa bunge.

Anasema huku anasitasita, ameingiza wasifu wa serikali ya Chama cha Mapinduzi, ameisifu serikali kwa kutekeleza mazimio mengi ya bunge.

Eng. Manyanya noma, eti anasema leo wananchi msishangae wote tunaunga mkono, tunaomba mtuelewe, tunaelekea kwenye uchaguzi, hivyo tunawaomba wananchi, mturudishe sisi tuliotimiza wajibu wetu.
Spika atetea shule ya Dr. Matayo na kuliahirisha mpaka jioni.

Pasco, asante sana kwa kutuhabarisha mapema "what was behind the scene". Nimesikiliza kwa masikio yangu via Radio Maria-TBC saa saba mchana eti kuwa "tume imeridhika na hatua zilizochukuliwa, ikiungwa mkono na Mwakyembe na shelukindo " na kumpongeza EL kwa kuwajibika.

This is Tanzania. "if you claim to fight corruption...it will fight you back"

Let the big fishes fry themselves....ewaaaaaaa...nani atakubali kujitumbukiza kwenye sufuria la mafuta? Eng Manyanya lol!!!! I am shocked.

Ngoja nikanywe kikombe cha chai, nijipange namna nami naweza kushiriki keki ya nchi yetu kwa kuwa CORRUPT. Wanangu lazima wasome USWIS piga ua!!! Apaaaaaa....
 
Haiwezekani ntakua naota..
Ee Mungu wangu nitoe ndani ya hii ndoto
Mwenyezi wasaidie wabunge woooote wa bunge hili wasirudi bungeni haswa wa CCM..
Mapambano yameanza mabadiliko katika siasa zetu na mustakabali wa nchi yetu lazima yaanze sasa..
Shime Tuamke popote tulipo kampeni ni moja Viongozi mbadala muhimu!!!!!!!!
 
watakwisha wengi, Mzee Malecela na Mkewe Kirango nadhani ndo itakuwa maumivu ya kifamilia zaidi!
 
Mmmhhh hii ni hatari sana..! yani tumepigwa changa namna hii? Wapiganaji dhidi ya ufisadi ndani ya ccm sasa tunataka tuone watafanya nini? au hili swala ndilo lililowachochea kuandika ule waraka uliotolewa na Enigma??? yangu macho.....!
 
Yeah! Hi ndiyo TZ. Sasa tusubiri kununuliwa kwa mitambo ya Dowans baada ya kiwingu cha Richmond kuyeyuka. Lakini Mwakyembe and co. ndio wajue kuwa wako njiani kujiunga na akina Lamwai. Na hapo wasisingizie media. Bw. Rostam anatikisa guu tu bungeni; hahitaji kutoa kauli yoyote. What a country!
 
Yeah! Hi ndiyo TZ. Sasa tusubiri kununuliwa kwa mitambo ya Dowans baada ya kiwingu cha Richmond kuyeyuka. Lakini Mwakyembe and co. ndio wajue kuwa wako njiani kujiunga na akina Lamwai. Na hapo wasisingizie media. Bw. Rostam anatikisa guu tu bungeni; hahitaji kutoa kauli yoyote. What a country!

Ndiyo maana siku zote nimekuwa napinga uwepo wa Bunge. Sijawahi kuona faida yake na sitakaa niione.
 
Achana na akina Eng. wa Nyanya wa CCM, hawafai kutumainiwa kwa lolote! @#4#&9f05gg^$$$#!!!!!!!!!!111
 
Makyembe na PhD yake amempigia magoti Makamba, Simba na Malima mh. Amedhalilisha usomi wake
 
.......hili sakata lilikuwa ovasaiz kwa Kamati ya Mwakyembe......CCM ni hatari we unataka kumwangusha PM wao aliyejiuzuru??hujui mkakati wake kwa kurejea kwa kishindoo?? eeh unataka kumchafua chafua Swahiba wa MKULU WA NCHI eeh.
 
I never expected a miracle under CCM

Sure. No miracles under CCM in any matter, you can always predict what will happen in along run. Nadhani sasa watanzania tumekuwa kama tiara. Hakuna maamuzi magumu ambayo nimeshuhudia yakifanyika kwa kipindi kirefu sana. Kinachotokea ni kuwapotezea watu concentration kila litokeapo jambo. Watu wanasahau hata mambo ya msingi na kujikuta tukishabikia ama kufuatilia 'matukio muhimu' ya kitaifa. Mwisho wa siku yale tuliyotarajia hayatokei, yanapigwa danadana na kuibuliwa mikasa mipya tofauti kabisa. Tunahamia huko na kusahau yale ya mwanzo ambayo baada ya muda watu wanayakubali kama yalivyo kiasi kwamba hata kama uamuzi uweje, watu hawajali tena maana yameshakuwa...ya-kale na kama tujuavyo, "ya kale hayanuki...". Mambo haya yataendelea hadi lini, na je, tutafika?
 
kazi ipo mi nilisema mwakyembe hana lolote la maana na kweli litatimia leo

Mimi pia nilisema huko nyuma kuwa Mwakyembe na kundi lake ni wachumia tumboni kule kujipambanua ilikuwa kwa sababu hawakupata ulaji; sasa uchaguzi karibu lazima watapiga magoti ingawa huyu mbunge wa Kyela ana kibarua kizito ili kurudi mjengoni.
 
Ni mpaka hapo watanzania tutakapo amua kwa utashi wetu kuwa hatuwataki fulani na fulani watuongoze kwa sababu moja, mbili,tatu n.k,tutakuwa watu wa kuzungukazunguka huku na huko,yule kachemcha wizara hii anahamishiwa kule kama vile hakuna watu wenye uwezo...........na na kwambia CCM itatawala mpaka pale watu watakapokubali kubadilika(sio CCM Kubadilika)
 
Nilishasema before, ilimradi umo ndani ya CCM huna sifa za kujiita eti mpambanaji wa ufisadi, kitu gani!kila siku Richmond,Richmond mpaka wengine wamefanya mtaji wa kisiasa kwenye majimbo yao kisa Richmond. Hao kina shelukindo na wenzake nilijua watakumbana na the so called NIDHAMU YA CHAMA, na hapo ndo mwisho wao, walaaniwe kwa kuwalaghai watanzania eti kwamba wao ni wapambanaji wa ufisadi!!
Nakwambia mpambanaji mahiri yuko vyama vya upinzani. Kama tungewapata kina Slaa watano tu, weacha tu. Wanaoshupalia kukaa CCM wanaimba nyimbo tu, hakuna kitu kutarajia kutoka kule. Nani awezaye kumlaani mama yake akafanikiwa?
 
Ni mpaka hapo watanzania tutakapo amua kwa utashi wetu kuwa hatuwataki fulani na fulani watuongoze kwa sababu moja, mbili,tatu n.k,tutakuwa watu wa kuzungukazunguka huku na huko,yule kachemcha wizara hii anahamishiwa kule kama vile hakuna watu wenye uwezo...........na na kwambia CCM itatawala mpaka pale watu watakapokubali kubadilika(sio CCM Kubadilika)

SAFI nakuunga mkono hoja yako,

Hapa kuna swala lasisi watanzania kubadilika jamani, ivi idadi ya wabunge bungeni ni wangapi na sie wapiga kura ni wangapi? mbali na hilo sie watanzania ndi chanzo cha hayo yote mtu anakuja kukuhonga vijisenti na kesho waenda mchagua wategemea hao viongozi watatukumbuka tena????

Tuendelee kupigwa danadana mpaka siku wajukuu zetu watakapo amua sasa inatosha ndipo nchi itasonga mbele

 
Back
Top Bottom