Hatimaye ile taarifa ya serikali kuhusu utekezaji wa Azimio la Bunge kuhusu Richmond, inawasilishwa kwa mara ya tatu na ya mwisho katika kikao cha bunge cha leo, na wabunge wa CCM, wameshakubali kwa kauli moja, kuipokea taarifa hiyo na kuikubali bila kipingingamizi chochote, kwa mtindo wa funika kombe, mwanaharamu apite!.
Uamuzi huo umefikiwa usiku huu wa manane, katika kikao cha wabunge wa CCM, kilichofanyika ukumbi wa Msekwa kwa hoja kama hawatakubali kulimaliza suala hilo katika kikao hiki, muda uliobakia wa maisha ya bunge hili katika kikao kijacho ni miezi mitatu tuu, hivyo kuendelea kuisulubu serikali kuelekea uchaguzi, ni sawa na kukata mti huku umekalia tawi la mti uukatao.
Hivyo kesho kwa kauli moja, wabunge wote wa CCM, watakuwa kitu kimoja kuunga mkono taarifa hiyo ya serikali, hivyo kuhitimisha rasmi mjadala huu uliosubiriwa kwa hamu na umma wa watanzania.
Uungwaji mkono huo, pia ndio utakuwa ishara ya kuvunjwa rasmi kwa ile kambi ya wabunge, waliojipambanua kama wapambanaji dhidi ya ufisadi, baada ya kundi hili, kuishikia bango serikali kuiamuru kutekeleza azimio la bunge, ambapo serikali siku zote imekuwa ikakaidi.
Kama ni kweli, wabunge hao wapambanaji, watakubali kufunika kombe, huu pia ndio utakuwa uthibitisho wa jibu sahihi la swali la mwana JF, maarufu na mashuhuri, kuliko wana JF wengine wote, Mzee Mwanakijiji, alilouliza siku za nyuma, "Jee Wapiganaji Walioko CCM, Wanapigania Nini?".
Kuungwa mkono kwa hoja ya serikali, pia kutathibitisha ukweli wa kile kitisho dhidi ya Spika Sitta, wengi wakidhani kuwa anatishiwa nyau, hivyo atasimama imara, kumbe sio kitisho cha nyau, ni kitisho kweli, hivyo Bunge la Kasi na Viwango, hatimaye litapiga magoti kwa serikali na kusujidia.
Kama kweli, hao makamanda watakubali funika kombe hiyo, kwa kazi yote na mbwembwe na majigambo ya Kamati Teule ya Dr. Mwakyembe, huu ndio uthibitisho tena wa chama kushika hatamu za kuiongoza serikali, na kele zote za wapiganaji, kumbe hizo ndizo zilizokuwa tisha nyau.
Na mwisho kabisa, huu ndio utakuwa mwanzo mzuri wa utakaso kumsafisha Muzee, na consolidation ya ule mtandao uliosambaratika, kuunda the 'winning coalition' ya 2015, chini ya The King Maker in absentia, yuko kwa Mandela sasa hivi huku nyuma mambo yanaiva!.
Majibu ya hayo yote, yashuhudie live leo , baada ya kipindi cha maswali na majibu, Bungeni kupitia TBC na Star TV!
Update 1: Ripoti inashushwa live na Mwenyekiti, wa Kamati ya Nishati na Madini, Mbunge wa Bumbuli, Mhe. William Shelukindo.
Ripoti imeridhia kujiuzulu kwa EL imetosheleza na kuridhika na uamuzi wa serikali. Kwa vile bunge lilitaka Hosea awajibishwe, na Hosea akaamua kuwachunguza wabunge, Kamati imeonelea imwachie mkuu wa nchi kuamua cha kufanya.
Kombe limefunikwa, Mwendawazimu Richmond, kapita!
Wachangiaji ni 6 tuu.
Uchangiaji unafuatia...