Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Na Born Again Pagan
Kutoka gazeti la KWANZAJAMII juma hili


Production Sharing Agreement (PSA)

KATIKA mikataba mingi kati ya Tanzania na wawekezaji wa nje kuna kifungu cha PSA (Production Sharing Agreement): Mfano, mwekezaji kubaliwa A anaweza kushirikiana na mwekezaji mwingine mpya chaguliwa B katika mkataba uliosainiwa na mwekezaji A, endapo ataiarifu na kupata idhini ya serikali ya Tanzania.

Ukiangalia makampuni yaliyokwishajiingiza katika mikataba mingi ya awali baina ya Tanzania na wawekezaji wa nchi za nje, utagundua msululu wa makapuni mapya ya PSA, kwa mifano, mikataba ya migodi ya madini na gesi.

Ndio maana ingawa Rais Jakaya Kikwete aliamuru mikataba mingine mipya isisainiwe, hadi hapo Tume ya Jaji Bomani itakapopitia na kutoa ripoti yake kwa serikali, bado mikataba ya PSA mipya inafunguliwa na kutiwa saini.

Tunayangoja hayo ya Utekelezaji wa Ripoti ya Jaji Bomani!

Ukiachilia mbali hayo ya Tume ya Jaji Bomani, si siri kwamba makampuni ya madini ya dhahabu na gesi yamekuwa yakiongeza wawekezaji wapya, kupitia PSA, na serikali ya Tanzania kuridhia makubaliano hayo bila kizuizi chochote.

PSA imulikwe wazi. Makampuni ya migodi ya dhahabu (Barrick), almasi, nickel na uranium, na visima vya gesi (Songas) na mafuta huingiza wawekezaji wapya kupitia PSA, hususan pale ambapo serikali yetu huwapa hao wawekezaji kumiliki maliasili yetu kwa 100%! Inakuwa ni mali yao; na wanayo haki ya kuigawa mali hiyo kwa wale wawapendao.

Nashauri kuwepo na u-wazi wa kuhusu si makampuni mapya yaliyojiingiza kupitia psa bali pia uwazi wa kuhusu wazawa wapi walio na hisa katika makampuni hayo. Kwa nini nashauri hivyo? Mambo matatu ya wazi yanayozalisha “vi-ji-senti”.

Moja, ni utata wa kampuni ya Richmond Development Corporation LLC, ambayo mambo yaliyojitokeza yalifunua shinikizo la “vigogo” na “wakubwa” wa serikali kukiuka maadili yenye maslahi ya taifa!

Mbili, Mheshimiwa m-Bunge “kijana” Kabwe Zuberi Zitto (CHADEMA Kigoma Rural) alikuja na tuhuma dhidi ya aliyekuwa Waziri wa Umeme na Nishati Nizar Karamagi kukimbia hima huko London na kusaini mkataba hotelini na kampuni ya migodi ya dhahabu ya Barrick huko Buzwagi!

Pengine, Mheshimiwa Waziri wa Umeme na Nishati Nizar Karamagi alitia saini kuridhia tu mkataba wa awali wa Barrick kwa kupitia mapatano ya PSA!

Tatu, aliyekuwa Waziri wa Umeme na Nishati Bwana Nizar Karamagi, huyo huyo, ana pia kampuni yake ya “ukuli” hapo Bandarini. Sijui naye aliiunda lini? Pengine, alijua kuwepo kwa PSA. Hivyo, kaiunda kampuni hiyo, ambayo hatuwajui wenye hisa, na hapo baadaye Rais Benjamin Mkapa kuiongezea muda wa kumiliki “ukuli” hapo bandarini kutoka miaka 15 hadi 25 bila kibali rasmi!

Tunaambiwa kuwa Tanzania iliingia mkataba na kampuni moja ya Houston, Texas, Amerika, ya Richmond Development Corporation, LLC, yenye kufua umeme wa dharura kutokana na ukame uliosababisha mabwawa yetu ya maji kutosetri ufuaji wa umeme. Wamiliki wa Richmond Development Corporation, LLC. Ndio walikuwa na 100% za hisa za kampuni hii.

Lakini cha kushangaza ni kwamba “wamiliki’ fulani walipoona uhondo upo katika mkataba huo, waliunda kampuni yao ya Richmond Tanzania Ltd na kuisajili “mwezi zaidi ya mmoja baada ya mkataba huo kusainiwa, pengine, kupitia psa.

Wana hisa wa kampuni hii ni LLC na Naeem Gire, kulingana na habari rasmi tupatazo, kama ifuatavyo: “(k)atika mchanganuo wa hisa, Gire ana miliki 250,000 na LLC 750,000 huku ikianza na mtaji wa Sh1,260,000,000 (1.2 bilioni).”

Je, si huyu huyu “mfanyabiashara” aliyeshindwa kabisa kuweza kupata mapesa ya kusafirishia mitumba yake hadi hapo serikali yetu ilipoingilia kati kupitia CDRB?

Serikali iweke wazi “offshore bank accounts” zote, bila kujali mwenye akaunti ni nani! Uswisi imepokea na kukubali ombi la Amerika la kuitaka Uswisi ifungue akaunti za wa-Amerika mafisadi katika benki ya Union Bank of Switzerland (UBS)!

Zaidi, kama tunataka kupambana na ufisadi, serikali iamke kuwa taifa letu limehujumiwa na linaendelea kuhujumika. Kwahiyo, sheria itungwe ya kumulika wenye hisa katika makampuni ya ugeni na ya uzawa ili tujue ni wa-Tanzania walionunua hisa katika makampuni hayo.

Mianzo Mingine ya Nishati!

Kwa nini Tanesco imekuwa ikiigeuka kinyonga? Tanesco ilikataa kununua mitumba ya Dowans; Tanesco ikakubali na kukiuka msimamo wa Bodi yake; na sasa Tanesco imekataa tena! Kulikuwa na tetesi kwamba Tanesco ilitaka kununua mitambo hiyo mitumba tena!

Je, Tanesco haikutuambia, “Potelea mbali hata kama nchi inazama gizani?”

Je, Bodi ya Tanesco nayo ilifanya uamuzi mzuri wa kutaka kutuma tena wataalamu wa Tanesco waende huko Houston, Texas, kuzatiti bei hasa ya mitambo (turbines) hiyo ya kufua umeme?

Ni kupoteza mapesa ya umma; Ofisi yetu ya u-Balozi, Washington, DC, inaweza kufanyakazi hiyo (kulingana na sera ya diplomasia ya uchumi) na huyo “Balozi Maalum” Kjell Bergh anaweza, pia kusaidia!

Brela iliamua kuifuta “Richmond” ifikapo Septemba 15, 2008 kutokana na ufisadi na utata uliozalisha kashfa ya “Richmond”! Lakini kufuatia kushindwa kufua umeme wa dharura, leo hii bado tunaikumbatia “Richmond” kwa jina la “Dowans”! Malumbano yalijitokeza ya kukidhi mahitaji ya umeme kwa kununua mitumba ya mashini za “Richmond/Dowans”!

Wenye kutaka mitumba hiyo inunuliwe, walizua mantiki ya kuunda na kutekeleza sera za umeme na nishati hadi 2014! Waliihurunmia “Dowans” kwa kuvaa nondo ya uzalendo: Tanesco na Kamati ya Bunge ya Ununuzi – Mashirika ya Umma).

Sasa hivi Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ununuzi, Mheshimiwa m-Bunge Kabwe Zuberi Zitto analilia mitambo mitumba ya Dowans itaifishwe ili kukidhi uhaba wa umeme.

Waziri wa Nishati na Madini, na akili zake, aliamuru hiyo mitumba inunuliwe! Hata kwa Ikulu ikadiriki kutamka eti Tanesco ni kampuni kamili yenye kufanya itakalo ni kukiuka uwajibikaji – uongozi unaokwenda kombo!

Kwa nini tunang’ang’ania mitambo mitumba, tena ya ghali, ya “Dowans” – kampuni ambayo haistahili kuwepo na ambayo imetushitaki huko Paris?

Lini tutaamka! Ama tuliishaga-kula “vi-ji-senti” vingi vya wawekezaji ambavyo vinatufunga nongwa na mitambo ya kufua umeme kwa mabwawa ya maji? Si ni afadhali tufuge samaki kwa wingi katika mabwawa hayo au tuyatumie katika umwagiliaji mashamba?

Hivi tuliambiwa na Muumba kuwa chanzo cha umeme na nishati ni mabwawa yetu tu? Mbona hatufundishiki kuwa tunaathiriwa na ukame kila mwaka?

Tufikirie mbinu nyinginezo za kufua umeme:

Moja, yatubidi tufikirie kwa makini namna ya kuigawa Tanesco. Kwani Tanesco ya Dar es Salaam ikikohoa tu, mikoa yote inapata homa!

Mfano, hapa Amerika kulikuwa na shirika kubwa la simu la Bell System au kwa jina la uzazi, Ma-Bell. Shirika hili lilikuwa limetamalaki karibu nchini kote. Lilishindwa kutoa huduma kwa wananchi. Ilibidi Ma-Bell igawanywe kwa watoto wake, “Baby-Bells” - wengi.

Hivyo hivyo, sioni sababu kwa nini tusiwe na Tanesco za Kanda ili kama Tanesco ya Dar ikishindwa nchi nzima isipate homa!

Mbili, tulijaliwa kuwa na mito mingi. Sioni sababu, kama tunazidi kutegemea maji/mabwawa tusijenge mitambo mingine kwenye mito yetu, kwa mifano, Mto mara hapo Kirumi na mto Simiyu. Mito hii pamoja na mitambo ya Rubanda? Kagera inaweza kutosheleza mahitaji ya umeme kanda za Ziwa Victoria.

Tatu, Tanzania ni lazima idumishe uhusiano na nchi za Kusini mwa Afrika, SADC. Jumuia hii isiwe ya mikutano ya wakubwa tu bali ifikirie namna ya kuweza kufua umeme kwa mahitaji ya Kusini mwa Afrika kutoka vyanzo vya Mto Kongo ,ambao maji yake yananyesha misitu na mengi kuingia bahari ya Atlatiki.

Nne, twende nuklia kwa matumizi ya amani (utabibu na nishati – kwani uranium tunayo kwa wingi)! Kwa nini wawekezaji wachimbe na kuuza nje kwa manufaa yao na kutuachia mashimo na mazingira yaliyoharibika)!

Tano, jua tunalo, tena la masaa 12!

Sita, upepo tunao tena wa nguvu kuweza kuzungusha mapanga ya mitambo ya kufua umeme huko milimani, mabondeni na tambarare!

Saba, gesi tunayo tena inachotwa pengine kuuzwa nchi za nje ili makapuni yapate faida – uwekezaji wa kutoka nje sio asisi ya Mama Tereza!

Nane, maji-mvuke moto moto tunayo!

Bio-gesi tunaweza kuzalisha!

Tisa, na hata mawimbi ya maziwa na bahari yanaweza kuchangia hilo la uhaba wa umeme!


romuinja@yahoo.com
 
• Kimaro asema anaweweseka kutaka Dowans inunuliwe

na Deogratius Temba

KAULI aliyoitoa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), akiliomba Bunge liunde kamati huru kuchunguza upya sakata la kuhusika kwake na Kampuni ya Richmond Development LLC ili apate nafasi ya kusikilizwa, imewatibua baadhi ya wabunge wa chama chake.

Wabunge hao walisema Rostam anaweweseka na kashfa ya Richmond, na kumtaka akasome vizuri kanuni za Bunge ili ajue kwamba suala likishaamuliwa na Bunge, haliwezi kuundiwa tume nyingine nje ya Bunge.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana katika mahojiano maalum na Tanzania Daima, Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro, James Lembeli (Kahama) na Lucas Selelii (Nzega), walisema Bunge likishahitimisha hoja, haliwezi kurudi nyuma kuijadili upya, na kwamba Rostam anapaswa kufuata kanuni za Bunge.

Kimaro alisema hakuna sheria wala kanuni ya Bunge inayotamka kuwa kamati teule ya Bunge ikifanya kazi yake na Bunge likaridhia, inaweza kuundiwa tena kamati nyingine nje ya Bunge.

“Bunge limeshamaliza kazi yake, hakuna cha kurudia hapo, wala kanuni za Bunge haziruhusu kufanya vile, nafikiri hajakisoma kitabu cha kanuni za Bunge ndiyo maana anaweweseka, vinginevyo asingesema hayo.

“Ninawashauri Watanzania kutojiingiza katika mjadala huo, umeshafungwa na Bunge likatoa mapendekezo yake, na sasa tunaisubiri serikali itekeleze na si mtu mwingine aje tena bungeni kuleta hoja hiyo hiyo, hapana sisi tunapiga hatua nyingine mbele,” alisema.

Alisema kama kuna watu hawakuridhika na kazi iliyofanywa na kamati teule ya Bunge iliyokuwa ikiongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, wasifikiri kuwa kuna huruma tena au wakipiga kelele watapata msamaha.

“Tena wasifikiri kuwa kwa kupiga kelele vile serikali inaweza kuifikiria tena Dowans, hilo limepita na serikali haitainunua mitambo hiyo kwani hata sheria hairuhusu. Sheria ya umeme ya mwaka 2008, imeeleza waziwazi kuwa kama kuna watu waliohusika kudai ‘capacity charge’ wasipewe nafasi ya kuiuzia TANESCO umeme,” alisema Kimaro.

Alidai kuwa, kinachomsumbua Rostam hadi kufikia kuliomba Bunge liunde kamati upya, ni kutaka mitambo ya Dowans inunuliwe.

“Mimi ninataka kujua kinachomkera au kinachomfanya aweweseke ni nini? Awaeleze Watanzania waelewe, atumie muda huu kuueleza umma kama ana maslahi gani na Dowans au iliyokuwa Kampuni ya Richmond na si kulitakia Bunge kazi ambayo si yake,” aliongeza Kimaro.

Naye Lembeli, alisema Bunge ni kwa ajili ya Watanzania wote na maamuzi yaliyotoka ni ya wote.

Alisema Rostam hajaonewa na kamati kwani ilitoa ripoti na wabunge wote wa CCM wakaiunga mkono kwa pamoja, kwa hiyo ilifanya kazi yake.

“Tatizo si kuonewa wala kamati teule ya Bunge, Rostam atafute kanuni za Bunge azisome na aelewe zinasemaje, kwanza asiionee kamati, sisi wabunge ndio tuliopitisha ripoti, kama tungeona ina makosa na kubaini kuna mtu ameonewa, tungeikataa.

“Anapotumia muda mwingi kudai kuwa iundwe kamati upya, mara jopo la majaji kuchunguza upya, mbona alishajitokeza mara kadhaa kwenye vyombo vya habari akadai kuwa hausiki? Kwani hilo halitoshi? Mbona maelezo anayoyatoa kwenye magazeti kuwa hakuhusika hayaelezi kama alionewa? Na alionewa wapi?” anahoji Lembeli.

Akizungumzia suala hilo, Selelii, ambaye alikuwa mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo teule, alisema ndoto za Rostam ni za mchana na hazitekelezeki katika Bunge hili na kwa kutumia kanuni hizi za Bunge zilizopo.

“Hizo ni ndoto, tena za mchana, hakuna kitu kama hicho, Bunge lilishafanya kazi yake na kuimaliza, anachokitaka yeye hakiwezekani kwa Bunge la Tanzania, na kama ni kwa Bunge la hapa Tanzania basi si kwa kanuni hizi tulizonazo,” alisema.

Alisisitiza kuwa, siku zote mtu anayetuhumiwa kwa kukosa, hawezi kukubali kosa hata kama atachapwa namna gani, kwa hiyo huo ni ujanja ambao unatumika kujinasua na tuhuma hizo.

Selelii alimtaka Rostam achukue ripoti ya kamati hiyo, aangalie vipengele vyote vinavyomtaja kuwa anahusika na Richmond na Dowans, halafu aende kwenye hoja bila kuzunguka.

“Kama kweli Rostam ana uhakika na hayo malalamiko ambayo anayatoa kila mara na hata kupitia baadhi ya vyombo vya habari, arejee kwenye ripoti yetu ya kamati, asome maeneo yote yanayomgusa na kumhusisha na Richmond na Dowans, halafu ajenge hoja,” alisema Selelii.

Hivi karibuni, Rostam alikaririwa na chombo kimoja cha habari akiliomba Bunge liunde jopo la majaji watatu kuchunguza upya sakata hilo ili kutoa hukumu ya haki.

Siku chache baada ya Rostam kuomba Bunge liunde jopo hilo la majaji, Spika wa Bunge, Samuel Sitta, alisisitiza kuwa haiingii akilini, kwa mbunge huyo kutaka uchunguzi wa suala hilo ufanywe na majaji, na juzi mbunge huyo wa Igunga alirejea tena ombi lake la kutaka iundwe tume huru.

“Kwanza, labda nikwambie tu, maamuzi yaliyofikiwa na Bunge katika Richmond hayawezi kuchunguzwa upya na mhimili mwingine wowote wa dola.

“Tunazungumzia kumaliza suala la Richmond si kuanza upya, kama ana pesa zake (Rostam) za kulipa majaji, ni huko huko, lakini hilo haliwezekani,” alisema Sitta.

Alisema ushahidi mbalimbali ulionyesha uhusiano wa mawasiliano ya mbunge huyo na Richmond kisha Dowans.

“Hivi mnataka ushahidi upi zaidi? Ushahidi wa mawasiliano ulionyesha jinsi mtu huyu alivyokuwa akiratibu Richmond kisha Dowans,” aliongeza Spika.

Rostam, mjumbe wa Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, amekuwa akitajwa kama mmoja wa vigogo walioshiriki katika kufanikisha Richmond kupewa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura katika mazingira tata.

Mkataba na kampuni hiyo yenye taarifa tata kutoka Costa Rica na Marekani, ulisainiwa na TANESCO Juni 23, 2006.

Lakini baada ya kusakamwa kwa muda mrefu, alipopata nafasi katika kikao cha Kamati ya Mzee Mwinyi na wabunge wa CCM, iliripotiwa kuwa Rostam aliongelea kuundwa kwa tume huru kuchunguza kashfa nzima ya Richmond kwa madai ile ya Bunge iliyoongozwa na Dk. Mwakyembe, ilipotosha.

“Ripoti ya Richmond imeidhalilisha serikali kwa maslahi ya kisiasa. Ili mambo yaishe ni vema uchunguzi huru ukafanyika. Tusipofanya hivyo tutaendelea kuwachanganya wananchi.

“Msimamo wangu tangu kamati teule ya Bunge itoe taarifa yake bungeni, uko pale pale. Ripoti ilijaa upotoshaji na uongo. Nilitaka kuongea bungeni nikazuiwa,” alisema Rostam.

Kamati hiyo teule ilisema katika taarifa yake kuwa, Rostam aliitwa ili aeleze uhusiano wake na Richmond kutokana na kampuni hiyo kutumia anuani ya barua pepe na fax ya Kampuni Caspian na sababu za kuitafutia Richmond kampuni ya ushauri wa mambo ya habari, lakini hakujitokeza.

Rostam alijieleza katika mchango wake wa maandishi wakati wa kujadili ripoti ya Richmond kuwa, Kamati ya Mwakyembe ilimuita kumhoji Desemba 24, mwaka jana wakati ikijua kuwa siku hiyo asingeweza kupatikana kwa sababu ya sikukuu.


Source: Tanzania Daima
 
Rostam ingawa sio Mkiristo anapaswa kujua kwamba Bunge sio kama kanisani. Kanisani ni mahala ambapo injili unarudiwa rudiwa na kila wakati inatafusiriwa (tafakari) tofauti wakati ni injili ile ile! Bunge likisha jadili na kunena basi. Hakuna kurudia rudia kama kanisani. File closed.
 
Rostam ingawa sio Mkiristo anapaswa kujua kwamba Bunge sio kama kanisani. Kanisani ni mahala ambapo injili unarudiwa rudiwa na kila wakati inatafusiriwa (tafakari) tofauti wakati ni injili ile ile! Bunge likisha jadili na kunena basi. Hakuna kurudia rudia kama kanisani. File closed.

ByaseL, sio Mkiristo ni Mkristo! Huyu bwana Rostam alipotaka kuhojiwa na kamati teule ya Bunge chini ya uenyekiti wa Mwakyembe alikimbilia nje ya nchi, leo analidharau Bunge kwa kutaka Kamati nyingine "huru!" Hivi jamani uhuru wa Kamati unatokana na nini? Huyu mwarabu arudi kwao Iran asitubabaishe!
 
JIANG ALIPO, 27th January 2010 @ 04:14,
Daily News

The government is expected to table to the parliament report on the implementation of the Parliament’s resolution on the Richmond issue on February 12 this year.

According to the timetable that was released yesterday evening, the 18th session, which normally goes for two weeks, has been extended to three weeks.

The Richmond issue was expected to be discussed on the 17th session, in November, however, to the disappointment of many it was not tabled due to unknown reasons.

According to the timetable, the Richmond report, along with the report on poor performance of Rites, report on poor performance of TICTS, and report on privatization of Kiwira coal mine, are all going to be tabled on the same day.

Moreover, the timetable shows that opposition leader, Mr Hamad Rashid Mohamed (Wawi-CUF) and Mr Lazaro Nyalandu (Singida North-CCM) each will table private motions in the House.
 
Haha hii ndiyo byebye. Kinachofanyika hapa ni delay tactic kwa nini masuala yote yenye utata yamepangiwa kujadiliwa mwisho?. Believe me utaambiwa muda hautoshi, bunge likvunjwa August ndiyo imetoka. Na wabunge wapya wataambiwa kabisa tuanze upya tuache yaliyopita. This is TZ bwana!
 
tumechoka sasa, ya richmond yalishawekwa wazi na kamati... lakini kwasababu ya upupu wa wale imbecile walio bungeni kila kitu wanarudiarudia

kuna siku tutasikia bill ya azimio la arusha kupitia maamuzi ya kamati iliyokaa january 1967

inaf is inaf enyi wanasiasa
 
Hayo Mazingaombwe! Playing Dilly dally! Mnataka Moto Ushukuke toka Mbinguni ndio mjue kwambo hao ni mafisadi?? I hate indecisiveness! Sirikali Kibogoyo! Anyway your time is up! Mtuachie hizo kesi October mwaka huu mtatusikia!


 
Big joke! Halafu kumbe hizi mbinu za mwaka 47 bado zinatumika mpaka sasa?


Annina
 
Date::1/29/2010Porojo za Richmond zaendelea bungeni
spikasitta.jpg

Spika wa Bunge Samwel Sitta (kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk Emmanuel Nchimbi nje ya ukumbi wa Bunge jana mjini Dodoma, baada ya kumalizika kwa kikao cha tatu cha mkutano wa 18 wa Bunge.

Habel Chidawali Dodoma na Ramadhan Semtawa, Dar
Mwananchi

NGOJERA za kutolewa kwa taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge dhidi ya kashfa ya Richmond, bado zinaendelea baada ya serikali kushindwa kuiwasilisha katika mikutano mitatu iliyopita na jana Spika Samuel Sitta alilazimika kuwatoa hofu wabunge kuwa safari hii suala hilo litajadiliwa.


Katika mkutano uliopita kulikuwa na ahadi kama hizo kuwa suala hilo lingejadiliwa, lakini hilo halikufanyika na Spita Sitta alieleza kuwa lilitokana na Bunge la bajeti kupunguza muda kutokana na mtikisiko wa kiuchumi.


Hata hivyo, kabla ya suala hilo kuzimwa, suala hilo lilitawaliwa na sarakasi nyingi wakati wa vikao vya kamati za Bunge ambako pia serikali haikuwasilisha taarifa yake baada ya Waziri wa Nishati na Madini kueleza kuwa wamekubaliana na wajumbe wa kamati ya sekta hiyo kuwa ripoti hiyo isomwe Dodoma, ambako pia haikusomwa.


Jana wabunge walionekana kuwa na wasiwasi kuwa mkutano unaoendelea wa 18 wa Bunge unaweza usipatiwe ripoti hiyo kutokana na kujazwa pamoja na masuala mengine nyeti katika siku ya mwisho wa Bunge.


Mbunge wa Mpanda Kati (Chadema), Said Arfi jana alionyesha hofu hiyo wakati aliposimama kuomba mwongozo wa spika kutokana na kuhofu kama ratiba inaweza kutoa fursa ya kutosha kwa wabunge kujadili vema masuala mazito ya Richmond na Kiwira.


"Mheshimiwa spika, ukiangalia ratiba inaonyesha kuna mambo mengi mazito kama Kiwira na Richmond, lakini kwa mtazamo wako unafikiri siku zilizopangwa kwa mujibu wa ratiba zitatosha kwa wabunge kujadili mambo hayo kwa kina," alihoji Arfi.


Hata hivyo, Spika Sitta alimtoa hofu mbunge huyo akimtaka asiharakishe mambo kwa kuwa yeye (Sitta) anajua wajibu wake katika kutoa nafasi kwa wabunge.


"Aaa... sijui hii hofu ya nini, haya mambo yapo; yamepangwa katika ratiba na kila kitu kitajadiliwa kama kilivyopangwa, likiwemo suala hilo la Richmond," alisema Sitta.


Wasiwasi wa Arfi, ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa Chadema, pia unaongezwa nguvu na ratiba iliyotolewa juzi ambayo katika ukurasa wa sita inaeleza:


"Taarifa zitawasilishwa bungeni endapo yatakuwepo makubaliano kati ya kamati na serikali kuhusu ukomo na kufikia mwisho wa maazimio haya."


Ratiba hiyo inaonyesha taarifa hizo kuwa ni ya Richmond, kampuni ya Rites, Ticts, mgodi wa Kiwira pamoja na hoja binafsi kutoka kwa kiongozi wa kambi ya upinzani, Hamad Rashid Mohamed na mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu.


Kipengele hicho kinatia wasiwasi kama serikali ina nia ya dhati ya kuwasilisha taarifa hizo katika mkutano unaoendelea, ikiwa imebakia mikutano miwili kabla ya kuvunjwa kwa Bunge la tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kupisha uchaguzi mkuu.


Sakata la Richmond linahusu utoaji zabuni ya ufuaji umeme wa dharura kwa kampuni ya Richmond Development LLC kwa kukiuka sheria ya manunuzi, huku kampuni hiyo ikidhihirika baadaye kuwa haikuwa na uwezo. Bunge liliunda kamati teule ambayo ilitoa ripoti iliyoanika uozo uliozingira zabuni hiyo.


Edward Lowassa, ambaye hakutajwa kwenye ripoti ya kamati hiyo lakini akatakiwa atumie busara zake kufanya uamuzi baada ya vyombo vya habari kumtuhumu kuhusika, alijiuzulu uwaziri mkuu na kufuatiwa na mawaziri wengine wawili walioshika uwaziri wa nishati na madini kwa nyakati tofauti, Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha.


Baada ya kujadili ripoti hiyo ya kamati teule, Bunge lilitoa maazimio 23 ambayo ilitaka serikali iyashughulikie, lakini hadi sasa ni mambo machache ambayo yanaonekana yameshashughulikiwa na serikali inaonekana kusita kutoa taarifa tangu Waziri Mkuu Mizengo Pinda atangaze utekelezaji wa hatua za awali.


Sakata la Kiwira linahusu kitendo cha familia ya rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa kutuhumiwa kujiuzia mgodi huo wa makaa ya mawe kwa bei rahisi na kutouendeleza.


Miongoni mwa maazimio ambayo hayajatelekelezwa ni pamoja na kutowajibishwa kwa mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Edward Hosea), ambaye mamlaka yake ya juu ni rais.


Waziri Pinda alieleza kuwa Hoseah alishajitetea kwa Katibu Mkuu Kiongozi (Philemon Luhanjo), lakini mamlaka ya juu haijamwajibisha.


Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki, Spika Sitta alisema sasa hivi mzigo huo uko kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ambaye atatoa taarifa bungeni.


"Watu wasiulize bunge litafanya nini, tayari bunge limeagiza na anayesubiriwa ni waziri mkuu ambaye ndiye atapaswa kueleza nini kimefanyika lakini siyo tena bunge kuulizwa," alisema Sitta ambaye wakati akifunga mkutano wa 17 mwaka jana alisema asingependa kuona mwaka 2010 ukianza huku suala la Richmond likiendelea.
Jana mchana, Kamati ya Nishati na Madini ilitarajiwa kukutana kwa ajili ya mambo mbalimbali, ikiwemo kashfa hiyo.
 
Basi tuwasubirie tuone ukweli na uongo uliopo, japo hata mi siamini kama utajadiliwa! Halafu nadhani hiyo repoti itakuwa imefanyiwa proofreeding na kuwa edited to make majority of us blind. I don't even believe kama bado ni mbichi.
 

pix.gif
“Watanzania wanataka kujua mwisho wa mjadala huu kwa sababu kubwa mbili, moja kashfa yenyewe ya Richmond imeichafua serikali yao na pili kamati teule ya Bunge imetumia mamilioni ya fedha kufanyia uchunguzi na kukusanya taarifa ya jambo hilo."...
Bila shaka ndugu zangu hamjambo na Mungu amewajalia kuwa na afya njema, tumshukuru kwa hilo.
Wiki hii niwakumbushe tu waheshimiwa wabunge ambao wanatarajia kwenda Dodoma kwenye kikao chao kuwa, pamoja na mambo mengine watakayokwenda kufanya, suala la Kampuni ya Richmond iliyopewa mkataba wa kufua umeme Juni 23, 2006 baada ya nchi kukumbwa na tatizo la ukame na kusababisha mabwawa kukauka limechosha na linahitaji kufikia mwisho.

Watanzania wengi tuna kumbukumbu kuwa suala la Richmond litawekwa mezani ndani ya bunge katika kikao kijacho kitu ambacho tunaomba safari hii liishe kwa kuwa wananchi wamechoshwa nalo na wanataka mjadala wa kitu kipya kwa manufaa ya nchi yetu.

Kitu ambacho kinasababisha maneno yasiishe kuhusu sakata la Richmond ni maazimio ya bunge kutotekelezwa na serikali hasa kwa kuwa chombo hicho cha kutunga sheria za nchi kilishayatoa kikitaka baadhi ya watendaji ndani ya serikali wawajibishwe.

Ndugu zangu hakuna siri, waliotakiwa kuwajibishwa ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Dk Edward Hosea, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Arthur Mwakapugi na Mkurugenzi wa Nishati Bw. Bashir Mrindoko. Sababu za watu hao kutakiwa kuwajibishwa, kamati teule ya Bunge chini ya Dk Harisson Mwakyembe ilisema wazi na sina haja ya kuzirudia.

Mimi sijui sababu ya serikali kuendelea kuvutana na wabunge kuhusu sakata hilo, ambapo kitu kinachosababisha kila kikao cha bunge suala la Richmond kuzua mjadala mkali. Hakika Watanzania wana haki ya kujua nini sababu ya wabunge wetu kuchukua muda wao mwingi kujadili kitu kile kile kila wanapofanya kikao mara baada ya sakata hilo kuibuka.

Watanzania wanataka kujua mwisho wa mjadala huu kwa sababu kubwa mbili, moja kashfa yenyewe ya Richmond imeichafua serikali yao na pili kamati teule ya Bunge imetumia mamilioni ya fedha kufanyia uchunguzi na kukusanya taarifa ya jambo hilo.

Watanzania wengi wanakumbuka jinsi wajumbe wa kamati hiyo walivyotembea na kufika hadi Marekani kuchunguza sakata hilo kwa kutumia fedha za walipa kodi, hivyo, wananchi wana kila sababu ya kutaka kujua mwisho wa kashfa hiyo katika kikao kijacho cha bunge.

Ndugu zangu, mtakubaliana nami kuwa suala la Richmond limekera Watanzania wengi na hata baadhi ya viongozi wakiwemo wabunge wenyewe ambao wameonesha kukereka kutokana na kutokwisha kila linapofikishwa bungeni.

Ndugu zangu, wabunge wanapaswa kujua kwamba si vema kuchukua muda mwingine mrefu kujadili kitu ambacho kamati teule yake iliona na bunge lenyewe kuelekeza nini kifanyike baada ya kutoa maazimio.

Kama nilivyosema hapo juu, nchi yetu ina matatizo mengi ambayo wabunge kama wawakilishi wa wananchi wanapaswa kujadili kama vile hivi sasa majanga ya mafuriko, barabara kuu kukatika kwa maji, njaa, matatizo katika sekta ya elimu, afya na kadhalika.

Watu wa kuyatafutia ufumbuzi mambo haya ni wabunge kwa kuwa wao wana nafasi ya kukutana na watendaji wa serikali kuu moja kwa moja ndani ya bunge. Wasikwepe jukumu hili.

Pili, hivi sasa hakuna asiyejua kuwa nchi yetu imeingia katika mwaka wa uchaguzi na kuna mambo mengi ya msingi ambayo wananchi wanapaswa kueleweshwa. Kwa mfano, baadhi ya wapiga kura wahamasishwe kujiandikisha (wale ambao hawajajiandikisha kutokana na kufikia umri wa kupiga kura mwaka huu au kutokana na kutojiandikisha siku za nyuma.)

Ndugu zangu, huwa inasikitisha sana kuona kati ya Watanzania milioni zaidi ya 15 wanaostahili kupiga kura, wanaojiandikisha wanakuwa wachache mno, hii inamaanisha kuwa elimu ya uraia hakuna kabisa kwa wananchi wetu. Watu wanashindwa kujua kuwa wana wajibu wa kuhakikisha anapatikana kiongozi safi katika maeneo yao wanayoishi.

Hakika hili la kuhamasisha watu kupiga kura, ni jambo zito linalopaswa kufanywa nchini mwetu na wabunge, hivyo wasikwepe jukumu hilo.

Jipu limepasuka siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.

http://www.globalpublisherstz.com/pasua_jipu/
 
Tatizo liko kwa "wapiganaji" ambao wanaona wasipoongelea suala la Richmond hawatapata kura majimboni mwao ambako hawajafanya chochote cha kujitetea kwa wapiga kura wao! Wamesahau kwamba waliyotoa yalikuwa ni "mapendekezo" na sio "maagizo" kwa Serikali! Badala yake Bunge limegeuza mapendekezo 23 kuwa maagizo kwa Serikali! Wabunge wamedai eti mapendekezo yasipotekelezwa "wataenda mbali zaidi," wengine wamedai "wataishtaki Serikali kwa wananchi!" Sasa Bunge ni "Baba wa Serikali?" Wabunge fuateni mipaka ya kazi yenu, si vinginevyo! Mkijiingiza kwenye utendaji kama mtakavyoanza kwa upande wa "posho za maendeleo ya majimbo" mtajiharibia sifa zenu!
 
tatizo ni jinsi ya kutekeleza hayo mapendelezo / maazimio ya kamati ya bunge ndiyo inakuwa kikwazo kikubwa kwa serikali - na kama bunge likingangania msimamo wake kwamba lazima maazimio yote yatekelezwe mmhh tusubiri mengine yaja.
 
Jamani nimesikia kuwa majibu juu ya utekelezaji wa azimio la bunge kuhusu tenda ya umeme na sakata la RICHMOND yatatolewa mwishoni mwa kikao cha bunge kinachoendelea. Wenzangu mnasemaje kuhusu hilo, je mnadhani itakuwa ni kwa faida ya Watanzania au Vigogo wataendelea kulindana? Au ndo litasogezwa hadi Bunge litakalo anza baada ya uchaguzi mwishoni mwa mwaka huu? Kazi ipo!😕
 
Back
Top Bottom