Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Wakati kuna kila dalili ya suala la Richmond kujadiliwa kwenye Kikao cha NEC ya CCM mwezi ujao baadhi ya Wabunge wa chama hicho ambao wameshtushwa na uamuzi huo wamedai kwamba kufanya hivyo ni kuvunja Kanunig na Sheria za Bunge na kuwavunja moyo wapiga kura!

Wabunge hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe walienda mbali kwa kusema iwapo hoja hiyo itafikishwa katika vikao hivyo na kujadiliwa, itaonesha dhahiri jinsi chama hicho kinavyoendeshwa na watu wachache wenye ushawishi wa fedha badala ya kuwatumikia wananchi.

"Kushindwa kuwasilisha hoja ya Richmond katika Mkutano wa 17 wa Bunge na kutaka iwasilishwe katika vikao vya chama ni ushahidi tosha kuwa nchi hii inaongozwa na kundi fulani la watu wenye fedha ambao wana uwezo wa kuamua jambo lolote ndani ya chama na serikali kwa maslahi yao binafsi na si ya taifa." Alisema mbunge mmoja.

Mbunge wa Nzega Mh Lucas Selelii alisema kuwa tayari Bunge limetoa mapendekezo 23 kwa ajili ya hoja hiyo, Chama hakina nafasi ya kujadili jambo hilo la sivyo litakuwa limevunja kanuni na Sheria za Bunge!

SOURCE: Majira, tr 15/11/2009, uk. 1, 4.
 
Haka kawimbo ni katamu sana kanaonekana "Richmond" Kila kukicha kamo! ila mie nimekachoka kabisa
 
CCM kupitia NEC ikifanya hivyo itakuwa imetenda kosa la UHAINI na inastahili adhabu kali toka kwa wananchi.
 
Dawa yao imeshatimia,......ki kutowachagua Mafisadi wote...na wala kutorudisha majina yao.....hivi jeshi na vyombo vya usalama vinafanya nini??wanaangalia tu ujinga wa wanasiasa???wanafanya wanavyotaka??inasikitisha sana.....hawajui wajibu wao kama vyombo vya dola...na usalama pia....corrupt....
 
Dawa yao imeshatimia,......ki kutowachagua Mafisadi wote...na wala kutorudisha majina yao.....hivi jeshi na vyombo vya usalama vinafanya nini??wanaangalia tu ujinga wa wanasiasa???wanafanya wanavyotaka??inasikitisha sana.....hawajui wajibu wao kama vyombo vya dola...na usalama pia....corrupt....

Kaka naona umesahau, TZ inaongozwa na wanasiasa na si wengine, hivyo hakuna vyombo vya dola vyenye nguvu kuliko wanasiasa. Ndo maana wakuu wa hivyo vyombo baadaye hukimbilia kwenye siasa. Pili wanasiasa ndo wanawateua wakuu wa usalama wa nchi hii nao ni marafiki je ni lini rafikiyo mnaekula wote akakugeuka eti kisa professionalism? Huwezi kuona mfano polisi wanamaisha magumu lakini angalia maafisa wao wanaishi kama wafalme. The same to JWTZ.

So, wake up! ingawa Lucky dube alisema "if i m dreaming don wake me up, if it's a lie don tell me the truth cause what the truth will do? it will only hurt my heart"
 
jamani eeh...sisi ccm tumekuwa tukisema na tunarudia tena kwamba tuacheni tulivyo....eeh mwenye wivu ajinyonge kazi kutuonea gele tu jamani vipi,,,,,subirini tule vya kwetu tumepigania uhuru sisi wenyewe kwani nyie mlikuwa wapi? mbona hivo wajameni? hayo mnayosema ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa,,,hatusikii hatuambiliki.....kagoda yetu,richmond yetu,deep green finance yetu,mambo ya trl aka rites ni sie,tics,kiwira ndio ccm,tuacheni kwani tunafaidi vya kwetu.
hata hivyo mnalalamika tu na hamuwezi kutufanya lolote la sivyo yangekuwa yametimia mpaka leo
 
sisi ccm baba lao ,watz wote tumewaweka mfukoni.hakuna anayeweza kutuondoa madarakani na wajinga ndio waliwao....sisi tuna mbinu nyingi sana za kushinda na tunashinda kwa vyovyote vile,nchi yetu............
 
Mafisi-adi kama wangekuwa na uwezo wa kumhonga Mungu wangemhonga ili awasahaulishe wadanganyika kuhusu Richmond, TRL, Deep Green Finance, Kagoda, Meremeta, EPA, etc lakini wapi! Haya mambo hayatasahaulika mpaka wadanganyika watakapoamka na kuichukua nchi yao toka makucha ya mafisi-adi!
 
Haka kawimbo ni katamu sana kanaonekana "Richmond" Kila kukicha kamo! ila mie nimekachoka kabisa

Huu wimbo (Richmond) utaisha pale mdundo (utekelezaji wa maazimio 23 ya Bunge) utakapoisha! That's the only and final solution!
 
Swala la Richmond ni la kila mwananchi wa Tanzania na si kila mwana CCM, wasijewakajaribu kufanya NEC ndio mwamuzi wa mwisho. Wameshafulia!! wamelikoroga, walinywe sasa...
 
namkumbuka nyerere....hakuna kesi ...unaenda jela bila kutaka...

Si hivyo tu mkuu, bali ulikuwa unaliwa fimbo 12 wakati unaingia na 12 wakati unatoka ili ukamwonyeshe mkeo. Kuna kile kiboko kinaitwa aswa ishirini (hebu nipe correct spelling) ukichapwa tu kinabiringika na wewe ni kama cha chuma vile. Alama hazifutiki ati.
 
CCM ni kichaka cha wezi hakina budi kuwa 'cleared', mijizi isipate pa kujifichia
 
Ibara ya 15:1 inafanya kazi na hakuna Mbunge timamu wa CCM anayeweza kupinga hilo hadharani. Hajipendi?
 
Ibara ya 15:1 inafanya kazi na hakuna Mbunge timamu wa CCM anayeweza kupinga hilo hadharani. Hajipendi?

Ha ha ha. Mwanakijiji mimi nimepiga Magoti namuomba Mungu amtie Nguvu na Ujasiri Makamba aihitaji hiyo Ripoti kwenye NEC. Nitafurahi sana kama Ripoti ikifika NEC
 
Back
Top Bottom