Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,192
- 1,972
Wakati kuna kila dalili ya suala la Richmond kujadiliwa kwenye Kikao cha NEC ya CCM mwezi ujao baadhi ya Wabunge wa chama hicho ambao wameshtushwa na uamuzi huo wamedai kwamba kufanya hivyo ni kuvunja Kanunig na Sheria za Bunge na kuwavunja moyo wapiga kura!
Wabunge hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe walienda mbali kwa kusema iwapo hoja hiyo itafikishwa katika vikao hivyo na kujadiliwa, itaonesha dhahiri jinsi chama hicho kinavyoendeshwa na watu wachache wenye ushawishi wa fedha badala ya kuwatumikia wananchi.
"Kushindwa kuwasilisha hoja ya Richmond katika Mkutano wa 17 wa Bunge na kutaka iwasilishwe katika vikao vya chama ni ushahidi tosha kuwa nchi hii inaongozwa na kundi fulani la watu wenye fedha ambao wana uwezo wa kuamua jambo lolote ndani ya chama na serikali kwa maslahi yao binafsi na si ya taifa." Alisema mbunge mmoja.
Mbunge wa Nzega Mh Lucas Selelii alisema kuwa tayari Bunge limetoa mapendekezo 23 kwa ajili ya hoja hiyo, Chama hakina nafasi ya kujadili jambo hilo la sivyo litakuwa limevunja kanuni na Sheria za Bunge!
SOURCE: Majira, tr 15/11/2009, uk. 1, 4.