Na Born Again Pagan
Kutoka gazeti la KWANZAJAMII juma hili
Production Sharing Agreement (PSA)
KATIKA mikataba mingi kati ya Tanzania na wawekezaji wa nje kuna kifungu cha PSA (Production Sharing Agreement): Mfano, mwekezaji kubaliwa A anaweza kushirikiana na mwekezaji mwingine mpya chaguliwa B katika mkataba uliosainiwa na mwekezaji A, endapo ataiarifu na kupata idhini ya serikali ya Tanzania.
Ukiangalia makampuni yaliyokwishajiingiza katika mikataba mingi ya awali baina ya Tanzania na wawekezaji wa nchi za nje, utagundua msululu wa makapuni mapya ya PSA, kwa mifano, mikataba ya migodi ya madini na gesi.
Ndio maana ingawa Rais Jakaya Kikwete aliamuru mikataba mingine mipya isisainiwe, hadi hapo Tume ya Jaji Bomani itakapopitia na kutoa ripoti yake kwa serikali, bado mikataba ya PSA mipya inafunguliwa na kutiwa saini.
Tunayangoja hayo ya Utekelezaji wa Ripoti ya Jaji Bomani!
Ukiachilia mbali hayo ya Tume ya Jaji Bomani, si siri kwamba makampuni ya madini ya dhahabu na gesi yamekuwa yakiongeza wawekezaji wapya, kupitia PSA, na serikali ya Tanzania kuridhia makubaliano hayo bila kizuizi chochote.
PSA imulikwe wazi. Makampuni ya migodi ya dhahabu (Barrick), almasi, nickel na uranium, na visima vya gesi (Songas) na mafuta huingiza wawekezaji wapya kupitia PSA, hususan pale ambapo serikali yetu huwapa hao wawekezaji kumiliki maliasili yetu kwa 100%! Inakuwa ni mali yao; na wanayo haki ya kuigawa mali hiyo kwa wale wawapendao.
Nashauri kuwepo na u-wazi wa kuhusu si makampuni mapya yaliyojiingiza kupitia psa bali pia uwazi wa kuhusu wazawa wapi walio na hisa katika makampuni hayo. Kwa nini nashauri hivyo? Mambo matatu ya wazi yanayozalisha vi-ji-senti.
Moja, ni utata wa kampuni ya Richmond Development Corporation LLC, ambayo mambo yaliyojitokeza yalifunua shinikizo la vigogo na wakubwa wa serikali kukiuka maadili yenye maslahi ya taifa!
Mbili, Mheshimiwa m-Bunge kijana Kabwe Zuberi Zitto (CHADEMA Kigoma Rural) alikuja na tuhuma dhidi ya aliyekuwa Waziri wa Umeme na Nishati Nizar Karamagi kukimbia hima huko London na kusaini mkataba hotelini na kampuni ya migodi ya dhahabu ya Barrick huko Buzwagi!
Pengine, Mheshimiwa Waziri wa Umeme na Nishati Nizar Karamagi alitia saini kuridhia tu mkataba wa awali wa Barrick kwa kupitia mapatano ya PSA!
Tatu, aliyekuwa Waziri wa Umeme na Nishati Bwana Nizar Karamagi, huyo huyo, ana pia kampuni yake ya ukuli hapo Bandarini. Sijui naye aliiunda lini? Pengine, alijua kuwepo kwa PSA. Hivyo, kaiunda kampuni hiyo, ambayo hatuwajui wenye hisa, na hapo baadaye Rais Benjamin Mkapa kuiongezea muda wa kumiliki ukuli hapo bandarini kutoka miaka 15 hadi 25 bila kibali rasmi!
Tunaambiwa kuwa Tanzania iliingia mkataba na kampuni moja ya Houston, Texas, Amerika, ya Richmond Development Corporation, LLC, yenye kufua umeme wa dharura kutokana na ukame uliosababisha mabwawa yetu ya maji kutosetri ufuaji wa umeme. Wamiliki wa Richmond Development Corporation, LLC. Ndio walikuwa na 100% za hisa za kampuni hii.
Lakini cha kushangaza ni kwamba wamiliki fulani walipoona uhondo upo katika mkataba huo, waliunda kampuni yao ya Richmond Tanzania Ltd na kuisajili mwezi zaidi ya mmoja baada ya mkataba huo kusainiwa, pengine, kupitia psa.
Wana hisa wa kampuni hii ni LLC na Naeem Gire, kulingana na habari rasmi tupatazo, kama ifuatavyo: (k)atika mchanganuo wa hisa, Gire ana miliki 250,000 na LLC 750,000 huku ikianza na mtaji wa Sh1,260,000,000 (1.2 bilioni).
Je, si huyu huyu mfanyabiashara aliyeshindwa kabisa kuweza kupata mapesa ya kusafirishia mitumba yake hadi hapo serikali yetu ilipoingilia kati kupitia CDRB?
Serikali iweke wazi offshore bank accounts zote, bila kujali mwenye akaunti ni nani! Uswisi imepokea na kukubali ombi la Amerika la kuitaka Uswisi ifungue akaunti za wa-Amerika mafisadi katika benki ya Union Bank of Switzerland (UBS)!
Zaidi, kama tunataka kupambana na ufisadi, serikali iamke kuwa taifa letu limehujumiwa na linaendelea kuhujumika. Kwahiyo, sheria itungwe ya kumulika wenye hisa katika makampuni ya ugeni na ya uzawa ili tujue ni wa-Tanzania walionunua hisa katika makampuni hayo.
Mianzo Mingine ya Nishati!
Kwa nini Tanesco imekuwa ikiigeuka kinyonga? Tanesco ilikataa kununua mitumba ya Dowans; Tanesco ikakubali na kukiuka msimamo wa Bodi yake; na sasa Tanesco imekataa tena! Kulikuwa na tetesi kwamba Tanesco ilitaka kununua mitambo hiyo mitumba tena!
Je, Tanesco haikutuambia, Potelea mbali hata kama nchi inazama gizani?
Je, Bodi ya Tanesco nayo ilifanya uamuzi mzuri wa kutaka kutuma tena wataalamu wa Tanesco waende huko Houston, Texas, kuzatiti bei hasa ya mitambo (turbines) hiyo ya kufua umeme?
Ni kupoteza mapesa ya umma; Ofisi yetu ya u-Balozi, Washington, DC, inaweza kufanyakazi hiyo (kulingana na sera ya diplomasia ya uchumi) na huyo Balozi Maalum Kjell Bergh anaweza, pia kusaidia!
Brela iliamua kuifuta Richmond ifikapo Septemba 15, 2008 kutokana na ufisadi na utata uliozalisha kashfa ya Richmond! Lakini kufuatia kushindwa kufua umeme wa dharura, leo hii bado tunaikumbatia Richmond kwa jina la Dowans! Malumbano yalijitokeza ya kukidhi mahitaji ya umeme kwa kununua mitumba ya mashini za Richmond/Dowans!
Wenye kutaka mitumba hiyo inunuliwe, walizua mantiki ya kuunda na kutekeleza sera za umeme na nishati hadi 2014! Waliihurunmia Dowans kwa kuvaa nondo ya uzalendo: Tanesco na Kamati ya Bunge ya Ununuzi Mashirika ya Umma).
Sasa hivi Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ununuzi, Mheshimiwa m-Bunge Kabwe Zuberi Zitto analilia mitambo mitumba ya Dowans itaifishwe ili kukidhi uhaba wa umeme.
Waziri wa Nishati na Madini, na akili zake, aliamuru hiyo mitumba inunuliwe! Hata kwa Ikulu ikadiriki kutamka eti Tanesco ni kampuni kamili yenye kufanya itakalo ni kukiuka uwajibikaji uongozi unaokwenda kombo!
Kwa nini tunangangania mitambo mitumba, tena ya ghali, ya Dowans kampuni ambayo haistahili kuwepo na ambayo imetushitaki huko Paris?
Lini tutaamka! Ama tuliishaga-kula vi-ji-senti vingi vya wawekezaji ambavyo vinatufunga nongwa na mitambo ya kufua umeme kwa mabwawa ya maji? Si ni afadhali tufuge samaki kwa wingi katika mabwawa hayo au tuyatumie katika umwagiliaji mashamba?
Hivi tuliambiwa na Muumba kuwa chanzo cha umeme na nishati ni mabwawa yetu tu? Mbona hatufundishiki kuwa tunaathiriwa na ukame kila mwaka?
Tufikirie mbinu nyinginezo za kufua umeme:
Moja, yatubidi tufikirie kwa makini namna ya kuigawa Tanesco. Kwani Tanesco ya Dar es Salaam ikikohoa tu, mikoa yote inapata homa!
Mfano, hapa Amerika kulikuwa na shirika kubwa la simu la Bell System au kwa jina la uzazi, Ma-Bell. Shirika hili lilikuwa limetamalaki karibu nchini kote. Lilishindwa kutoa huduma kwa wananchi. Ilibidi Ma-Bell igawanywe kwa watoto wake, Baby-Bells - wengi.
Hivyo hivyo, sioni sababu kwa nini tusiwe na Tanesco za Kanda ili kama Tanesco ya Dar ikishindwa nchi nzima isipate homa!
Mbili, tulijaliwa kuwa na mito mingi. Sioni sababu, kama tunazidi kutegemea maji/mabwawa tusijenge mitambo mingine kwenye mito yetu, kwa mifano, Mto mara hapo Kirumi na mto Simiyu. Mito hii pamoja na mitambo ya Rubanda? Kagera inaweza kutosheleza mahitaji ya umeme kanda za Ziwa Victoria.
Tatu, Tanzania ni lazima idumishe uhusiano na nchi za Kusini mwa Afrika, SADC. Jumuia hii isiwe ya mikutano ya wakubwa tu bali ifikirie namna ya kuweza kufua umeme kwa mahitaji ya Kusini mwa Afrika kutoka vyanzo vya Mto Kongo ,ambao maji yake yananyesha misitu na mengi kuingia bahari ya Atlatiki.
Nne, twende nuklia kwa matumizi ya amani (utabibu na nishati kwani uranium tunayo kwa wingi)! Kwa nini wawekezaji wachimbe na kuuza nje kwa manufaa yao na kutuachia mashimo na mazingira yaliyoharibika)!
Tano, jua tunalo, tena la masaa 12!
Sita, upepo tunao tena wa nguvu kuweza kuzungusha mapanga ya mitambo ya kufua umeme huko milimani, mabondeni na tambarare!
Saba, gesi tunayo tena inachotwa pengine kuuzwa nchi za nje ili makapuni yapate faida uwekezaji wa kutoka nje sio asisi ya Mama Tereza!
Nane, maji-mvuke moto moto tunayo!
Bio-gesi tunaweza kuzalisha!
Tisa, na hata mawimbi ya maziwa na bahari yanaweza kuchangia hilo la uhaba wa umeme!
romuinja@yahoo.com