Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kengele ya pili imelia kabla Mhe. Mnyaa hajahitimisha kuunga mkono hoja. Sasa anayechangia ni Eng. Stela Manyanya, ameanza kwa kuunga mkono hoja kwa asilimia 100.
Sasa anapiga nyundo media eti ndio waliolikuza Richmond!
Bunge ni wajibu kuisimamia serikali, eti media inawachonganisha bunge na serikali.
CCM kiboko!.
Amempongeza EL kwa kuwajibika na anaipongeza serikali kwa kulisikiliza bunge, anaisifu kwa kuwajibika kwa bunge.
Anasema huku anasitasita, ameingiza wasifu wa serikali ya Chama cha Mapinduzi, ameisifu serikali kwa kutekeleza mazimio mengi ya bunge.
Eng. Manyanya noma, eti anasema leo wananchi msishangae wote tunaunga mkono, tunaomba mtuelewe, tunaelekea kwenye uchaguzi, hivyo tunawaomba wananchi, mturudishe sisi tuliotimiza wajibu wetu.
Spika atetea shule ya Dr. Matayo na kuliahirisha mpaka jioni.
Yeah! Hi ndiyo TZ. Sasa tusubiri kununuliwa kwa mitambo ya Dowans baada ya kiwingu cha Richmond kuyeyuka. Lakini Mwakyembe and co. ndio wajue kuwa wako njiani kujiunga na akina Lamwai. Na hapo wasisingizie media. Bw. Rostam anatikisa guu tu bungeni; hahitaji kutoa kauli yoyote. What a country!
I never expected a miracle under CCM
kazi ipo mi nilisema mwakyembe hana lolote la maana na kweli litatimia leo
Nakwambia mpambanaji mahiri yuko vyama vya upinzani. Kama tungewapata kina Slaa watano tu, weacha tu. Wanaoshupalia kukaa CCM wanaimba nyimbo tu, hakuna kitu kutarajia kutoka kule. Nani awezaye kumlaani mama yake akafanikiwa?Nilishasema before, ilimradi umo ndani ya CCM huna sifa za kujiita eti mpambanaji wa ufisadi, kitu gani!kila siku Richmond,Richmond mpaka wengine wamefanya mtaji wa kisiasa kwenye majimbo yao kisa Richmond. Hao kina shelukindo na wenzake nilijua watakumbana na the so called NIDHAMU YA CHAMA, na hapo ndo mwisho wao, walaaniwe kwa kuwalaghai watanzania eti kwamba wao ni wapambanaji wa ufisadi!!
Ni mpaka hapo watanzania tutakapo amua kwa utashi wetu kuwa hatuwataki fulani na fulani watuongoze kwa sababu moja, mbili,tatu n.k,tutakuwa watu wa kuzungukazunguka huku na huko,yule kachemcha wizara hii anahamishiwa kule kama vile hakuna watu wenye uwezo...........na na kwambia CCM itatawala mpaka pale watu watakapokubali kubadilika(sio CCM Kubadilika)