Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,122
- 5,104
Umeongea kweli kabisa kakangu, lakini poa huwezi kuzungumzia Richmond bila kumzungumzia JK, ni kama issue ya ESROW au EPA bila jina la JK issue haiswii
na ndio maana inakuwa vigumu sana kwa mtu kama Lowassa kustakiwa, maana wakimwaga mboga yeye atatoboa kabisa masufuria yote
Inawezekana kuwa kashfa ya Richmond inamgonga zaidi EL na haimhusu sana JK (sijui kwa nini, lakini nimetokea kuamini sana hilo). LAKINI tatizo ni kuwa hawa (pamoja na vigogo wengi wa chama waliopo na wazamani) ni partners in crime katika mengi tu ikiwa ni pamoja na hayo ya EPA, IPTL na mengineyo tusiyoyajua. Wamelindana kwa mengi sana ambayo tukiyajua yote yatatuzidishia huzuni! Hivyo umesema vyema kabisa: hakuna aliye tayari kwa kadhia la masufuria yote kutobolewa. Akina Mwakyembe, Sitta na, sasa, Slaa ni kete tu zinazotumika katika mchezo wao kuzidiana dau (battle of wits). Ninachoona hivi sasa wanacheza kijinga mchezo huo. Labda kwa vile wanaelewa sehemu kubwa ya jamii ya Watanzania ni mazoba wasioujua wala kuelewa wameuzwa kiasi gani na, hivyo, kubakia na ushabiki wa kizani.
