Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

sasa wabunge wamelala ndio maana naona kimya,kukicha tu ni matangazo mchana kutwa.mimi nasubiri kwa hamu nani atakuwa bingwa 2008 hapo dodoma nikiangalia timu hizi mbili kati ya mafisadi na wabunge sioni kama tunaweza kupata hata bao la mkono.Yaani hii list ya mafisadi,naona langoni yupo che-nkapa akisaidiwa na beki wa kushoto mkono,kwa upande wa kulia yupo yona.katikati yupo J.M.Kiwete na namba nne mzee mzima B.P. Mramba.basi nitawataja wengine kwa haraka haraka 6. karamagi,7.r.azizi 8.E. lowasa 9.g.mgonja 10.Z.meghji na 11,mzee wtu j.malechela.
Kwa upande wa waamuzi ni refaree na s.six akisaidiwa na washika vibendera makamba na mudhihiri mudhihiri.
Je kunaushindi kweli hapo
 
Posted Date::2/4/2008
Bunge: Fukuto la Richmond,Spika aahirisha ziara ya Marekani
* Waziri Mkuu, Makamba wateta kwa saa tatu
* Wabunge CCM kukutana leokuweka mkakati

* Yadaiwa kuna mpango wa kuzuia mjadala

Na Tausi Mbowe, Dodoma
Mwananchi

SPIKA wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta ameahirisha safari yake ya kwenda Marekani.

Taarifa ya kusitishwa kwa ziara hiyo ilitolewa jana na Naibu Spika, Anna Makinda na kufahamisha kwamba leo Spika atakuwepo Bungeni kuendelea na shughuli za Bunge.

Hata hivyo katika tangazo hilo la Naibu Spika Makinda hakutaja sababu ya Spika kuahirisha safari hiyo.

"Wabunge kama mnakumbuka, Spika alitangaza kuwa atasafiri leo na kurudi siku ya Alhamisi, ameniagiza kutangaza kuwa amesitisha safari hiyo ya Marekani na kwamba kesho (leo) atakuwepo bungeni kuendelea na shughuli za Bunge kama kawaida," alisema Makinda.

Hata hivyo wachunguzi wa masuala ya siasa wanasema kuwa Spika amefikia uamuzi huo ili kuokoa jahazi kutokana na hali ya kisiasa kuchafuka kufuatia msimamo ulionyeshwa na wabunge kutaka ripoti ya Richmond iletwe bungeni kwanza kwaajili ya kujadiliwa.

Wakati anawaaga wabunge, Spika Sitta alimuagiza Naibu Spika, Anna
Makinda asije akakurupuka na kuyavamia mambo yote nyeti na kuyazungumza au kuyatolea maamuzi katika bunge hilo wakati yeye hayupo.

Sitta alisema kuwa mambo yote 'nyeti' yatasubiri mpaka atakapokuwepo na kwamba Naibu Spika asije akarudhusa kujadili mambo makubwa wakati hayupo.

Spika alitolea mfano wa sakata la ufisadi la Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na la Richmond na kusisitiza kuwa ili kujadili masuala hayo lazima yeye awepo.

Kauli hiyo ya Spika ina maana kuwa ripoti hiyo isingejadiliwa mpaka yeye yaani wiki ya mwisho ya kikao cha 10 cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma.

Juzi wabunge walisusia semina iliyoandaliwa na na Wizara ya Nishati na Madin ikwa lengo la kuwaelimisha kuhusu muswaada wa Sheria za Umeme na Biashara ya mafuta ya Petrol wakidai wapewe kwanza ripoti ya Kamati ya Richmond ili waijadili kabla ya kuupitisha muswada huo.

Wabunge hao pia walisema kuwa hawana imani na wizara hiyo pamoja na Shirika lake la Umeme Tanesco kwa kuwa taasisi hizo zimejaa uchafu na kwamba hawawezi kujadili masuala ya mikataba mengine mpaka wajisafishe.

Taarifa zilizopatikana kutoka miongoni mwa wabunge mjini hapa, zilieleza kuwa ili kuua mjadala bungeni, serikali inataka kutumia Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (Takukuru), kukamata baadhi ya maafisa na kuwafikisha mahakamani.

Chanzo chetu cha habari kilisema, juhudi zilikuwa zikifanyika tangu mwishoni mwa wiki kwa viongozi wakuu wa serikali kuwasiliana na Takukuru kwa ajili ya kuchukua hatua hizo.

Inadaiwa kuwa, kupelekwa kwa maafisa hao kuwatanyima haki wabunge kujadili suala hilo kwasababu ya utaratibu wa kuheshimu utawala wa sheria, lengo likiwa ni kuwaziba midomo wabunge hasa kutokana na cheche walizoonyesha mwishoni mwa wiki.

"Viongozi wanahaha kuhusu Richmond. Zimeenea habari kuwa viongozi wanaotaka kuua hoja hiyo bungeni wataitumia Takukuru kuwafungulia kesi maafisa kadhaa wa serikali kuwa walikula njama za kuihujumu Tanesco, iliwa na lengo la kuzuia mjadala bungeni," alisema Mbunge mmoja wa CCM na kuongeza:

"Upo uwezekano mkubwa watu hao watakamatwa kabla ya kikao cha wabunge wa CCM kinachofanyika leo."

Hata hivyo, Takukuru iliwahi kutoa taarifa za kuwasafisha maafisa waliohusika na kwamba hakuna rushwa iliyotumika kwenye mchakato mzima wa kufikia utoaji wa zabuni yenye mashaka ya Richmond.

Taarifa hiyo ya Takukuru ilipingwa na wananchi, huku Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Edward Hosea akisimama kidete kuwa hisia za rushwa ni juu ya mkataba huo ni majungu.

Kwa mujibu wa maelezo ya awali ya Spika, safari ya nchini Marekani ilikuwa na lengo la kuliongezea Bunge uwezo katika masuala mbalimbali yanayohusu shughuli zake na kwamba ingekuwa ya muda mfupi na kuahidi kurudi siku ya Alhamisi na kuendelea na shughuli kama kawaida na kujadili mambo hayo nyeti.

Siku hiyo pia Spika aliliambia Bunge kuwa bado mashauriano baina ya ofisi yake na serikali yanaendelea kuhusu ripoti nzima ya Mahesabu ya Akaunti ya Nje ya Nchi (EPA), kupelekwa bungeni kwaajili ya kujadiliwa.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Yussuf Makamba jana walikutana kwa dharura kuweka mikakati itakayowezesha Wabunge wa CCM kuwa na kauli moja kutokana kuwepo kwa mgawanyiko mkubwa kwa wabunge hao dhidi ya ripoti ya Richmond.

Viongozi hao wajuu wa chama hicho walikutana jana kwa zaidi ya saa tatu katika Ofisi za Bunge ili kuokoa jahazi kutokana na mgawanyiko huo unaonekana kutokea wazi wazi.

Habari zaidi zinasema kuwa wabunge wote wa CCM watakutana leo kwa ajili ya kuweka mkakati kabambe ikiwa ni pamoja na kuwa na kauli moja katika sakata hilo lilosababisha Spika Sitta kukatisha safari yake ya Marekani.

Kwa upande wa wabunge wengi walionekana kuwa na shauku kubwa kutaka ripoti hiyo ifikishwe bungeni kwanza ili wapate fursa ya kuijadili kwa undani ripoti hiyo.

Ndo kusema Spika Sita akifa tutasubiri mpka siku ya ufufuo?
 
sasa wabunge wamelala ndio maana naona kimya,kukicha tu ni matangazo mchana kutwa.mimi nasubiri kwa hamu nani atakuwa bingwa 2008 hapo dodoma nikiangalia timu hizi mbili kati ya mafisadi na wabunge sioni kama tunaweza kupata hata bao la mkono.Yaani hii list ya mafisadi,naona langoni yupo che-nkapa akisaidiwa na beki wa kushoto mkono,kwa upande wa kulia yupo yona.katikati yupo J.M.Kiwete na namba nne mzee mzima B.P. Mramba.basi nitawataja wengine kwa haraka haraka 6. karamagi,7.r.azizi 8.E. lowasa 9.g.mgonja 10.Z.meghji na 11,mzee wtu j.malechela.
Kwa upande wa waamuzi ni refaree na s.six akisaidiwa na washika vibendera makamba na mudhihiri mudhihiri.
Je kunaushindi kweli hapo

striker chenge yupo bench akisoma move na mchezo unakwenda je?ili aje apige mabao ya visigino.
wakati makamisaa Ana kiwango na lakus sileli wakijaribu kuihadaa timu pinzani .
 
wasituletee za kuleta hapa,hebu uza hayo mashirika yote kwa watu wanaoweza kufanya kazi maana serikali haiwezi tena sio kazi yake kufanya biashara,wananchi hatutaki kujua nani anamiliki watu wanataka umeme tuu na bei poa ambao naamini utapatikana kwenye free market sio monopoly ya Tanesco...uza haraka sana na ruhusu watu wazalishe,wasambaze na wauze na ondoa monopoly mara moja,hakikisha tuu mnawapa kazi makampuni yenye uwezo wa hiyo kazi na kipesa,hawa wabunge naona wana mawazo ya zamani sana ya kijamaa kufikiri tuko proud na Tanesco kwa sababu ni mali ya serikali.

Tatizo si kukataa kubinafsisha, issue hapa ni kujifunza kwanza what went wrong tulipoanza kufanya biashara na kampuni binafsi kama mambo ya IPTL na Richmond, halafu tukosoe hitilafu zilizotokea katika vitu hivyo ndio tuweze kuwaachia kampuni nzima kabisa. Tulitoa kidole tu tukaumia, tukaona hamna noma tukatoa mkono pia tukaumia, sasa kabla hata ya kujua ni meno gani yalituumiza yaani tuwape mwili mzima watafune?

Jamani jamani tupendane tusiumizane kwa pupa hivyo!Suicide tuwaachie wagonjwa wa akili kwa sababu hawajui watendalo, sisi tujuao tunachokitenda tufanye vitu hivi taratibu kwa kutumia datas zinazoeleweka na hata mambo yakiharibika tuwe na uwezo wa kuweka vitu wazi na kila mtu aone nia yetu ilikuwa njema, sio kukurupuka tu na kuguarantee kwamba mambo yataharibika na yakiharibika tunakuwa hatuna hata ujasiri wa kuonyesha wazi kipi kiliharibika na kiliharibika vipi na wapi ile tuweze kurekebisha, hivi shule gani wameenda hawa watu wanaotetea upuuzi? ni zile zile boarding tulizoenda? maana kule ulikuwa ukileta ujinga fimbo nje nje na tukajifunza haraka sana kufanya vitu kwa uhakika.
 
Koba,
Kama swala ni huduma na upatikanaji wa Umeme.. Je, umewahi kujiuliza kwa nini miaka ya 70 na 80 hatukuwa na hizi habari za mgao wa Umeme?..hizo generator tulikuwa tunazisikia tu, wakitumia Wakenya - Tena basi chini ya Ujamaa na hakuna biashara, leo tumepewa nafasi ya kufanya biashara ndio kwanza tumeua shirika...na hizo IPTL mara sijui mvua za uchawi (sayansi)..

Mimi nasema vyanzo vyote viwe chini ya serikali na hao wafanya biashara watagombea ugawaji.... hapo ndipo watakapo shindana bei lakini serikali ina jukumu la kuhakikisha umeme unapatikana na hakuna njama za mtu binafsi kuuweka mji mzima kizani.
Sisi Wadanganyika kwa hulka zetu na vile biashara sii utamaduni wetu tunachoangalia zaidi ni kuiba..kinachotokea Tanesco ni wizi na Ufisadi mtupu toka ngazi za juu.
 
wasituletee za kuleta hapa,hebu uza hayo mashirika yote kwa watu wanaoweza kufanya kazi maana serikali haiwezi tena sio kazi yake kufanya biashara,wananchi hatutaki kujua nani anamiliki watu wanataka umeme tuu na bei poa ambao naamini utapatikana kwenye free market sio monopoly ya Tanesco...uza haraka sana na ruhusu watu wazalishe,wasambaze na wauze na ondoa monopoly mara moja,hakikisha tuu mnawapa kazi makampuni yenye uwezo wa hiyo kazi na kipesa,hawa wabunge naona wana mawazo ya zamani sana ya kijamaa kufikiri tuko proud na Tanesco kwa sababu ni mali ya serikali.

..wauze haraka,ili nchi iingie matatizoni haraka,ili tuwe kama kenya haraka iwezekanavyo sio?

..liangalie swala hili kwa mapana. hiyo haraka itakutoka,infact hutataka hata kusikia!
 
....Bubu nafikiri unaongelea hizo community power plant ambazo coverage yake ni ndogo sana na sio community zote zenye huo uwezo kwa hiyo lazima uruhusu corporate ifanye kazi yake lakini kuendelea kutegemea serikali kwenye vitu kama hivi ndio kujirudisha nyuma,kwanini mnaogopa kubinafsisha na kumbuka watu wanataka umeme sio nani anendesha huo umeme,kuhusu maji nakubaliana na wewe kwa sababu almost kila sehemu wana source ya maji

..koba,

..lazima uzingatie mazingira,tamaduni,watu na wakati unapotaka kufanya vitu kama hivyo.

..hebu tueleze,city water ilikuwaje?

..hii ni africa si europe ambako watendaji wa serikali wanawajibika ipasavyo.
 
striker chenge yupo bench akisoma move na mchezo unakwenda je?ili aje apige mabao ya visigino.
wakati makamisaa Ana kiwango na lakus sileli wakijaribu kuihadaa timu pinzani .

..tusubiri dakika tisini tuone! mechi hii ime-create tension kubwa!
 
Wabunge CCM wajipaga kuikabili joto la Kashfa ya Richmond
Na Tausi Mbowe, Dodoma

WABUNGE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanakutana leo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kwa ajili ya kupanga msimamo wa pamoja katika mjadala kuhusu ufisadi unaodaiwa kufanywa kwenye mchakato wa zabuni ya kampuni ya Marekani ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond (RDC).

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda aliliambia Bunge jana kuwa mkutano huo unafanyika leo saa 2:00 usiku katika Ukumbi wa Pius Msekwa uliopo katika viwanja vya Bunge mjini hapa.

Hata hivyo, Makinda hakutaja ajenda zitakazozungumzwa katika mkutano huo. lakini uchunguzi uliofanywa na Mwananchi umegundu kuwa moja ya ajenda kubwa katika mkutano huo, inahusu ripoti ya uchunguzi wa tuhuma za ufisadi zinazoikabili Richmond, uliofanywa na Kamati Teule ya Bunge.

Kwa mujibu wa Makinda, kikao hicho kilitakiwa kufanyika jana, lakini kikaahirishwa hadi leo bila kutaja sababu hasa za kuahirishwa.

�Waheshimiwa wabunge, naomba niwatangazie wabunge wote wa CCM, kile kikao kilichotakiwa kufanyika leo, hakitakuwapo, kimeahirishwa mpaka kesho saa 2:00

usiku. Hivyo wabunge wote wa CCM mnaombwa kufika bila kukosa kwani kikao hiki ni muhimu sana,�alisema Makinda.

Baadhi ya wabunge wa CCM ambao hawakutaka kutaja majina yao, waliliambia Mwananchi kuwa kikao hicho kinalenga kuwaunganisha wabunge wa chama

hicho ili kuondoa mgawanyiko mkubwa uliodhidhirika miongoni mwao na wawe na kauli moja kwa yale yatakayojitokeza kwenye ripoti hiyo.

�Hawa watu wanataka kutufanya sisi ni watoto wadogo. Tunachotaka ni ripoti yetu tuijadili. Suala la nguvu ya chama kutetea masuala ya kitaifa sasa limepitwa na wakati. Mambo ya chama yasichanganywe kabisa na maslahi ya taifa,� alisema mbunge mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Habari za awali, ziliarifu kuwa wabunge wote wangegaiwa ripoti hiyo ili waweze kuisoma kabla ya kuijadili kwa undani, lakini Makinda jana hakuzungumzia suala hilo kabisa.

Hata hivyo, mwandishi wa habari hii alipomfuata ofisini kwake kwa ajili ya kupata ufafanuzi juu ya suala hilo, Naibu Spika kupitia Katibu wake, alisema masuala yote yanayohusu Richmond yatazungumzwa leo bungeni yeye mwenyewe akiwapo.

Jana Spika Sitta alikuwa akifanya kikao na kamati ya uongozi kuongelea mustakabali wa Richmond.

Wakati huo huo, Makinda alisema kwamba leo saa tisa, Rais Kikwete anarajiwa kuwasili Dodoma na kuwataka wabunge watakaopenda kwenda kumpokea kufanya hivyo.

Hata hivyo, hakueleza Rais Kikwete anakwenda kufanya nini Dodoma, lakini vyanzo vya habari vinasema kwamba anakwenda kusimamia kikao cha kiutendaji na kikao cha Baraza la Mawaziri.

Katika hatua nyingine, Wabunge jana walipitisha kwa kauli moja azimio la kumpongeza Rais Kikwete kufutia kuchaguliwa kwake kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).

Azimio hilo lililowasilishwa na Mbunge wa Ilala Mussa Azzan kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje pamoja na mambo mengine lilimpongeza Rais

Kikwete kufutia ushindi huo kufutia imani kubwa ilioonyeshwa na viongozi wa Bara la Afrika.

Kwa mujibu wa azimio hilo, uchaguzi wa Rais Kikwete ni heshima kwa Watanzania wote na kwamba ni lazima kuuezi kwa vitendo ili aweze kufanya kazi aliyotumwa na wakuu hao ipasavyo.

Wakichagia azimio hilo, Mubunge wa Sumbawanga Mjini, Paul Kimiti alisema tatizo bado kubwa kwa viongozi kwani bado ni wachafu na kwamba wanashika vitabu vitakatifu na kuapa huku mikono yao ikiwa ni michafu.

Kimiti pia alisema kuwa ni lazima viongozi kuhakikisha wanapambana na ufisadi bila woga ili kuhakikisha maisha ya wananchi yanakuwa mazuri.

Alisema Rais Kikwete ni mtu anayesimamia haki na harakati za demokrasia katika bara la Afrika na kwamba kazi hiyo aliinza zamani tangu akiwa mdogo wakati akisoma katika shule mbalimbali.

Naye Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamadi Rashid alimpongeza Rais Kikwete, lakini akasema kuwa pongezi hizo ziende kwa vitendo na viashiria vinavyoweza kuleta amani katika nchi yetu na kutoa mfano wa ufisadi na migogoro.

Kiongozi huyo alisema Rais Kikiwete anapaswa kupongezwa kwa kuwa ni kiongozi pekee katika Bara la Afrika aliyetamka hadharani na kukubali kuwa nchini mwake kuna matatizo ya kisiasa na kukubali kushirikiana na vyama vya upinzani.

�Huu ni mfano wa kuigwa kwa Rais wetu ni kiongozi pekee ambaye amekubali katika nchi yake kuna matatizo ya kisiasa viongozi wengine wanapaswa kuja kwetu

kujifunza, katika Bara la Afrika mambo haya huyakuti popote ni Tanzania pekee,� alisema.

Naye Mbunge wa Mtera (CCM), John Malecela aliwataka Watanzania kuacha kulalamika pindi Rais atakapokuwa anasafiri sana na kuongeza kuwa ni lazima wakubali kubeba mzingo wa matumizi kwa kuwa ni lazima ataongeza matumizi yake kwa kiasi kikubwa.

Malecela pia aliwataka wapinzani kuacha kualalamika na kukubali kubebeka na kuufafanisha upinzani ni sawa na mototo asiyebebeka na mzazi wake na badala yake

anatoa miguu nje.

Naye Mbunge wa Peramiho CCM, Jenista Muhagama alisema kuwa heshima iliyolewatwa na Rais Kikwete si ya kwake peke yake bali niya Bunge nzima na wananchi wote, hivyo ili kumuenzi ni lazima wananchi wamuunge mkono kwa vitendo na kuiletea heshima

nchi.

Akihitimisha azimio hilo Azzan alisema kuwa Afrika ni bara tajiri na kwamba migogoro inaletewa kwa makusudi na mataifa ya nje.

Tuma maoni kwa Mhariri
 
Ama! Huyu ndiye mzee Cigwiyemis S Malechela...jamani kumbe mtoto akitoa mguu nje ndo habebeki? au aliyembeba kambeba vibaya au hajui kubeba mtoto? au inawezekana mtoto mwenyewe kishakuwa mkubwa hahitaji kubebwa lakini mzazi anamlazimisha kumbeba?

Mkuu Mwanakijiji upo apo?
 
PM alishasema hausiki na sakata la RICHMONDULI, sasa kulikoni tumbo joto? na haya majibu ya "serikali ilikuwa na nia njema" wakati wametutia hasara,likome kabisa

Shukurani,

Unajua EL alisahau kidogo kwamba siku zote serikali thru matamko, sera na mikakati yake ina nia nzuri lakini watendaji wabovu kama yeye ndiyo wenye nia mbaya kwa WADANGANYIKA.
 
Ama! Huyu ndiye mzee Cigwiyemis S Malechela...jamani kumbe mtoto akitoa mguu nje ndo habebeki? au aliyembeba kambeba vibaya au hajui kubeba mtoto? au inawezekana mtoto mwenyewe kishakuwa mkubwa hahitaji kubebwa lakini mzazi anamlazimisha kumbeba?

Mkuu Mwanakijiji upo apo?

Ubongo wa Mzee Malesela Sigwiye-mis unamomonyoka gradually. Sasa hivi imefikia hatua hajui kutofautisha Pumba na Mchele.
 
Naye Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamadi Rashid alimpongeza Rais Kikwete, lakini akasema kuwa pongezi hizo ziende kwa vitendo na viashiria vinavyoweza kuleta amani katika nchi yetu na kutoa mfano wa ufisadi na migogoro.

Kiongozi huyo alisema Rais Kikiwete anapaswa kupongezwa kwa kuwa ni kiongozi pekee katika Bara la Afrika aliyetamka hadharani na kukubali kuwa nchini mwake kuna matatizo ya kisiasa na kukubali kushirikiana na vyama vya upinzani.

"Huu ni mfano wa kuigwa kwa Rais wetu ni kiongozi pekee ambaye amekubali katika nchi yake kuna matatizo ya kisiasa viongozi wengine wanapaswa kuja kwetu kujifunza, katika Bara la Afrika mambo haya huyakuti popote ni Tanzania pekee," alisema.

Ndio uzuri wa bongo, sio wananchi na viongozi wote katika taifa letu ni vilema wa akili ya siasa yetu, respect kwa mkuu wa upinzani bungeni kwa kusimamia siasa zilizokomaaa, na kukubali kutokubaliana bila matusi, ndio njia pekee kwa wapinzani kuwavuta wananchi wasioelewa, na hata kuwashawishi baadhi ya viongozi wa CCM, kuwa siasa sio matusi, wala ugomvi, isipokuwa ni hoja, kwa mwendo huu wa Rashid, mkuuu wa upinzani, kuna uwezekano siku moja wananchi wengi wakawakubali upinzani bongo.

Naomba kuuliza wakuu, huyu Rashid anatoka chama gani cha upinzani lazima hicho chama kitakuwa ni kichwa?
 
Ukimwona mtoto hatulii mgongoni na miguu haachi kuitoa, basi ujue mgongo wa mama unatumika visivyo na mafisadi.
 
PM anatapatapa awaache watu waseme kwanini kuwafunga mdomo? kwa kweli sasa nakumbuka Shaaban Robert alipoandika katika kitabu chake cha adili na nduguze kuwa "wakati sasa umefika, wa miti kusema,mawe kujibu, na wanyama kuwa watu" huu wakati hata kama sio kesho utafika tu
 
Wakati wenyewe ndio huu, mawaziri wanapozomewa, spika anapolazimika kuitikia matakwa ya wengi na Rais anaporuka kulekea Dodoma kuweka mambo sawa kabla hayajaharibika zaidi.
 
Waungwana,
Kwa siku tatu mfululizo hali Dodoma sio shwari. Vigogo wanapigana vikumbo, na mikakati ya kulindana na kuumbuana kama desturi. Tusubiri kesho, lakini Kuna uwezekano mkubwa wa mkutano wa baraza la mawaziri kesho ukafungua ukurasa mpya wa siasa zetu. Lakini kubwa kuliko yote, unaweza kubadilisha mahusiano ya serikali kwa upande mmoja na bunge kwa upande mwingine kwa kiwango ambacho hatujawahi kushuhudia. Mungu Ibariki Tanzania.
 
FM, huyu jamaa ni wa CUF..KICHWA KWELI HUYU

Mkuu viongozi vichwa kama Zitto, Slaaa, Freeman, na Obama, huwa hawatukani mtu, wao hutoa hoja tu na wananchi huitikia, tena mpaka kuwazomea viongozi wabovu, ndio inaitwa nguvu ya hoja, ila kwenye siasa siku zote huwa hawakosekani mazumbukuku, ukipita humu utawaona!
 
Back
Top Bottom