Mheshimiwa Spika, Kamati Teule sasa inaelewa chimbuko la tabia mbaya iliyoenea nchini ya ajali ikitokea watu kukimbilia kusaidia. Lakini si wote wenye dhamira ya kusaidia, kuokoa. Baadhi yao lengo kuu ni kuiba, kupora! Viongozi tunaobuni miradi kutokana na majanga ya kitaifa, hatuna tofauti na watu wanaokimbilia ajali kama waokoaji kumbe wezi. Ukame nchini ulitabirika, lakini hatukuchukua hatua mapema pengine kwa kusubiri janga kubwa litokee ili kupata fursa ya miradi ya akina Richmond
KUMBE WALIKUWA VIBAKA