Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Nina moja tu, wezi wa kuku(Vibaka) huchomwa MOTO AU KIFUNGO CHA MIAKA KADHAA, hawa MAFISADI WAPELEKWE JELA KWA UHAI WAO WOTE ULIOBAKIA NA WACHAPWE VIBOKO 12 KILA MMOJA. Manake wamesababisha vifo, dhiki kubwa sana kwa Wadanganyika. Kuna watu waliopoteza uhai kwa kuwa baadhi ya hospitali hazikuwa na Umeme kusapoti upasuaji, Kisa EL na timu yake, shame on you.. Hata hivyo bado nina Shaka na JK kwani anaogopa EL asimwage kuku kwenye mtama wengi.
 
....inavyoonekana ni kuwa kama lowassa hatawajibishwa basi na hawa wa chini kina karamagi...wataweza kupona...

kikao cha kamati ya chama ambacho huongozwa na lowassa jioni hii kasimamia malecela...huyu mzee atabiriki ..ana uwezo wa kumuokoa na watu msiamini...pamoja na kuwa mkewe wazi anampinga lowassa[mnakumbuka kuna hisia kuwa wale vibaka waliomfanyia kitu mbaya wakati ule pale moro ..anasadikika walitumwa na mtandawoo]

hatima ya yule waziri ofisi ya waziri mkuu ambaye alikuwa akiwajibu nyodo wajumbe wa kamati na kutetea kuwa waziri mkuu hakuhusika wala hawezi hojiwa pale karimjee..sijui itakuwa ipi...

lowassa na jk ni marafiki wa yamini na wana siri nzito zinazoweza waangusha wote pamoja ..kama kutakuwa na kuwajibika ni jambo ambalo wataliamua woote na jk kwa pamoja na bila mikwaruzo...tusubiri..

Mzee Malecela ni kweli hatabiriki, lakini kwenye hili ndio tutaupima kweli uzee wake ni wa "konyagi" zile walizokuwa wanamsema nazo mwenzao au ni wa busara (any of the "busara's!).

Kama kweli Lowasa na JK wamekula yamini, inategemea ni ya wapi. Kama ni ya kimasai kweli ni nzito, huwa ina-backfire vibaya, lakini JK si mmasai, apate tu ushauri wa wazee isimtishe hiyo. Lakini kama ni ile ya Kibosho, ni hatari zaidi, ile inaitwa "mma", na wenyenayo wanaitana "munamma", ni balaa, kiapo chake ni kutanua wote au kufa wote, haivunjwi hiyo! Na inamhusu mtu wa kabila lolote. Kazi ipo. [media]http://www.youtube.com/watch?v=eiurobLjA88[/media]
 
Tanzania ukiiba pesa nyingi za umma- unapeta! Ila ole wako uibe kuku- yaani utafungwa tu!
 
Kamati ya Rais ya kuchunguza ushiriki wa viongozi katika kashfa ya Richmond inakuja..
 
Kwa mara ya kwanza kuanzia kuanzishwa kwa bunge la vyama vingi Tanzania. Nimeshuhudia mbunge shujaa kutoka chama tawala akielezea, kinaga ubaga, mapungufu ya serikali ya chama tawala, katika bunge bila ya kujali maslahi ya chama tawala.

Dr. Mwakyembe anstahili kila sifa iwe kutoka kwa wapinzani, chama tawala, au wasio na chama chochote cha kisiasa. Kwani amejitowa muhanga kwa ajili ya wananchi wote wa Tanzania.

Leo, Dr. Mwakyembe amefunguwa ukurasa mpya wa siasa Tanzania, kwa mara ya kwanza serikali inaanikwa madhambi yake hadharani na mbunge wa chama tawala.

Heko Dr. Mwakyembe, nakuombea Mwenyeezi Mungu akulinde na maadui na wote uliowa-wafichuwa wana kila sababu ya kukufanyia uadui.

Ni kweli uliyosema Zomba, huyu mheshimiwa amejitoa haswa, yaani ukisoma hiyo ripoti hadi unasisimka, jinsi mwanaume alivyomwaga kila kitu kwa ujasiri "kama wa mwendawazimu vile", alivyosema Nyerere. Nampongeza kwa dhati yeye na timu yake yote. Na pia hakika anahitaji kuombewa dua njema Mungu amuepushe na maadui maana sasa watachipua kama uyoga!
 
sijawahi kufurahiswa na siasa kama alivyo nifurahisha mwakyiembe! vyovyote iwavyo sijali sana nini kitatokea mbele! ila maneno yaliyo tumika kwenye riport hayana kujivunga wala kujiumauma! BELESHI NI BELESHI NA KIJIKO NIKIJIKO! Hii pekee inanifanya nisikie raha moyoni! kazi ni kwa wabunge hiyo kesho na kwa KIkwete! huu ni muda wa kuwalk the talk!

..............MANENO HAYANA NAFASI TENA..........
 
Jamani Kama EL atasimama Bungeni na kuwaambia wabunge kwamba JAMANI KWELI YAMETOKEA NA TUSAMEHEANE NA SASA TUGANGE YAJAYO, wabunge makoooooooooooooofi kwa wingi na yame kwisha?

..ushafanya bunge "day care center"?
 
Naona leo tulijazana sana online, hebu angalia quote hizo!

Most users ever online was 1,227, Today at 02:55 PM.
IDIMI, akoe, alles, august_shao, BabaH, Bimkubwa, Bin Maryam, bob, Bowbow, chamchana, Chuma, DAR si LAMU, dash, DawaKali, Dotori, Echolima, Endeleaaa, Fundi Mchundo, Gembe, green29, humble servant, ibrahim dahir, Icadon, Invincible, Jasusi, Juakali, Kalamu, kamakaranga, kapinga, katibu tarafa, keiawa, kibunango, kinetiq01, kinyambiss, Kisura, Kithuku, Koba, kudi shauri, Kulikoni, Lunyungu, MADELA WA- MADILU, mahesabu, malila, Masatu, Masikini Jeuri, maya, mbishi, mfwatiliaji, mihengeli, mkamap, Mkandara, mkuu, Mlalahoi, mpanda merikebu, mtambo, Mtanzania, mtimkavu, Mtu Mzima, Mtu wa Pwani, mtu66, mTz, Mugo"The Great", Muhunzi, mwafrika wa kike, mwana siasa, mwanawasa, Mwiba, mwijage112, Mzalendohalisi, Mzee Mwanakijiji, Mzuzu, naamnani, NAJIKOPA MWENYE, NakuliliaTanzania, Nurujamii, Nyangumi, Nyani Ngabu, Nzokanhyilu, Ogah, Ole Matolo, pangupakavu, peace2007, phillemon mikael, prince andrew, princejafari, Pundamilia07, QuickMover, Rubabi, Rufiji, Scorpion, senator, sensitive, serengeti, Siriha, Sura-ya-Kwanza, tanzactive, TzPride, UFUNUO WA YOHANA, ulate, Ushirombo, wanzagi, watu wewe, Wicked3, Yebo Yebo, Yombayomba, YournameisMINE, Zee la shamba, zomba

Inaonyesha wengi tuliisubiria ripoti hii ya Mhe Mwakyembe kwa hamu kubwa!
Long Live JF
 
Mkuu JK akiwatimua kazi wote waliotajwa kwenye hii kashfa na kuahidi kuwafikisha mahakamani nitatimiza ahadi yangu iwapo tu atatimiza hayo kabla ya keshokutwa. Kwenye tawi lake la CCM la London keshokutwa kuna sherehe ya CCM kutimiza miaka 31, akifanya kweli nitakata kadi siku hiyo. Ndio zawadi nitakayompa.
 
Leo ni Hatari maana wengi hadi sasa wapo ONLINE wakisubiri Breaking News Mpya KUTOKA DOM. NASI WA BUMBULI TUPO LIVE...
Mwakyembe ametumia fursa yake kufikisha hio ripoti. NI MATUMAINI YANGU JK ATAFANYA JAMBO/MAMBO AMBAO WENGI TUTASHINDWA KUAMINI.
BAADA YA HAPO NEXT STEP NI KUFICHUA NA KUWACHUKULIA HATUA KALI WOTE WANAOHUSIKA.(TIMU YA MWAKYEMBE INAHITAJI PONGEZI, KWANI MARA NGAPI TUMEONA RIPOTI KAMA HIZI ZIKICHEZEWA)

NISINGEPENDA KUPENDEKEZA MTU KAMA AMBAVYO BAADHI YETU TUMEANZA. BADO CCM WENGI NI MAFISADI INATUPASA KUMCHAMBUA MTU KABLA YA KUPENDEKEZA ISIJE IKAWA UNAMPENDEKEZA MTU ILI NAWE UWE KARIBU KIULAJI.
UKICHUNGUZA WABUNGE WENGI WA CCM WALIVYOINGIA NAO WALIINGIA KIFISADI. MALECELA NAE ANA UFISADI WAKE MWACHENI KWASASA ASISIMAMIE KIKAO KWA LEO.
 
Je Mwakyembe ana beef na EL? Je hawpatani? Je ndani aya CCM kuna mgawanyiko?

Au simply watu wamechoshwa na skandali za kila siku wakaona waseme ukweli?

Je Mwakyembe ni mwadilifu nae? Rekodi yake ikoje?

kwa nini kila mtu anapotimiza wajibu wake kunaibuka hisia kuwa watu hawaaminiani?

Mwakyembe katimiza wajibu wake na ni wajibu wa kila kiongozi kusema ukweli sio kuficha maovu kama haya .

Wanaelewana sana ila yeye mwakyembe ni mkweli.

Hapana Mpaka Kieleweke, si lazima kwamba kuna kutoaminiana, mimi pia niko very impressed na kazi ya Mwakyembe (especially kwa ripoti iliyo makini), ila ukweli uko wazi, ana bifu na wakuu wachache wa CCM. Inawezekana ameamua kwenda nao sambamba! Sasa hayo ya kwao na bifu hayatuhusu sasa at this point, sisi tunajali ukweli unaowekwa wazi!
 
Hii report in deep kuliko nilivyotegemea...Yaani Dr na Timu yake wamefanya kazi kwenye ndani ya mwezi mmoja...kwa mara ya kwanza narithika na kazi ya Mbunge yoyote wa CCM

Wakuu nimesoma hii ripoti ya Dr Mwakyembe hadi nimesisimka! Amemkoma nyani balaa! Au niseme ameikoma minyani! Namkubali, naikubali kamati yake yote, na bado siamini kama waliweza kuandika ripoti ndefu kiasi hicho katika muda waliopewa, mahojiano yaliendelea hadi 27 Dec, na 31 Dec ripoti tayari! Walikuwa hawalali hawa jamaa! Hongera zao kwa sana.

Kumbe waTanzania tunaweza kufanya kazi na ku-deliver tukiweka mind zetu tunapotaka! Kumbe WaTanzania hatuko wazembe/wavivu kama kila pande ya dunia inavyotaka tuamini!
 
Mwakyembe Ujasiri Aliokua Nao Leo Ulikuwa Wa Ajanu Hatahivyo Inabidi Ajilinde Kweli...mafisadi Wana Mikono Mirefu.................
 
I hope hii ripoti imerudisha imani ya Mwafrika wa Kike kwa Mheshimiwa Dr. Mwakyembe!

Duh! ndio raha ya blog, nakumbuka baadhi ya waungwana walivyokuwa wakipinga kuchaguliwa kwa Dr. Mwakyembe, sijui walikuwa mapandikizi au!
 
...................mwakyembe Is Always Good..na Kabla Ya Mawaziri Kutajwa Wakati Ule Alikuwa Akijua Angekuwamo....jk Alimvuta Mtandao Kuogopa Asijiunge Kwa Mwandosya...ila Nasgangaa Kwa Nini Akawa Mtandao Matumaini..kati Ya Wana Mtandao Original Kuna Ambaye Haziivi.....

Katika Historia Ya Bunge Sijawahi Kuona Ripoti Iliyokuwa Nzito Namna Hii Kwa Uwazi Wa Kila Kitu...nina Imani Hata Spika Na Waziri Mkuu Hawakujua Ingesomwa Kavu Kavu Namna Hii..

Sasa Ndio Mtaona Kwa Nini Spika Alikuwa Akijaribu Kuikwepa Isisomwe ..alikuwa Ame Pre View Akaona Ni Motoo..

Kwa Analysis Ya Haraka Ujasiri Alioonesha Mwakyembe Inaonekana Una Baraka Za Mkuu....kaamua Kujisafisha ...mnajua Jk Is Always A Good Politician...nitoke Vipiii????...sasa Kwa Muda Tutasahau Za Bot..alafu Baada Ya Hili ...akiwaletea Na Single Iliyopo Jikoni Ya Tume Ya Jaji Bomani Aka Zitto Commetee..itakuwa Funika Bovu ..na Itazima Yote Haya...mtakuwa Na Mengi Ya Kumshabikia Sterling Jk Mwaka Huu...hadi Mwisho Wa Mchezo....
 
...................mwakyembe Is Always Good..na Kabla Ya Mawaziri Kutajwa Wakati Ule Alikuwa Akijua Angekuwamo....jk Alimvuta Mtandao Kuogopa Asijiunge Kwa Mwandosya...ila Nasgangaa Kwa Nini Akawa Mtandao Matumaini..kati Ya Wana Mtandao Original Kuna Ambaye Haziivi.....

Katika Historia Ya Bunge Sijawahi Kuona Ripoti Iliyokuwa Nzito Namna Hii Kwa Uwazi Wa Kila Kitu...nina Imani Hata Spika Na Waziri Mkuu Hawakujua Ingesomwa Kavu Kavu Namna Hii..

Sasa Ndio Mtaona Kwa Nini Spika Alikuwa Akijaribu Kuikwepa Isisomwe ..alikuwa Ame Pre View Akaona Ni Motoo..

Kwa Analysis Ya Haraka Ujasiri Alioonesha Mwakyembe Inaonekana Una Baraka Za Mkuu....kaamua Kujisafisha ...mnajua Jk Is Always A Good Politician...nitoke Vipiii????...sasa Kwa Muda Tutasahau Za Bot..alafu Baada Ya Hili ...akiwaletea Na Single Iliyopo Jikoni Ya Tume Ya Jaji Bomani Aka Zitto Commetee..itakuwa Funika Bovu ..na Itazima Yote Haya...mtakuwa Na Mengi Ya Kumshabikia Sterling Jk Mwaka Huu...hadi Mwisho Wa Mchezo....

PM,

Hili limeshaonekana mapema hapa na kwa wengine sasa hivi ni tik tak tik tak tik tak..... Maneno mengi makali na selective reporting ... watu wanapoa na kisha zinaundwa tume za kuchunguza kamati.... Mheshimiwa sana anaanza kusafiri na anaweza kumpa nafasi Mwakyembe kama bosi mpya wa Tanesco or samthing na life inaendelea!..... tik tak tik tak......
 
Jamani Lakini isije ikawa ni njia za kufunika maMbo ya BOT Kwani inaweze ikawa sababu ya kujfunua huku na kujifunika kwengine wanawani.
 
Back
Top Bottom