Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

JK kaja kutangaza kuwa na waziri mkuu mpya? hilo ndio swqali huku dodoma muda huu.

Natabiri new PM mr PINDA...hii natabiri sio nyeti kutoka Dodoma
 
Lunyungu,

Ina maana JK hahudhurii hicho kikao cha wabunge wa CCM? Sasa kama Lowassa hajaenda kwenye hicho kikao, kweli kitafanyika? Au itabidi wamsubiri.

Ni kama yeye ndio kiongozi wa wabunge wa CCM kwahiyo ni muhimu kuwepo kwenye huo mkutano mpaka pale wabunge wakiamua asiwe mwenyekiti kwasababu ni mtuhumiwa.

Mtanzania mimi nina kuhabarisheni hali halisi bila ya kuchuja .Kumbuka pia kwamba hata Kikao kilicho pita ilikuwa Lowasa aongoze lakini wakamtosa. Nasema yanayo tokea nyie fanyeni uchambuzi.

Watuhumiwa wa ufisadi Richmond washindwa kumpokea Rais Kikwete
Na Waandishi Wetu, Dodoma

WATUHUMIWA wote wa ufisadi ambao walihusika katika kuipa zabuni ya uzalishaji wa

umeme wa dharura hatimaye kuipa ushindi Kampuni ya Richmond Development ya nchini Marekani mwaka 2006 jana walishindwa kumpokea Rais Jakaya Kikwete alipowasili mjini hapa kutokana na watuhumiwa hao kuwa na kikao maalumu na Kamati ya Uongozi ya wabunge.


Rais Kikwete aliwasili jana saa 9 alasiri akitokea jijini Dar es Salaam ingawa haikuwekwa bayana sababu ya ziara hiyo ya ghafla, lakini wachunguzi wa mambo wanasema kuwa amekuja ili kuweka sawa mgawanyiko unaonekana kutokea ndani ya CCM.


Mara tu baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge ambapo pamoja na mambo mengine

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dk Harrison Mwakyembe aliwasilisha muhtasari wa ripoti hiyo, viongozi wote waliotajwa kuhusika na ubadhirifu huo wakiongozwa na Waziri Mkuu, Edward Lowassa walijifungia ndani ya ofisi za Spika kwa ajili ya kikao

maalum.


Watuhumiwa hao ni pamoja na Waziri wa Afrika Mashariki, Dk Ibrahimu Msabaha, Waziri

wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Mwanansheria Mkuu wa Serikali Johnson

Mwanyika waliingia katika ofisi hiyo ili kukutana na Kamati ya Uongozi ya Bunge

tangu kuahirishwa kwa shughuli za Bunge, lakini mpaka tunaenda mitamboni walikuwa

bado hawajatoka.


Kamati ya Uongozi wa Bunge inaongozwa na Spika wa Bunge ambaye ni Mwenyekiti,

Naibu wake ni Makamu Mwenyekiti na Wakuu wote wa Kamati za Kudumu za Bunge ni

Wajumbe wa Kamati hiyo ambapo kwa upande wa serikali inawakilishwa na Waziri Mkuu.


Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Injinia Stella Manyanya aliwasilisha Bungeni hapo hoja ya ya kuwasilisha Taarifa ya Kamati hiyo huku shughuli za maswali ziliendelea kama kawaida.


Mara baada ya shughuli za maswali kwisha Spika alimuita Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dk Mwakyembe kuja kutoa ripoti hiyo kwa wabunge kwa muhtasari kwa kuwa ripoti hiyo ilikuwa kubwa sana na ilikuwa na viambatanisho zaidi ya viwili.


Baada ya Kauli hiyo, Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge alisimama na kuomba muongozo wa Spika kuwa kutokana na utaratibu wa Bunge shughuli za maswali zilipaswa kuisha kwanza ndipo shughuli nyingine zifuate kama kuwasilisha ripoti

hiyo hivyo kutaka hoja hiyo isijadiliwe kwa wakati huo.


Hata hivyo, Spika alipinga hoja hiyo na kusema kuwa �kwa utaratibu Bunge linaongozwa kwa kuzingatia Kamati ya Uongozi ambayo katika Kamati hiyo Serikali ina mwakilishi wake na walikuwepo tumekutana na kuamua ripoti hii ijadiliwe kabla ya kipindi cha maswali kuisha,�alisema.


Alisema kama tukio la Jumapili la wabunge kususia semina iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati isingetokea taratibu za Bunge zingeendelea kama kawaida, lakini hali imechafuka na moto mkubwa unafukuta Bungeni kutokana na ripoti hiyo.


Kauli hiyo ya Spika ilishangiliwa na wabunge wote na kushindwa kujizuia kwa kupinga meza zao kuonyesha kufurahishwa na uamuzi huo uliotolewa na Spika huyo.


Hatimaye Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dk Mwakyembe alienda mbele ya Bunge hilo na kuanza kusoma muktasari wa ripoti hiyo huku wabunge wakiwa wametulia kimya kumsikiliza kwa makini na wakishangilia katika sehemu kadhaa zilizowataja watuhumiwa hao kuhusika moja kwa moja kitendo hicho.


Hata hivyo, Dk Mwakyembe muda wa kuwasilisha hoja hizo ambao kwa taratibu za Bunge

ni saa moja, uliisha hivyo Mwenyekiti huyo aliomba muongozo wa Spika kuomba asome

mapendekezo kutokana huo kuisha jambo lililopingwa vikali na wabunge.


Spika wa Bunge ilibidi kuingilia kati na kusema kuwa kwa taratibu za Bunge hoja inapaswa kuwasilishwa kwa muda wa saa moja hivyo kama wanataka hoja hiyo iendelee ni lazima wabadili kanuni za Bunge hilo ambapo hata hivyo taratibu zinaruhusu kuongezwa kwa dakika 30 pekee.


Dk Willibrod Slaa aliomba muongozo wa Spika na kutaka hoja hiyo iendelee kwakusema kuwa

ripoti hiyo ni muhimu kwa maslahi ya wananchi na kwamba ilitumia pesa nyingi za walala hoi hivyo ni muhimu kuongezewa muda jambo lililokubaliwa na Spika.


Mara baada ya kumaliza kusoma ripoti hiyo, Spika wa Bunge alihairisha shughuli za Bunge na kutangaza kuwa ripoti hiyo itajadiliwa kwa siku mbili yaani leo na kesho hivyo ni vyeme kupeana nafasi ya kusoma akisisitiza kuwa mambo hayo ni mazito.


Hata hivyo, mara baada ya kuharishwa shughuli za Bunge watuhumiwa wote wa ufisadi

huo wakiongozwa na Waziri Mkuu, walishindwa kutoka ndani ya Ukumbi wa Bunge kwa

zaidi ya dakika 10 huku wakikaa kikao kujadili.


Hata hivyo, haikujulikana nini walichokuwa wakijadili watuhumiwa hao, lakini walionekana kuwa wanyonge na kuishiwa nguvu kutokana na matokeo ya ripoti hiyo.
 
Kwa maneno mengine, Kamati inapendekeza Waziri Mkuu ajiuzulu...Uzuri wa Kamati hii ni kuwa EL hakujua wametumia maneno gani humo...
 
Moderator.Unganisha hizi thread ili tupate mtiririko uliokamili..
 
Kambi ya upinzani yajipanga kuwasha moto kuhusu Richmond
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

KAMBI ya Upinzani Bungeni imekutana na kuweka mikakati ya jinsi ya kuchangia

ripoti hiyo kwa kuchangua watu maalumu kutoka kambi hiyo watakaoweza kutoa maoni

yao kwa umakini mkubwa.


Kambi hiyo imesema kuwa hatua hiyo itawawezesha kutoa mchango thabiti utakaokuwa

na lengo la kutetea maslahi ya Taifa.


Habari kutoka katika ndani ya kikao hicho, zinasema kwamba kambi hiyo ina wazungumzaji 14 watakaowakilisha, na wamepewa kazi ya kuisoma ripoti hiyo.


Mbunge wa Ole CUF, Bakari Shamis Faki alisema kuwa wabunge wengine wa upinzani pia

wanatakiwa kusoma kwa makini ripoti hiyo, lakini baadhi ya wabunge waliochangulia ili kuwa wazungumzaji wakuu wanajukumu zaidi la kuhakikisha wanaelewa zaidi.


Faki alisema kuwa kwa sasa Watanzania wameujua ukweli wa mambo kuwa ni nani aliyeipeleka ICU Tanesco na kwamba watahakikisha kambi hiyo inajipanga katika kutetea maslahi ya taifa na kumtaka Waziri Mkuu kujiuzulu kwa kuwa ripoti hiyo imemnyooshea kidole moja kwa moja.


�Lazima Waziri Mkuu awajibike katika hili, hapa hawezi kukwepa, atumie busara za

kawaida kupisha watu wengine waendelee na kazi ya kujenga Taifa, nchi imekuwa ni

maisha bora kwa viongozi sasa na si maisha bora kwa kila Mtanzania kama

tunavyoambiwa kila siku", alisema Faki
 
Sitaki kusikia mambo ya kuundiwa kamati wachunguzwe.Hapo ndipppo nitamdharau mara mia ndugu Jakaya
 
Mwaga vitu Mzee Lunyungu, nikiona upo offline ndo nami naondoka.Mambo matamu kwelikweli.JF ni kiboko
 
Naomba kuuliza,

Hivi hii reporti ilisomwa moja kwa moja bila Spika kuiona?

Kwani taratibu huwaje?
 
waziri mkuu kapewa achague kusuka au kunyoa.

haki ya nani kama ataachiwa abakie haiba yake kwenye macho ya watanzania itashuka sana

na ile tabia yake ya kujifanya yeye ndie mtendaji pekee na wenziwe wapuuzi na kuwaumbua sijui wale wakuu wa mikoa na wilaya na watendaji mwengine furaha yao saa nii ni kwa kiwango gani


nnaamini wako watu saa hii wanapiga lager kwa sana kusema mungu anatulipia kwa kiongozi huyyu mamvi
 
Naomba kuuliza,

Hivi hii reporti ilisomwa moja kwa moja bila Spika kuiona?

Kwani taratibu huwaje?

Spika alikuwa nayo kwa wiki zaidi ya tatu.

Nitashangaa kama Lowassa alikuwa hajaiona.

Angalia mapendekezo ya kamati juu ya maadili ya viongozi, je was it purely coincidental kwamba rais alikuwa anawaza kitu copy right na mapendekezo ya hiyo kamati?

Ninahisi hata rais alishaiona hiyo report.
 
Halisi yuko wapi?maana alisema jamaa wamesema hawajiuzuru Ng'o!
sasa itakuwa vipi?Halisi lete za ndani kabisa.Natamani niende Dodoma nikashangilie kuangushwa kwa dola ya Mafisadi.
 
i was trying to figure out the same thing...good point
 
Tusimlaumu Hosea wala msabaha.hawa wote walipata Maelezo kutoka kwa Bwana Mkubwa<ndanda Lowassa E.N Al fasadi>
 
Halisi yuko wapi?maana alisema jamaa wamesema hawajiuzuru Ng'o!
sasa itakuwa vipi?Halisi lete za ndani kabisa.Natamani niende Dodoma nikashangilie kuangushwa kwa dola ya Mafisadi.

Hapa hajiuzulu mtu mpaka kieleweke kama mtandao unakufa au unaendelea. Kila mtu anaogopa anachojua mwenzake na kuna mambo ya kumwaga mboga na ugali yanaweza kufanyika hapa.

So far ni usanii tu utaendelea kwa muda hapa! Lowasa amekataa kutoka, Rostam Aziz anapigia simu waandishi wa habari kama kawaida yake kuwaweka sawa na story za Dodoma, Usanii tu na Kikwete mwenyewe anafikiria kama aunde kamati nyingine ya kuchunguza hii kazi au aunde TAKUTAKUKURU (Taasisi ya Kuchunguza Taasisi ya kuchunguza (kuzuia) na kukomesha rushwa) baada ya hii skendo ya Hosea!

tik tak tik tak tik ...........
 
Hapa hajiuzulu mtu mpaka kieleweke kama mtandao unakufa au unaendelea. Kila mtu anaogopa anachojua mwenzake na kuna mambo ya kumwaga mboga na ugali yanaweza kufanyika hapa.

So far ni usanii tu utaendelea kwa muda hapa! Lowasa amekataa kutoka, Rostam Aziz anapigia simu waandishi wa habari kama kawaida yake kuwaweka sawa na story za Dodoma, Usanii tu na Kikwete mwenyewe anafikiria kama aunde kamati nyingine ya kuchunguza hii kazi au aunde TAKUTAKUKURU (Taasisi ya Kuchunguza Taasisi ya kuchunguza (kuzuia) na kukomesha rushwa) baada ya hii skendo ya Hosea!

tik tak tik tak tik ...........
hapa ndipo tutajua mengi kuhusu nani aliyemchafua Dr. Salim ahmed Salim.Ukwli wote Nje.

watu wangematfuta Mhe. Sumaye atoe MAoni yake kuhusu hili.
 
Lowassa alisema wananchi walipata steki na maini kutoka kwenye bajeti , kweli nimeamini maneno yake sasa ! JK amepata nafasi ya kipekee ya kukomesha rushwa katika nchi yetu , tafadhali itumie vizuri kwa kuwajibisha wote waliohusika.
 
Spika alikuwa nayo kwa wiki zaidi ya tatu.

Nitashangaa kama Lowassa alikuwa hajaiona.

Angalia mapendekezo ya kamati juu ya maadili ya viongozi, je was it purely coincidental kwamba rais alikuwa anawaza kitu copy right na mapendekezo ya hiyo kamati?

Ninahisi hata rais alishaiona hiyo report.

Mtanzania,

Naafikiana na wewe- naona JK alizipata hizi repoti mbili- EPa NA Richmond. Akaamua kuwa na mktutano CCM kuelezea nia ya viongozi kuamua kati ya majukumu ya biashara na uwaziri!

Hivyo JK hii reporti nae anayo! Sasa swali is he bold enough- to make Cabinet Changes ikiwa ni pamoja kumtosa Lowassa?

Nadhani JK -this time atakemea tu -kama mara zote na kusema CCM ni kitu kimoja -wasigawanyike!

Sidhani kama JK ana ujasiri kumtosa EL jamaa yake ambaye Mwal. 1995 alisema wazi kuwa EL sii mwadilifu na alikuwa anahonga vyombo vya habari akiwa Ardhi ili kumnyanyua kisiasa!

Swali jingine- je JK yuko tayari kwa hizi skandali kuendelea kila siku?

Na atakuwa mwoga hadi lini kuchukua hatua?
 
Back
Top Bottom