Lunyungu,
Ina maana JK hahudhurii hicho kikao cha wabunge wa CCM? Sasa kama Lowassa hajaenda kwenye hicho kikao, kweli kitafanyika? Au itabidi wamsubiri.
Ni kama yeye ndio kiongozi wa wabunge wa CCM kwahiyo ni muhimu kuwepo kwenye huo mkutano mpaka pale wabunge wakiamua asiwe mwenyekiti kwasababu ni mtuhumiwa.
Mtanzania mimi nina kuhabarisheni hali halisi bila ya kuchuja .Kumbuka pia kwamba hata Kikao kilicho pita ilikuwa Lowasa aongoze lakini wakamtosa. Nasema yanayo tokea nyie fanyeni uchambuzi.
Watuhumiwa wa ufisadi Richmond washindwa kumpokea Rais Kikwete
Na Waandishi Wetu, Dodoma
WATUHUMIWA wote wa ufisadi ambao walihusika katika kuipa zabuni ya uzalishaji wa
umeme wa dharura hatimaye kuipa ushindi Kampuni ya Richmond Development ya nchini Marekani mwaka 2006 jana walishindwa kumpokea Rais Jakaya Kikwete alipowasili mjini hapa kutokana na watuhumiwa hao kuwa na kikao maalumu na Kamati ya Uongozi ya wabunge.
Rais Kikwete aliwasili jana saa 9 alasiri akitokea jijini Dar es Salaam ingawa haikuwekwa bayana sababu ya ziara hiyo ya ghafla, lakini wachunguzi wa mambo wanasema kuwa amekuja ili kuweka sawa mgawanyiko unaonekana kutokea ndani ya CCM.
Mara tu baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge ambapo pamoja na mambo mengine
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dk Harrison Mwakyembe aliwasilisha muhtasari wa ripoti hiyo, viongozi wote waliotajwa kuhusika na ubadhirifu huo wakiongozwa na Waziri Mkuu, Edward Lowassa walijifungia ndani ya ofisi za Spika kwa ajili ya kikao
maalum.
Watuhumiwa hao ni pamoja na Waziri wa Afrika Mashariki, Dk Ibrahimu Msabaha, Waziri
wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Mwanansheria Mkuu wa Serikali Johnson
Mwanyika waliingia katika ofisi hiyo ili kukutana na Kamati ya Uongozi ya Bunge
tangu kuahirishwa kwa shughuli za Bunge, lakini mpaka tunaenda mitamboni walikuwa
bado hawajatoka.
Kamati ya Uongozi wa Bunge inaongozwa na Spika wa Bunge ambaye ni Mwenyekiti,
Naibu wake ni Makamu Mwenyekiti na Wakuu wote wa Kamati za Kudumu za Bunge ni
Wajumbe wa Kamati hiyo ambapo kwa upande wa serikali inawakilishwa na Waziri Mkuu.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Injinia Stella Manyanya aliwasilisha Bungeni hapo hoja ya ya kuwasilisha Taarifa ya Kamati hiyo huku shughuli za maswali ziliendelea kama kawaida.
Mara baada ya shughuli za maswali kwisha Spika alimuita Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dk Mwakyembe kuja kutoa ripoti hiyo kwa wabunge kwa muhtasari kwa kuwa ripoti hiyo ilikuwa kubwa sana na ilikuwa na viambatanisho zaidi ya viwili.
Baada ya Kauli hiyo, Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge alisimama na kuomba muongozo wa Spika kuwa kutokana na utaratibu wa Bunge shughuli za maswali zilipaswa kuisha kwanza ndipo shughuli nyingine zifuate kama kuwasilisha ripoti
hiyo hivyo kutaka hoja hiyo isijadiliwe kwa wakati huo.
Hata hivyo, Spika alipinga hoja hiyo na kusema kuwa �kwa utaratibu Bunge linaongozwa kwa kuzingatia Kamati ya Uongozi ambayo katika Kamati hiyo Serikali ina mwakilishi wake na walikuwepo tumekutana na kuamua ripoti hii ijadiliwe kabla ya kipindi cha maswali kuisha,�alisema.
Alisema kama tukio la Jumapili la wabunge kususia semina iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati isingetokea taratibu za Bunge zingeendelea kama kawaida, lakini hali imechafuka na moto mkubwa unafukuta Bungeni kutokana na ripoti hiyo.
Kauli hiyo ya Spika ilishangiliwa na wabunge wote na kushindwa kujizuia kwa kupinga meza zao kuonyesha kufurahishwa na uamuzi huo uliotolewa na Spika huyo.
Hatimaye Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dk Mwakyembe alienda mbele ya Bunge hilo na kuanza kusoma muktasari wa ripoti hiyo huku wabunge wakiwa wametulia kimya kumsikiliza kwa makini na wakishangilia katika sehemu kadhaa zilizowataja watuhumiwa hao kuhusika moja kwa moja kitendo hicho.
Hata hivyo, Dk Mwakyembe muda wa kuwasilisha hoja hizo ambao kwa taratibu za Bunge
ni saa moja, uliisha hivyo Mwenyekiti huyo aliomba muongozo wa Spika kuomba asome
mapendekezo kutokana huo kuisha jambo lililopingwa vikali na wabunge.
Spika wa Bunge ilibidi kuingilia kati na kusema kuwa kwa taratibu za Bunge hoja inapaswa kuwasilishwa kwa muda wa saa moja hivyo kama wanataka hoja hiyo iendelee ni lazima wabadili kanuni za Bunge hilo ambapo hata hivyo taratibu zinaruhusu kuongezwa kwa dakika 30 pekee.
Dk Willibrod Slaa aliomba muongozo wa Spika na kutaka hoja hiyo iendelee kwakusema kuwa
ripoti hiyo ni muhimu kwa maslahi ya wananchi na kwamba ilitumia pesa nyingi za walala hoi hivyo ni muhimu kuongezewa muda jambo lililokubaliwa na Spika.
Mara baada ya kumaliza kusoma ripoti hiyo, Spika wa Bunge alihairisha shughuli za Bunge na kutangaza kuwa ripoti hiyo itajadiliwa kwa siku mbili yaani leo na kesho hivyo ni vyeme kupeana nafasi ya kusoma akisisitiza kuwa mambo hayo ni mazito.
Hata hivyo, mara baada ya kuharishwa shughuli za Bunge watuhumiwa wote wa ufisadi
huo wakiongozwa na Waziri Mkuu, walishindwa kutoka ndani ya Ukumbi wa Bunge kwa
zaidi ya dakika 10 huku wakikaa kikao kujadili.
Hata hivyo, haikujulikana nini walichokuwa wakijadili watuhumiwa hao, lakini walionekana kuwa wanyonge na kuishiwa nguvu kutokana na matokeo ya ripoti hiyo.