Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Nilianza kumtambua Dr. Mwakyembe pale alipojiuzulu kutoka ktk Bodi ya NBC...........ukitaka kujua zaidi ujasiri wake na uzalendo wake ulizia sababu za kujiuzulu kwake.....
 
Wakuu..sidhani..hisia zangu zinaonyesha hapa kuna watu watawajibika seriously...hilola Mwakyembe kupewa 'ulaji; kwa namna moja au nyingine...well sina tatizo nalo..after all walau yeye ena baseline tayari kwa kufanya kazi ilivotakiwa kwenye hii ripoti.....
 
...................mwakyembe Is Always Good..na Kabla Ya Mawaziri Kutajwa Wakati Ule Alikuwa Akijua Angekuwamo....jk Alimvuta Mtandao Kuogopa Asijiunge Kwa Mwandosya...ila Nasgangaa Kwa Nini Akawa Mtandao Matumaini..kati Ya Wana Mtandao Original Kuna Ambaye Haziivi.....

Katika Historia Ya Bunge Sijawahi Kuona Ripoti Iliyokuwa Nzito Namna Hii Kwa Uwazi Wa Kila Kitu...nina Imani Hata Spika Na Waziri Mkuu Hawakujua Ingesomwa Kavu Kavu Namna Hii..

Sasa Ndio Mtaona Kwa Nini Spika Alikuwa Akijaribu Kuikwepa Isisomwe ..alikuwa Ame Pre View Akaona Ni Motoo..

Kwa Analysis Ya Haraka Ujasiri Alioonesha Mwakyembe Inaonekana Una Baraka Za Mkuu....kaamua Kujisafisha ...mnajua Jk Is Always A Good Politician...nitoke Vipiii????...sasa Kwa Muda Tutasahau Za Bot..alafu Baada Ya Hili ...akiwaletea Na Single Iliyopo Jikoni Ya Tume Ya Jaji Bomani Aka Zitto Commetee..itakuwa Funika Bovu ..na Itazima Yote Haya...mtakuwa Na Mengi Ya Kumshabikia Sterling Jk Mwaka Huu...hadi Mwisho Wa Mchezo....

PM,

Dr. Mwakyembe alikuwa campaign manager wa Prof. Mwandosya na mpaka sasa bado
ndiye mpiga debe mkuu wa prof. ingawaje siku za karibuni amekuwa akifanya kile kinachoitwa kwenye marketing positioning, amekuwa akisogelea upande wa JK taratibu.

Wakati anataka kuacha kuwa mbunge wa East Afrika, alienda kumwambia JK, wakati huo JK ni mgombea (sijui kwanini alienda kuomba ruhusa kwa JK). JK akafanya kama kile alichofanya kwa Msekwa, kwamba sawa.

Matumaini ya Dr. Mwakyembe yalikuwa kwamba mambo ya kampeni za CCM yameisha na kwamba angelipewa cheo, lakini JK na wafuasi wake nasikia wakawa wanamcheka.

Jamaa ana uwezo mkubwa sana, ukiongea naye unaona ni mtu mwenye uwezo, pia mambo anayoahidi yanatia matumaini ila njoo kwenye utekelezaji, mmmhhhh!!! kule Kyela pamoja na kuingia kwa mbwembwe zote lakini hakuna anachofanya zaidi ya kusimamia shule za usanii za Lowassa.

Kule Mbeya wanasema Kyela ilikuwa just a stepping stone na baada ya kukosa ukubwa hakuwa na ari na moyo tena wa kuchapa kazi.

Labda sasa amepata ari ya kuchapa kazi kwenye kamati, tunamwombea mafanikio mema.
 
Kwa mara ya kwanza kuanzia kuanzishwa kwa bunge la vyama vingi Tanzania. Nimeshuhudia mbunge shujaa kutoka chama tawala akielezea, kinaga ubaga, mapungufu ya serikali ya chama tawala, katika bunge bila ya kujali maslahi ya chama tawala.

Dr. Mwakyembe anstahili kila sifa iwe kutoka kwa wapinzani, chama tawala, au wasio na chama chochote cha kisiasa. Kwani amejitowa muhanga kwa ajili ya wananchi wote wa Tanzania.

Leo, Dr. Mwakyembe amefunguwa ukurasa mpya wa siasa Tanzania, kwa mara ya kwanza serikali inaanikwa madhambi yake hadharani na mbunge wa chama tawala.

Heko Dr. Mwakyembe, nakuombea Mwenyeezi Mungu akulinde na maadui na wote uliowa-wafichuwa wana kila sababu ya kukufanyia uadui.

Asante mkuu. Wengine maboksi yanatukosesha uhondo. Sijawahi kusisimka kwa siasa ya nchi yangu kama kusoma hii ripoti. Jamani kumbe nchi yetu ina wasomi. Yaani hakuwabakisha hata kidogo amewavua nguo sijui hata wana wezaje kutoka nje na kutembea. Hongera Dr Mwakyemebe. Nawapongeza wana JF wote waliokua mstari wa mbele kututetea haki zetu. Naamini mambo mengi haya yanayotokea JF imetoa machango usio kipimo. Tuendelee kumkoma nyani giladi. Wengine hatuchangii lakini tupo pamoja. Leo nitalala usingizi mnono.
IPO SIKU TUTAFIKA.
 
Kamati yawahusisha Waziri Mkuu, mawaziri Kashfa ya Richmond
* Richmond ni ujasiri wa kifisadi
* Zabuni ilitolewa kwa shinizo

* Uongozi wa Takukuru kitanzini


Na Waandishi Wetu, Dar na Dodoma


KAMATI Teule ya Bunge ya Kuchunguza Mchakato wa Zabuni ya Uzalishaji Umeme wa Dharura imependekeza kuwa viongozi wote waliosimamia na kuhakikisha kuwa Kampuni ya Richmond Development LLC inashinda zabuni hiyo wawajibishwe.


Akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo bungeni jana, Mwenyekiti wake, Dk Harrison Mwakyembe, alisema wamebaini na kuridhika ukiukaji mkubwa wa taratibu na sheria za nchi.


Dk Mwakyembe alisema, kamati imeona mawasiliano ya karibu kati ya Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Waziri wa Nishati na Madini wa zamani, Dk Ibrahim Msabaha na wa sasa, Nazir Karamag, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Arthur Mwakapungi katika hatua mbalimbali za zabuni hiyo, lakini hawakukiri kutumwa au kuagizwa kubeba kampuni hiyo ya Marekani na kwamba, kwa mfumo wa uongozi na utawala bora wanawajibika wenyewe.


Baada ya uchunguzi wake na kubaini mianya inayoashiria rushwa, kamati imependekeza wahusika kuwajibishwa na mamlaka husika, huku Waziri Mkuu akitakiwa kupima uzito wa suala hilo kwa kuamua kuwajibika mwenyewe au bunge kumwajibisha.


Alisema uhuru mkubwa ambao viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini waliutumia bila wasiwasi kuhakikisha kampuni waliyotaka inapewa zabuni ya umeme unoanyesha kuwa ulitokana na maelekezo ya mara kwa mara waliyopata kutoka kwa Waziri Mkuu katika kila hatua ya mchakato huo.


Aliendelea kuwa, upendeleo wa dhahiri ambao Richmond ilipata kutoka taasisi mbalimbali za serikali ni kama Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ambacho kilifikia hatua ya kufumbia macho baadhi ya taratibu zake za msingi ili kuipa kampuni tanzu ya Richmond Development Company LLC cheti cha uwekezaji haraka iwezekanavyo bila kutimiza masharti ya Bodi za Makandarasi na Wahandisi na Wizara ya Nishati na Madini kuikingia kifua kampuni hiyo isichukuliwe hatua za kisheria.


Lowassa amehusishwa na upendeleo wa kampuni hiyo kutokana na barua yake Juni 21, 2006 akiagiza kuwa Richmond ipewe zabuni hiyo na kwamba.


Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema, Ibara ya 52 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inatamka wazi kuwa Waziri Mkuu ndiye mwenye madaraka ya juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hadi siku wa kazi na shughuli za serikali na ndiye kiongozi wa shughuli za serikali Bungeni.


Alisema kamati haikufurahishwa na taarifa zinazomgusa moja kwa moja Lowassa katika kupendelea Kampuni ya Richmond Development na kwamba, kamati imetimiza wajibu wake kwa uwazi na ukweli kama ilivyoagizwa na Bunge.


"Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shughuli za serikali na uongozi wa nchi kwa ujumla, ni wajibu wake yeye mwenyewe kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya Bunge," alisema na kuongeza:


"Vile vile ni wajibu wa Bunge ambalo linathibitisha uteuzi wake kwa mujibu wa Ibara ya 51 inayothibitisha uteuzi wake kuangalia ikiwa matokeo ya uchunguzi huu hayajaathiri hadhi na uzito wake ndani ya Bunge."


Wengine waliopendekezwa kuwajibishwa ni Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, aliyeshabikia na kuingilia uhuishaji wa mkataba huo ambao ulikuwa tayari umekoma, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Msabaha ambaye alikuwa waziri katika wizara hiyo kabla ya kuhamishwa.


Hata hivyo, Dk Mwakyembe alisema, Dk Msabaha akiwa nje ya kiapo alieleza kamati kwamba, yeye ni mbuzi wa kafara kwa sababu biashara hiyo ilikuwa ya Lowassa na mshirika wake, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.


Viongozi wengine ambao wamehusihwa na tuhuma hizo za kuingiza taifa kwenye mkataba na kampuni ya mfukoni na kusababisha hasara kwa nchi.


Maafisa wa wizara hiyo waliopendekezwa kuwajibishwa ni Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi na Kamishna wa Nishati, Bashir Mrindoko.


Mrindoko anadaiwa kushindwa kumshauri Katibu Mkuu mpya wa Wizara kuhusu udhaifu wa Richmond Development ambao ulijulikana na wizara hiyo tangu mwaka 2004 kwenye Mkataba wa bomba la mafuta.


Rungu la uwajibika ambalo linashikiliwa na Rais Jakaya Kikwete pia, limeelekezwa kuangukia Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) kutokana na taarifa yake kuwa taifa halikupata hasara kutokana na mkataba huo.


"Taarifa hiyo imemong’oa kwa kiasi kikubwa hadhi na heshima ya chombo hiki muhimu cha kitaifa kilichopewa dhamana na rushwa na sio kuipamba, ili kurejesha heshima ya umma katika taasisi hiyo, Kamati teule inapendekeza yafanyike mabadiliko ya haraka ya uongozi wa taasisi hiyo," alisema.


Wengine wanatatakiwa kuwajibishwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika ambaye katika majadiliano yake na Kamati Teule alionyesha kutoelewa kabisa kilichokuwa kinatendeka na wasaidizi wake na mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Wakili wa Serikali, Donald Chidowu ambaye ushiriki wake katika GNT haukuwa na tija yeyote, hivyo kuchangia kuingiza nchi katika mkataba wa aibu.


Kamati Teule imeanisha katika taarifa hiyo vitendo vya ubabe, ujeuri na kiburi vilivyofanywa na viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini alimradi kampuni waliyotaka iteuliwe kiasi cha kupindisha hata maamuzi ya Baraza la Mawaziri bila wasiwasi wowote.


Dk Mwakyembe alisema, wengine wanaotakiwa kuwajibishwa ni wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanesco ambao walishindwa kuzuia shinikizo kutoka uongozi wa juu.


Naye Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndullu, ametakiwa kuendesha uchunguzi na kubaini wakurugenzi waliohusika kwenye malipo ya kampuni hiyo na kuwachukulia hatua za nidhamu.
http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=4372
 
Mimi naona kwa sasa hongeza ziende kwa Mwakyembe na kamati yake, they have done their job without fear or favour. JK nitampongeza kama recommendations zilizotelewa atazifanyia kazi bila kumuangalia mtu usoni. Nitaboreka sana kama huu mpira nao ataamua kuwatupia PCCB, Polisi na Mwanasheria Mkuu, he needs to make a decision now.
Kwa upande mwingine, nadhani sasa wabunge wetu wameamka na hawataki tena kutumika kama rubber stamp which is a good thing kwetu walalahoi.

TAKURU (TAKUKURU)Walishapewa hiyo kazi na walitoa lipoti iliyosisitiza kuwa Richmond si mchanga wa macho bali kuna dosari ndogondogo tu!!!!!!!!!!!!??? Leo hii Dr. Mwakyembe na wajumbe wake wa kamati wameona ni dosari kubwa hivyo inaonyesha kuwa TAKUKURU nao inabidi wang'oke na wakubwa, kwani kule kwetu tunasema "mti mkubwa ukianguka basi na ile midogo iliyo chini yake nayo itaanguka" tu. Hongera Kamati yote
 
Tusimlaumu Hosea wala msabaha.hawa wote walipata Maelezo kutoka kwa Bwana Mkubwa<ndanda Lowassa E.N Al fasadi>

Unafikiri Dr. Mwakyembe hakupewa maelekezo? alipewa sana!!!!!! lakini hakutaka kuwa "Bangusilo" kama Mh. Msabaha. Ana uchungu na wadanganyika.
 
Hapa nilipo nasubiri.........BUSARA za...........the WEAKEST LINK = Mzee Stta

.......Wakuu Mnakumbuka ripoti ya Jaji Kisanga ilivyopigwa chini na BWM kinamna....eti haikufuata ToRs na kwamba alifanaya kazi ya ziada ambayo hakuambiw aifanye.....mnakumbuka!!???....... subirini tuone busara zao sasa...........

.............nawaunga mkono wanaosema
.....tik tak tik tak tik tak
 
Ukisoma hii thread then ukafanya comparison na ile ya Kamati ya Bunge kuhusu Richmonduli utacheka sana mfano
Huyu Dr Mwakyembe ninamjua vyema na ninaweza kutoa opinion yangu kuwa ni mbovu tu amekuwa akisapoti ufisadi na wizi wa ccm kinafiki underground.

Alikuwa wapi wakati kina Shivji na wasomi wengine wakichambua mikataba ya madini na suala la kufukuzwa zitto bungeni. This guy amekuwa ndio source ya magazeti ya mwizi na mkoloni Rostam Aziz kwa kutoa vigezo vya kisheria ambavyo vinapindishwa ili kutetea serikali.

Mwakyembe hafai kabisa na kuwamo kwake kwenye hii kamati ni ushahidi tosha kuwa huu ni usanii Kikwete anacheza hapa


Wanasheria wasomi wengi Tanzania walipondea hadharani issue ya bunge kufukuzwa bungeni na uhalali wa Buzwagi, huyu the so called rebel Mwakyembe alikuwa wapi?

Uko Kyela Mwakyembe wanamwona kama msanii tu,jimbo limemshinda na naona mwaka 2010 kazi ipo na ndo maana ameanza kujipendekeza kwa mwungwana....Mwakyembe sio yule wa zamani naona siasa zimemshinda na ameshindwa kujifunza toka kwa Mwandosya pamoja na kukaa naye kwa karibu sana,hana msimamo na ameanza kuunga mkono mwungwana.

na hawa kina Mwakyembe, is all that we have, Mzindakaya the former real leader wa kutotishika na serikali, sasa amekuwa a compromise, kaput finish wamepa hela kidogo that was it,

Mtanzania, bwana usianze kunitega ndugu yangu. Majina yao hayakutajwa hadharani na vyombo vingine vya habari kwa sababu ya nafasi zao na mimi niliombwa kuheshimu hilo na ninaheshimu. Ila nakuahidi endapo yatatokea mabadiliko ya Baraza hilo na wakawekwa nje kama wao wenyewe wanavyotarajia basi I'll be at liberty kuwataja

Mwakyembe anabadilika sana siku hizi, ila inaonekana anaenda zaidi kwenye usanii kuliko kwenye usmart wake uliomjenga all these years
Hizo ni comments ya watu then ukisoma comment zao za leo kuhusu Dr. HM unamsifia sana.

Je wanaJF tunacensor maneno yetu ama tunamcheka Sitta et al kwa kukana statement zao walizozisema siku za nyuma?
 
Wana JF nashangaa kwa nini tunaanza ku mu asses Dr HM wakati ambapo yeye ktk kamati hii alikuwa ni chairman tu...
 
Dr Mwakyembe ni Mtaalmu wa sheria. Kwa kutumia uzoefu wake katika uwanja wa sheria ameiongoza kamati ya kuchunguza mauza uza ya Richmond katika mzani wa haki kupima maovu kwa kutumia mwavuli wa vifungu vya sheria, mazingira na taratibu za kuendesha shughuli za kila siku ndani ya serikali.

Heshima ya shule imekuwa ikipindishwa kwa makusudi na watu wachache wenye Roho za hayawani kama Waziri wetu mkuu MH Lowassa.

Nampongeza Dr Mwakyembe kwa dhati kwa kurudisha tena heshima ya Wasomi wote, Wenye Phd,wenye Masters na wale wenye Bachelor.Wasomi wengi wamekuwa wakitumia elimu yao kuharibu na kuangamiza maendeleo ya nchi, kama vile shoka litumikavyo vibaya kuteketeza miti katika misitu ili kuanzisha maafa ya jangwa.

Lowassa amekua akitumia Vibaya Fani yake kama msomi aliye bobea katika Viwanja vya Tamthiria na Maagizo.

Badala ya kutumia fani yake ya maigizo na ngonjera kwa kuanzisha Dariwood na kujiingizia fedha halali katika TV na kuuza DVD?
MH lowassa ametumia fani yake ya kuwa bingwa wa Maagizo kucheza michezo ya kuigiza kwenye vichwa vya Watanzania.
MH Lowassa kwa kipimo chcochcote kile huna adabu kabisa mbele ya wananchi wate wa Tanzania Rais Bunge Wazazi Wako na wakwe zako.

MH Lowassa na kundi lake la Manyang'au wanastahili adhabu kali ambayo hawataisahau hadi siku ya kuingia kaburini.

MH JM Kikwete pamoja na ukweli kwamba wewe pia una mambo yako, ni vema uchukue nafasi hii kusafisha mikono yako na kumshushia MH Lowassa dhoruba kali ya Rungu lako ili;
1 Kurudisha Tena Heshima ya rungu la rais ambayo kwa zaidi ya miaka sawa na umri wa Watanzania wengi imepotea kabisa

2 MH Lowasa na wenzie warudi kwao madongo Arusha na kwingineko kuchunga ng'ombe na kulinda ndezi na tumbiri wasile mazao yao.
 
Tulisema toka siku ya kwanza kuwa Dr. Mwakyembe ni kichwa na kwenye hii ya kamati atakuja kulia mtu, maana huyu ndiye aliyeongoza ile kamati huru ya wabunge waliofanya kazi usiku na mchana kumpitisha Mwandosya, NEC Mbeya, baada ya wabunge kukasirishwa na Mtandao na matusi ya Tomasi na baba yake kwa senior mbunge mwenzao Mwandosya,

Kwa maoni yangu Dr. Mwakyembe, ana a lot ya ku-settle na Mtandao, waliomrubuni aache EAC kwamba watampa uwaziri, halafu wakamnyima, sasa Mnyakyusa amesema "po nifwe" na huyu atawaumbua sana tena kisheria maana yeye ni mjuzi wa Sheria, tena bunge zima anaheshimika, the matter of fact as of dataz hata rais mwenyewe humtumia sana kwa ushauri wa kisheria kwenye shughuli za taifa kwa hiyo kwetu CCM tulijua na tulisema mapema kuwa kwenye rais kumchagua Mwakyembe, kuna moto unakuja, kwa hiyo tunampa tena hongera Mwakyembe kwa kazi safi,

Now kwa Muungwana, tunataka kuamini kuwa nia na madhumuni ilikuwa yeye kutafuta reasonable cause ya kuwaondoa marafiki zake, ndio maana hakumchagua Kimiti au Mzindakaya, kwenye kamati, sasa amepewa nondo alizozitaka, tena za kisheria sio za kisiasa, meaning kwamba waliohusika, Kiwete akitaka anaweza kuwatosa kwenye sheria, au kuwatupa kisiasa kabisa wakawa kaputi, anything less itakuwa ni Banana Republic, na itakuwa ni haki ya wananchi ku-react as they want.

Kwa Mkuu Mwakyembe, sasa kuna mawili either wampe cheo, au amalizwe kisiasa kabisaaa, kama hakumwagiwa acid, yes I said it and yes I know it, lakini wananchi tuko pembeni tunaliangalia hili kwa macho yote tuone mwisho, ila kwa wale mlio karibu na Mwakyembe, mwambieni kuwa hii sasa ni saa mbaya, maana kuna wanaojitayarisha kupambana na Kikwete, kwenye 2010 na ni marafiki zake sana, ndio I said it na tunajua kuwa kuna mikakati inaendelea, tumesikia wana mpango wa kumgeuzia kibao Muungwana kuwa hana uwezo wa uongozi ndio maana wao wamekuwa wezi wa mchana, na wana mpango wa kujiosha kwa wananchi na kumsingizia Muungwana kuwa ndiye hafai, sasa umauzi ni wake aamue kunyoa au kusuka, ila kama anadhani kuwa ni marafiki zake, asubiri aone cha moto, nafikiri anakumbuka jinsi walivyotaka kumg'oa Mkapa kwenye term ya pili, sasa hilo linamsubiri na yeye, awatoe sasa ama sivyo wataishia kumtoa yeye,

Hongera Dr. Mwakyembe, Rais Kikwete sasa kazi kwako, kumbuka maneno yako mwenyewe kule Lusaka, the time is now, do it!


Ngoja tukaisome ripoti yote kwanza halafu tutarudi na more, nasikia kuna kina Kubenea huko, Duh! patamu hapo!
 
Quote:- Mwakyembe


1. Mheshimiwa Spika, matokeo haya yanaonesha hali halisi iliyopo Tanzania, hali ya uoga na ya kutojiamini inayowakumba Watanzania walio wengi wanapotakiwa kuelezea kwa uwazi maneno yale yale wanayoyanong’ona pembeni kwa hamasa kubwa. Kwa mtindo huu Taifa letu linaweza kuishia kuwa la walalamishi wasio na ujasiri wala dhamira ya dhati ya kukemea maovu pale inapobidi.
 
Quote:- Mwakyembe

2. Wataalam wa TANESCO, mathalan, waliikataa Richmond Development Company LLC mara tatu wakati wa kutathmini zabuni ya umeme wa dharura, kwa hoja za kitaalam kuwa haifai kwa vigezo vyote muhimu. Walipofika mbele ya Kamati Teule, wakawa wapambe nambari moja wa kampuni hiyo, wote wakiimba sifa za kulazimisha za kampuni hiyo!
 
Quote:- Mwakyembe

3. (a). Aidha, nyaraka nyingi ambazo Kamati Teule ilizipata toka Serikalini na taasisi mbali mbali, zilikuwa nakala zilizokosa mtiririko wa kimasijala.


(b). Kamati Teule ilipodai nyaraka halisi kulinganisha na nakala ilizokuwa nazo, ilipewa majalada yaliyoonyesha dalili zote za kukarabatiwa.

(c). Mheshimiwa Spika, hali hii ilijitokeza zaidi kwa TANESCO na Wizara ya Nishati na Madini. Jalada halisi kutoka TANESCO lilichukua siku tatu kuifikia Ofisi Ndogo ya Bunge likiwa na nyaraka zenye namba zilizokosa mtiririko stahili.


(d). Wizara ya Nishati na Madini ndiyo iliyotia fora kwa kumtuma Msaidizi wa Katibu Mkuu, Ndugu Julius Sarota tarehe 18 Disemba 2007 akiwa na maagizo ya kuwafungulia Wajumbe wa Kamati Teule kurasa maalum tu na si nyinginezo hivyo kuinyima Kamati Teule mtiririko halisi wa mawasiliano.
 
Quote:- Mwakyembe

4. Kamati Teule haikuridhishwa na utaratibu huo, hivyo ilimtaka Msaidizi huyo wa Katibu Mkuu aondoke na majalada yake na kumpelekea hati ya kuitwa Katibu Mkuu, Ndugu Arthur Mwakapugi afike yeye mwenyewe na majalada hayo.Tarehe 19 Disemba 2007 Katibu Mkuu huyo kwa maneno mengi na ya kuzunguka alithibitisha kuwa alichokifanya Msaidizi wake yalikuwa maelekezo ya Wizara.
 
Yap hayawi hayawi yamekuwaaaa!
Nakumbuka kuna watu walisema kuwa JF ni kijiwe ambacho hakiwezi kubadilisha kitu..
Trust me nimepitia taarifa yote ya Mh. Mwakyembe ni machache sana sikuyaona hapa JF mapema mwaka 2006...
Nitawashukuru sana wakazi wa Houston ambao walitufahamisha mapema kuhusu Richmond na ofisi zake lakini ndio hivyo tena...sikio la kufa halisikii dawa.

Kuhusu Mwakyembe hata kama ni mtandao jamani kamati hii imefanya kazi yake... Na sijui mwandishi nani huyu maanake lugha nzito sana iliyotumika... yaani roho yangu nyeupeee!...
Mambo mawili yaliyonifurahisha zaidi ktk report hii.
1. MAPENDEKEZO
2. kutambua kuwa ufisadi wa fedha hizi unatoka ktk misaada kutokana na kipende hiki cha taarifa hiyo;- Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha haikuridhishwa na mapendekezo yaliyotolewa kwani malipo yoyote ya awali kutoka fungu maalum la Multilateral Debt Relief Initiative ni lazima yafanyike kwa uthibitisho wa kuridhisha. Sehemu ya barua hiyo iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ndugu Gray Mgonja, inasema:

: "... tunaona kuwa tofauti na taarifa zilizotolewa wakati wa majadiliano ya Mkataba kuwa mkandarasi aliyechaguliwa alikuwa na vifaa tayari kuvileta nchini, sasa ni wazi kuwa si hivyo.

Kama unavyojua, msingi wa malipo kuhusu mitambo ya kununua au kukodisha chini ya Mradi wa Nishati ya Dharura unaofadhiliwa kupitia IMF MDRI, ni mkataba unaotokana na majadiliano.
3. Saga la BoT bado laendelea.. imekuwaje walipe karibu dollar millioni 35. badala ya 30..

JK kazi kwako sasa ushahidi ndio huo!.. tulisema sana ukatuona wababaishaji wasiokuzuia kulala (kupata usingizi)
Je, sasa wasemaje?
 
Quote:- Mwakyembe

Mheshimiwa Spika, leo tunapowasilisha taarifa hii mbele ya Bunge lako tukufu, tunajisikia kuutua mzigo mzito sana ulioanza kutuelemea kutokana na kuzongwa kila kukicha na kila aina ya uzushi, uchochezi, uchonganishi na hata vitisho. Tumezushiwa kuhongwa magari ya kifahari na fedha taslimu; tumetuhumiwa kuendesha vita dhidi ya Waislamu na mara nyingine tuhuma hiyo ikageuka kuwa vita dhidi ya Wakristo ndani ya Serikali; tumesingiziwa kuibadilisha taarifa yetu mara mbili, baadhi wakisema kwa ushawishi wa fedha, wengine wakidai kwa shinikizo la Mhe. Spika na wengine kwa shinikizo la Waziri Mkuu;
 
tumeshuhudia pilikapilika za usiku na mchana za kujipanga na kuwashawishi baadhi ya Mawaziri na Wabunge kuikana taarifa hii na mapendekezo yake kiasi cha wengine wetu kujiuliza: kulikoni mtu asiye na hatia kuweweseka?
Mheshimiwa Spika, naomba kwa niaba ya wajumbe wenzangu wa Kamati Teule, kukuhakikishia wewe binafsi na Bunge lako tukufu kuwa tumekamilisha kazi tuliyopewa kwa uaminifu na ujasiri mkubwa, dhamira safi, moyo wa uzalendo na kwa kumtanguliza mbele Mwenyezi Mungu katika kila tulilolifanya.
 
Back
Top Bottom