Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Mnaomlaumu Mwakyembe kuwa hakudeliver huko Kyela na East Africa...Binafsi nina mtazamo tofauti. kama mtindo wetu humu JF kurekebisha watu, that means wabunge wabadilike. Wabunge ni wanaadam kama wanadam wengine, hawawezi kuwa perfect all the time. Kwa hili Mwakyembe na Timu yake wamejitahidi, ni ujasiri wa Hali ya Juu. Hii ripoti sio sehem ya kupendekezwa kuwa Wazir, bali ni vitu vinavyomjengea Profile nzuri ktk siasa. Anaweza pia kupewa Tume ingine kuiongoza.its a Team, sio Mwakyembe pekee.


Kweli hii tutakuwa tunaplay cheap politics kufanya the whole issue ni Mwakyembe, mwakyembe, mwakyembe. This guy has done a good job, but we should remember that he was working in a team, and even what he said he did not cook by himself, a lot from the commission itself and out of comission were involved to reveal tricks in Richmond deal. He mentioned our embassies, MOF and other individuals who voluntariry offerd a hand.
Mwakyembe is relatively new kid in Tanzanian politics, his true colours are not well known to trust him 100%, give him more time to be in the game then we can be able to tell.
Kutokana na mfumo wa siasa zetu, Tanzania hakuna mbunge yoyote anayeweza kufanya lolote kubwa la kusema mimi nimefanya hivi kwenye jimbo langu, sana sana ni machache tu kama maji ya kisima, jengo la zahanati, kuomba mwalimu mmoja srikali etc etc, kwa hiyo yanayofanyika jimboni hayawezi kuwa kigezo pekee cha kuangalia uwezo wa mbunge. Ukiangalia takwimu za hali ya maendeleo kwenye majimbo ya uchaguzi ya Kigoma na Rukwa unaweza kusema wabunge wa majimbo hayo hawafanyi kazi kabisa, and that will be unfair!
 
Bado kabisa hatujafikia robo ya Ufisadi ulokwisha tokea hasa nikikumbuka Mada zilizokwisha kuwa raised hapa JF...kwa uchache tu NBC, Air Tanzania, TTCL, IPTL, Bandari, TRC, Fire, TRA, Tanganyika Packers, UDA n.k - Kwa uchache..
Kote watu wamekula kishenzi....
Ama kweli kama madai ya mchungaji Munishi - Misingi aliyojenga Nyerere ibomolewe!...
Na imebomolewa kweli.....


Hapa tunahitaji Chlorite solution yenye concentration kali sana ili kusafisha tambala letu letu hili lenye madoa yaliyokubuhu. Bado hatujamalizana na na la Madini, linalipuka la BOT, na kabla hilo halijaa sawasawa, twajionea la Richmond. Kumbukeni la rada bado linafukuta na vile vile lipo lile la ITPL, Kiwira, Bank M, Ikulu Business Co Ltd, na mengineyo mengi. Concentration ya kawaida ya Chlorite haiwezi kumaliza madoa hayo yote wakati watani wetu wa jadi Kenya nao wanaleta kiwingu kingine kuzuia jua lisikaushe tambala letu hilo.

LOL!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
JE kuna yeyote mwenye news ya mikutano ya CCM iliyofanyika huko Dom usiku?Moja was chaired by Malecela na ya pili was Chaired JK...tupen ndondondo
 
Wana JF ambao mko huko Houston nafikiria ingekuwa jema mkiwapa local media hiyo scandal ya Richmond...kumbuka ile scandal ya Bulayankulu...ni local media ya Canada ilitoa ikafanya hata SUTTON ika filisika....

nimewatumia leo Houston chronicle information scandal kuhusu hii kampuni , nimewatumia copy ya mkataba, jina la mwenye kampuni na link ya rdevco.com pamoja na contacts za magazeti yetu kama wakiamua kuchunguza wenyewe. Tuombe tu waandishi wao wachunguze zaidi.

Nimewaambia hii contract imecost $178 million, i think they might investigate. God willing
 
JE kuna yeyote mwenye news ya mikutano ya CCM iliyofanyika huko Dom usiku?Moja was chaired by Malecela na ya pili was Chaired JK...tupen ndondondo


Malecela ni mzee makini sana ambaye ni lulu pekee iliyobaki kwa CCM sasa hivi. Lakini kwa vile yeye siyo Vice Chairman tena, sielewi ilikuwaje akaendesha kikao hicho bila kuvunja katiba.
 
nimewatumia leo Houston chronicle information scandal kuhusu hii kampuni , nimewatumia copy ya mkataba, jina la mwenye kampuni na link ya rdevco.com pamoja na contacts za magazeti yetu kama wakiamua kuchunguza wenyewe. Tuombe tu waandishi wao wachunguze zaidi.

Nimewaambia hii contract imecost $178 million, i think they might investigate. God willing

Welldone i did the same regarding BOT i sent info to Washington Post rep stationed in NBI....na Boston Globe kwa vile Billal alilazwa Boston.

i hope watafuatilia na kumpasha BUSH atakapokuja Bongo
 
nimewatumia khou tv info as well. labda watacheki maana huyu Mohamed Gire anasema kwenye website that he serves in the mayor of houston's advisory board.
"Mr. Gire serves on numerous boards and commissions including a Houston's Mayoral Advisory Board for International Affairs and Development."
 
Tulisema toka siku ya kwanza kuwa Dr. Mwakyembe ni kichwa na kwenye hii ya kamati atakuja kulia mtu, maana huyu ndiye aliyeongoza ile kamati huru ya wabunge waliofanya kazi usiku na mchana kumpitisha Mwandosya, NEC Mbeya, baada ya wabunge kukasirishwa na Mtandao na matusi ya Tomasi na baba yake kwa senior mbunge mwenzao Mwandosya,

Kwa maoni yangu Dr. Mwakyembe, ana a lot ya ku-settle na Mtandao, waliomrubuni aache EAC kwamba watampa uwaziri, halafu wakamnyima, sasa Mnyakyusa amesema "po nifwe" na huyu atawaumbua sana tena kisheria maana yeye ni mjuzi wa Sheria, tena bunge zima anaheshimika, the matter of fact as of dataz hata rais mwenyewe humtumia sana kwa ushauri wa kisheria kwenye shughuli za taifa kwa hiyo kwetu CCM tulijua na tulisema mapema kuwa kwenye rais kumchagua Mwakyembe, kuna moto unakuja, kwa hiyo tunampa tena hongera Mwakyembe kwa kazi safi,

Now kwa Muungwana, tunataka kuamini kuwa nia na madhumuni ilikuwa yeye kutafuta reasonable cause ya kuwaondoa marafiki zake, ndio maana hakumchagua Kimiti au Mzindakaya, kwenye kamati, sasa amepewa nondo alizozitaka, tena za kisheria sio za kisiasa, meaning kwamba waliohusika, Kiwete akitaka anaweza kuwatosa kwenye sheria, au kuwatupa kisiasa kabisa wakawa kaputi, anything less itakuwa ni Banana Republic, na itakuwa ni haki ya wananchi ku-react as they want.

Kwa Mkuu Mwakyembe, sasa kuna mawili either wampe cheo, au amalizwe kisiasa kabisaaa, kama hakumwagiwa acid, yes I said it and yes I know it, lakini wananchi tuko pembeni tunaliangalia hili kwa macho yote tuone mwisho, ila kwa wale mlio karibu na Mwakyembe, mwambieni kuwa hii sasa ni saa mbaya, maana kuna wanaojitayarisha kupambana na Kikwete, kwenye 2010 na ni marafiki zake sana, ndio I said it na tunajua kuwa kuna mikakati inaendelea, tumesikia wana mpango wa kumgeuzia kibao Muungwana kuwa hana uwezo wa uongozi ndio maana wao wamekuwa wezi wa mchana, na wana mpango wa kujiosha kwa wananchi na kumsingizia Muungwana kuwa ndiye hafai, sasa umauzi ni wake aamue kunyoa au kusuka, ila kama anadhani kuwa ni marafiki zake, asubiri aone cha moto, nafikiri anakumbuka jinsi walivyotaka kumg'oa Mkapa kwenye term ya pili, sasa hilo linamsubiri na yeye, awatoe sasa ama sivyo wataishia kumtoa yeye,

Hongera Dr. Mwakyembe, Rais Kikwete sasa kazi kwako, kumbuka maneno yako mwenyewe kule Lusaka, the time is now, do it!


Ngoja tukaisome ripoti yote kwanza halafu tutarudi na more, nasikia kuna kina Kubenea huko, Duh! patamu hapo!

Mkuu FMES,

Hii inanifanya nifikiri kama kweli Muungwana alimwamini EL kwa asilimia mia moja. Kinamna flani naona kama ni usanii wa "keep your friends close and your enemies closer". Either way, CCM itanyooshwa na wanaCCM wenyewe, nchi itapata viongozi walio competent na mafisadi (wakiongozwa na BWM), Mola akijalia, wataenda lupango!!!
 
Unfortunately, yanayotokea sasa hivi huko Bungeni hayanishangazi kabisa kwa vile nilikuwa nayajua tangu mwaka juzi. Nilikuwa nakosa specifics tu.

L.O. Washa is a bogus material; Nyerere said then, and I believed him. Nyerere might have been wrong on many issues but not on this one about L. O. Washa.


Kichuguu hapo umefanya 'thought extraction'ya nilichotaka kusema,hahaha! Nyerere alikuwa anaona mbali, huyu L.O Washa alimjua ni fisadi toka mwanzo! kweli tuna very bogus PM.
 
Mkiiona ripoti ya kisheria (ambayo inaangalia mikataba sita ya Tanesco ikiwemo IPTL) na kutoa maoni ya mapungufu ya kisheria mtajiuliza ofisi ya Mwanasheria Mkuu inasimamia sheria za kijiji gani.

Hii ripoti bado ni ya siri na iliandaliwa na wanasheria wa Bunge kwa maagizo ya Kamati ya Mwakyembe.
 
Inawezekana Report Ikawa Siyo Accurate Mia Kwa Mia Lakini Kama Richmond Dev Company Ni Kampuni Hewa Kweli Basi Hakuna Utetezi Utakaokuwa Wa Maana Kwa Watanzania Bali Kuwaomba Radhi Na Hatimaye Kuwahjibika.hawa Watu Wanafanya Wananchi Kuichukia Serkali Yao Kwa Uroho Kujilimbikizia Utajiri Siku Za Mwizi Huenda Zimefika Tusitafute Mchawi
 
Mkiiona ripoti ya kisheria (ambayo inaangalia mikataba sita ya Tanesco ikiwemo IPTL) na kutoa maoni ya mapungufu ya kisheria mtajiuliza ofisi ya Mwanasheria Mkuu inasimamia sheria za kijiji gani.

Hii ripoti bado ni ya siri na iliandaliwa na wanasheria wa Bunge kwa maagizo ya Kamati ya Mwakyembe.

Hapo umenena Mzee Mwanakijiji. AG's Chamber inabidi itumbuliwe na kutoa usaha wote uliomo...mpaka kiini (AG). Ndio maana Kamati Teule ilisema mwakilishi wa AG alikuwa hana tija, this reflects the reality of the whole office of the AG of URT!
 
Mkiiona ripoti ya kisheria (ambayo inaangalia mikataba sita ya Tanesco ikiwemo IPTL) na kutoa maoni ya mapungufu ya kisheria mtajiuliza ofisi ya Mwanasheria Mkuu inasimamia sheria za kijiji gani.

Hii ripoti bado ni ya siri na iliandaliwa na wanasheria wa Bunge kwa maagizo ya Kamati ya Mwakyembe.

...tunaiomba!
 
naaam wakuu kumekucha hakuna mpya yeyote kutoka dom tokea vikao vya usiku hadi sasa?
 
lowassa mwakyembe.jpg

The Chairman of Parliamentary Probe Committee on Richmond Development Company LLD power generation contract, Dr Harrison Mwakyembe, makes a submission of his report in the House in Dodoma yesterday as Premier Edward Lowasa listens. (Photo: Selemani Mpochi
 
Kwa mara ya kwanza kuanzia kuanzishwa kwa bunge la vyama vingi Tanzania. Nimeshuhudia mbunge shujaa kutoka chama tawala akielezea, kinaga ubaga, mapungufu ya serikali ya chama tawala, katika bunge bila ya kujali maslahi ya chama tawala........................

Jamani msimsahau na Mhe. Agustine Lyatonga Mrema, nae alichukua hatua kama hii, na inawezekana zaidi, ya kuaniaka madhambi aya Chama tawala na kujiuzulu... (The motive known by himself!)
 
mwakiembe.jpg
Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge ya Kuchunguza Mkataba wa Richmond, Dkt. Harrison Mwakyembe, akiwapungia wabunge wenziwe wakati akiingia bungeni mjini Dodoma jana. (Picha na Emmanuel Kwitema)
 
Zaidi ya mwaka umepita toka nimwandikie barua ya wazi Bwana Lowassa kumtaka ajiuzulu Uwaziri Mkuu kutokana na matumizi mabaya ya madaraka ambayo yalilisababishia taifa kuingia hasara kubwa kupitia mkataba wa Richmond. Wakati huo nilimwandikia barua Hosea kutaka ajieleze kwanini ameisafisha Richmond wakati ambao hata ripoti yake mwenyewe pamoja na kufumba fumba bado ilionyesha bayana palikuwa na mazingira ya rushwa. Hii ilikuwa ni kabla ya ripoti ya PPRA. Hawa 'wahuni'(thugs) wote hawakujibu wala hawakuwajibika pamoja na kuwa sehemu ya barua hizo ziliandikwa na vyombo mbalimbali vya habari.

Sikubaliani na yoyote anayesema Lowassa ajiuzulu. Hastahili heshima hiyo kwa sasa, aliyashapewa onyo muda mrefu akapuuza. Sasa ni wakati wa mamlaka za juu yake kuchukua hatua.

Ni wakati wa Rais kuvunja baraza la Mawaziri na kumwondoa Lowassa- na kundi lake lote la Richmond. Lakini na kuwaondoa wote waliohusika na ufisadi wa BOT. Nilishawataja kwa majina wakati fulani. Hawa wote wanastahili kufukuzwa, sio kujiuzulu. Na hiki ndio kipimo cha JK kama yuko serious.

Kama Rais atashindwa kufanya hivyo leo, basi bunge lichukue nafasi yake kama boss wa serikali- the parliament has to play oversight function hapa. Lazima Bunge lipige kura ya kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu. Na hiki ndio kipimo kama bunge lililojaa CCM limeanza kujirekebisha au ni mchezo ule ule wa maigizo. Na wale waliodanganya kwa kiapo katika kamati nao wachukuliwe hatua- kauli ya Mwakyembe kwamba Kazaura na Msabaha, walisema mambo kwa mipaka na baada ya kiapo ndio wakasema kwamba hayo ni mambo ya wakubwa wao na kwamba mmoja wao ni kondoo wa kafara, ni ishara kwamba nao walidanganya- wakati wa kiapo walisema mambo pungufu walificha ukweli- wakati kiapo kiliwataka kusema ukweli na ukweli mtupu, nao wachukuliwe hatua za kibunge.

Naona adhabu nyingi zilizopendekezwa ni za kinidhamu na kiuwajibikaji- hawa wahusika wakuu wanatakiwa kuchukuliwa si tu hatua za kinidhamu. Wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria- ili iwe fundisho kwa watumishi wa umma kushiriki ufisadi kwa kizingizio cha kutekeleza majukumu yao. Ni Rais pekee ndiye mwenye kinga. Hawa wahujumu uchumi na wapindishaji wa sheria za ununuzi wengine hawa wanaweza kabisha kushtakiwa.

Lakini lazima tujiuize,fedha zetu hizi za RICHMOND/DOWANS zimekwenda wapi? Kwa nani? Zinarudishwa vipi? Maana tukiwaaacha hawa wakajiuzulu ama tukasitisha mkataba na wataenda tu 'honey moon' kwa fedha za wavuja jasho ambao ndio wanaopandishiwa bei ya umeme kila kukicha huku wakitozwa kodi nyingi na kuchangishwa miradi bubu ya maendeleo. Lakini huu ni wakati wa kufungua pia pandora box ya IPTL, Kiwira(Tan Power), Agrekko, Artumas, Songas.

Kila nikipita Jimbo la Ubungo na kuitazama mitambo ya RICHMOND/DOWANS na ile ya Songas- najua ni mabomu tu ya wakati kwa wananchi wa Tanzania. Walau sasa yanaanza kuvuja kabla ya kulipuka!

Leo TC ya ushirikiano wa vyama tunakutana kuipitia hiyo ripoti na kutafakari cha kufanya; haya mapambano ndio kwanza yameanza- na hongera wote waliyoyaanzisha.

Ukiitwa kuandamana utajitokeza? Ukichorwa mstari kati ya "HAKI/UKWELI" na UFIDADI/UOVU uko tayari kusimama na kuhesabiwa?

Nitarejea....

JJ
 
Back
Top Bottom