Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Kwenye Msafala wa Mamba Na kenge wamo..Mijusi Tunutunu...
Tafadhali!! endeleeni Kujiengua kama Kenge Kubwa lenu Lilivyo fanya...

Lowasa!!Bado Utatueleza ukweli tu...Ulitapeliwa au ulitutapeli..?

Lowasa..Meghji anafaa kua Waziri Mkuu?

Meghji??? Tutakuwa tunaruka mkojo tunakanyaga mavi!!!!! Kutukana na uwezo mdogo wa JK tunahitaji PM ambaye ni mbunifu, mchapakazi na ambaye atafanya maamuzi bila kumuogopa JK. So far naona Malecela atafaa kidogo, ingawa alishatuangusha huko juma enzi za mwinyi!!!!!!!
 
Kujiuzulu tu!!! naona kama haitoshii!

Kwanini wasishitakiwe???

Msabaha atajakuwa shahidi mzuri!!!
 
Waziri Mkuu wa Tanzania Edward Lowassa amejiuzulu baada ya kulaumiwa na kamati ya bunge iliyochunguza kashfa ya ufisadi mkubwa katika utolewaji zabuni ya umeme wa dharura.
Akitangaza hatua yake katika bunge Alhamis asubuhi, Bwana Lowassa alisema: "Nimetafakari sana kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya serikali yangu, nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumuomba niachie ngazi."


Hatua ya kujiuzulu
ninafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa


Waziri Mkuu Lowassa

Bwana Lowassa aliteta kwamba kamati teule ya bunge iliyomhusisha na kashfa ya Richmond ilimnyima haki ya kujieleza.

Alisema alikuwa ametafakari kwa makini kuhusu shutuma hizo na kufikia uamuzi kwamba, "tatizo ni uaziri mkuu."

"Kwamba ionenekane Waziri Mkuu ndiye amefanya haya, tumwondolee heshima au tumwajibishe."

Akielezea hatua yake ya kujiuzulu, Bwana Lowassa aliongeza "ninafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uajibikaji na pia kutokukubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya bunge kwa kumsingizia mtu."
source BBc
 
..msiwasahau wajumbe wengine wa tume.

..vilevile wale waliotoa ushahidi nao wana ujasiri mkubwa.

.. haswa haswa wale waliotoboa siri kwamba "bwana mkubwa" ndiye aliyekuwa akiweka shinikizo.
 
Huko ndiko kumkoma Nyani Giladi kwenyewe, Lowassa, Rostam, Msabaha, TAKUKURU et al. wamepewa kitu na boksi kavukavu inavyotakiwa sio longolongo ndefuuuu tunazoshuhudia kila kukicha.... sasa tusubiri kuona utekelezaji wa mapendekezo ya tume.
 
Mwakyembe 'the Giant Killer'. I have nothing but utmost respect for this formidable UDSM academician turned politician. Kwa wale wanaomjua Mwakyembe toka alipokuwa 'Daily News' ni mzalendo na mwanaharakati. Let us hope that he will continue that way. Aluta Continua.
 
Ripoti kamili hii hapa ina kurasa 105

[media]http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/2/7/richmond.pdf[/media]
 
Kufuatia ripoti ya Dk. Mwakyembe kuhusu Richmond, imebainishwa kwamba Mwanasheria Mkuu na maofisa wake walifanya makusudi au kuzembea katika mtiririko mzima tangu zabuni mpaka contract signing. Na vilevile, imebainishwa kwamba TAKUKURU walihusika kwa kiasi kikubwa kuuficha uhozo huu kinyume cha sheria. Kwa maana hiyo basi, Mwanasheria Mkuu na Mkurugenzi wa TAKUKURU wote kwa pamoja wanapaswa kuwajibika kwani si watu safi. Wawili hawa ni miongoni mwa wale watatu wanaopaswa kuchunguza ufisadi katika akaunti ya EPA pale BoT.!! Je, inawezekana vipi fisadi akamchunguza fisadi mwenzie? Si ndio hawahawa wanahusika na hata huko BoT? Sioni mantiki ya hii tume kwa sasa mpaka pale wazalendo halisi kama kina Mwakyembe watakapojumuishwa!
It's my expectation that JK can use a simple common sense on this.
 
Edward Lowassa said:
"tatizo ni uaziri mkuu. Kwamba ionenekane Waziri Mkuu ndiye amefanya haya, tumwondolee heshima au tumwajibishe."


..ama kweli mkuki kwa nguruwe.

..Lowassa alinunua magazeti wakawa wanamwandama Sumaye for 10 good yrs. sasa yote hayo yamemrudia mwenyewe.
 
Kwa wale ambao wataona ugumu kusoma ripoti yote mapendekezo 18 katika ripoti hiyo haya hapa

Mapendekezo 18 ya Kamati ya Mwakyembe

Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2004 (Public Procurement Act, 2004) ipitiwe upya ili kuiboresha kwa kuipa Mamlaka nguvu zaidi za udhibiti na uwezo wa kuchukua hatua pale sheria na kanuni zinapokiukwa, badala ya kutoa ushauri tu kama ilivyo sasa.

Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma isiwajibike Wizara ya Fedha ambayo nayo ni taasisi ya ununuzi (procurement entity) badala yake iwe chombo huru kinachowajibika Ofisi ya Rais na taarifa zake kuwasilishwa bungeni.

Mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC na sasa Dowans Holdings S.A, kama ilivyo mikataba kati ya TANESCO na IPTL, SONGAS, AGGREKO na Alstom Power Rentals inatoa unafuu usiostahili kwa makampuni hayo ya umeme na kuiumiza TANESCO na hatimaye watumiaji na walipa kodi kimapato, k.m mikataba hiyo kuwa na vipengele vya kuibana TANESCO kuyalipia makampuni hayo kodi zinazohusika na uendeshaji (operations), matengenezo/marekebisho ya mara kwa mara ya mitambo (maintenance) gharama za bima, ada za mawakili na washauri elekezi (consultants) gharama za mafuta na gesi ya kuendeshea mitambo, gharama za ukodishaji mitambo (capacity charges) ambazo TANESCO hulipa kila mwezi si chini ya wastani wa shilingi bilioni 2 kwa kila kampuni, izalishe au isizalishe umeme.

Serikali ipitie upya mikataba yote kati ya Tanesco na wazalishaji wa umeme binafsi mapema iwezekanavyo kama ambavyo mikataba ya madini inavyopitiwa upya sasa kwani bila kufanya hivyo, mzigo mkubwa wa gharama za umeme utawaelemea wananchi na kushindwa kufikia azma ya serikali ya maisha bora kwa kila Mtanzania.

Kwa kuwa mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC ulikuwa wa uzalishaji umeme wa dharura kipindi ambacho nchi ilikuwa katika hali ngumu ya ukame uliokausha mabwawa yote ya kuzalishia umeme, serikali itathmini upya uhalali wa kuwepo na kuendelea kuwepo na mkataba huo kutokana na udanganyifu bayana uliofanywa na Richmond Development Company LLC kuhusu uwezo wake kifedha, kiufundi na uzoefu wake katika masuala ya uzalishaji umeme; usajili na uwepo wake kisheria kama kampuni halali yenye ukomo wa hisa nchini Marekani na Tanzania; uhusiano wake kisheria na kampuni kubwa ya kimataifa ya Pratt & Whitney.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye katika majadiliano yake na Kamati Teule alionyesha kutokuelewa kabisa kilichokuwa kinatendeka na wasaidizi wake, na mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Wakili wa Serikali, Donald Chidowu, ambaye ushiriki wake katika GNT haukuwa na tija yeyote, wawajibishwe na mamlaka ya juu ya nchi kwa kuchangia kuiingiza nchi katika mkataba wa aibu.

Katika mikataba yote na makampuni ya nje, serikali ihakikishe kuwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) inatumika kikamilifu katika kupata taarifa kamili za kampuni hizo, kama vile wanahisa, mitaji na anwani. Aidha, ofisi zetu za ubalozi zilizo sehemu mbalimbali duniani zihusishwe katika majadiliano na makampuni yanayotoka nje ya nchi kwa lengo la kupata taarifa zao za msingi na kuboresha nguvu ya hoja ya serikali.

Wajumbe wote wa Kamati ya Serikali ya Mashauriano katika suala la Richmond ambao ni maafisa waandamizi wa serikali wawajibishwe mara moja kwa kushindwa kutumia elimu na ujuzi wao kulinda maslahi ya taifa.

Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi aliyeshabikia sana uhaulishaji huo, awajibishwe.

Yafanyike mabadiliko ya haraka ya uongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru ambayo ilitoa ripoti mbovu ya kuisafisha Richmond.

Wakati umefika sasa kwa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 (Public Leadership Code of Ethics Act) ifanyiwe marekebisho makubwa ili kudhibiti utaratibu unaoonekana wa kawaida sasa wa viongozi waandamizi wenye dhamana kisiasa kuendelea na biashara zao wakiwa madarakani, hivyo kuwaweka kwenye mtihani mkubwa wa mgongano wa kimaslahi katika maamuzi yao. Tufike mahali ambapo sheria iwalazimu kuchagua kati ya utumishi wa umma au biashara binafsi, viongozi waandamizi wenye dhamana kisiasa (mawaziri na kuendelea) kuendelea na biashara zao wakiwa madarakani hivyo kuwaweka kwenye mtihani mgumu wa mgongano wa kimaslahi.

Serikali iondokane kabisa na utaratibu wa kutumia mawakala katika ununuzi wa mitambo ya kuzalisha umeme nchini na kuhakikisha kuwa wizara husika ina taarifa za bei halisi ya mitambo kila wakati ili kujiepusha na mchezo wa kawaida wa mawakala kupandisha bei mara mbili au zaidi ya bei halisi.

Utaratibu tuliourithi kutoka kwa wakoloni na kuuzoea wa kuiona mikataba ya kibiashara kuwa ni siri hata kwa walipa kodi wenyewe na kuwa uwanja wa pekee wa watendaji, umepitwa na wakati.

Waziri wa Nishati na Madini wa wakati huo, Ibrahim Msabaha na Katibu Mkuu, Arthur Mwakapugi wachukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa kuliingiza taifa kwa makusudi kwenye mkataba na kampuni ya mfukoni ambao umesababisha hasara kubwa kwa nchi.

Kamishna wa Nishati, Bashir Mrindoko achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kumshauri Katibu Mkuu mpya wa wizara kuhusu udhaifu wa Richmond Development Company LLC ambao ulijulikana dhahiri na wizara toka mwaka 2004 kwenye mkataba wa bomba la mafuta.

Utaratibu wa kuteua wakurugenzi na makamishna katika wizara kuwa wajumbe wa bodi za wakurugenzi za mashirika yaliyo chini ya wizara, unazua mgongano wa kimaslahi, kudhoofisha usimamizi na uwajibikaji, hivyo serikali iupige marufuku mara moja.

Waziri Mkuu Edward Lowassa ambaye ndiye mwenye madaraka ya juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hadi siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ndiye kiongozi wa shughuli za serikali bungeni apime uzito wa matokeo ya uchunguzi huu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya Bunge.

Bunge ambalo linathibitisha uteuzi wa Waziri Mkuu kwa mujibu wa Ibara ya 51, liangalie matokeo ya uchunguzi huu kama hayajaathiri hadhi na uzito wake ndani ya Bunge.


http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/2/7/habari5.php
 
Mie pia Nampongeza, amekata na kufunua, lakini pia aombwe radhi na baadhi ya wana JF waliomponda pale alipoteuliwa kama m/kiti wa kamati hiyo. Bravo
 
Kufuatia ripoti ya Dk. Mwakyembe kuhusu Richmond, imebainishwa kwamba Mwanasheria Mkuu na maofisa wake walifanya makusudi au kuzembea katika mtiririko mzima tangu zabuni mpaka contract signing. Na vilevile, imebainishwa kwamba TAKUKURU walihusika kwa kiasi kikubwa kuuficha uhozo huu kinyume cha sheria. Kwa maana hiyo basi, Mwanasheria Mkuu na Mkurugenzi wa TAKUKURU wote kwa pamoja wanapaswa kuwajibika kwani si watu safi. Wawili hawa ni miongoni mwa wale watatu wanaopaswa kuchunguza ufisadi katika akaunti ya EPA pale BoT.!! Je, inawezekana vipi fisadi akamchunguza fisadi mwenzie? Si ndio hawahawa wanahusika na hata huko BoT? Sioni mantiki ya hii tume kwa sasa mpaka pale wazalendo halisi kama kina Mwakyembe watakapojumuishwa!
It's my expectation that JK can use a simple common sense on this.


Na ndio huko huko BOT ambako na TAKUKURU ambao Mwakyembe kawachafua na kuwavua nguo wapo! Ukishangaa ya Musa basi utazirai kwa kuyaona ya firauni!
Long Live Tanzania
 
I have read the report. imeandikwa kwa mantiki ndiyo maana amafisadi mameamua kuanza. Bado baba lao Che Nkapa.Mwema where are U? arrest them all!!
 
Kashfa ya Richmond, Waziri Mkuu,mawaziri wawili waomba kujiuzulu Tanzania
Muhibu Said na Kizitto Noya

WAZIRI Mkuu Edward Lowassa, Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Ibrahim Msabaha, wametangaza kujiuzulu nyadhifa zao kutokana na kuhusishwa katika kashfa ya zabuni ya Kampuni ya Richmond Development ya Marekani.

Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti katika Kikao cha Bunge mawaziri hao walisema tayari wameshamwandikia barua Rais Jakaya Kikwete kumtaka aridhie nia yao ya kujiuzulu kwa maslahi ya taifa.

Hata hivyo, Spika wa Bunge, Samuel Sitta aliliambia Bunge kuwa hadi kikao cha Bunge cha jana jioni mawaziri hao bado hawajajiuzulu rasmi kwani Rais hajatoa taarifa rasmi kwake kueleza kuwa ameridhia nia yao hiyo.

Lowassa ambaye ameshika nafasi ya Uwazi Mkuu kwa muda wa miaka miwili sasa alisema amefikia uamuzi huo ili kujenga dhana ya uwajibikaji.

"Mheshimiwa Spika, nimetafakari sana, kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya serikali yangu, nimeamua kumwandikia Rais barua kumwomba niachie ngazi. Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji, lakini na kutokukubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya Bunge wa kumsingizia mtu," alisema Lowassa.

Kabla ya kutangaza uamuzi wake huo, Lowassa alimpongeza Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dk Harrison Mwakyembe akisema kwamba aliwasilisha ripoti hiyo bungeni kwa mbwembwe.

"Lakini la pili, nimpongeze Dk Harrison Mwakyembe, Mwenyekiti wa Kamati Teule kwa kuwasilisha kwa mbwembwe nyingi sana taarifa yake, mbwembwe zilikuwa nzuri kweli," alisema Lowassa.

Hata hivyo, alisema aliamua kuzungumza bungeni jana ili kuweka kwenye kumbukumbu kwamba hakuridhika na jinsi kamati hiyo ilivyofanya kazi yake.

Alisema katika uchunguzi wake, kamati hiyo iliamua kusikiliza watu wengine, minong'ono ya mitaani na ilisafiri hadi nchini Marekani kwenda kutafuta mashahidi, lakini yeye ambaye ni mmoja katika watuhumiwa, hawakumhoji hata siku moja.

"Mheshimiwa Spika, nimesimama kueleza masikitiko yangu, Ofisi ya Bunge mpaka ofisini kwangu hata wangeniita ningekwenda kwa miguu kama hamna gari na nilikuwa tayari kufanya hivyo," alisema Lowassa.

Kutokana na hali hiyo, alisema anaona kuwa alichofanyiwa si sahihi, kimemfadhaisha, kumdhalilisha na ameonewa kwa jambo hilo.

"Maana zimechukuliwa tuhuma zikaja zikaelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo. Mimi sijaulizwa. Kulikuwa na shida gani ya kuniuliza, kwa nini muamini minong'ono ya mitaani kuliko maelezo yangu. Sisi wote hapa ni wanasiasa tukianza kuamini minong'ono ya mitaani niambieni mwanasiasa atakayesimama. Hatuwezi, tume imepewa muda wa kutosha, lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na wanamsema kwa kirefu sana," alisema Lowassa.

Alisema hata aliponong'onezwa na Spika wa Bunge, Samuel Sitta na kumuuliza kama anao ushahidi wowote, alimpa ushahidi huo wa maandishi, lakini katika ripoti ya kamati, hakuna ushahidi hata mmoja uliotoka kwa Waziri Mkuu.

"Kile kitabu cha majedwali kimejaa majedwali mengi pamoja na magazeti ya udaku, lakini maelezo ya Waziri Mkuu hakuna hata moja," alisema Lowassa na kuongeza:

"Mheshimiwa Spika, naamini ngekuwa ni heshima wangeiweka halafu wakasema tunakaa kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii, hiyo ndiyo imejengwa hoja. Lakini kujenga hoja na kuja hapa bungeni tunahutubia nchi nzima na kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya hiki bila ya kumsikiliza nachelea kuuliza hivi mtu wa chini itakuwaje?".

Hata hivyo, alisema ametafakari kwa makini jambo hilo na kujiuliza sababu za wajumbe wa kamati hiyo kufikia kuacha jambo la msingi kama hilo.

"Mimi…nadhani tatizo ni Uwaziri Mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndio amefanya haya, tumuondolee heshima au tumwajibishe," alisema

Alimshukuru Rais Kikwete kwa heshima aliyompa ya kutumikia nchi kwa wadhifa huo kwa miaka miwili, pia alimshukuru Spika, mawaziri, manaibu waziri, wabunge na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Spika Sitta alisema tamko hilo la Lowassa ambalo lilijenga wingu zito bungeni na kuzua mkanganyiko na minong'ono miongoni mwa wabunge, ni zito na hakulitegemea.

"Waheshimiwa wabunge tamko hilo ni zito na wala sikulitegemea. Sasa ningeomba ushauri tuendeje. Tuchangie tu hakuna haja ya kunong'ona na kupiga kelele," alisema Sitta.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe alikuwa mbunge wa kwanza kuomba mwongozo wa Spika bungeni jana iwapo tamko hilo la Lowassa akiwa ni Waziri Mkuu, linamaanisha kuwa Baraza zima la Mawaziri kuanzia wakati huo limejiuzulu.

Akijibu hoja hiyo, Sitta alisema hajapata mawasiliano yoyote na Rais kumueleza kama amekubali kujiuzulu kwa Lowassa au la na kwamba, kilichofanywa na Waziri Mkuu, ni kuwasilisha tu kusudio lake la kuomba kujiuzulu.

"Sasa hatuwezi kulifanyia kazi kusudio, kwa hiyo tuendelee tutaona mambo kadri yanavyokwenda. Hayo mengine yanayofuata sasa yananguka hayana maana kabisa," alisema Sitta.

Pamoja na Karamagi kutangaza nia yake hiyo, alisema hajahusika na kusainiwa kwa mkataba kati ya serikali na Richmond akisema kwamba, ulisainiwa miezi sita kabla ya yeye hajahamishiwa katika Wizara husika ya Nishati na Madini.

Hata hivyo, alisema kutokuwapo kwa nyaraka yoyote inayoonyesha alihusika na kusaini mkataba huo, hakumuondolei kuwamo katika utaratibu wa serikali wa "Uwajibikaji wa Pamoja".

Alisema akiwa wizarani hapo, waligundua kuwa Richmond ina dalili zote za tapeli na kutaka kufuta mkataba ili kumpata mwekezaji mwingine, lakini kamati katika ripoti yake haikupongeza hatua yake hiyo.

Naye Dk Msabaha akitangaza nia yake ya kujiuzulu wadhifa wake, alisema amefikia uamuzi huo akiamini katika uwajibikaji na utawala bora.

"Mimi si mwoga, ni mwadilifu, si mla rushwa, ni mchapakazi, ninaamini katika uwajibikaji na utawala bora," alisema Dk Msabaha.

Mapema wakichangia mjadala huo baadhi ya wabunge walipendekeza mawaziri wote waliohusishwa katika mkataba huo mbovu kufilisiwa ili kuziba pengo la hasara iliyopatikana.

Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela alisema kimsingi hakuna mtu aliyeonewa katika taarifa hiyo kwani kuna kila ushahidi wa kuborongwa kwa mkataba huo.

Kilango aliyesema kuwa anapotetea maslahi ya wananchi hana urafiki, aliwataka wabunge wenzake kukubaliana na mapendekezo ya kamati hiyo na kuipitisha bila kupoteza muda.

Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wenzake wa kamati na mwenyekiti wa kamati hiyo Mbunge wa Nzega (CCM) Lukas Selelii alisema mkataba wa Richmond ni mbovu kuliko mikataba yote ambayo serikali imewahi kuiingia na kumtaka Lowassa kufuta kauli yake kuwa taarifa ya kamati hiyo ni ya uwongo au kuithibitisha.

Akitetea hoja yake Lowassa alisema kuwa kauli anayoamini kuwa ya uwongo ni ile inayosema kuwa Kampuni ya Richmond ni yake na rafiki yake, Rostam Aziz.

Naye Mbunge Viti Maalum (Chadema) Anna Maulida Komu, alilaani tabia ya baadhi ya watandaji wa serikali na wabunge kutumia nyadhifa zao kujinufaisha kwa gharama za wapigakura wao.

"Naomba ndugu zangu tuache kuwageuza wananchi Kachumbari bali tufanye kazi waliotutuma kwa maendeleo yao na taifa," alisema Komu.

Wabunge wengine waliochangia hoja ya kushinikiza Mawaziri hao kuwajibika ni pamoja na Mbunge wa Simanjiro (CCM) Christopher Ole Sendeka na Dk Willibrod Slaa, mbunge wa Karatu (Chadema).

Dk Slaa alitaka pia Baraza lote la Mawaziri lijiuzulu kwa kile alichoita uzembe wa kushindwa kufuatilia ukweli wa kampuni ya Richmond kabla ya kukubali kuingia nayo mkataba.

Alitaka pia kufanyika kwa uchunguzi wa kipolisi ili kubaini ukweli wa mambo na kuchukua hatua zaidi kwa watuhumiwa wa sakata hilo.

Naye Mbunge wa Moshi Mjini (CCM) Philemon Ndesamburo alipendekeza rais awawajibishe Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kwamba waondolewa kwenye kamati ya EPA kwa kuwa wameonyesha kutokuwa waandidilifu katika kazi zao.

Mwananchi 08/02/2008
 
Mheshimiwa Spika, nimetafakari sana, kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya serikali yangu, nimeamua kumwandikia Rais barua kumwomba niachie ngazi. Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji, alisema Lowassa.

.....Now stop bashing and show the man a little respect...haha ahaha ahaha hah,anyway he's rich man and is not going to jail ...who cares!
 
Kuna kitu kimoja sikielewi labda wakuu mnaweza kunisaidia. Nimeipitia juu juu ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Dk. Mwakyembe. Naona watu wameongelea sana kutaka watu kujiuzulu, na wanaohusika kuchukuliwa hatua za kisheria.

Pia Dk. Mwakyembe amelalamika kuwa watu waliohojiwa hawakutoa ushahidi wa kutosha "officially" katika kiapo.Na wengine wametoa ushahidi nje ya kiapo.Sasa kama mtu hatoi ushahidi katika kiapo na anakuja kutoa ushahidi nje ya kiapo hapo hamna kesi ya "obstruction of justice" ili kuweza ku uphold rule of law?

Inawezekana hili ni swala dogo in the grand scheme of things na watu walifocus kumtoa Simba ndani ya nyumba kabla ya kupanga vikombe kwenye kabati, lakini inabidi tuweke standards za juu kuhusu utawala wa sheria ili kesho watu wajue kuwa ukiitwa na tume yenye mamlaka ya kisheria, inabidi utoe ushahid, utoe ushahidi wa kweli, na utoe ushahidi wote. Siyo mambo ya ma deal na ushahidi wa vichochoroni ambao unakosa nguvu.
 
Nd'o hapo mtu anakuambia we have an 800 pound gorilla in the house and we need to remove it..
Hoja zako safi sana Bw Pundit lakini swali linakuja hivi... hawa viongozi wetu wanajua hio kauli ya obstruction of justice kweli?Umesema freshi kua inabidi to lift up our standards na hilo liwe changamoto kwa hizo kamati teule zinazofanya uchunguzi wa mambo.Ukweli ni kwamba once under oath an individual cannot lie na iwapo atadanganya basi ni perjury which is punishable by a jail sentence.Kwa hivyo wanakamati pull up your socks on this matter!
 
Mtu ukisema uongo chini ya kiapo si 'perjury' hiyo? Kama Bill, mumewe Hillary,aliposema " I did NOT have sexual relations with that woman" Si alinyang'anywa leseni yake ya uwakili ktokana na hili? Au hawa wakuu hawakusema uongo bali walikataa kuji'commit one way or another'? Kwa vyovyote vile ni serious issue.
 
Back
Top Bottom