Rostam: Siwajui Richmond
na Mwandishi Wetu
MFANYABIASHARA na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), amesema hana uhusiano wowote, na wala haijui Kampuni ya Richmond Development Company LLC ambayo ilishinda zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura baada ya kuingia mkataba wenye utata na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
Kauli hiyo ya kwanza kutolewa hadharani nje ya Bunge na Rostam, mmoja wa wafanyabiashara na rafiki mkubwa wa Rais Jakaya Kikwete, na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, inakuja siku kadhaa sasa tangu jina lake lihusishwe kwa kiwango kikubwa na kampuni hiyo hewa, ambayo utata kuhusu kuwapo kwake na namna ilivyoshinda zabuni katikati ya mwaka 2006, vilibainishwa na Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe.
HAPA KALE KAMCHEZO KA KUMUINGIZA JK KATIKA KASHFA KANAANZA POLE POLE.
Rostam aliyepata kuwa Mweka Hazina wa CCM Taifa hadi mwaka ujana, alitoa kauli ya kuikana Richmond jana, wakati alipofanya mahojiano ya simu na Tanzania Daima, alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa kinachosababisha jina lake lihusishwe na kampuni hiyo ya kitapeli na ile ya Dowans ambayo ilirithi mkataba wa Richmond.
Alisema, haijui kabisa kampuni hiyo, hawajui wamiliki wake na wala hajapata kuwasiliana nayo. Mbali ya hilo, Rostam ambaye nyota yake ilianza kuingia doa tangu alipotajwa kuwa kwenye orodha ya mafisadi (The List of Shame) iliyotangazwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, aliieleza Tanzania Daima kwamba, iwapo kampuni hiyo ingelikuwa ni yake, basi isingekuwa rahisi kushindwa kuileta mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura kama ilivyotokea kwa Richmond.
Siijui hata kidogo, siwatambui na siwafahamu. Mimi ni mfanyabiashara, sina sababu ya kuficha, kama ingekuwa ni kampuni yangu, nisingeshindwa kutekeleza mradi huo. Leo hii kutokana na kuwepo kwa mawasiliano ya kutosha, si rahisi mmiliki wa kampuni hiyo asijulikane. Mimi sidhani kama imekuwa ni ngumu kiasi hicho, alisema Rostam.
HAPA ANASEMA HAWAJUI WAMILIKI WA RICHMOND wakati ndiye aliyeshiriki mchakato wote wa kuhakikisha Richmond inachukuliwa na Dowans, angalao mpaka hapo hakupaswa kukanusha.
Wakati akikana kuifahamu Richmond na wamiliki wake, Rostam, alikiri kuwahi kutaka kufanya kazi na Kampuni ya Dowans Holdings S.A ambako Kampuni ya Richmond ililazimika kuhamishia mkataba wake huko, baada ya kushindwa kuutekeleza kwa muda uliowekwa.
Mimi ni mkandarasi. Nina kampuni inaitwa Caspian. Sina uhusiano na Dowans ingawa niliomba kupatiwa kazi ya ukandarasi, alisema Rostam.
Anasema aliomba kazi kama ambavyo kampuni yake inafanya kazi Buzwagi
Matamshi haya ya Rostam yanatokana na shaka iliyojitokeza baada ya Kamati Teule ya Bunge kueleza katika ripoti yake kwamba, iligundua kuwa Dowans iliwahi kutumia anwani ya barua pepe ya Kampuni ya Caspian Construction Ltd inayomilikiwa na mfanyabiashara na mwanasiasa huyo.
Akifafanua kuhusu hilo, Rostam alisema alilazimika kuacha anuani yake kwa Dowans baada ya kuomba kazi kwa kampuni hiyo.
Nilipoomba kazi kama mkandarasi, nilitakiwa kuacha anuani, unapoomba kazi lazima uache anuani, alisema kwa ufupi.
HIKI NI KICHEKESHO, Kinachozungumzwa hapa si Dowans kuwa na anuani ya Rostam, bali Dowans kutumia anuani ya kampuni ya Rostam ya Caspian, ikiwamo ya E-mail na sanduku la Posta, lakini pia hata mtu aliyekua akisaini cheki za Dowans ni Mtumishi wa Caspian na zaidi ya yote, Rostam ndiye aliyekua anasimamia malipo ya Dowans kwa watu waliokua wakiidai Richmond na gazeti la Mwanahalisi liliwahi kuandika kuhusu hilo na kuweka hundi hizo ukurasa wa kwanza, waandishi angalieni kitabu chekundu cha vielelezo vya kamati. Kwa TAARIFA ni kwamba Rostam aliwatisha watu walikua wakifuatilia madeni ya Richmond kwa kuwaambia "we hujui sisi ndio tunashikilia nchi?" kabla ya jamaa kutishia kwenda mahakamani na ndipo Rostam akalipa deni, sasa alikua akiwalipa kama nani?
Akizungumza kuhusu kauli ya Kamati Teule ya Bunge kuwa alikwepa wito wa kwenda kuhojiwa juu ya anwani ya kampuni yake kutumiwa na Dowans, na pia baadhi ya wafanyakazi wa kampuni yake kusemekana kuwa wafanyakazi wa Dowans pia, alisema barua hiyo ya wito ilichelewa kumfikia.
Barua ya kuitwa kwenye kamati inaonekana iliandikwa Desemba 24, 2007 ikieleza kuwa niende kuwaona Desemba 27,2007, lakini hata hivyo barua niliipata tarehe 2 Januari, 2008 baada ya kamati kumaliza kazi yake. Kipindi hicho cha mwezi Desemba, mimi nilikuwa nje ya nchi nikiwa likizo na familia yangu, alisema Rostam.
Alipoulizwa kuhusu ushahidi uliotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salvatory Rweyemamu kuwa yeye ndiye aliyemuunganisha na Mkurugenzi wa Richmond, Mohammed Gire kufanya kazi ya ushauri wa habari katika kampuni hiyo, Rostam alikana kwa kusema kuwa, alichowahi kufanya ni kumuunganisha kufanya kazi kama hiyo kwa kampuni ya uwakala wa kupakua mizigo bandarini.
Si kweli. Mimi sikumuunganisha na watu wa Richmond, isipokuwa nilimuunganisha na Kampuni ya Freight Forwarders inayomilikiwa na Hassan Dala ya kupakua mizigo bandarini, walikuwa wanatafuta PR company (kampuni inayojihusisha na masuala ya mahusiano ya umma) na hiyo kampuni ya uwakala wa mizigo ndiyo ninayotumia mimi katika shughuli zangu, alisema Rostam.
HAPA ANAMKANA SALVA WA IKULU MCHANA KWEUPEEEEEEEE!!! Salva anawajua sana hawa jamaa kwa kuruka mambo lakini anavumilia tu
Aidha akizungumzia uamuzi wa Bunge wa kutaka athibitishe au afute kauli yake kuwa, Kamati Teule ilifanya kazi yake nje ya muda iliyopewa, alisema hilo atalizungumzia bungeni, ambako atatoa ufafanuzi wa kauli yake hiyo.
Katika majumuisho ya mjadala wa ripoti yake, Kamati Teule ililiomba Bunge limtake Rostam kufuta au kuthibitisha kauli yake kwamba ilifanya kazi nje ya muda iliyopangiwa.
Hata hivyo, Rostam hakuweza kufuta au kuthibitisha kauli yake hiyo kwa sababu hakuwepo bungeni kwa kipindi kirefu baada tu ya kamati kutangaza ripoti yake.
Kuhusu Kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd ambayo ilitajwa katika orodha ya kampuni zilizohusika kuchota fedha za akaunti ya madeni ya nje (EPA) ambayo jina lake linatajwa kuhusishwa nayo, Rostam ambaye jana alikuwa akitoa majibu mafupi kwa kila swali aliloulizwa, alikana pia na kusema kuwa haijui kabisa kampuni hiyo.
Kampuni ya Kagoda inadaiwa kuchotewa kiasi cha zaidi ya sh bilioni 40 kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wiki nne tu baada ya kusajiliwa. Na yapo madai zaidi kwamba, sehemu ya fedha hizo zilitumika katika kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 zilizomuingiza madarakani Rais Jakaya Kikwete, jambo ambalo hata hivyo lilipata kukanushwa na Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba.
Katika kuonyesha kuwa tuhuma zinazoelekezwa kwake hazijamyumbisha kisiasa, Rostam alisema kutajwa kwa jina lake katika kashfa ya Richmond na ile ya BoT hakujamshushia hadhi kama mbunge wa Igunga, kwa sababu bado wapigakura wake wanampenda na kumuunga mkono.
Kashfa hizi hazijanishushia hadhi, wananchi wa Igunga wananiunga mkono. Hizo ni chuki za kisiasa, hata Mwakyembe alipotoa ripoti yake, hakusema kama Kampuni ya Richmond ni ya kwangu, alisisitiza Rostam kisha akakata simu.
HII YA KUKATA SIMU NI DANGANYA TOTO, TANZANIA DAIMA NAO WAMEINGILIWA? HUYU MWANDISHI KAMA HAJAKUTANA NA ROSTAM WALIZUNGUMZA NA KUMALIZA KILA KITU NA KUELEKEZANA NAMNA YA KUANDIKA BILA SHAKA KWA MAKUBALIANO MAALUMU CHINI YA MPANGO KAMAMBE WA "AGENDA 21"... JAMANI ROSTAM HAWEZI KUKATA SIMU BAADA YA KUZUNGUMZA MANENO YOTE HAYA NA BILA KUFUATILIA HADI KUJUA KILICHOANDIKWA KABLA YA STORI KUCHAPISHWA GAZETINI. HUU NDIO UKWELI NA TANZANIA DAIMA AMA HATA CHADEMA NAO WAMEINGILIWA!!!!?