Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

RDC ime shake Nchi na utawala wake kama Zitto kutolewa Bungeni pia .Lakini makubwa bado yamelala chini ya RDC na walicho kifanya kwa uharaka ni kumwambia Lowasa ondoka kufa wewe mmoja tubakie madarakani .Leo issue RDC bungeni inaanza kupangia chenga , bado BoT ambayo inaweza kuona Rais anaomba kujiondoa .Naamini BoT hawatataka ifike Bungeni kwa kweli .Nasema Polisi take over upelelezi ufanywe na ripoti iwe wazi isije ikawa kama mambo ya ujambazi na madawa ya kulevya hadi sasa hayujui nini kinaendelea .

Kosa la Lowasa na wenzake ni kosa la kuhujumu Uchumi wa Nchi .Kujiondoa pekee hakutoshi bali Mahakama ijue na iamue swala hili .

Kazaura tupe nafasi tumalize moja hili kwanza then tutakuja kukuchambua na kukueleza ni wapi umeibia Tanzania vya kutosha.

Na ndio hapo Lowassa atakaposema kwamba ule mradi ulikuwa ni wa ushirika (mtandao)! Tutayajua mengi akifikishwa panapo haki!
Huenda naye ni Bangusilo wa mtandao pia!
 
RDC ime shake Nchi na utawala wake kama Zitto kutolewa Bungeni pia .Lakini makubwa bado yamelala chini ya RDC na walicho kifanya kwa uharaka ni kumwambia Lowasa ondoka kufa wewe mmoja tubakie madarakani .Leo issue RDC bungeni inaanza kupangia chenga , bado BoT ambayo inaweza kuona Rais anaomba kujiondoa .Naamini BoT hawatataka ifike Bungeni kwa kweli .Nasema Polisi take over upelelezi ufanywe na ripoti iwe wazi isije ikawa kama mambo ya ujambazi na madawa ya kulevya hadi sasa hayujui nini kinaendelea .

Kosa la Lowasa na wenzake ni kosa la kuhujumu Uchumi wa Nchi .Kujiondoa pekee hakutoshi bali Mahakama ijue na iamue swala hili .

Kazaura tupe nafasi tumalize moja hili kwanza then tutakuja kukuchambua na kukueleza ni wapi umeibia Tanzania vya kutosha.

Mkuu Lunyungu,Unachosema ni sahihi kabisa ila siku zote mimi nasema tatizo kubwa lipo kwetu sisi watanzania.Yaana hata kama baada ya hiyo ripoti El na wenzake wasingejiuzuru wala kuchukuliwa hatua na Bunge,Watanzania tungekuwa kimya bila kuchukua hauta yeyote.Mambo mengine Watanzania tuna haki na wajibu wa kuyalazimisha yafanywe kwa kuishinikiza serikali kwa maandamano na migomo.
Wabunge na hasa Watanzania hatuna budi kuelewa kuwa kilichofanyika sasa ni kufyeka majani ya juu tu ,shina na mizizi bado ipo palepale.Ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa mizizi hii inang'olewa.
 
Jamani naombeni msaada wenu, naomba kama kuna mtu anaviambatanisho vya ripoti ya Dr. Mwakyembe. Ripoti nimeshaisoma na kuimaliza sasa nataka kujiridhisha na hivo viambatanisho. Hivo viambatanisho ndio kuna kila kitu na ushaidi wa kuelezea mambo....! tafadhali aliyenavyo namuomba viweke online....!
 
Ni Wakati Muafaka Wa Rais Kulisikiliza Bunge Na Sio Bunge Kumsikiliza Rais!wananchi Tuko Upande Wa Bunge..serikali Yote Ivunjwe!
 
Hata wakijitetea kama serikali iko makini na inataka kujua ukweli utajulikana siku moja:
--------------------------------------------------

Rostam: Siwajui Richmond

na Mwandishi Wetu

MFANYABIASHARA na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), amesema hana uhusiano wowote, na wala haijui Kampuni ya Richmond Development Company LLC ambayo ilishinda zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura baada ya kuingia mkataba wenye utata na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
Kauli hiyo ya kwanza kutolewa hadharani nje ya Bunge na Rostam, mmoja wa wafanyabiashara na rafiki mkubwa wa Rais Jakaya Kikwete, na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, inakuja siku kadhaa sasa tangu jina lake lihusishwe kwa kiwango kikubwa na kampuni hiyo hewa, ambayo utata kuhusu kuwapo kwake na namna ilivyoshinda zabuni katikati ya mwaka 2006, vilibainishwa na Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe.

Rostam aliyepata kuwa Mweka Hazina wa CCM Taifa hadi mwaka ujana, alitoa kauli ya kuikana Richmond jana, wakati alipofanya mahojiano ya simu na Tanzania Daima, alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa kinachosababisha jina lake lihusishwe na kampuni hiyo ya kitapeli na ile ya Dowans ambayo ilirithi mkataba wa Richmond.

Alisema, haijui kabisa kampuni hiyo, hawajui wamiliki wake na wala hajapata kuwasiliana nayo. Mbali ya hilo, Rostam ambaye nyota yake ilianza kuingia doa tangu alipotajwa kuwa kwenye orodha ya mafisadi (The List of Shame) iliyotangazwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, aliieleza Tanzania Daima kwamba, iwapo kampuni hiyo ingelikuwa ni yake, basi isingekuwa rahisi kushindwa kuileta mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura kama ilivyotokea kwa Richmond.

“Siijui hata kidogo, siwatambui na siwafahamu. Mimi ni mfanyabiashara, sina sababu ya kuficha, kama ingekuwa ni kampuni yangu, nisingeshindwa kutekeleza mradi huo. Leo hii kutokana na kuwepo kwa mawasiliano ya kutosha, si rahisi mmiliki wa kampuni hiyo asijulikane. Mimi sidhani kama imekuwa ni ngumu kiasi hicho,” alisema Rostam.

Wakati akikana kuifahamu Richmond na wamiliki wake, Rostam, alikiri kuwahi kutaka kufanya kazi na Kampuni ya Dowans Holdings S.A ambako Kampuni ya Richmond ililazimika kuhamishia mkataba wake huko, baada ya kushindwa kuutekeleza kwa muda uliowekwa.

“Mimi ni mkandarasi. Nina kampuni inaitwa Caspian. Sina uhusiano na Dowans ingawa niliomba kupatiwa kazi ya ukandarasi,” alisema Rostam.

Matamshi haya ya Rostam yanatokana na shaka iliyojitokeza baada ya Kamati Teule ya Bunge kueleza katika ripoti yake kwamba, iligundua kuwa Dowans iliwahi kutumia anwani ya barua pepe ya Kampuni ya Caspian Construction Ltd inayomilikiwa na mfanyabiashara na mwanasiasa huyo.

Akifafanua kuhusu hilo, Rostam alisema alilazimika kuacha anuani yake kwa Dowans baada ya kuomba kazi kwa kampuni hiyo.

“Nilipoomba kazi kama mkandarasi, nilitakiwa kuacha anuani, unapoomba kazi lazima uache anuani,” alisema kwa ufupi.

Akizungumza kuhusu kauli ya Kamati Teule ya Bunge kuwa alikwepa wito wa kwenda kuhojiwa juu ya anwani ya kampuni yake kutumiwa na Dowans, na pia baadhi ya wafanyakazi wa kampuni yake kusemekana kuwa wafanyakazi wa Dowans pia, alisema barua hiyo ya wito ilichelewa kumfikia.

“Barua ya kuitwa kwenye kamati inaonekana iliandikwa Desemba 24, 2007 ikieleza kuwa niende kuwaona Desemba 27,2007, lakini hata hivyo barua niliipata tarehe 2 Januari, 2008 baada ya kamati kumaliza kazi yake. Kipindi hicho cha mwezi Desemba, mimi nilikuwa nje ya nchi nikiwa likizo na familia yangu,” alisema Rostam.

Alipoulizwa kuhusu ushahidi uliotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salvatory Rweyemamu kuwa yeye ndiye aliyemuunganisha na Mkurugenzi wa Richmond, Mohammed Gire kufanya kazi ya ushauri wa habari katika kampuni hiyo, Rostam alikana kwa kusema kuwa, alichowahi kufanya ni kumuunganisha kufanya kazi kama hiyo kwa kampuni ya uwakala wa kupakua mizigo bandarini.

“Si kweli. Mimi sikumuunganisha na watu wa Richmond, isipokuwa nilimuunganisha na Kampuni ya Freight Forwarders inayomilikiwa na Hassan Dala ya kupakua mizigo bandarini, walikuwa wanatafuta PR company (kampuni inayojihusisha na masuala ya mahusiano ya umma) na hiyo kampuni ya uwakala wa mizigo ndiyo ninayotumia mimi katika shughuli zangu,” alisema Rostam.

Aidha akizungumzia uamuzi wa Bunge wa kutaka athibitishe au afute kauli yake kuwa, Kamati Teule ilifanya kazi yake nje ya muda iliyopewa, alisema hilo atalizungumzia bungeni, ambako atatoa ufafanuzi wa kauli yake hiyo.

Katika majumuisho ya mjadala wa ripoti yake, Kamati Teule ililiomba Bunge limtake Rostam kufuta au kuthibitisha kauli yake kwamba ilifanya kazi nje ya muda iliyopangiwa.

Hata hivyo, Rostam hakuweza kufuta au kuthibitisha kauli yake hiyo kwa sababu hakuwepo bungeni kwa kipindi kirefu baada tu ya kamati kutangaza ripoti yake.

Kuhusu Kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd ambayo ilitajwa katika orodha ya kampuni zilizohusika kuchota fedha za akaunti ya madeni ya nje (EPA) ambayo jina lake linatajwa kuhusishwa nayo, Rostam ambaye jana alikuwa akitoa majibu mafupi kwa kila swali aliloulizwa, alikana pia na kusema kuwa haijui kabisa kampuni hiyo.

Kampuni ya Kagoda inadaiwa kuchotewa kiasi cha zaidi ya sh bilioni 40 kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wiki nne tu baada ya kusajiliwa. Na yapo madai zaidi kwamba, sehemu ya fedha hizo zilitumika katika kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 zilizomuingiza madarakani Rais Jakaya Kikwete, jambo ambalo hata hivyo lilipata kukanushwa na Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba.

Katika kuonyesha kuwa tuhuma zinazoelekezwa kwake hazijamyumbisha kisiasa, Rostam alisema kutajwa kwa jina lake katika kashfa ya Richmond na ile ya BoT hakujamshushia hadhi kama mbunge wa Igunga, kwa sababu bado wapigakura wake wanampenda na kumuunga mkono.

“Kashfa hizi hazijanishushia hadhi, wananchi wa Igunga wananiunga mkono. Hizo ni chuki za kisiasa, hata Mwakyembe alipotoa ripoti yake, hakusema kama Kampuni ya Richmond ni ya kwangu,” alisisitiza Rostam kisha akakata simu.
 
HAPA KALE KAMCHEZO KA KUMUINGIZA JK KATIKA KASHFA KANAANZA POLE POLE.

HAPA ANASEMA HAWAJUI WAMILIKI WA RICHMOND wakati ndiye aliyeshiriki mchakato wote wa kuhakikisha Richmond inachukuliwa na Dowans, angalao mpaka hapo hakupaswa kukanusha.

Wakati akikana kuifahamu Richmond na wamiliki wake, Rostam, alikiri kuwahi kutaka kufanya kazi na Kampuni ya Dowans Holdings S.A ambako Kampuni ya Richmond ililazimika kuhamishia mkataba wake huko, baada ya kushindwa kuutekeleza kwa muda uliowekwa.

“Mimi ni mkandarasi. Nina kampuni inaitwa Caspian. Sina uhusiano na Dowans ingawa niliomba kupatiwa kazi ya ukandarasi,” alisema Rostam.

Anasema aliomba kazi kama ambavyo kampuni yake inafanya kazi Buzwagi

Matamshi haya ya Rostam yanatokana na shaka iliyojitokeza baada ya Kamati Teule ya Bunge kueleza katika ripoti yake kwamba, iligundua kuwa Dowans iliwahi kutumia anwani ya barua pepe ya Kampuni ya Caspian Construction Ltd inayomilikiwa na mfanyabiashara na mwanasiasa huyo.

Akifafanua kuhusu hilo, Rostam alisema alilazimika kuacha anuani yake kwa Dowans baada ya kuomba kazi kwa kampuni hiyo.

“Nilipoomba kazi kama mkandarasi, nilitakiwa kuacha anuani, unapoomba kazi lazima uache anuani,” alisema kwa ufupi.

HIKI NI KICHEKESHO, Kinachozungumzwa hapa si Dowans kuwa na anuani ya Rostam, bali Dowans kutumia anuani ya kampuni ya Rostam ya Caspian, ikiwamo ya E-mail na sanduku la Posta, lakini pia hata mtu aliyekua akisaini cheki za Dowans ni Mtumishi wa Caspian na zaidi ya yote, Rostam ndiye aliyekua anasimamia malipo ya Dowans kwa watu waliokua wakiidai Richmond na gazeti la Mwanahalisi liliwahi kuandika kuhusu hilo na kuweka hundi hizo ukurasa wa kwanza, waandishi angalieni kitabu chekundu cha vielelezo vya kamati. Kwa TAARIFA ni kwamba Rostam aliwatisha watu walikua wakifuatilia madeni ya Richmond kwa kuwaambia "we hujui sisi ndio tunashikilia nchi?" kabla ya jamaa kutishia kwenda mahakamani na ndipo Rostam akalipa deni, sasa alikua akiwalipa kama nani?

Akizungumza kuhusu kauli ya Kamati Teule ya Bunge kuwa alikwepa wito wa kwenda kuhojiwa juu ya anwani ya kampuni yake kutumiwa na Dowans, na pia baadhi ya wafanyakazi wa kampuni yake kusemekana kuwa wafanyakazi wa Dowans pia, alisema barua hiyo ya wito ilichelewa kumfikia.

“Barua ya kuitwa kwenye kamati inaonekana iliandikwa Desemba 24, 2007 ikieleza kuwa niende kuwaona Desemba 27,2007, lakini hata hivyo barua niliipata tarehe 2 Januari, 2008 baada ya kamati kumaliza kazi yake. Kipindi hicho cha mwezi Desemba, mimi nilikuwa nje ya nchi nikiwa likizo na familia yangu,” alisema Rostam.

Alipoulizwa kuhusu ushahidi uliotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salvatory Rweyemamu kuwa yeye ndiye aliyemuunganisha na Mkurugenzi wa Richmond, Mohammed Gire kufanya kazi ya ushauri wa habari katika kampuni hiyo, Rostam alikana kwa kusema kuwa, alichowahi kufanya ni kumuunganisha kufanya kazi kama hiyo kwa kampuni ya uwakala wa kupakua mizigo bandarini.

“Si kweli. Mimi sikumuunganisha na watu wa Richmond, isipokuwa nilimuunganisha na Kampuni ya Freight Forwarders inayomilikiwa na Hassan Dala ya kupakua mizigo bandarini, walikuwa wanatafuta PR company (kampuni inayojihusisha na masuala ya mahusiano ya umma) na hiyo kampuni ya uwakala wa mizigo ndiyo ninayotumia mimi katika shughuli zangu,” alisema Rostam.

HAPA ANAMKANA SALVA WA IKULU MCHANA KWEUPEEEEEEEE!!! Salva anawajua sana hawa jamaa kwa kuruka mambo lakini anavumilia tu

Aidha akizungumzia uamuzi wa Bunge wa kutaka athibitishe au afute kauli yake kuwa, Kamati Teule ilifanya kazi yake nje ya muda iliyopewa, alisema hilo atalizungumzia bungeni, ambako atatoa ufafanuzi wa kauli yake hiyo.

Katika majumuisho ya mjadala wa ripoti yake, Kamati Teule ililiomba Bunge limtake Rostam kufuta au kuthibitisha kauli yake kwamba ilifanya kazi nje ya muda iliyopangiwa.

Hata hivyo, Rostam hakuweza kufuta au kuthibitisha kauli yake hiyo kwa sababu hakuwepo bungeni kwa kipindi kirefu baada tu ya kamati kutangaza ripoti yake.

Kuhusu Kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd ambayo ilitajwa katika orodha ya kampuni zilizohusika kuchota fedha za akaunti ya madeni ya nje (EPA) ambayo jina lake linatajwa kuhusishwa nayo, Rostam ambaye jana alikuwa akitoa majibu mafupi kwa kila swali aliloulizwa, alikana pia na kusema kuwa haijui kabisa kampuni hiyo.

Kampuni ya Kagoda inadaiwa kuchotewa kiasi cha zaidi ya sh bilioni 40 kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wiki nne tu baada ya kusajiliwa. Na yapo madai zaidi kwamba, sehemu ya fedha hizo zilitumika katika kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 zilizomuingiza madarakani Rais Jakaya Kikwete, jambo ambalo hata hivyo lilipata kukanushwa na Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba.

Katika kuonyesha kuwa tuhuma zinazoelekezwa kwake hazijamyumbisha kisiasa, Rostam alisema kutajwa kwa jina lake katika kashfa ya Richmond na ile ya BoT hakujamshushia hadhi kama mbunge wa Igunga, kwa sababu bado wapigakura wake wanampenda na kumuunga mkono.

“Kashfa hizi hazijanishushia hadhi, wananchi wa Igunga wananiunga mkono. Hizo ni chuki za kisiasa, hata Mwakyembe alipotoa ripoti yake, hakusema kama Kampuni ya Richmond ni ya kwangu,” alisisitiza Rostam kisha akakata simu.

HII YA KUKATA SIMU NI DANGANYA TOTO, TANZANIA DAIMA NAO WAMEINGILIWA? HUYU MWANDISHI KAMA HAJAKUTANA NA ROSTAM WALIZUNGUMZA NA KUMALIZA KILA KITU NA KUELEKEZANA NAMNA YA KUANDIKA BILA SHAKA KWA MAKUBALIANO MAALUMU CHINI YA MPANGO KAMAMBE WA "AGENDA 21"... JAMANI ROSTAM HAWEZI KUKATA SIMU BAADA YA KUZUNGUMZA MANENO YOTE HAYA NA BILA KUFUATILIA HADI KUJUA KILICHOANDIKWA KABLA YA STORI KUCHAPISHWA GAZETINI. HUU NDIO UKWELI NA TANZANIA DAIMA AMA HATA CHADEMA NAO WAMEINGILIWA!!!!?
 
Mkuu Halisi, hii inatisha!! Lakini kama ni kuingiliwa ni huyohuyo mwandishi, not otherwise!
 
Quote: Halisi

Mheshimiwa, najua sentesi ya mwisho ni kali lakini ni muhimu kusemwa kwa !!!??? Yaani kushangaa na kuuliza, maana kwa siasa za sasa za Tanzania lolote linawezekana. Hebu kumbuka ni Chadema kupitia Vijana wake, John Mnyika walitoa statement kumtaka Lowassa ajiuzulu kuhusiana na Richmond, lakini leo baadhi ya viongozi wanasema Lowassa kaonewa!!!! INAINGIA AKILINI KWELI!!! Au anapanga kuhamia Chadema?

CHADEMA pins down Lowassa on Richmond deal

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

THE opposition party Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) has formally castigated what it describes as the Prevention of Corruption Bureau (PCB)'s poor handling of the Richmond power deal investigation, going so far as to allege Prime Minister Edward Lowassa's personal involvement in the matter.

In a strongly-worded letter addressed to PCB, CHADEMA questions why a task force appointed by the PM had picked Richmond Development Company as the eventual winner of the power generation contract in complete disregard of the Tanzania Electric Supply Company (TANESCO)'s stated rejection of the US-based company.

The opposition party criticized PCB over its decision to rule out corruption in the whole deal, insisting that the government�s anti-corruption watchdog comes clean on the matter.

The CHADEMA letter is in reaction to a declaration by PCB director general Edward Hosea that ''there is no evidence to support the allegations of corruption, criminal negligence or payment of secret commissions to government officials in the Richmond deal.''

The opposition party demands a more detailed explanation from PCB over the statement, which it asserts has not only discredited the anti-corruption watchdog, but also frustrated the campaign against graft.

''PCB should remain with its noble duty of preventing corruption, rather than turning into an institute of protecting, defending and clearing suspects of corruption charges,'' says the letter signed by CHADEMA's acting secretary general John Mnyika.

It queries the rationale behind the decision to award the multi-billion shilling power deal to the 'incompetent' Richmond, ignoring TANESCO's proposal for competitive international tendering.

The party faults Hosea's claim that the Richmond deal occasioned no loss to the government, noting that: ''Tanzanians went without emergency power for many months�and the president has since admitted that the power blackout lowered the country�s economic growth.''

According to local economic analysts, last year's extended nationwide blackout - caused principally by prolonged drought - was the cause of fast-rising inflation and depreciation of the local currency.

The CHADEMA letter called on PCB to make a copy of the full investigative report over the Richmond deal available for public perusal.

It furthermore pressed the anti-corruption watchdog chief to clarify on reports quoting him as saying investigations over corruption charges against members of the parliamentary rights, ethics and privileges committee ceased after the Speaker of the National Assembly closed debate over the issue.

''To call off an investigation on corruption allegations simply because one leader has declared the debate over the issue closed� it only goes to show how vulnerable to outside influence the bureau is,'' Mnyika said in the letter also copied to the president, the speaker and the media.

The letter insisted that any infringement of PCB's independence and autonomy was not healthy for effective anti-corruption campaigning. It noted that PCB did not stop investigating the Richmond deal ''when the prime minister told Tanzanians to stop discussing the company because the rains have come and power was being supplied.''

CHADEMA also dug into PCB for its paid-up advertisements in local media early this year, in which it dismissed as unfounded claims by CHADEMA national chairman Freeman Mbowe to the effect that President Kikwete was in possession of a list of corrupt leaders.

''Unfortunately, just a few weeks after these adverts, the president himself publicly stated that he indeed had such a list. PCB has not tried to refute that statement, or admitted that it previously erred in its denunciation,'' the letter noted.

It said PCB's stance meant that nothing substantive was likely to be done against those named in the list.

''Corruption is a criminal offence�to give corruption suspects too much leeway or decide not to investigate cases of corruption, is tantamount to protecting the criminals.Which in itself is also against the law,'' the letter charged.

http://www.thisday.co.tz/News/1991.html THISDAY Monday May 21, 2007
 
Mheshimiwa, najua sentesi ya mwisho ni kali lakini ni muhimu kusemwa kwa !!!??? Yaani kushangaa na kuuliza, maana kwa siasa za sasa za Tanzania lolote linawezekana. Hebu kumbuka ni Chadema kupitia Vijana wake, John Mnyika walitoa statement kumtaka Lowassa ajiuzulu kuhusiana na Richmond, lakini leo baadhi ya viongozi wanasema Lowassa kaonewa!!!! INAINGIA AKILINI KWELI!!! Au anapanga kuhamia Chadema?

Hii ya CHADEMA kumtetea Lowasa imenipita, ndio naisikia hapa. Sitatoa comments kwa sasa hadi nipate more info
 
Hii ya CHADEMA kumtetea Lowasa imenipita, ndio naisikia hapa. Sitatoa comments kwa sasa hadi nipate more info

Halisi

CHADEMA kama taasisi, msimamo wetu kuhusu suala la Lowassa uko very consistent. Usichanganywe na utofauti kidogo wa kimtizamo kwamba aidha alipewa kupewa nafasi ya kusikilizwa na kamati au kamati ilifanya sawa tu kutokumpa nafasi- lakini hakuna kiongozi anayetetea ufisadi wa Lowassa. Wengine tunataka Lowassa akamatwe sasa rejea:
http://www.chadema.net/habari/2008/habari5.php

Kwa kweli bado tunasafari ndefu!

JJ
 
Richmond/Dowans yajizolea bilioni 75/-

2008-03-05 08:49:24
Na Restuta James

Jumla ya Sh. bilioni 75.2 zimelipwa na serikali kwa kampuni ya Richmond/ Dowans kama malipo ya kuweka mitambo nchini (capacity charge), kati Desemba, 2006 na sasa.

Kadhalika, kampuni hiyo imelipwa dola milioni 2.4 za Marekani (karibu sawa na Sh. bilioni 2.5) kama fedha za kununua gesi inayoendesha mitambo hiyo.

Hayo yalielezwa jana jijini Dar es Salaam na Ofisa Mkuu wa masuala ya Fedha wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), Bw. Jamhuri Ngelime wakati wa mahojiano maalum na Nipashe ofisini kwake.

Alisema malipo hayo yanafanywa kwa ushirikiano wa Tanesco na serikali.

Alifafanua kuwa, shirika lake linalipia gharama za gesi inayofua umeme unaozalishwa na Dowans wakati serikali inalipia gharama za capacity charge.

Bw. Ngelime alisema jumla ya malipo yote kwa kampuni hiyo hadi sasa, ni dola milioni 63.9 za Kimarekani (karibu sawa na Sh. bilioni 77.7).

``Tunalipia vitu viwili, capacity charge na gesi inayofua umeme ambayo inatoka Songosongo,`` alifafanua na kuongeza ``tunaendelea kulipa maana tuna mkataba na kampuni hii na hiyo capacity charge inalipwa kila siku na kama haitafanyika hivyo Dowans wanakuwa wamechelewesha invoice,`` alisema.

Aliongeza kuwa, malipo ya awali yalifanyika Desemba, 2006 ambapo kampuni ya Richmond ililipwa dola 200,000 za Kimarekani na baadaye malipo yalihamishwa kwa Dowans baada ya kuhamishia mkataba.

Aidha, mwaka 2006, serikali iliingia mkataba na kampuni ya Richmond kwa malengo ya kuzalisha umeme wa dharura kipindi nchi ilipokumbwa na uhaba wa maji kwenye mabwawa yanayozalisha nishati hiyo.

Kampuni hiyo ilishindwa kutekeleza mkataba huo ambapo baadaye ilihamishia kwa kampuni ya Dowans.

Hata hivyo, mkataba huo ni moja kati ya mikataba tata inayoelezwa kulitia hasara taifa.

SOURCE: Nipashe
 
Je, Hosea wa TAKUKURU kuwajibishwa? Je, Kamapuni ya Richmond itatakiwa kurudisha pesa ilizolipwa $172 million bila kufanya kazi yoyote?

Posted Date::3/19/2008
Hatima ya watuhumiwa wa Richmond wiki ijayo
*Timu yakamilisha kazi kabla ya mwezi
*Pinda aisifia, asema imefanya kazi nzuri

Na Waandishi Wetu
Mwananchi

TIMU ndogo ya wataalam kutoka idara mbalimbali za serikali, iliyopewa jukumu la kupitia upya mapendekezo ya Kamati ya Bunge iliyochunguza mchakato wa zabuni ya mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura ulioipa ushindi Kampuni ya Richmond, imemaliza kazi yake na inatarajia kuwasilisha ripoti yake wiki ijayo.

Timu hiyo iliyopewa miezi mitatu kukamilisha kazi hiyo imeweka historia kwa kuweza kukamilisha kazi yake kabla ya muda iliyopewa.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema jana kuwa ripoti ya timu hiyo itawasilishwa ofisini kwake Machi 26 siku ambayo ni Jumatano ya wiki ijayo.

Pinda aliyekuwa akifungua semina ya sheria ya Umeme nchini kwa wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana, alisema timu hiyo imefanya kazi yake vizuri sana.

"Napenda kuwajulisha waheshimiwa wabunge kwamba, kamati hii imefanya kazi yake vizuri sana. Taarifa ya Kamati inatarajiwa kuwasilishwa ofisini kwangu ifikapo tarehe 26 Machi 2008," alisema Waziri Mkuu Pinda.

Pinda alisema baada ya kuipokea ripoti hiyo ataifanyia kazi na hatimaye kuiwasilisha kwa Rais Jakaya Kikwete kwa hatua na maelekezo yake.

"Ninaahidi kwamba baada ya kuipokea ripoti hiyo ya wataalamu, tutaifanyia kazi na hatimaye kuiwasilisha kwa Rais Kikwete kwa hatua na maelekezo yake," alisisitiza Pinda na kuongeza kuwa ni matumaini yake kwamba kazi hiyo itakamilika mapema kama alivyoahidi.

Hata hivyo Waziri Mkuu Pinda aliwaambia wabunge hao kuwa wataarifiwa juu ya hatua zinazochukuliwa mara zoezi la utekelezaji wa mapendekezo hayo utakapokamilika.

Aliwataka wabunge hao kuwa na subira kwa kuwa watapata majibu yanayostahili katika ripoti hiyo ili kutatua tatizo hilo.

Ripoti ya tume hiyo inafuatia taarifa ya Kamati Teule ya Bunge, iliyochunguza mchakato wa Zabuni ya Kampuni ya Richmond ya Houston, Texas Marekani ambapo Wabunge hao walijadili taarifa hiyo na kutoa jumla ya mapendekezo 23 ambayo serikali iliahidi kuyafanyia kazi.

Waziri Mkuu aliunda timu ndogo ya wataalamu Februari 15 mwaka huu kutoka idara mbalimbali za serikali kupitia upya mapendekezo ya Kamati hiyo ya Bunge, kama hatua ya kwanza ya kutekeleza mapendekezo hayo.

Pinda alisema hayo alipokuwa akifunga Mkutano wa Kumi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa, serikali ilipokea mapendekezo hayo na kwamba ingejitahidi kuyafanyia kazi ili iweze kuyatekeleza ndani ya miezi mitatu kama ilivyopendekezwa na kamati hiyo.

Alisema timu hiyo inayohusisha wawakilishi kutoka Ikulu, sekretarieti ya mawaziri,Tume ya Maadili, TAMISEMI, Wakala wa Manunuzi (PPRA), Makandarasi, Utumishi wa Umma na Mipango, itapitia mapendekezo hayo na kutoa dira ya namna ya kuyatekeleza.

Katika hotuba yake wakati wa kufunga kikao hicho cha Bunge, Waziri Mkuu alikiri uzembe katika uwajibikaji kwenye serikali na kusema kuwa ripoti ya Richmond imeipa serikali changamoto mpya katika utendaji wake wa kazi.

Alisema chini ya uongozi wake, atahakikisha kuwa Baraza jipya la Mawaziri linafanya kazi kwa umakini, bidii, ushirikiano na uwajibikaji kwa maslahi ya umma, ili kupunguza malalamiko ya wananchi dhidi ya serikali yao.

Alisema historia inaonyesha kuwa kuundwa kwa Kamati za Bunge kunatokana na uzembe katika utendaji wa serikali na kama serikali haitaki kuundiwa kamati, haina budi kufanya kazi kwa uzalendo.

Kauli ya Pinda ilitoka baada ya hotuba ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Dk Harrison Mwakyembe kutoa mapendekezo ya kamati yake juu ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa na serikali baada ya uchunguzi huo.

Alitaja baadhi ya mapendekezo hayo kuwa Msajili wa Ofisi ya BRELA kuifuta Kampuni ya Richmond na wamiliki wake wote kufunguliwa kesi ya jinai, kisha serikali kuangalia uwezekano wa kusitisha malipo kwa Kampuni ya Dowans.

Alisema serikali pia ilitakiwa kuendesha uchunguzi wa kina kubaini taarifa tete kuwa, taarifa ya Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kuhusu Richmond ilichezewa na kuitafuta taarifa halisi ya taasisi hiyo.

Mapendekezo mengine ni serikali kujiepusha na utaratibu wa matumizi ya mawakala katika manunuzi ya Umma, Sheria ya manunuzi (PPRA) ipewe meno zaidi na ifanye kazi kwa kujitegemea bila kusimamiwa na Wizara ya Fedha.

Kamati hiyo pia ilipendekeza serikali kupitia upya mikataba yote na kuweka kumbukumbu ya mikataba hiyo katika ofisi za bunge, timu ya serikali inayoshauri mikataba (GNT) iwajibishwe, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali,wawajibishwe.

Imeandaliwa na Tausi Mbowe na Glory Kimath
 
Mwakyembe denounces 'defenders' of Richmond

By Rodgers Luhwago
THE CITIZEN

The chairman of the parliamentary select committee on the Richmond scandal yesterday denounced attempts by some MPs to undermine its recommendations and challenged Parliament to nullify the report.

Dr Harrison Mwakyembe took the tough stance in the National Assembly in Dodoma, incensed by the apparent criticism of the report on the floor of the august House.

The Kyela MP said that some of his colleagues had been trying to defend individuals implicated in the scam, in which the Government lost $172 million (Sh223.7 billion) in a suspect emergency energy generating contract, claiming that Parliament did not do justice to them.

Speaking emotionally, Dr Mwakyembe said that to clear the matter before the public, Parliament may have to annul Sections 53 and 54 of the Parliamentary Standing Orders that bar MPs from going back to issues already decided by the House so that the report can be discussed afresh.

''Honourable chairperson, there are some MPs who have been technically criticising the decisions reached by this august House after the committee tabled the report and even trying to cleanse individuals involved in the matter,'' Dr Mwakyembe told an attentive National Assembly.

Said he: ''Tanzanians are not fools. If we think justice was not done, let's annul those sections in the Standing Orders so that MPs can again deliberate on the report.''

On February 6, the select committee stunned the National Assembly as well as the entire nation when it implicated former Prime Minister Edward Lowassa in the controversial $172 million (Sh223.7 billion) Richmond Development Corporation contract.

Mr Lowassa became the first Prime Minister to be implicated by a parliamentary committee in any fraudulent deal since independence 47 years ago.

Other big shots who were forced to resign from their posts over the multi-billion shilling scandal that rocked the Kikwete Government were the then East African Affairs minister, Dr Ibrahim Msabaha, and Mr Nazir Karamagi, who held the Energy and Minerals portfolio.

Dr Msabaha was the minister for Energy and Minerals when the controversial deal was sealed in early 2006.

He was later transferred to the ministry of East African Affairs, paving the way for Mr Karamagi to head the portfolio.

The Mwakyembe committee also concluded that the Government was ''conned'' by Richmond through what it described as forged documents showing it had the backing of a leading US company, Pratt & Whitney.

Yesterday, contributing to the 2008/2009 the Prime Minister's office (PMO) budget speech, Dr Mwakyembe said it was ''amazing'' to see that some MPs from the same Parliament that passed the Richmond resolutions, have taken a new stance, defending those implicated in the report.

Dr Mwakyembe, who was recently admitted to Tumaini Hospital in Dar es Salaam, after he was taken ill in Parliament, said if it would be proved that the committee did not do justice, then all its members would resign from their parliamentary seats.

''We cannot be speaking about Richmond every day in this House and in the Press.

We are grown-ups If it will be proved that we didn't do justice to the affected individuals when we presented the report to Parliament, we as members of the committee will resign from our parliamentary seats,'' Dr Mwakyembe said.

The other committee members were Special Seats MP (CCM Nominated) Stella Manyanya, Nzega MP Lucas Selelii, Muheza MP (CCM) Herbert Mntangi and Mkanyageni MP (CUF) Mohammed Habib Mnyaa.

Dr Mwakyembe also challenged individuals implicated in the scandal to resign from the parliamentary seats if it will be confirmed that the committee did not err in its decision.

''Some of us here have been trying to cleanse people affected by the decisions reached by Parliament,'' he said.

If the matter was sent back to the House for fresh deliberations, he said, the ''MPs who did not get an opportunity to say what they are saying now will get the chance to speak what they have in mind now with regard to the report and the decisions reached.

''If this matter comes back into this House for fresh deliberations, we as members of the committee, will also get the chance to say what we didn't say last time just to protect integrity of the Government,'' he told the House.

The chairperson of the session, Ms Jenister Mhagama (CCM- Peramiho), and the other MPs followed his contribution attentively.

There have been reports that some individuals implicated in the Richmond scandal are now waging war against members of the select committee and Speaker Samwel Sitta on what is described as a plan of revenge for their political downfall.

Before contributing to the budget debate, Dr Mwakyembe allayed the public fear over the status of his health, saying that he was fine.

He also thanked those who prayed for his quick recovery.
 
Mwakyembe anguruma

na Mwandishi Wetu, Dodoma
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza utata katika mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura kati ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na Kampuni ya Richmond, Dk. Harrison Mwakyembe ameeleza kushtushwa kwake na uamuzi wa baadhi ya wabunge, wa kuwasafisha baadhi ya watu waliotajwa katika ripoti yao.

Mwakyembe ambaye ni Mbunge wa Kyela kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) alieleza masikitiko yake hayo bungeni mjini hapa, jana wakati akichangia mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu iliyosomwa bungeni mwishoni mwa wiki.

Akizungumza katika hali ya utulivu na kujiamini, Mwakyembe alieleza kushangazwa na hatua ya baadhi ya wabunge hao kuvunja kinyemela kanuni ya 54 na 55 ya Bunge, inayozuia jambo ambalo lilikwishaamuliwa bungeni kuendelea kujadiliwa.

Kutokana na hali hiyo, Dk. Mwakyembe ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alimtaka Spika wa Bunge, Samuel Sitta aruhusu kuvunjwa kwa kanuni hizo ili kutoa fursa kwa wabunge kulijadili kwa kina sakata zima la Richmond ambalo Februari mwaka huu, lilisababisha kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri wengine wawili.

Waliojiuzulu wakati huo sambamba na Lowassa kutokana na majina yao kutajwa katika ripoti hiyo, ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha ambaye wakati mkataba wa Richmond ukisainiwa mwaka 2006, alikuwa Waziri wa Nishati na Madini.

Akizungumza kwa mara ya kwanza toka arejee bungeni mapema wiki hii baada ya kuwa nje kwa muda kutokana na kuugua ghafla na baadaye kuzushiwa kifo, Dk. Mwakyembe alisema anakerwa na jinsi baadhi ya wabunge wanavyolizungumzia suala hilo.

Alisema yameibuka makundi ya wabunge, ambao wanalizungumza suala hilo chini chini, huku baadhi yao wakitoa michango inayojaribu kukosoa maamuzi ya Bunge yaliyotokana na ripoti ambayo kamati yake iliiwasilisha bungeni.

Dk. Mwakyembe alisema pia kuwa, wapo baadhi ya wabunge ambao wamekuwa wakijaribu kuwasafisha watu waliotajwa kuhusika na ukiukwaji wa masuala kadhaa ndani ya ripoti hiyo.

Ingawa hakutaja jina la mbunge, ni wazi kwamba, Mwakyembe alikuwa akiwalenga wabunge wa aina ya Mbunge wa Buchosa, Samuel Chitalilo (CCM) ambaye juzi alimtetea Lowassa akisema kujiuzulu kwake kulifanyika kisiasa.

Kutokana na hilo, Mwakyembe aliwaonya wabunge wanaofanya hivyo, kwani wanalidharau Bunge ambalo ndilo lililopitisha maamuzi hayo.

Alisema wanaodhani kuwa maamuzi hayo bado ni dhamana ya waliokuwa wajumbe wa kamati teule aliyoiongoza, wanafanya makosa makubwa.

"Bado wapo wanaodhani kuwa yale ni maamuzi ya Dk. Mwakyembe, Selelii (Lucas), Injinia Stella Manyanya na Mnyaa. Yale ni maamuzi ya Bunge, tunaokosoa maamuzi ya Bunge tunajidhalilisha wenyewe," alisema Dk. Mwakyembe huku akipigiwa makofi na baadhi ya wabunge.

Mbali ya hilo, alikwenda mbali zaidi na kuhoji sababu zinazowafanya wabunge hao kuanza sasa kufanya kazi ya kuwasafisha baadhi ya watuhumiwa.

"Mnamsafisha nani? Nchi hii si ya mabwege, watu wanaelewa," alisema mbunge huyo ambaye ni mwanasheria na mwandishi wa habari kitaaluma.

Katika hatua nyingine, Mwakyembe alimlaumu pia Spika akisema kiti chake ndicho kinachoruhusu kuendelea kwa mjadala huo wa Richmond kinyemela bungeni kinyume cha kanuni.

Alisema yeye na wajumbe wenzake wa iliyokuwa kamati teule, wako tayari kuona Spika akivunja kanuni hiyo ya Bunge na kulirejesha upya suala hilo la Richmond lijadiliwe kwa mapana na marefu ili kutoa fursa ya kujua ni nani anasema kweli.

"Kama wana mambo ambayo hawakuyasema waseme yote, waseme wanayoyajua na sisi tupo tayari kueleza hata yale ambayo tuliacha kuyaeleza kwa kulinda heshima ya serikali.

"Tumechoka na maneno ya pembeni na ya kwenye magazeti… tuje tuseme hapa, na iwapo tutaonekana tulimuonea mtu, sisi tupo tayari kujiuzulu ubunge wa Jamhuri ya Muungano, lakini tukithibitisha tuliyoyaeleza na wao wawe tayari kujitoa na kuachia nyadhifa zote walizonazo katika taasisi za umma," alisema Dk. Mwakyembe.

Alisisitiza kuwa Bunge lina heshima yake na wanaoanzisha mjadala huo kinyemela wanavunja kanuni na kulidhalilisha Bunge, na wao wenyewe pia.

Akichangia mjadala wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mbunge wa Sikonge, Juma Nkumba (CCM) naye aliibua hisia za baadhi ya wabunge pale alipokanusha taarifa mbalimbali kuwa wabunge wa CCM wamegawanyika.

Alisema umoja wa wabunge wa CCM ulioonekana wakati wa kupiga kura za kupitisha bajeti ya serikali kwa mwaka 2008/09, sasa haupo tena.

Hata hivyo, wakati baadhi ya wabunge wa chama hicho wakiwa na msimamo wa kutojadili masuala yanayohusu ufisadi, Nkumba alisema kuwa ni lazima wabunge wa CCM nao wajadili na kulikemea suala la ufisadi.

Jambo hilo lilimfanya Chacha Wangwe (Tarime-CHADEMA) kusimama na kutaka mwongozo wa Spika akisema kuwa kauli iliyotolewa na mbunge huyo si ya kweli, kwani wakati wenzake wakikataza kuujadili ufisadi, yeye anaujadili.

Hata hivyo, aliyekuwa akiongoza kikao kwa wakati huo, Mwenyekiti Jenista Mhagama, alimtaka Wangwe akae chini kwani alikuwa anapoteza muda bila kusema jambo la msingi.
 
Nimesoma makala ya mwandishi mmoja nikakutana na hili kwa kweli Mwakyembe kama ni kukosea hapa ulikosea sana. Inakuwaje anasema kuwa 'walificha baadhi ya mambo kulinda 'heshima' ya serikali?'. Naomba nieleweshwe kidogo hapa. Ni heshima gani hii serikali inayo kama siyo ujinga. Angesema wanaficha baadhi ya mambo 'kulinda usalama wa taifa' hapo angeeleweka japo kidogo.

Ni bora mheshimiwa huyu ambaye siku za karibuni amejizolea sifa kemkem kama shujaa wetu yeye na kamati yake kufafanua hii kauli tete.

Hivyo basi hatutashangaa hata pale mmoja wa 'majeruhi' mmoja wa kisiasa kudai kulikuwa na uwezo wa 'kuchomekea' baadhi ya mambo ili kuhalalisha makosa ya baadhi ya waheshimiwa waliotuhumiwa na kamati hiyo?

Mheshimiwa kwa niaba ya wakereketwa wengi tunakuomba utoe ufafanuzi wa ziada kuhusu kauli yako.
 
umetoa conclusion kwenye heading yako na sasa maswali ni ya nini? kama ulitaka majibu ya maswali yako basi heading yako nayo ingekuwa ya swali na sio conclusive remark kuwa Mwakyembe hakufai wewe unayedhani kuwa ni msemaji wa watanzania.
 
I was just airing out my opinion on what I thought he was very much mistaken.
 
No matter the case, I will cut Dr. Mwakyembe some slack for that!!
 
Back
Top Bottom