Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Mwishimiwa Mwakyembe kwa hakika ni shujaa!!!!!!!

Ila kache-nsha kwa ile statement yake!! Kwamba kuna mengine alifunika kwa manufaa ya nani??? Nadhani kazi ile ya kizalendo aliifanya kwa manufaa ya Taifa na kwa hilo hakuna kilicho muhimu zaidi yake!!!

KAMA KATELEZA SI AOMBE MSAMAHA TU!! KWANI MWADHANI MASHUJAA HAWAJUI NENO "KUNRADHI"
 
Kama kuna vitu ambavyo hukuviweka hadharani kwa sababu za "kulinda heshima ya serikali" "usalama wa taifa" na maanjumati mengine kama hayo, basi hata kusema "kuna vitu sikuviweka hadharani" kunakuwa na effect ile ile ya ku undermine heshima ya serikali na usalama wa taifa. kwa mfano sasa hivi watu wanajadili hatua ya Mkwakyembe kuficha vitu hivi in the same breath with wizi wa hela za serikali BOT ulivyofanyika "kwa usalama wa taifa".Tunaona kuna pattern ya kutumia vitu kama usalama wa taifa na heshima ya serikali kutetea ufisadi, kwa nini tukupe free pass Mwakyembe?

Kama kuna vitu hujaviweka hadharani usiviongelee kabisa, ama sivyo utafungua the proverbial can of worms na watu wakifanya kichuguu kuwa mlima Kilimanjaro huwezi kuwalaumu.

Ni sawa sawa na kumwambia mtu "najua siri yako lakini sikwambii kwa kulinda heshima" automatically human nature itamfanya mtu afikirie unajua the worst about him, au hata kuinvent vitu ambavyo havipo.

That whole statement was unfortunately distracting and should not have been made.
 
Hizo ni siasa za huko majuu, Mwakyembe ametoa ripoti swali mmefanya nini zaidi tu ya kuanza kumlaumu?

Wewe kama mwananchi so far umefanya nini?
 
I thought this was JF, where we set new standards...

Mimi kama mwananchi na set new standards, kwamba hata hawa mashujaa wetu hawako above reproach.

Wakina Zitto wanakuja na kunufaika na maoni tofauti ya watu wa JF, pamoja na yale yanayotaka wafanye zaidi au wafanye vitu tofauti. Sioni ubaya wa ku point out vitu visivyofanywa sawa na Dr. Mwakyembe, anaweza kunufaika na yeye pia kutokana na contribution yetu.
 
Mwishimiwa Mwakyembe kwa hakika ni shujaa!!!!!!!

Ila kache-nsha kwa ile statement yake!!

"We Chiligati nini?"

Hivyo vitu viwili ulivyovisema hapo, kwa washabiki wengi wa maendeleo na wapinga ufisadi, haviingii akilini kuvisema pamoja. Utaambiwa wewe Makamba unatumia user name ya Bokassa.

Haingii akilini kabisa kwa wengi kusema shujaa kakosea.

Ni kama Yesu vile, huwezi kumkosoa kama umekulia kanisani. Lakini ambacho hatuambiwi, ni kwamba hata Yesu nae kuna siku aliharibu alipomwambia Mungu, Mungu niepushe na kikombe hiki, siku ile walipokuwa wanaelekea Calvary kumfanyia. Yesu hapo hapo akajishtukia kakurupuka, akarekebisha, "ikiwa ni mapenzi yako." That same morning, Yesu alikuwa ametoka kumwambia Pilato kwamba nguvu zote za kunitesa tumekupa sisi, yani yeye Yesu na Mungu. Lakini wakati anaenda kugongelewa misumari, Yesu mwenyewe akataka kuchomoa. Aliogopa. Alichemka. Akarekebisha.

Sembuse Mwakyembe?
 
Kuna dalili ya watu kuwa very harsh on people. Kwamba mtu akisema kitu basi asikosee au asiseme asichomaanisha na hatuko tayari kumpa nafasi ya kusahihisha, kuifafanua, au kuifuta. Standard hiyo ya wanasiasa wasiokosea kwenye matamshi au maelezo ni standard ambayo ni ngumu kufuatilia.

Wanasiasa husema vitu ambavyo wakati mwingine wasingepaswa kusema kwa sababu hawakufikiria jinsi watu watapokea. Lakini katika ulimwengu usio na makosa na ambako watu hawanjing'ati ndimi basi watu hawafanyi makosa.

Ninapokaa chini na kusoma ripoti ya Kamati Teule na details zilizomo kiasi cha kuweza kuiangusha serikali, najikuta siyo tu nampa benefit of the doubt Mwakyembe lakini pia najaribu kumuelewa. Kwa mara ya kwanza Taifa letu lilishuhudia Waziri Mkuu (mtu wa tatu katika mnyororo wa urithi wa Urais) akiachia ngazi kwa kashfa. Yote yametokea kwa kile kidogo alichokisema. Na tena hakusema kama alivyotaka kusema kumbuka hakuitisha hata Lowassa ajiuzulu yeye alisema "waziri mkuu apime uzito" wa hoja za Kamati na achukue hatua anazoona zinafaa, Lowassa akaamua kujiuzulu.

Je kuna vitu vilifichwa au havikusemwa vyote kwa ajili ya kulinda serikali au Rais n.k siwezi kushangaa; anayefikiria kuwa ile ripoti ilisema kila kitu hajui au hafahamu mambo haya ya siasa yanavyofanya kazi. Ile ripoti licha ya kuwa ni ya kiutaalamu ndani yake kulikuwa na siasa kwani waliokuwemo ni wanasiasa.

Kamati ingesema yote iliyotaka kusema? yes! Je ingekuwa ni hekima kusema yote iliyotaka kusema, I doubt it. Kumbuka ilikuwa wiki moja kabla ya Rais Bush kuja Tanzania, na mambo mengine kadha wa kadha.

Ninachoona mimi katika hili ni jambo moja muhimu sana, nalo ni ile tunu ya hekima. Kwa vile unaweza haina maana fanya! Hekima ni uwezo wa kupima matokeo ya vitu au maamuzi, hekima ni uwezo wa kuona athari ya vitendo na maneno utakayosema. Kwa maoni yangu Mwakyembe amewathibitishia wakosoaji wake kuwa licha ya utaalamu na ujasiri alionao ambao wengi tuliiona pale Bungeni, amejaa hekima pia.

Ni kwa sababu hiyo basi tangu alipowabeep kwa hili la "kulinda serikali" sasa hivi wanaoogopa kuzungumzia suala la Richmond Bungeni tena bali pembeni.

Kwa vile mimi sitegemei viongozi kutoka mbinguni, I still have my confidence kwa Dr. Mwakyembe. Of course, kuna mipaka ambayo sitovuka lakini huu wa sentensi moja, tuje tumhukumu mtu na maisha ya mtu na juhudi zake zote, na kumtupa mbali kwa vile kasema kitu ambacho kimetukwaza, ni kiburi cha kujiona ni wenye haki sana kuliko mtu yeyote.

Dr. Mwakyembe keep up the good work, and next time... measure your words, kuna watu wanasubiri mkono udondoke!
 
Kevo,
umeshindwa kusoma alama za nyakati kabla hujaweka mtundiko wako hapo juu. Hapa hakuna kulala mpaka kieleweke, kama mafisadi walidhani wanaweza kucapitalize kwa statement hiyo ya "kulinda heshima ya selikali" wameliwa, kwani hapa tunakata issue nzima na sio vipande vipande ili kudivert from the main issue.
 
"We Chiligati nini?"

Hivyo vitu viwili ulivyovisema hapo, kwa washabiki wengi wa maendeleo na wapinga ufisadi, haviingii akilini kuvisema pamoja. Utaambiwa wewe Makamba unatumia user name ya Bokassa.

Haingii akilini kabisa kwa wengi kusema shujaa kakosea.

Ni kama Yesu vile, huwezi kumkosoa kama umekulia kanisani. Lakini ambacho hatuambiwi, ni kwamba hata Yesu nae kuna siku aliharibu alipomwambia Mungu, Mungu niepushe na kikombe hiki, siku ile walipokuwa wanaelekea Calvary kumfanyia. Yesu hapo hapo akajishtukia kakurupuka, akarekebisha, "ikiwa ni mapenzi yako." That same morning, Yesu alikuwa ametoka kumwambia Pilato kwamba nguvu zote za kunitesa tumekupa sisi, yani yeye Yesu na Mungu. Lakini wakati anaenda kugongelewa misumari, Yesu mwenyewe akataka kuchomoa. Aliogopa. Alichemka. Akarekebisha.

Sembuse Mwakyembe?

Halafu hii ngoma council of Nicea walikuwa hawajaishtukia, wangeishtukia Constantine angeifutilia mbali kama countless other similarly controversial verses.
 
Kwa kifupi ni kwamba kuna watu wetu wa uwt waliohusika na hii ishu kwa nia njema na mbaya, lakini bado huwezi kuziweka habari hizo zote hadharani kwa sababu wengine wahusika bado ni active wa uwt, sasa hizi ndio tunaita siasa za kiutu-uzima,

Mbunge na Shujaaa Mwakyembe, amefanya the best he could kulingana na mazingara ya kiserikali na kisiasa tuliyonayo Tanzania, kumbukeni wakuu kuwa siasa za bongo sio za huko majuu, naona mara nyingi tunachanganya sana hili,

Mwakyembe bado ni shujaa wangu na wa taifa langu, asiyekubali uwanja uko wazi na wewe ni kuingia tuone vitu vyako, nafikri Mwakyembe anayo haki ya kuwauliza wabongo kama muanzisha topic kuwa je toka atoe hii ripoti iliyowapeleeka mwaziri wawili na waziri mkuu kujiuzulu, wewe kama mwananchi umefanya nini hasa kama nyongeza ya pale alipoishia?

Mkuu ni haki yako kuuliza, kama ilivyo haki yetu not only kukuuliza ila ni pamoja kukuelimisha zaidi, kwani sio siri kuwa uwezo wako wa kufikiri na kuelewa unapoishia ni level ndogo sana kwa hii JF.

Ahsante Mkuu!

Mkuu maelezo ni mazuri sana!
Ni kama ile hotuba yako ya kumkaribisha Slaa...Kwa kweli ilikuwa ni kama hotuba kwa niaba ya wana jf wote.
Hivyo basi...Mimi ninakuunga mkono kwa hayo uliyoyasema hapo juu,ila kwa mashart kwamba...Ni LAZIMA ccm MTANDAO IFE...Na pia ni LAZIMA ashirikiane na wazalendo wengine wapambanaji kama kina SLAA,ZITTO NA WENGINEO.
Ni hayo tu MKUU kwa sasa.
Ahsante.
 
"We Chiligati nini?"

Hivyo vitu viwili ulivyovisema hapo, kwa washabiki wengi wa maendeleo na wapinga ufisadi, haviingii akilini kuvisema pamoja. Utaambiwa wewe Makamba unatumia user name ya Bokassa.

Haingii akilini kabisa kwa wengi kusema shujaa kakosea.

Ni kama Yesu vile, huwezi kumkosoa kama umekulia kanisani. Lakini ambacho hatuambiwi, ni kwamba hata Yesu nae kuna siku aliharibu alipomwambia Mungu, Mungu niepushe na kikombe hiki, siku ile walipokuwa wanaelekea Calvary kumfanyia. Yesu hapo hapo akajishtukia kakurupuka, akarekebisha, "ikiwa ni mapenzi yako." That same morning, Yesu alikuwa ametoka kumwambia Pilato kwamba nguvu zote za kunitesa tumekupa sisi, yani yeye Yesu na Mungu. Lakini wakati anaenda kugongelewa misumari, Yesu mwenyewe akataka kuchomoa. Aliogopa. Alichemka. Akarekebisha.

Sembuse Mwakyembe?

tatizo ambalo umetolea mfano wa Yesu ni kutokuelewa theolojia ya Ubinadamu na Uungu wa Yesu. Kwa wanatheolojia tatizo ambalo wewe unaliona sisi wengine hatulioni, for it make sense. And no.. Yesu hakumuambia kuwa "nguvu zote za kunitesa tumekupa sisi"... check your Bible again.
 
Mwakyembe ni shujaa wa taifa, ambaye ni bina-adam na kiongozi amefanya mazuri kwa taifa na kushia alipoishia, sasa wananchi wanamapinduzi kazi yao inatakiwa kubeba tochi na kusonga mbele kutokea pale alipoachia,

I can understand, kwamba hapa JF wananchi wanamapinduzi walibeba tochi na kuendeleza pale alipoachia Mwakyembe, sasa wamekwama kwa sababu Mwakyembe hakutoa habari zote, sasa wanataka Mwakyembe awape more info ili wamalizie kazi yao njema kwa taifa, lakini hizi filimbi tuu matendo hakuna?

Off course JF siku zote tuna-set new standard, lakini hatuwi wasadikika in the process, hapa tunaangalia kwa kina mazingara ya kisiasa na record yetu Tanzania ya uwazi na ukweli on a national level katika siasa, na hsa kwenye ku-deal na viongozi wa juu wa ccm, ndio tunampa Mwakyembe ushujaa kwa kuweza kusimama kidete mpaka kukataa mapesa mengi waliyoyakubali kina Serukamba na Chintalilo, na Anna Abdallah, Mwakyembe ameyakataa na kutoa ripoti ambayo pamoja upungufu wake kwa manufaa ya taifa, bado imepelekea kuwaondoa kazini mawaziri wa wawili na waziri mkuu, ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa letu, sasa what else do you want from Mwakyembe?

I mean vijana mfike mahali muwe na shukrani, badala ya kujifanya kujua tu wakati hamjui kitu, kwani Mwakyembe angeamua kuwasafisha wote kwenye Richimonduli kama Hosea tungefanya nini? Mwakyembe amefanya kazi nzuri na kwa uwezo wake wote, asiyetosheak nafikiri inaruhusiwa kubeba tochi, lakini kumlaumu kwa sababu ambazo wa-Tanzania wote tunazijua vizuri tunakuwa ni wananchi tusiokuwa na shukrani!
 
Some spades are big spoons; however sometimes dont dare to talk openly.
 
Kuna dalili ya watu kuwa very harsh on people. Kwamba mtu akisema kitu basi asikosee au asiseme asichomaanisha na hatuko tayari kumpa nafasi ya kusahihisha, kuifafanua, au kuifuta. Standard hiyo ya wanasiasa wasiokosea kwenye matamshi au maelezo ni standard ambayo ni ngumu kufuatilia.

Wanasiasa husema vitu ambavyo wakati mwingine wasingepaswa kusema kwa sababu hawakufikiria jinsi watu watapokea. Lakini katika ulimwengu usio na makosa na ambako watu hawanjing'ati ndimi basi watu hawafanyi makosa.

Ninapokaa chini na kusoma ripoti ya Kamati Teule na details zilizomo kiasi cha kuweza kuiangusha serikali, najikuta siyo tu nampa benefit of the doubt Mwakyembe lakini pia najaribu kumuelewa. Kwa mara ya kwanza Taifa letu lilishuhudia Waziri Mkuu (mtu wa tatu katika mnyororo wa urithi wa Urais) akiachia ngazi kwa kashfa. Yote yametokea kwa kile kidogo alichokisema. Na tena hakusema kama alivyotaka kusema kumbuka hakuitisha hata Lowassa ajiuzulu yeye alisema "waziri mkuu apime uzito" wa hoja za Kamati na achukue hatua anazoona zinafaa, Lowassa akaamua kujiuzulu.

Je kuna vitu vilifichwa au havikusemwa vyote kwa ajili ya kulinda serikali au Rais n.k siwezi kushangaa; anayefikiria kuwa ile ripoti ilisema kila kitu hajui au hafahamu mambo haya ya siasa yanavyofanya kazi. Ile ripoti licha ya kuwa ni ya kiutaalamu ndani yake kulikuwa na siasa kwani waliokuwemo ni wanasiasa.

Kamati ingesema yote iliyotaka kusema? yes! Je ingekuwa ni hekima kusema yote iliyotaka kusema, I doubt it. Kumbuka ilikuwa wiki moja kabla ya Rais Bush kuja Tanzania, na mambo mengine kadha wa kadha.

Ninachoona mimi katika hili ni jambo moja muhimu sana, nalo ni ile tunu ya hekima. Kwa vile unaweza haina maana fanya! Hekima ni uwezo wa kupima matokeo ya vitu au maamuzi, hekima ni uwezo wa kuona athari ya vitendo na maneno utakayosema. Kwa maoni yangu Mwakyembe amewathibitishia wakosoaji wake kuwa licha ya utaalamu na ujasiri alionao ambao wengi tuliiona pale Bungeni, amejaa hekima pia.

Ni kwa sababu hiyo basi tangu alipowabeep kwa hili la "kulinda serikali" sasa hivi wanaoogopa kuzungumzia suala la Richmond Bungeni tena bali pembeni.

Kwa vile mimi sitegemei viongozi kutoka mbinguni, I still have my confidence kwa Dr. Mwakyembe. Of course, kuna mipaka ambayo sitovuka lakini huu wa sentensi moja, tuje tumhukumu mtu na maisha ya mtu na juhudi zake zote, na kumtupa mbali kwa vile kasema kitu ambacho kimetukwaza, ni kiburi cha kujiona ni wenye haki sana kuliko mtu yeyote.

Dr. Mwakyembe keep up the good work, and next time... measure your words, kuna watu wanasubiri mkono udondoke!
 
Demokrasia inapoburuzwa, ukimya si ishara ya amani!
Joseph Mihangwa
 
Hivi kile alichosema Mwakyembe hadi kusababisha kuvunjika kwa serikali, kilikuwa kimelinda heshima ya serikali? Je kwa ripoti yake na kilichomo siyo kwamba amethibitisha kuwa alichoheshimu ni nchi zaidi kuliko serikali kwani kama kweli angetaka kulinda heshima ya serikali hiyo ripoti ingelingana na ile ya TAKUKURU.
 
angesema vyote, saa hizi may be tungekuwa kwenye process ya uchaguzi mwingine, kwa nini hakusema, kuna ufisadi ambao hakuusema ili kulinda taifa labda?!
 
labda angesema yote, hakuna ambaye angeadhibiwa au kuwajibika! na kusingekuwa na uchaguzi wala nini. Unafikiri nani angekuwa tayari kumfunga paka kengele kama watu wenyewe ni design ya kina Chitalilo. I'm glad he said what he said and we got what we got! Kufikiri kwamba angesema yote basi tungepata zaidi ya tulichopata ni kutokupima siasa. Kama daktari, manesi, na raia wote wagonjwa, nani atampeleka nani hospitali!? mnabakia kuuguzana tu.
 
Kwani Bubu kasema nini kuhusu hiyo habari?

Ahsante sana Mkuu kwa kunitetea...🙂. Mimi siyo niliyoiandika hiyo habari, nimeichukua kama ilivyo online, kitu ambacho nimebadilisha ni kutoweka picha ya Mwakyembe tu.
 
Back
Top Bottom