Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Mtu mzima mwenye akili timamu na Mtanzania, anajua wazi kuwa Mkapa ni mwizi na Mwakyembe sio mwizi ila ni shujaaa wa taifa, kwa kuweza kuandika ripoti ambayo imeweza kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa letu kumtoa kazi waziri mkuu na mawazri wawili tena marafiki wa karibu wa rais,

Lakini hawezi kulilia kuwa Mkapa na Mwakyembe ni sawa, that is pathetic!

claiming not to question credibility na honest ya mwakyembe kwa watanzania kwa kuficha baadhi ya siri za ufisadi is TOTALLY EXTRA PATHETIC
 
Mama ahsante.

Labda aseme mwingini. Mimi nikimkosoa huyo mtu huwa kinageuka ki-bifu kama personal personal hivi.

Hebu msaidieni huyo mtu kuelewa jamani.

Ukweli haufichiki, kuwa stereotype ni kitu ambacho kimepelekea ufisadi. Let a spade be called a spade not a big spoon. Here we dare to talk openly! GOD BLESS JF
 
aachwe mwakyembe! asikosolewa! kwa vile ameficha mambo kwa hehima ya serikali!

Mwakyembe aachwe kwa sababu hawezi kuisema serikali, kama Pinda alivyosema juzi kuwa meremeta ni mali ya jeshi, full stop.

Vile vile Mkapa aachwe kwa heshima ya serikali.

Mkuu najua ni lazima umtetee mkapa lakini mkapa ni mwizi period hawezi linganishwa na shujaa Mwakyembe.

Hakuna Tofauti yeyote katika ya Mwakyembe na Balali................wote wameficha mambo kwa heshima ya serikali....

unachoweza kufanya sana ni kubadili majina tu, lakini hoja huwa huna hata siku moja, Balali aliwahi kuandika ripoti ipi hiyo ambayo alisema kuwa hawezi kutoa yote kwa sababu ya heshima kwa serikali?

Mwakyembe unaweza kumfananisha na Balali? You must be kidding me?

kuwataja siri za ufisadi serikalini ni kuivunjia heshima serikali.....anayeficha siri za ufisadi naye ni FISADI. Ufisadi ni ufisadi hakuna ufisadi mkubwa wala mdogo.[/

Fisadi ni mkapa sio Mwakyembe, tunasubiri tu maana naye siku zake zinakaribia kufikia ukingoni, Mwakyembe ni saafi na tunaheshimu sana kazi yake kubwa kwa taifa letu na Mungu ambariki sana.
 
Jamani tumsikilize tena Mwakyembe na context aliyokuwa anazungumza. Kumekuwepo na njama za kutaka "kuwasafisha" wote wale waliohusika katika sakata la Richmond. Wengine wakija juu kuwa tume ya Mwakyembe iliendelea kuongezea mambo katika ripoti hata baada ya ripoti hiyo kuwasilishwa bungeni. Huu ulikuwa ni uwongo. Baada ya ripoti kuwasilishwa bungeni na kujadiliwa, baada ya Lowassa Karamagi na Msabaha kujiuzulu it was a given kuwa huo mjadala umeisha na suala lenyewe limewekewa fullstop. Mnakumbuka Rostam alipotaka kuliibua upya swala hilo mapema mwaka huu na Mr6 akamwekea fullstop? Sasa hawa wabunge (watetea mafisadi) walidhani wamepata mwanya mwingine wa kuliibua swala hilo na Mwakyembe akawaambia kama ni hivyo, basi tubadilishe kanuni za bunge tulilete swala hilo upya na mimi (Mwakyembe) nitarudi kwenye mafaili yangu na mimi nitaleta details ambazo (for editing reasons: my opinion) tuliamua kuziacha nje kwa ajili ya kulinda heshima ya serikali. Simple as that.
Actually nilivyosikia mimi, Rostam mpaka sasa anaamini kuwa kulikuwepo na editions mbili za ripoti ya Mwakyembe. Kilichotokea ( na hii nimetonywa na vyanzo vinavyoaminika) ni kwamba baada ya ile ripoti kumalizika, alipelekewa Spika (lakini bila viambatanisho.) Sasa genge la Rostum wakafanya njama kuingia ofisini kwa spika na kukopi ile ripoti (bila viambatanisho) Lakini siku ya siku Mwakyembe alitoa ripoti kamili bungeni ikiwa na viambatanisho vyote na ndiyo sababu Lowassa alishindwa kujitetea, na ndiyo sababu Rostam anaamini kulikuwa na ripoti mbili. It is as simple as that.
 
claiming not to question credibility na honest ya mwakyembe kwa watanzania kwa kuficha baadhi ya siri is TOTALLY EXTRA PATHETIC

Kwa mwananchi wa Tanzania, kutoelewa alichofanya Mwakyembe kwa kutotoa siri za serikali ndio hasa a pathetic thinking na wala sio spirit ya JF, ni lazima siku zote ujionyeshe kuwa uanjau sana, jana Dr. slaa anajiandikisha unadai kuhusu PHD yake na nonesense kibao, ni lazima siku zote ujionyeshe kuwa unajua sana wakati ukweli unajisema wazi mkuu!
 
Mwakyembe aachwe kwa sababu hawezi kuisema serikali, kama Pinda alivyosema juzi kuwa meremeta ni mali ya jeshi, full stop.

Mkuu najua ni lazima umtetee mkapa lakini mkapa ni mwizi period hawezi linganishwa na shujaa Mwakyembe.

unachoweza kufanya sana ni kubadili majina tu, lakini hoja huwa huna hata siku moja, Balali aliwahi kuandika ripoti ipi hiyo ambayo alisema kuwa hawezi kutoa yote kwa sababu ya heshima kwa serikali?

Mwakyembe unaweza kumfananisha na Balali? You must be kidding me?

Fisadi ni mkapa sio Mwakyembe, tunasubiri tu maana naye siku zake zinakaribia kufikia ukingoni, Mwakyembe ni saafi na tunaheshimu sana kazi yake kubwa kwa taifa letu na Mungu ambariki sana.

hII NI TABIA YAKO MBAYA YA KUWA NA DOUBLE STANDARD; ilikuwa hivi kwa Anne Kilango, ukasema aachwe, kwa Kimaro na Mwakyembe. Mashujaa wa kweli ni Slaa na Zitto, period! Hao wengine hawataachwa hadi watakapoacha kuuma na kupuliza kama panya. Kama wanataka kuwa upande wa wananchi basi wawe 100% kama wanataka upande wa serikali wawe huko 100% shujaa haogopi kitu. Huyo ni shujaa nusu na ninampongeza kwa hilo.
 
Kuna kila sababu ya vyombo vya habari kumhoji Mwakyembe kwamba ni nani aliyempa madaraka ya kuamua nini kiandikwe/kisiandikwe katika ripoti ile.

Alichokifanya hakiwezi kuwa sawa hata siku moja na tunaomkosoa hatufanyi hivyo kwa kutaka kumchafua Mwakyembe au tuko upande wa akina RA, Karamagi, Lowassa na Msabaha.

Mnaosoma hapa mnafahamu kuhusu mchango wangu hapa sijawahi hata siku moja kuwatetea hao jamaa na sitaanza leo, lakini ukweli ni kwamba alichokifanya Mwakyembe siyo sawa. Hatuwezi kuogopa kusema eti kufanya hivyo tunawapa faida wale wanaomchukia Mwakyembe kutokana na kuanguka kwao toka madarakani kulikosababishwa na ripoti ya Mwakyembe na kamati yake.
 
Mkuu kwa hiyo kama US walificha ripoti yao na sisi tuwaige tufiche ripoti yetu? Tangu lini tumeanza kuiga yanayofanywa na US? Kwa kuwa US walifanya basi ni halali na Tanzania wafanye?

Mkuu ni tabia za serikaloi zote duniani kulindwa na sheria kwa mambo yake muhimu ya ndani, Tanzania sio nchi ya kwanza kufanya hivyo, nenda bungeni kuna ripoti yote lakini kuna sehemu zimezibwa kwa wino mweusi, hilo zoezi linafanyika dunia nzima it has nothing to do na Mwakyembe na anything ni sheria tu!
 
Mi Naona Wa Kumshika Shati Ni Kikwete Mwenyewe.
Ye Ndiyo Ajibu Ni Kwanini Ilikuwa Vizuri Kwa Lowassa Kujiuzulu Na Ni Kwanini Ilikuwa Ni Vibaya Kwake Kufanya Hivyo.
Na Hao Wanaotaka Kumsafisha Mtu Yoyote Waache!
Wa Kuulizwa Ni Kikwete Kwani Hapa Muda Unaisha!
Hapa Si Majina...!
Hapa Ni Justice! Haki Kwa Mtanzania Inaamuliwa Kwa Sheria Za Nchi Zilizowekwa!
Kikwete Kesharudi....atoe Maamuzi Ya Ripoti...!
Ripoti Pamoja Na Zile Za Kaguzi Zote Zimwagwe Bungeni Na Hapa!
Nilidhani Ni Wasomi Hapa!
Sasa Watuletee Tu Hayo Maripoti Na Sisi Tutawaambia Wananchi Nani Wa Kukamata!
Otherwise Hapa Ni Kama Serikali Nzima Inataka Kusafishwa!
Kwasababu Hakuna Anayetaja Kikwete Amabaye Ni Mkuu Wa Nchi...wao Wanakuna Pembeni Mwa Kidonda Tuuu!
Mwakyembe Na Sijui Lowassa!
Hapa...tukate Issue!
Taifa Linatuangalia Na Tuzingatie Ule Usemi Maarufu Wa Hapa Jf...where We Dare To Talk Openly...!
Jf Mbele!
 
...It is as simple as that.

No.

Kutunza heshima ya Serikali maana yake nini?

Sasa hivi hujali hiyo heshima? Wewe una integrity kweli au unaenda na upepo wa Kisiasa unavyopuliza?

Kwamba maadui wako wa Kisiasa wakifanya usiyoyapenda unarusha nje hiyo heshima ya Serikali?

Mwakyembe hana integrity ya kuwa Mwenyekiti wa tume. Ameficha ukweli "kwa heshima ya Serikali." Bull...
 
Kwa mwananchi wa Tanzania, kutoelewa alichofanya Mwakyembe kwa kutotoa siri za serikali ndio hasa a pathetic thinking na wala sio spirit ya JF, ni lazima siku zote ujionyeshe kuwa uanjau sana, jana Dr. slaa anajiandikisha unadai kuhusu PHD yake na nonesense kibao, ni lazima siku zote ujionyeshe kuwa unajua sana wakati ukweli unajisema wazi mkuu!

Mimi kuquestion PhD ya Slaa? YOU ARE COMPLETELY PATHETIC! Rudia tena ile thread, hukawii kusema unanijua na utamwaga siri hata za mume wangu. Maana ndio tabia yako ya kutisha watu hapa pale unapoona wanaenda tofauti na unavyotaka wewe, pole sana sio wote wa kuburuzwa na mawazo yako.
 
Hakuna siri za serikali bwana!!!! Serikali iko pale kwa kuwekwa na wananchi na hivyo hawastahili kuficha chochote dhidi ya wale waliowaweka madarakani. Hizo siri za serikali zina kashfa mbali mbali ambazo zinawagusa wakubwa serikalini ndiyo maana zinaitwa siri za serikali, lakini serikali yoyote iliyo safi haistahili kuwa na siri yoyote dhidi ya Wananchi wake.
 
Kuna kila sababu ya vyombo vya habari kumhoji Mwakyembe kwamba ni nani aliyempa madaraka ya kuamua nini kiandikwe/kisiandikwe katika ripoti ile.

Mwakyembe ni Mwanssheria aliyebobea, aliyekuwa anajua wazi uwezo wa kamati yake na anyoweza kuandika yakasemwa wazi na anyoweza kuandika yasisemwe wazi kwa niaba ya serikali, hiyo mkuu ni sheria sio uamuzi wa Mwakyembe, ambaye alikuwa kila analofanya ana-abide na sheria, kama unatka ripoti yote itolewe basi ilazimishe serikali lakini sio kumlaumu Mwakyembe, yeye kama mwenyekiti wa ile kamati alikuwa anajua wazi uwezo wa ile kamati unaponzia na kuishia.
 
Nasema Kama Mnasema Mwakyembe Fisadi...then Nataka Mtu Aseme Nani Si Fisadi Serikalini.
 
Mimi kuquestion PhD ya Slaa? YOU ARE COMPLETELY PATHETIC! Rudia tena ile thread, hukawii kusema unanijua na utamwaga siri hata za mume wangu. Maana ndio tabia yako ya kutisha watu hapa pale unapoona wanaenda tofauti na unavyotaka wewe, pole sana sio wote wa kuburuzwa na mawazo yako.

Kama vile ambavyo hukawii kubadili majina ukishaona umezidiwa, ulipoona kwenye dini kuna mtoto tu uakanza, hata mimi mkuu si unajua kuwa hujawahi kuniburuza ingawa unaburuza wnengi sana hapa, pole sana sio mimi. Ila sihitaji kurudia nani kati yangu na wewe ni pathetic maana ni aibu sana hata kusema! damn!
 
Majina...anza Kuhani Na Mama Na Bubu...weka Majina Ya Wale Ambao Si Mafisadi Huko Serikalini.
 
Hakuna siri za serikali bwana!!!! Serikali iko pale kwa kuwekwa na wananchi na hivyo hawastahili kuficha chochote dhidi ya wale waliowaweka madarakani. Hizo siri za serikali zina kashfa mbali mbali ambazo zinawagusa wakubwa serikalini ndiyo maana zinaitwa siri za serikali, lakini serikali yoyote iliyo safi haistahili kuwa na siri yoyote dhidi ya Wananchi wake.

Mkuu haya maswali ya siri za serikali kuwa uongo au ukweli ni ya Waziri Mkuu, sio ya Mwakyembe.
 
Mimi kuquestion PhD ya Slaa? YOU ARE COMPLETELY PATHETIC1 Rudia tena ile thread, hukawii kusema unanijua na utamwaga siri hata za mume wangu. Maana ndio tabia yako ya kutisha watu hapa pale unapoona wanaenda tofauti na unavyotaka wewe, pole sana sio wote wa kuburuzwa na mawazo yako.

Thank you Mama, thank you!

Jamaa alinambia sijui ananifahamu kutoka kwenye basement DC. Nilicheka mpaka kufa!
 
Mwakyembe ni Mwanssheria aliyebobea, aliyekuwa anajua wazi uwezo wa kamati yake na anyoweza kuandika yakasemwa wazi na anyoweza kuandika yasisemwe wazi kwa niaba ya serikali, hiyo mkuu ni sheria sio uamuzi wa Mwakyembe, ambaye alikuwa kila analofanya ana-abide na sheria, kama unatka ripoti yote itolewe basi ilazimishe serikali lakini sio kumlaumu Mwakyembe, yeye kama mwenyekiti wa ile kamati alikuwa anajua wazi uwezo wa ile kamati unaponzia na kuishia.

Kubobea kwenye uanasheria bado hakumpi haki ya kuamua nini cha kuandikwa/kutoandikwa. Alitakiwa aitoe ripoti kamili na siyo nusu nusu au robo robo. Sheria ipi iliyomruhusu Mwakyembe kuamua kwamba kuna baadhi ya mambo hayastahili kuandikiwa ili 'kulinda heshima ya serikali' vimwage vipengele vyake hapa tuvijadili.

Hakuna sheria yoyote inayolinda ufisadi unaofanywa na mafisadi wachache dhidi ya Watanzania. Baadhi ya Watanzania wanamkosoa hata Mwalimu Nyeyere hadi hii leo(Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi~AMEN) sasa huyu Mwakyembe ni nani yeye hata asikosolewe anapofanya makosa? Amefanya makosa kama hamtaki kuyaona makosa aliyoyafanya hilo ni tatizo lenu, lakini wengine tunaona kuna makosa na inabidi atufafanulie na pia atupe ripoti kamili bila kubakisha chochote. Analinda heshima ya serikali, hii serikali ina heshima gani? mbona heshima yake imeshaanguka siku nyingi zilizopita!!
 
Back
Top Bottom