Mama,
Hivi kweli mnafahamu jinsi report inavyotayarishwa?... Kuna mtu kawambia kuwa hiyo tume ilikuwa kutafuta watu waliohusika na mkataba wa Richmond au?... Kwanza ni vizuri mfahamu utaratibu kabla hamjarukia mambo.. nakuombeni someni tena report ya Mwakyembe mtaona kwamba vitu vingi kaviacha ili korti (Bunge) lipate kujadili..
Swala lilikuwa uhalali wa Mkataba wa Richmond....
Hata report ya Zitto kuhusiana na Buzwagi kuna watu wengi wengine wanahusiaka amabo Zitto anaweza kuwa anawafahamu lakini hawezi kuwataja bila kuwepo na sheria itakayo ruhusu Upelelezi kuhisiana na wahusika...
Mwakyembe ktk mapendekezo yake ni wazi aliweka vitu wazi na ilikuwa ni kazi ya serikali kuamua kusuka ama Kunyoa.
Tazameni report ya wahasibu wa Ernst and Young ilitaja watu waliohojiwa na kuhusika na mahojiano lakini hakuna hata sehemu moja wamewataja watu wote waliohusika kuhujumu.. Sii kazi yao na ndio maana Kikwete akawakabidhi kina Said Mwema..
Sasa imekuwaje serikali ktk swala hili la Richond wamekataa kabisa kulizungumzia tena Bungeni kwa kuweka kanuni chafu halafu hata Kikwete hakuchagua timu maalum ya kuhakikisha fedha zetu zinarudi kama alivyofanya ktk sakata la EPA..
Kwa sababu kule EPA kuna samaki wadogo kina Johnson ambao wamaweza kutumiwa kama chambo cha kufuta madhambi, lakini ktk sakata la Richmond, Buzwagi, IPTL, Rada na kadhalika kuna ma Sangara!..
Hivyo wakuu report ni report ya kile kilichotokea haina maana wahusika ndio kweli wenye deal.. Mimi kama karani naweza kupitisha kitu ambacho nimepewa amri na fulani.. Tulimsikia Msabah akisema yale ya Bangusilo.. tumemsikia Mwakyembe akimtaja Lowassa na Rostam wazi wazi.. mlitaka aseme kipi zaidi ikiwa report yenyewe haitakiwi kuwekwa wazi bungeni ikajadiliwa kama wanavyofanya Marekani kuunda tume maalum inayosikiliza kesi nzima...
Kumbukeni kwa sababu Mwakyembe na watu wake hawakuwa na sheria, watu akam Rostam alikataa kusema chochote na hakuna sheria inayomlazimu lakini kama ni bungeni na wamepewa baraka za rais au Spika, Rostam atakuja kujieleza..