Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

MKJJ: Well, nafikiri mtunzi wa kichwa cha habari ana mambo personal na Mwakyembe au tuseme kwamba alikuwa anajaribu kuvuta hisia za watu ili waisogelee zaidi mada yake. Otherwise, katika maandishi yangu, ambayo ndiyo ulikuwa unayajibu, hakuna mahala ninapoushuku umuhimu na nafasi ya Mwakyembe katika taifa letu ,hasa kwa wakati huu tunapohitaji watu makini na wanaotumia akili katika siasa-dhidi ya ujanjaujanja na ubabaishaji-kwa hakika Mwakyembe ni mojawapo na ni mtu mjinga pekee atakayemdharau Mwakyembe.

Nilichokipinga na ambacho naendelea kukipinga ni jitihada za kujaribu kuonyesha kwamba makosa aliyoyafanya Mwakyembe katika report ni madogo na ya kawaida. Mimi nasema ni makosa makubwa sana na ambayo sio ya kawaida kwa uzito wa kazi ya ile kamati na kwa kuweza kufanywa na mtu mwenye umakini na elimu ya kiwango cha Mwakyembe, ambayo, kama tulivyokwishaona na inaelekea tutaona zaidi huku mbele, yamedhoofisha kwa kiasi cha kutosha ubora wa report yake. Udhaifu wenyewe, kama alivyosema JokaKuu na unaotokana na kauli yake ya juzi, ni kwamba kumbe hakusema kweli yote kwenye report yake-kwa tafsiri nyingine ni kwamba Mwakyembe hakusemi ukweli, tena bungeni, uwiiii!!! Sasa mkuu huwezi kusema tena hili ni kosa la kawaida. Sasa cha kujiuliza alitumia vigezo gani kuchagua aseme ukweli upi na aacha upi na kwa manufaa ya nani?

Unanifurahisha sana unapojaribu kumtenga Lowasa na report ya Mwakyembe. You must be joking kwa sababu sote tunajua kwamba bila report ya Mwakyembe hadi leo Lowasa angekuwa waziri mkuu. Kitu kingine ambacho unakifumbua macho, ama kwa makusudi au kwa sababu zingine-na naamini ni kwa makusudi- ni ukweli kwamba umaarufu wa kamati ya Mwakyembe haukutokana na report yenyewe; umaarufu wa kamati hii na Mwakyembe mwenyewe unatokana na ukweli kwamba report yao hii ilisababisha Waziri Mkuu, tena kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, ajiuzulu. Bila hitimisho ambalo alilitoa Mwakyembe katika report yake, ambalo umelinukuu vizuri sana kwenye post yako, Lowasa asingejiuzulu. Most importantly, Mwakyembe asingefikia hilo hitimisho kama kweli Lowasa hakuwa mlengwa mkuu kwenye hiyo kazi ya kamati. Conclusively then, it's unforgivingly and undeniably wrong for this committee not to have questioned the main character portrayed in the report, namely Lowasa.

Namalizia tena kusema hivi salama ya Mwakyembe kutokana na kauli yake ni ukweli kwamba alijenga good will kwa kuweza kumwachisha kazi Ndugu Lowasa ambaye, in the first place, wananchi walio wengi hawakupenda ashike nafasi aliyopewa na rafiki yake JK. Vinginevyo, na kama kungekuwa na umakini mkubwa wa mijadala bungeni, ingetokea mbunge atake marejesho ya uhakika wa mjadala wa report ya Mwakyembe. In any case, kwa kauli zake hizi, report ya kamati yake haiwezi tena ikawa sehemu ya marejeo muhimu ya kitaaluma. This is to say, if I were to write an intellectual and academic piece
about the Richmond crisis, I would be very cautious in citing Mwakyembe's report as part of my references!
 
... Ndugu Lowasa ambaye, in the first place, wananchi walio wengi hawakupenda ashike nafasi aliyopewa na rafiki yake JK.

ambae wawakilishi wa hawa Wananchi, kwa kusikitisha, walimpitisha Bungeni kwa kura 99.99%
 
Mimi sipingani na nyie mnaodai kumkosoa MWAKYEMBE!
Sasa mumefanya hivyo na huku mkitaja watu mnaofikiri kuwa ni safi...Sasa nimeanzisha thread ya kumjadili kila mtu bila UNAA!
 
Mgaya,

..hakuna uwezekano wa Mwakyembe kuchafuliwa, sana sana atajichafua mwenyewe.

..ni mambo gani hayo ambayo mwanzoni Dr.Mwakyembe aliona asiyasema kwa manufaa ya nchi, lakini sasa baada ya watu kuanza kuhoji ripoti yake anaona hayana manufaa tena na anatishia kuyasema?

Mwanakijiji,

..serikali ni ya wananchi, kwa ajili ya wananchi.

..hilo la kulinda heshima ya serikali haliko mikononi mwa Dr.Mwakyembe.

..alichopaswa kufanya Dr.Mwakyembe ni kusema ukweli wote. wananchi ndiyo tunaopaswa kutamka ndani ya demokrasia yetu kwamba serikali[wananchi] imevunjiwa heshima etc etc.

..i am very tempted kuamini kwamba kuna ufisadi/mafisadi wamefichwa na Mwakyembe. kwa mtizamo wake amefanya hivyo ili kulinda heshima ya serikali. nadhani mtizamo huo ni POTOFU, na haujengi nchi.

I Love JF, Thank you JK....🙂
 
Kitila,'
Hakukuwepo ripoti mbili za tume ya Mwakyembe kama vile akina Rostum na Lowassa wanataka tuamini. Kilichotokea ni kwamba Spika alipelekewa advance copy ( bila vielelezo) ambayo majasusi wa Rostum na Lowassa waliidaka wakidhani ni the real mckoy na kuwapelekea mabosi wao. Siku ya kikao cha Bunge Mwakyembe alikuja na ripoti kamili ikiwa na viambatanishi vyote ( ambavyo havikuwemo katika ripoti waliyopora maejenti wa Rostum ofisini kwa Spika) Kwa hiyo ukisikia kilio cha ripoti mbili ni kilio cha watu waliojiona wajanja kumbe wamechezewa.
 
Mama,
Na ukiona rafiki yako kila siku anakukosoa tu hana hata jema la kusema juu yako huyo pia si rafiki wa kweli. Ana jambo na wewe!

Lakini pia kukosolewa kwa mwakyembe kwenye hili ni la kumfanya akaze nuts zake na ajue kila analofanya or kusema linacount mbele ya wananchi! Kiukweli, elite kama yeye akisoma critics toka kwa elite wenzie anajua jinsi ya kujirekebisha.
 
mama kilichojaribiwa kufanywa mwanzoni (angalia mwanzo wa thread hii) hakikuwa kumkosoa, kilikuwa ni jaribio dhaifu la kumtupa pembeni kwa kuwa "hatufai watanzania". Kuna baadhi ya watu ambao kwa sababu wanazozijua wao wenyewe walipoona hicho kinachodaiwa kusemwa mara moja wakaona kuwa Mwakyembe hawafai.

Pole pole hata hivyo naona tone imekuwa ni ya kumkosoa kitu ambacho sidhani kuna mtu ana tatizo nalo. Lugha iliyokuwa inatumika mwanzoni haikuwa ya rafiki bali adui. Waliojaribu kumtosa angalau kwa wakati huu wameshindwa, na wale wenye kumkosoa wanaendelea na jukumu hilo vizuri.

Kama maoni yako yalikuwa ni katika "spirit" ya kukosoa, tuko pamoja.
 
Pole pole hata hivyo naona tone imekuwa ni ya kumkosoa kitu ambacho sidhani kuna mtu ana tatizo nalo.

Wrong!

Or, wrongly said!

Wapo wengi tuna tatizo na gaffe ya Mwakyembe. Mimi na huyo unaejadiliana nae ni wamoja wao.

Wewe na wengine hamuoni tatizo, na ninaheshimu mawazo yenu kwa taadhima . Lakini waongelee hao. Hao tu.
 
Nafikiri hii ingetumiwa kama constructive critism na wala sio kama heading ya post inavyosuggest.
 
Wrong!

Or, wrongly said!

Wapo wengi tuna tatizo na gaffe ya Mwakyembe. Mimi na huyo unaejadiliana nae ni wamoja wao.

Wewe na wengine hamuoni tatizo, na ninaheshimu mawazo yenu kwa taadhima . Lakini waongelee hao. Hao tu.

You accuse me what you do yourself.. ni wapi nimesema hakuna tatizo? Sijasema hivyo kwani nina akili zangu timamu.. ninaweka vitu kwenye context yake. Halafu umesema "wengi" wewe na huyo ninayejadiliana naye na wamoja wa "kina nani" wao? Na unaposeme mimi na "wengine" ni kina nani hawa ambao hatuoni tatizo?
 
mama kilichojaribiwa kufanywa mwanzoni (angalia mwanzo wa thread hii) hakikuwa kumkosoa, kilikuwa ni jaribio dhaifu la kumtupa pembeni kwa kuwa "hatufai watanzania". Kuna baadhi ya watu ambao kwa sababu wanazozijua wao wenyewe walipoona hicho kinachodaiwa kusemwa mara moja wakaona kuwa Mwakyembe hawafai.

Pole pole hata hivyo naona tone imekuwa ni ya kumkosoa kitu ambacho sidhani kuna mtu ana tatizo nalo. Lugha iliyokuwa inatumika mwanzoni haikuwa ya rafiki bali adui. Waliojaribu kumtosa angalau kwa wakati huu wameshindwa, na wale wenye kumkosoa wanaendelea na jukumu hilo vizuri.

Kama maoni yako yalikuwa ni katika "spirit" ya kukosoa, tuko pamoja.

we dare to talk openly, aaaaight?calling a spade a spade and not a big spoon. Jamaa akikosea hata kama anapendwa kiasi gani akosolewe na sio kufagiliwa. Na anayekosoa asionekane traitor. I love one signature sijui ni ya nani inasema IF WE ARE ALL THINKING ALIKE; THEN SOMEONE IS NOT THINKING.
 
Mama kama vingine vilivyoandikwa humu vinaitwa kukosoa, basi neno kukosoa limepoteza maana yake. Na kama mtu anakuja kwangu na kuniambia ananikosoa kwa jinsi ilivyoandikwa humu nitamuambie aendelee na kujikosoa mwenyewe.
 
wengine wanakuwa provoked na kejeli, na kuamua kubwatuka kucounter attack kejeli. Vijana wanasema ngoma droo, mwenye cheni kauza cheni bandia na mnunuzi katoa pesa bandia.
 
... ni wapi nimesema hakuna tatizo?

Hapa:

... hata hivyo naona tone imekuwa ni ya kumkosoa kitu ambacho sidhani kuna mtu ana tatizo nalo.

Tanzania nzima hatuna tatizo na gaffe ya Mwakyembe?

Unamuongelea nani hapo?

Mimi nina tatizo na gaffe ya Mwakyembe. Yule unaejadiliana nae ana tatizo na gaffe ya Mwakyembe. Na wengine kadha wa kadha umewasikia wana tatizwa na gaffe ya Mwakyembe.

Ningekuwa mimi wewe ningeichomoa hiyo sentensi ya 'sidhani mtu ana tatizo...'
 
Twende kule kwenye forum ya Dini nikakupe somo alikuwa ana maana gani aliposema nguvu na mamlaka ya huo Upilato umepewa na Baba yangu, na alikuwa na maana gani alipo mstopisha mfuasi wake aliyetaka kuanzisha fujo baada ya Yesu kuchapwa kibao, akamtumliza akamwambia hawa nguvu ya kutuchapa sio tatizo, naweza kuamuru majeshi ya Mungu yakaibuka hapa sasa hivi. Mimi sina haya ya ku refer neno kwa neno, najaribu kuelewa the whole concept. Hicho kitu hukuambiwa na Padre Mwanakijiji.

you do not want to go there with me... ask.
 
Hapa:

Tanzania nzima hatuna tatizo na gaffe ya Mwakyembe?

Unamuongelea nani hapo?

Mimi nina tatizo na gaffe ya Mwakyembe. Yule unaejadiliana nae ana tatizo na gaffe ya Mwakyembe. Na wengine kadha wa kadha umewasikia wana tatizwa na gaffe ya Mwakyembe.

Ningekuwa mimi wewe ningeichomoa hiyo sentensi ya 'sidhani mtu ana tatizo...'

tatizo linaloongelewa hapo ni kuwa hakuna tatizo na kukosoa na sio kuwa hakuna tatizo na alichosema Mwakyembe.
 
Hapa:

Tanzania nzima hatuna tatizo na gaffe ya Mwakyembe?

Unamuongelea nani hapo?

Mimi nina tatizo na gaffe ya Mwakyembe. Yule unaejadiliana nae ana tatizo na gaffe ya Mwakyembe. Na wengine kadha wa kadha umewasikia wana tatizwa na gaffe ya Mwakyembe.

Ningekuwa mimi wewe ningeichomoa hiyo sentensi ya 'sidhani mtu ana tatizo...'

Kuhani,
Nilivyomuelewa mimi Mzee Mwanakijiji ni hivi: Hadhani kama kuna mtu yeyote ana tatizo na kitendo cha kumkosoa Dr. Mwakyembe.

Labda kwa kuondoa utata uliojitokeza kwenye sentensi yake, Mzee Mwanakijiji angeweka walau mkato kabla ya maneno hayo uliyoyanukuu.

Nadhani anacholia nacho Mzee Mwanakijiji ni ile sentensi ya "Hatufai Watanzania" ambayo inaashiria kama sio kupendekeza Dr. Mwakyembe atoswe, kitendo ambacho hakuna mtu yeyote humu ndani aliyekiunga mkono maana wote tunatambua na kuheshimu mchango wake kwa taifa ila hatufumbii macho makosa yake.
 
Kitila Mkumbo JF Senior Expert Member Join Date: Sat Feb 2006

Re: Kwa Hili Mwakyembe hutufai Watanzania!

Ili kuweka huu mjadala katika context inabidi kwanza tukumbushane ni kwa nini hasa watanzania tukiwemo sisi hapa JF tulishangilia report ya Mwakyembe na kumuingiza Mwakyembe katika orodha ya mashujaa wa taifa letu. Kwa maoni yangu ni kwamba tulimshangilia sana Mwakyembe na kamati yake kwa kufanya kile ambacho kamati nyingi huko nyuma zilishindwa kukifanya. Kamati nyingi zilizoundwa huko nyuma zilitumika kuwasafisha wakubwa na kufunika ukweli badala ya kuufunua. Kwa hiyo utaona kwamba tulimshangilia Mwakyembe kwa sababu alithubutu kufunua ukweli bila kuwaangalia wakubwa usoni kama ilivyozoeleka katika siasa za Tanzania.

Mkuu Kitila,

Heshima mbele, na hapa tupo ukurasa mmoja mkuu sawa sawa.
 
Back
Top Bottom