Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,355
- 1,956
MKJJ: Well, nafikiri mtunzi wa kichwa cha habari ana mambo personal na Mwakyembe au tuseme kwamba alikuwa anajaribu kuvuta hisia za watu ili waisogelee zaidi mada yake. Otherwise, katika maandishi yangu, ambayo ndiyo ulikuwa unayajibu, hakuna mahala ninapoushuku umuhimu na nafasi ya Mwakyembe katika taifa letu ,hasa kwa wakati huu tunapohitaji watu makini na wanaotumia akili katika siasa-dhidi ya ujanjaujanja na ubabaishaji-kwa hakika Mwakyembe ni mojawapo na ni mtu mjinga pekee atakayemdharau Mwakyembe.
Nilichokipinga na ambacho naendelea kukipinga ni jitihada za kujaribu kuonyesha kwamba makosa aliyoyafanya Mwakyembe katika report ni madogo na ya kawaida. Mimi nasema ni makosa makubwa sana na ambayo sio ya kawaida kwa uzito wa kazi ya ile kamati na kwa kuweza kufanywa na mtu mwenye umakini na elimu ya kiwango cha Mwakyembe, ambayo, kama tulivyokwishaona na inaelekea tutaona zaidi huku mbele, yamedhoofisha kwa kiasi cha kutosha ubora wa report yake. Udhaifu wenyewe, kama alivyosema JokaKuu na unaotokana na kauli yake ya juzi, ni kwamba kumbe hakusema kweli yote kwenye report yake-kwa tafsiri nyingine ni kwamba Mwakyembe hakusemi ukweli, tena bungeni, uwiiii!!! Sasa mkuu huwezi kusema tena hili ni kosa la kawaida. Sasa cha kujiuliza alitumia vigezo gani kuchagua aseme ukweli upi na aacha upi na kwa manufaa ya nani?
Unanifurahisha sana unapojaribu kumtenga Lowasa na report ya Mwakyembe. You must be joking kwa sababu sote tunajua kwamba bila report ya Mwakyembe hadi leo Lowasa angekuwa waziri mkuu. Kitu kingine ambacho unakifumbua macho, ama kwa makusudi au kwa sababu zingine-na naamini ni kwa makusudi- ni ukweli kwamba umaarufu wa kamati ya Mwakyembe haukutokana na report yenyewe; umaarufu wa kamati hii na Mwakyembe mwenyewe unatokana na ukweli kwamba report yao hii ilisababisha Waziri Mkuu, tena kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, ajiuzulu. Bila hitimisho ambalo alilitoa Mwakyembe katika report yake, ambalo umelinukuu vizuri sana kwenye post yako, Lowasa asingejiuzulu. Most importantly, Mwakyembe asingefikia hilo hitimisho kama kweli Lowasa hakuwa mlengwa mkuu kwenye hiyo kazi ya kamati. Conclusively then, it's unforgivingly and undeniably wrong for this committee not to have questioned the main character portrayed in the report, namely Lowasa.
Namalizia tena kusema hivi salama ya Mwakyembe kutokana na kauli yake ni ukweli kwamba alijenga good will kwa kuweza kumwachisha kazi Ndugu Lowasa ambaye, in the first place, wananchi walio wengi hawakupenda ashike nafasi aliyopewa na rafiki yake JK. Vinginevyo, na kama kungekuwa na umakini mkubwa wa mijadala bungeni, ingetokea mbunge atake marejesho ya uhakika wa mjadala wa report ya Mwakyembe. In any case, kwa kauli zake hizi, report ya kamati yake haiwezi tena ikawa sehemu ya marejeo muhimu ya kitaaluma. This is to say, if I were to write an intellectual and academic piece
about the Richmond crisis, I would be very cautious in citing Mwakyembe's report as part of my references!