Wamegongana kimawazo!...Yani mkuu mpaka leo hujamstukia huyu Zitto kuwa ni CCM Lowasa. Na hapo alipo yupo kwenye ngwe ya mwisho ya kumalizia moja kazi zake kuu alizopewa nayo ni KUIVURUGA CHADEMA ishindwe kutoa credible oposition.
Yani umeona wapi mpigania "maslahi ya taifa" ghafla, akaanza kuwa na mawazo yanayofanana word to word na mafisadi papa?....Kwenye mitambo chakavu ya Dowans alikuja na kutaka sheria ipindishwe mpaka inunuliwe, kwenye nafasi ya bunge kwenye kuisimamia serikali maneno yake ni kama amekua kipaza sauti cha kingunge Ngombale Mwiru Fisadi, kwa kutumia janja ya kuipotosha katiba(MKJJ alimuelewesha vizuri kwenye hili as if alikua hajui kumbe ni mkakati wa kupotosha makusudi), Halafu hili la tume huru ya majaji alikuja nalo hapa(nia ni ileile, hao majaji wanunuliwe halafu watumike kuwasafisha watuhumiwa wa Richmond), wenye akili walistuka, leo Rostam kaja na hio hoja word to word kama Zitto.
Mi namshauri kama yeye ni jasiri kama anavyopenda watu wamuone, atoke kwenye kichaka cha kupigania "maslahi ya taifa" na ajitoe muhanga kama Peter Serukamba. Ule ndio ujasiri wa kifisadi. Mheshimiwa mbunge kijana, please spare us with your cheap "napigania maslahi ya taifa" rhetoric and go collect your CCM Lowasa membership card. Si kosa la jinai kujiunga nao, ila usitake kufanya watanzania ni mabwege!