Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na Kagoda je, iundwe tume ya akina nani ili imchunguze Papa Fisadi Rostam Azizi!? Kishapata kiburi sasa anajua Kikwete hawezi akamgusa au kusema lolote baya dhidi ya ya huyu fisadi hivyo kapata nguvu ya kuongea upupu wake. Kigumu chama cha mafisadi! KIGUMU!
.
Hilo ndilo tatizo kubwa la sisi wana jf.utafikiri watu hawajaenda shule.
Nikisema soma gazei la mtanzania alivyosema Sophia simba juu ya Anna Kilango, ndiyo ya ukweli?.Nikisema soma Nipashe aliyovyasema Mwakyembe juu ya Lowasa ni kweli?..
Mh Zito juzi alifafanua hapa kuwa kila mmoja ana mhariri wake.mara wakitoka uko kwenye vikao wanawapigia simu.
Sasa ,Mh Sererii kumchambua RA ndiyo hukumu ya mahakama?Walianza lini kumchambua RA?.Mbona mengi alichambuliwa na mpaka vielelezo kupelekwa pccb?haya ya ukweli?.Usiwe kasuku ndugu yangu.
Ifikike mahali sasa tusema basi.Wao wamezidiana kete humo ndani na kutuletea kelele za kuigiza hapa.
Hivi Mheshimwa Rostam anafikiria yeye ni nani kiasi cha kufika mahali:
a. Kutotambua uamuzi halali wa BungeJibu langu ni jepesi:
b. Kuamua aina gani ya tuhuma dhidi yake zichunguzwe - kwanini asitake kuchunguzwa katika Dowans, Kagoda, Uraia n.k?
c. Kuamua nani amchunguze - Kwanini aamue "majaji" ndio waunde tume hiyo? Itakuwaje na uhuru wakati mtuhumiwa ndiye aliyependekeza watu wa kumchunguza? HIvi tukimuomba baadhi ya majina ya majaji ambao angependa wafanye kazi hiyo kweli atakuwa hana kichwani?
d. Iweje yeye mwenyewe apendekeze aina gani ya adhabu endapo atakutwa na hatia na hazihusishi yeye kuishia lupango isipokuwa kujiuzulu nafasi zake za kiuongozi ndani ya chama.
e. Kwa uspesheli gani alionao hadi atoe wazo la namna hiyo. HIvi tukimkubalia ni mtu gani mwingine ambaye atatii uamuzi wa chombo halali ambaye naye hatataka 'uchunguzi huru' utakaofanywa na watu atakaowapendekeza yeye?
NOT ON OUR WATCH MR. ROSTAM!
Kama hukuridhika na yaliyotokea Bungeni jiuzulu sasa katika kupinga! Kama unaona hukutendewa haki na wabunge wenzako zungumza Bungeni kudai kuwa "ulizuiwa" ni kufanya nchi nzima hatuna akili. Wewe ni mtu mzima, huyo aliyekuzuia wewe Mbunge wa Jamhuri ya Muungano kuzungumza Bungeni ni nani na kwanini usiende mahakamani kumpinga mtu huyo. Ulipoapa kushika nafasi ya Ubunge uliapa kuilinda na kuihifadhi Katija ya JMT na siyo Katiba ya CCM! Sasa kama ulionewa au kuzuiwa kimbilia Katiba ikulinde, vinginevyo;
Majaji wetu tayari wana kesi na mambo muhimu ya kufuatilia kuliko kukaa na kuanza kuangalia "Rostama alihusika vipi". Kama ungependa kuwe na uchunguzi huru kweli, omba waje Scotland Yard wakuchunguze kuanzia mwaka 1980!
Vinginevyo, kaa pembeni au kaa kimya
.Ni vizuri ukaelewa au ukajua kuwa hata hao unaowatuhumu, Sitta, Malecela n.k tushukuru kwani wametuonyesha mwanga wa nchi hii ikoje.
We fikiria kama wote wangekaa kimya wakaacha kila kitu kiende kilivyo bila hata kushtuka mimi au wewe haya yote ungeyajua wapi? Je, anayehumia na huu umaskini ni nani? Unadhani huyo Sitta au Malecela anashida na njaa kama mimi na wewe? Yaani wanyamaze kimya kudhani wao ni kundi la mafisidi! Lakini kwa ajili ya Utaifa wao wamerudi nyuma wameona kuwa Taifa zima linaangamia basi tubadilishe mwelekeo!!
Ni vizuri kuwaunga mkono, kama kuna mengine yatarekebishika na wao itakuja zamu yao, kwani Roma haikujengwa siku moja!!
mkuu achana nae mimi naujua uadilifu wako Personally tangu ukiwa Stakishari, inatosha kuubeba mzigo wako , na wazee wakabeba wao, wewe ni mtu mzima, jiamini simama mwenyewe kama ambavyo siku zote umekua ukisimama, huna haja yakujiingiza kwenye mijadala ya kitoto.
.
Labda wewe K4jolly ndiyo kwanza unayasikia leo hayo.Tulisema na kuandika sana tangu miaka ya 90
Mrema aliyahubiri sana kuhusu serikali ya mwinyi na waziri mkuu wake john malecela .watu walitoroshea nje urithi wa nchi yetu.Mrema alijaribu ata kwenda uwanja wa ndege kwenda kukamata na ni huyohuyo John Malecela na mwinyi walinyamazisha.
Mrema amehamia upinzania na alisema yote maovu ndani ya serikali ya awamu ya pili,lakini ni huyohuyo john malecela akamwita mrema ni kichaa na apelekwe mirembe.Leo hii baada ya kukataliwa marambili kugombea urasi na kuenguliwa umakamu wa rais tanzania bara, naye anajiita kinara wa ufisadi.
Nani mpuuzi atakubali ujinga huu?.Nyerere aliwahi kumwambia Gama, ambaye alikuwa katibu mkuu wa ccm wakatiu huo,kuwa kama watashindwa kuliondoa jina la John Malecela,basi yeye asingeshiriki kwenye mchakato mzima wa mgombea urais ndani ya ccm.Kwann alisema Hivyoo?''we kalia bao''
Vyama vya upinzani vimenza kusema siku nyingi sana kuhusu ufisadi ndani ya ccm.Kama wewe unataka mpaka samwel sitta ndiye aseme ndipo uhamini kuwa kweli kuna ufisadi,pole sana.
Kwa kauli anazotoa huyu jamaa, inaonesha wazi kuwa amesha jizatiti na hakuna mtu wa toka serikali wa kumshooshea kidole. Nadhani kiburi chake kinatokana na kuwafahaamu in and out Viongozi wa juu serikalini pamoja na maovu waliyo tenda na wanayo endelea kuyatenda. Imefikia mahali anaona kuwa yuko juu ya sheria na pasipo yeye basi serikali haiwezi kuwepo.
Kauli zake zinazakikisha serikali na mahakama pia, na sijui kwa nini serikali na mahakama ikubali kuburuzwa na jamaa huyu, labda yeye ndo kawaweka na wakimguza tu basi, na wao watakuwa hatarini
- Mkuu Malecela ni a politician anyejua kwamba siasa ni mchezo wa aina gani, kushindwa na kushinda ni the name of the game kwenye siasa, ndio maana Mboma ameshindwa ubunge lakini bado anasonga mbele, ipi bora kukataliwa na Mwalimu au wananchi kama yalivyomtokea Mboma?
Mrema aliitwa kichaa na CCM as chama tena kiongozi wa kwanza kumpa hilo jina in the public alikuwa Sozigwa, unalilia point ya Mwalimu na Malecela, lakini hutaki kukubali kwamba hakutusaidia kitu Tanzania alipotuletea Mkapa, kama sio Malecela leo Lowassa angeendelea kutusumbua Tanzania, Mwinyi ndiye aliyekwua Rais sio Malecela, Rais wa sasa ni Kikwete sio Pinda ndiye mwenye uamuzi wa mwisho dhahabu za Airport zilikuwa za Sitti Mwinyi na Mwalimu alisema wazi kule Mwanza na Mwinyi hakubisha,
- Malecela hakutorosha kitu chochote inasikitisha kwa mtu kama wewe unajiita Sheikh, mpaka kufungisha ndoa za wananchi wa dini yako, kuja hapa na kusema uongo wa kitoto kama huu, ndio maana huwa tunaziogopa sana hizi dini zingine maana kama wewe kiongozi wa dini na unafahamika na jamii unapokuja kwenye internent na kusema uongo namna hii sasa tutaisemaje hiyo dini ambayo wewe ni kiongozi?
Aibuuuu baba, Bwa! ha! ha!
FMEs![/QUOTE
Andika unachojua na mimi nitaandika ninachojua kuhusu Fisadi John Malecela
Kama unaona Malecela ni msafi,basi endelea kumsifia.
Domo ni jumba la maneno na usema kila jambo baya na zuri
Sasa mimi siwezi kulizua domo lako kusema uongo hapa kwa wana jf.
Ni tabia yako.
hapa, tunajaribu kuuficha ukweli ila sijui kwa manufaa ya nani kwa kuwa jambo lenyewe liko wazi kabisa kwa kuwa kama Mwakyembe ana uhakika kuwa ripoti yake ni ya uhakika kwanini walimzuia RA kutoa maelezo yake bungeni wakatui ule na kwa nini wanaogopa tume huru ili kujua yupi ni mkweli na yupi ni muongo