Ripoti ya uchafuzi mto Mara, ukweli uko wapi?

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Taarifa ya uchafuzi wa mto mara na kufa kwa samaki, je taarifa iliyotolewa imejaa siasa au uhalisia?
Au ni mkakati maalum kama tulivyoanza na machinga (wanachafua jiji) tukaja kwa wamasai ngorongoro wamevamia mbuga,
sasa ni zamu ya wanaoishi kandokando ya mito, na pengine hatmaye ni tz nzima, inachafua dunia, tupelekwe sayari nyingine! 🙌

Kama kinyesi kimewezekana kuchafua mto, iweje taka za mgodini zishindwe?

Screenshot_20220319-164915_1647697956561.jpg

Screenshot_20220319-165031_1647697920024.jpg

Screenshot_20220319-165109_1647697897805.jpg
 
Kuna uhasama Kati ya mgodi na WANANCHI ambao hauwezi kuisha kila siku WANANCHI kuuzunguka mgodi WANAFANYA kila wanachoweza ili kujaribu kuvamis na KUPORA madini imelazimika kuweka ulinzi mkubwa Kwa ghalama kubwa.Wazee wa mazingira wamekuwa wakipishana ili kuhakiki hali ya usalama na namna MAJI taka yanavyo tibiwa.

Migodi binafsi inaendelea na Kazi bila TAHADHALI yoyote na hakuna kinachofanyika.

Kuhusu uchafuzi wa MTO taasisi za uchunguzi zinapaswa kuaminika.
 
Mkuu hakuna anayebishia uchunguzi.
Isipokuwa unahitajika ufafanuzi zaidi, kwamba kinyesi cha mifugo kina uwezekano mkubwa wa kuchafua mto kuliko taka za mgodi? Je,kabla ya hapo hali ilikuwaje? Kwamba kinyesi cha wanyama kinaweza kusababisha samaki kufa ndani ya mto? Na maji kubadili rangi?🤔
 
Ni ngumu kuelewa inahitaji dozi ya mwaka MZIMA wabobevu wa mambo wanasema taka za mgodi zimezibitiwa kikamilifu na wamewakaribisha WATAALAMU mbalimbali kujionea kuhusu kinyesi cha ng'ombe sina uhakika ingawa kinyesi huwa kinatumika hata kuzalisha gas ya kupikia NK.
nilichosikia mto umepitia kwenye bonde oevu maeneo kama hayo yanatabia zake kitaalamu je, umewahi kuyaona magugu MAJI ? Je,umewahi kuona Chini yake Kuna nini?
 
Kwahio wananchi wameongeza kwenda Haja kwa ghafla ?

Yaani kipindi hicho quantity ilizidi ghafla, na sasa hivi wameacha ndio maana tatizo haliendelei ?
 
Ni ngumu kuelewa inahitaji dozi ya mwaka MZIMA wabobevu wa mambo wanasema taka za mgodi zimezibitiwa kikamilifu na wamewakaribisha WATAALAMU mbalimbali kujionea kuhusu kinyesi cha ng'ombe sina uhakika ingawa kinyesi huwa kinatumika hata kuzalisha gas ya kupikia NK.
nilichosikia mto umepitia kwenye bonde oevu maeneo kama hayo yanatabia zake kitaalamu je, umewahi kuyaona magugu MAJI ? Je,umewahi kuona Chini yake Kuna nini?
sina uhakika kama umesoma hii taarifa kwa umakini? Ndio maana nikauliza kuna ukweli au ni siasa?
Wamewezaje kupima lita za mkojo ndani ya maji na kubaini kiwango walichotaja?

•~Kinyesi cha mifugo chatajwa kuwa chanzo cha kufa samaki mto Mara*
SATURDAY MARCH 19 2022

Summary
Kamati maalum ya kitaifa iliyoundwa na serikali kuchunguza mabadiliko ya maji ndani ya mto Mara, imetoa taarifa ya chanzo cha mabadiliko katika mto huo yaliyosababisha maji kuwa meusi na kutoa harufu, huku samaki wakifa ambapo chanzo kimeelezwa kuwa ni shughuli za binadamu pamoja na nguvu za asili.

Musoma: Kamati maalum ya kitaifa iliyoundwa na serikali kuchunguza mabadiliko ya maji ndani ya mto Mara, imetoa taarifa ya chanzo cha mabadiliko katika mto huo yaliyosababisha maji kuwa meusi na kutoa harufu, huku samaki wakifa ambapo chanzo kimeelezwa kuwa ni shughuli za binadamu pamoja na nguvu za asili.

Akitoa matokeo ya uchunguzi leo Jumamosi Machi 19, 2022 mjini Musoma, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Samuel Manyele amesema kuwa hali hiyo imetokana na kuwepo kwa kiwango kikubwa cha kinyesi cha mifugo mtoni pamoja na uozo wa mimea ndani ya mto hasa mimea vamizi kama vile magugu maji na matete.

Amesema kuwa hali hiyo ilisababisha kupungua kwa kiasi kikubwa kiwango cha oksijeni ndani ya mto na hivyo maji kubadilika rangi na kuwa na harufu mbaya huku samaki wakikosa chakula na hivyo kusababisha vifo vyao.

Hata hivyo, amekanusha picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilizokuwa zikionyesha samaki wakiwa wamekufa kwa wingi, akisema sio kutoka mkoani Mara.

Amesema kuwa kwa mujibu wa uchunguzi waliofanyana walibaini kuwa mabadiliko hayo ni matokeo ya mvua kubwa iliyonyesha ghafla kwa muda mfupi katika kipindi cha mwezi huu hivyo kutibua uchafu uliokuwa umejikusanya chini ya mto kwa muda mrefu.

"Mvua zingeendelea kunyesha hali hii ingeisha kwani uchafu ungetiririshwa lakini kwa vile mvua zimenyesha na kukatika ghafla ina maana uchafu ule unatoka taratibu na hii hali inaweza kudumu kwa zaidi ya miezi mitatu hadi minne endapo mvua hazitanyesha hapa katikakati," amesema.

Profesa Manyele amesema kuwa mto huo umeathiriwa kuanzia katika kijiji cha Marasibora wilayani Rorya na kijiji cha Wegero wilayani Butiama huku akisema kuwa mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara hauhusiki na uchafuzi huo.

"Mgodi upo mbali sana na maeneo yaliyoathirika na hata kama uchafu unaozalishwa mgodini pale ungezidishwa mara ishirini na kumwagwa mtoni maji yasingebadilika rangi wala kuwa katika hali iivyo sasa na maji ya mto kelekea kule mgodini ni masafi na hayana shida yoyote," amesema.

Amesema kuwa wamebaini uwepo wa kinyesi cha ng'ombe zaidi ya tani 1.8 milioni pamoja na mkojo wa ng'ombe lita 1.5 bilioni uchafu uliotokana na kuwepo kwa ng'ombe zaidi ya laki 3 waliokuwepo katika eneo oevu la mto Mara kwa kipindi cha miezi minane mwaka jana wakati wa kiangazi.

"Ng'ombe mmoja ana toa kilo 25 za kinyesi kwa siku moja na mkojo lita 21 kwa siku kwahiyo ukizidisha kwa idadi hiyo ya ng'ombe mara miezi minane utapata kiwango hicho na hapo bado hatujaweka kinyesi na mkojo wa kondoo, mbuzi na punda," amesema.

Waziri atoa siku saba kwa timu kuchunguza mabadiliko mto Mara

Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Suleiman Jafo ametoa muda wa siku mbili kwa kamati hiyo kuandaa taarifa kamili yenye mpango kazi juu ya nini kifanyike na muhusika ni nani kisha taarifa hiyo ikabidhiwe kwake kwaajili ya utekelezaji.

"Hii taarifa imenipa faraja baada ya uchunguzi kubaini kuwa hakuna kemikali mtoni maana kama kungekuwa na kemikali hii ingekuwa ni habari mbaya sana lakini taarifa hii inaonyesha kuwa tuna kazi kubwa sana ya kufanya ili mto uweze kuendelea kuwepo na tusipochukua hatua za haraka mto unaweza kupotea," amesema Jafo.
 
Umesema anaitwa MAYELE??

Basi kacheza kama UTOPOLO kwenye taarifa yake[emoji28][emoji28]
 
Taarifa ya uchafuzi wa mto mara na kufa kwa samaki, je taarifa iliyotolewa imejaa siasa au uhalisia?
Au ni mkakati maalum kama tulivyoanza na machinga (wanachafua jiji) tukaja kwa wamasai ngorongoro wamevamia mbuga,
sasa ni zamu ya wanaoishi kandokando ya mito, na pengine hatmaye ni tz nzima, inachafua dunia, tupelekwe sayari nyingine! 🙌

Kama kinyesi kimewezekana kuchafua mto, iweje taka za mgodini zishindwe?

View attachment 2156897

View attachment 2156898

View attachment 2156899
Akapimwe mkojo
 
Hata hivyo, amekanusha picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilizokuwa zikionyesha samaki wakiwa wamekufa kwa wingi, akisema sio kutoka mkoani Mara.
Anapokanusha pia aseme ni picha za wapi anakofahamu zimetoka
 
Hii ripoti naitilia shaka kwa kuwa hayo maji ya mgodi huko Mto Mara kuwa na sumu sio mara kwanza kutokea, ilishatokea tena mara kadhaa miaka iliyopita ikionesha kwamba hiyo ni tabia ya huo mgodi kutiririsha maji yenye sumu mtoni.

Wanaposema hivyo vifo vya samaki vimetokana na kinyesi cha mifugo wangetakiwa watuambie kwa vipi hali hiyo imetokea, siamini kama wakazi wa pembezoni mwa mto Mara hawajawahi kuwa na mifugo siku za nyuma iweje hii hali itokee sasa?

Hapa naona wanahamisha lawama kijanja kutoka kwa uongozi wa mgodi na kuzipeleka either kwa wakulima (mbolea wanayotumia mashambani iliingia mtoni) au wafugaji (walienda kunywesha mifugo yao mtoni).

Hizi chunguzi zinatakiwa siku zote zifanywe na taasisi huru, zisiundwe na kusimamiwa wanasiasa wala mawakala wao, kwani hawa wanasiasa mara nyingi hujuana na mabosi wa migodi kwa kusaidiana mambo mengi ikiwemo kuwafadhili wakati wa kampeni zao, hivyo huwa rahisi kwao kulindana wakati kama huu.
 
je, umewahi kuyaona magugu MAJI ? Je,umewahi kuona Chini yake Kuna nini?
Mkuu issue ya magugu maji siwezi nikaisemea vibaya kwa upande wa huu wa mto Mara, natambua magugu maji yalipoanza kutinga Ziwa Victoria miaka ya 1988 (kama sijakosea) ilipingwa kwa nguvu zote na serikali kupitia wananchi ilifanyika kazi kubwa kuyapunguza.

But till now naona hata samaki wamezoea kuishi mazingira hayo na toka miaka hiyo mpaka sasa hakuna jipya juu ya magugu maji.

Hili suala la uchafuzi wa mazingira wa namna hii unaleta sintofaham maana raia wa kiafrika (baadhi) huwa hawana thamani mbele ya mwekezaji kutoka ughaibuni.

Hiyo taarifa sijaikubali ila nothing to do that so!.
 
Muda wa wawekezaji kula bata,tayari kibano kimewageukia ng`ombe wa maskini...
 
sina uhakika kama umesoma hii taarifa kwa umakini? Ndio maana nikauliza kuna ukweli au ni siasa?
Wamewezaje kupima lita za mkojo ndani ya maji na kubaini kiwango walichotaja?

•~Kinyesi cha mifugo chatajwa kuwa chanzo cha kufa samaki mto Mara*
SATURDAY MARCH 19 2022

Summary
Kamati maalum ya kitaifa iliyoundwa na serikali kuchunguza mabadiliko ya maji ndani ya mto Mara, imetoa taarifa ya chanzo cha mabadiliko katika mto huo yaliyosababisha maji kuwa meusi na kutoa harufu, huku samaki wakifa ambapo chanzo kimeelezwa kuwa ni shughuli za binadamu pamoja na nguvu za asili.

By Beldina Nyakeke

Musoma. Kamati maalum ya kitaifa iliyoundwa na serikali kuchunguza mabadiliko ya maji ndani ya mto Mara, imetoa taarifa ya chanzo cha mabadiliko katika mto huo yaliyosababisha maji kuwa meusi na kutoa harufu, huku samaki wakifa ambapo chanzo kimeelezwa kuwa ni shughuli za binadamu pamoja na nguvu za asili.

Akitoa matokeo ya uchunguzi leo Jumamosi Machi 19, 2022 mjini Musoma, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Samuel Manyele amesema kuwa hali hiyo imetokana na kuwepo kwa kiwango kikubwa cha kinyesi cha mifugo mtoni pamoja na uozo wa mimea ndani ya mto hasa mimea vamizi kama vile magugu maji na matete.

Amesema kuwa hali hiyo ilisababisha kupungua kwa kiasi kikubwa kiwango cha oksijeni ndani ya mto na hivyo maji kubadilika rangi na kuwa na harufu mbaya huku samaki wakikosa chakula na hivyo kusababisha vifo vyao.

Hata hivyo, amekanusha picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilizokuwa zikionyesha samaki wakiwa wamekufa kwa wingi, akisema sio kutoka mkoani Mara.

Amesema kuwa kwa mujibu wa uchunguzi waliofanyana walibaini kuwa mabadiliko hayo ni matokeo ya mvua kubwa iliyonyesha ghafla kwa muda mfupi katika kipindi cha mwezi huu hivyo kutibua uchafu uliokuwa umejikusanya chini ya mto kwa muda mrefu.

"Mvua zingeendelea kunyesha hali hii ingeisha kwani uchafu ungetiririshwa lakini kwa vile mvua zimenyesha na kukatika ghafla ina maana uchafu ule unatoka taratibu na hii hali inaweza kudumu kwa zaidi ya miezi mitatu hadi minne endapo mvua hazitanyesha hapa katikakati," amesema.

Profesa Manyele amesema kuwa mto huo umeathiriwa kuanzia katika kijiji cha Marasibora wilayani Rorya na kijiji cha Wegero wilayani Butiama huku akisema kuwa mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara hauhusiki na uchafuzi huo.

"Mgodi upo mbali sana na maeneo yaliyoathirika na hata kama uchafu unaozalishwa mgodini pale ungezidishwa mara ishirini na kumwagwa mtoni maji yasingebadilika rangi wala kuwa katika hali iivyo sasa na maji ya mto kelekea kule mgodini ni masafi na hayana shida yoyote," amesema.

Amesema kuwa wamebaini uwepo wa kinyesi cha ng'ombe zaidi ya tani 1.8 milioni pamoja na mkojo wa ng'ombe lita 1.5 bilioni uchafu uliotokana na kuwepo kwa ng'ombe zaidi ya laki 3 waliokuwepo katika eneo oevu la mto Mara kwa kipindi cha miezi minane mwaka jana wakati wa kiangazi.

"Ng'ombe mmoja ana toa kilo 25 za kinyesi kwa siku moja na mkojo lita 21 kwa siku kwahiyo ukizidisha kwa idadi hiyo ya ng'ombe mara miezi minane utapata kiwango hicho na hapo bado hatujaweka kinyesi na mkojo wa kondoo, mbuzi na punda," amesema.

Waziri atoa siku saba kwa timu kuchunguza mabadiliko mto Mara

Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Suleiman Jafo ametoa muda wa siku mbili kwa kamati hiyo kuandaa taarifa kamili yenye mpango kazi juu ya nini kifanyike na muhusika ni nani kisha taarifa hiyo ikabidhiwe kwake kwaajili ya utekelezaji.

Chanzo cha samaki kufa mto Mara chatajwa

"Hii taarifa imenipa faraja baada ya uchunguzi kubaini kuwa hakuna kemikali mtoni maana kama kungekuwa na kemikali hii ingekuwa ni habari mbaya sana lakini taarifa hii inaonyesha kuwa tuna kazi kubwa sana ya kufanya ili mto uweze kuendelea kuwepo na tusipochukua hatua za haraka mto unaweza kupotea," amesema Jafo.
Naona ndg zangu wakiamishwa kunusuru mto Mara, vipi ziwa Victoria halihitaji kunusuliwa?
 
Mkuu hakuna anayebishia uchunguzi.
Isipokuwa unahitajika ufafanuzi zaidi, kwamba kinyesi cha mifugo kina uwezekano mkubwa wa kuchafua mto kuliko taka za mgodi? Je,kabla ya hapo hali ilikuwaje? Kwamba kinyesi cha wanyama kinaweza kusababisha samaki kufa ndani ya mto? Na maji kubadili rangi?[emoji848]
Kasikilize ripoti yote hakuongelea kinyesi pekee bali kuna mengine pia.
 
Taarifa ya uchafuzi wa mto mara na kufa kwa samaki, je taarifa iliyotolewa imejaa siasa au uhalisia?
Au ni mkakati maalum kama tulivyoanza na machinga (wanachafua jiji) tukaja kwa wamasai ngorongoro wamevamia mbuga,
sasa ni zamu ya wanaoishi kandokando ya mito, na pengine hatmaye ni tz nzima, inachafua dunia, tupelekwe sayari nyingine! 🙌

Kama kinyesi kimewezekana kuchafua mto, iweje taka za mgodini zishindwe?

View attachment 2156897

View attachment 2156898

View attachment 2156899
Hicho kinyesi in cha tembo na nyumbu au cha wanyama gani?Je,kuna uwezekano mto mkubwa kama Mto Mara unaweza kuchafuka kwa vinyesi?
Pengine hizi Tume in kupoteza raslimali zetu bila sababu maana majibu yake hayalingani na uhalisia wala kulinganishwa na aina/uwezo Wa wajumbe.Ona Sasa,mnamsababishia fedheha Professor wangu.
 
Kuna uhasama Kati ya mgodi na WANANCHI ambao hauwezi kuisha kila siku WANANCHI kuuzunguka mgodi WANAFANYA kila wanachoweza ili kujaribu kuvamis na KUPORA madini imelazimika kuweka ulinzi mkubwa Kwa ghalama kubwa.Wazee wa mazingira wamekuwa wakipishana ili kuhakiki hali ya usalama na namna MAJI taka yanavyo tibiwa.

Migodi binafsi inaendelea na Kazi bila TAHADHALI yoyote na hakuna kinachofanyika.

Kuhusu uchafuzi wa MTO taasisi za uchunguzi zinapaswa kuaminika.
Yaani uamini ripoti ya kijinga namna hiyo??
Angalia ripoti ya ufugaji wa samaki na ng'ombe hapa chini

IMG-20220319-WA0038.jpg
 
Back
Top Bottom